Duh, hii ni hatari! Kumbe wananchi walikusudia kumuua mkuu wa Wilaya

Jambo la kwanza kuhusu wananchi kutaka kumuua mkuu wa wilaya ni jambo la kusikitisha sana na ni la aibu kubwa,lazima tufahamu kwamba tuna nchi yenye katiba na sheria na mahakama na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo tunajivunia,kama mkuu huyo inavyodaiwa kuwa alijibu maneno ya kuudhi wananchi au kuwakejeli basi ingefaa wananchi hao wajitokeze kwa pamoja na kufanya kampeini kabambe ya kutaka mkuu huyo aondolewe katika wilaya hiyo au aombe radhi na baadae kuua si suluhisho ila wangemtia discpln tu kwa kichapo cha haja ili iwe fundisho kwa wote wanaojifanya mungu mtu pindi wanapopata madaraka.
 
Serkali isiyo sikivu wanaoiwakilisha ndio watabeba lawana. Mambo mangapi yanatendeka hapa rais anaambiwa amekaa kimya hana mpango wala nini? Wananchi wamechoshwa . Nidhamu za woga ndio zinapelekea wananchi wasipate ufumbuvi wa matatizo yako. Tatizo la rais huyu ni kuchagua mcd badala ya madc
 
Kama matatizo ya wananchi yanaimbwa kama ngonjera na rais anayasikia na asiyafanyie kazi. Unafikiri wananchi wafanyeje? Tatizo huyu rais siyo msikivu na hafanya kama watu wanvyomtarajia anaambiwa atulie nchini yeye kiguu na njia siku moja atakuja shangaa wawakilishi wote wako chini ya ulinzi na wananchi wamechukua chao. Badala ya kuteua madc yeye anateua mcd.
 
Hiyo kumbe ni tetesi tu,hamna ushahidi wenye uthibitisho hivyo wewe utakuwa hatiani kwa kuzusha mambo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom