Kuna Select 1 & 2 na Blitz tu. Na hata channel ya BBA haimo. Ukitaka BBA ni lazima ikutoke 59,000. Kwa channel za Select ktk sports wala sijakikubali hiki kifurushi kihivyo, coz mara nyingi hizi channel huonesha marudio ya mechi, na huonesha live mechi za Ligi za Afrika.
Angalau wangeingiza hata Maximo moja ningeweza kuwaelewa, wao wameona kitu cha maana ni channel ya Maisha Magic Swahili ambayo siifagilii sana kwani ina vipindi vingi vya marudio ya channel za Afrika Mashariki, maana kama ni mtazamaji mzuri wa Citizen, KBC, KTN na EATV utaona vipindi vya mwaka mmoja uliopita vikiwa humo.
Ila nimewaelewa katika channel za Discovery World, angalau inaweza kufukia mashimo. Bado nawasubiri katika kupunguza bei za vifurushi vyao, jamaa wako ghali sana.
Ova