Drones ni muhimu sana kuzima moto

Hakuna drone za kuzima moto mkubwa! Narudia tena, hakuna drone za kuzima moto mkubwa!
Izo ndo zinafanya mashambulizi ndani ndani ambapo ni hatari kwa binadamu kuingia na zinaleta taarifa za logistic jinsi ya kuingia
images%20(14).jpeg
bourdon-de-lutte-contre-l-incendie-61288360.jpeg
M600%2BElideFire%2B-2%2B-%2BV2.jpeg
DRONE_INCENDIE-5484-1404ac34.jpeg
120725085839-french-firefighter-drone-story-top.jpeg
571aa364a065f.image_.jpeg
421765-firefighting-drones.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mpiga picha za harusi usinichoshe na ulimbukeni wako, unajifanya eti umetumia drones zote duniani, ivyo vidubwasha vya kitoto unavyotumia kupiga picha kwenye harusi ndo unajiona umemaliza kila kitu duniani. Hebu kaa kimyaView attachment 1339599View attachment 1339603View attachment 1339605View attachment 1339606View attachment 1339607View attachment 1339608

Sent using Jamii Forums mobile app
Una-google! Google yenyewe ndiyo umeujua siku za karibuni. Nyie ni wale wabongo ambao wanadhani kila kitu wanacho-google kina uhalisia. Sasa mimi nakuhakikishia niko dunia ya kwanza na huku hakuna drone zenye uwezo wa kupambana na moto mkubwa. Hivi unavyo-google havina uhalisia wowote. Sidhani hata kama unajua moto unavyozimwa (labda u-google na uje na nadhania nyingine ambayo huielewi). Australia imeteseka sana sana na moto na ndege kubwa zikisaidiwa na watu (wakiwa na vifaa) ndiyo zilihusika kuzima. Ingekuwa hiyo teknologia ina uhalisia moto ungezimika mara moja! Ficha ushamba wako wa ku-google...
 
Mkuu yaani field yako halafu hujui kama drones zinatumika kwenye kuzima moto? Kweli hii Jf.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hazina uwezo wa kuzima moto mkubwa... Achana na hizi picha za ku-google... Hizi ziko nyingi tu na mimi nilijua zipo na najua zipo na bado nasisitiza duniani hakuna drone zenye uwezo wa kupambana na moto mkubwa.. Labda zitengezwe baadae lakini kwa sasa hakuna
 
Akirudi kubisha hapa tena achana nae mkuu. Hajui drone huyo anakupotezea muda.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa kama hao ndio washauri watia ndimu Kwanini wasiweke Fitna “mzeee wanaiba hizo drone pale kwa Sapna ni milioni 2 “... mnamtia presha bure
Hakuna kitu Kibaya mtu kukosa Exposure alafu ukae na watu ambao hawana Exposure Au hata kama wanayo ni wanafiki
 
Hazina uwezo wa kuzima moto mkubwa... Achana na hizi picha za ku-google... Hizi ziko nyingi tu na mimi nilijua zipo na najua zipo na bado nasisitiza duniani hakuna drone zenye uwezo wa kupambana na moto mkubwa.. Labda zitengezwe baadae lakini kwa sasa hakuna

Ushamba mzigo

Ushaambiwa jukumu namba moja la drone ni kupiga picha maalum Eneo kwenye moto kwa kuwa zimeundwa kihimili moto na zinarusha real time pictures kwenye gari ya scene Control kumuwezesha kamanda kuelekeza wazima moto na waokozi
Hiyo uwezo wa kubeba fire extinguishers ni ziada tu
 
Mwenye mamlaka ya kukopa ni wizara ya fedha kosa ndio hilo Haya mengine ni maelezo ya mambo yaliopo kwenye kukopa.drones,kulipwa dola 800 kulipiwatiketi za ndege .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Ushamba mzigo

Ushaambiwa jukumu namba moja la drone ni kupiga picha maalum Eneo kwenye moto kwa kuwa zimeundwa kihimili moto na zinarusha real time pictures kwenye gari ya scene Control kumuwezesha kamanda kuelekeza wazima moto na waokozi
Hiyo uwezo wa kubeba fire extinguishers ni ziada tu
U-mjini nao mzigo zaidi! Kwa haya haya mazingira ya Tanzania, nyumba inawaka moto, badala ya kuzima unatuma drone kupiga picha? Hebu tutumie walau robo ya ubongo wetu tunapoelezea vitu kama hivi. Hayo magari ya kuzimia yapo? Akili zako za 'ki-mjini'' zinakutuma kuwa tukimbilie kununua drone badala ya magari? Katika mikasa yote ya nyumba kuungua eg jiji la Dar, ni mara ngapi umeshasikia kuwa majanga yametokea kwa sababu wazimamoto walishindwa kujua kama ndani kuna watu au la na wako wapi? Ndugu, kuna vitu vya msingi na lazima kufanya kabla huja-complicate kununua vitu visivyo na umuhimu wowote kwenye mazingira yetu.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
instagram,

Pamoja na Ukomedi wake Kangi kwenye hili kaonewa

Na hata ni aibu kuwa Kamishna General Andengenye na MAJ general Kingu wametakiwa kujiuzulu kwenye hili ; ni uonevu na majungu tu

Kwanza hakuna Memorandum Of Understanding inayohitaji kibali Cha Bunge ; kwenye manunuzi nyeti ya vifaaa vya ki usalama hakuna kampuni inayoweza kukupa tpur kwenye facility zake ikiwemo demonstrations bila mwisho kutaka msaiini MoU.

Hapo haitaongelea uwezekano wa kununua tu bali nao wanajilinda juu ya uwezekano wa kuwatembelea wakawapa taarifa zao na nyie mkazitumia kuwapa washindani wao... kuna mambo mengi.

Kuwa na MoU haikua inawalazimisha kununua bali ni “Nia Njema ya uwezekano wa kununua; intention “
Ni aibu kuwa wanaomzunguka Rais wametuhusu atumie sababu isio na mshiko kufukuza watu kazi
Hii itakua inauwa ubunifu ; moja ya kazi ya majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni kuzunguka duniani kote kutafuta teknelojia mpya na hakuna kampuni au nchi watakayoenda na kuruhusiwa kuonyeshwa technology bila kusainishwa MoU hata kama ni “non disclosures “ bado ziko in the form of bilateral mou ... Sasa kama wanafungwa mikono watakuwa wanasafiri wanarudi hawajaonyeshwa lolote la Maana kwakua wanaogopa kusaini .. na hizo terms huwa zinakuwa shared hata kabla ya Safari

Hadi kuchukua uamuzi wa kununua teknelojia ya Kiulinzi na usalama Timu zilizoenda nchi mbali mbali hufanya presentation kwenye Kamati maalum na ndio huamua kampuni gani ichukuliwe mkataba wa mwisho wa kujadiliana Malipo hapo hujadiliwa na Hazina na lazima Rais ahusike na kama ni pesa nyingi lazima Rais wa nchi yenye kampuni ahusike kama kunahitajiika dhamana ya mikopo.

Pia kuna baadhi ya vifaaa ikiwemo hizo high tech lazima pia kibali Cha kuruhusu technology na mitambo kuuzwa hata kama mnanunua kampuni Binafsi Rais wa nchi inayouza akubalii kwa kusaini na pengine kwa mazungumzo na mwenzake wa nchi inayonunua.

Hiyo hatua waliyowafukuza ni jambo la kawaida mno kwenye sourcing na ni hatua ya awali sana ambayo sio lazima hata Rais kutaarifiwa pengine ingeweza kuchukua hata miaka miwili mbele kabla ya mkataba halisi wa mauziano kufikiwa

Kwenye hili kama ni harufu ya hujuma itakuwa kuna waliomzunguka Rais wana kampuni zao au yao ambayo wangependa itembelewe wakaona haijapewa kioaumbele wakaamua kupotosha

Kwa watu weledi kama MAJ gen Kingu na CGF andengenye wana uzoefu wa kutembelea hizo kampuni kutokana na historia zao na kabla ya kufanya shortlist ya kampuni za kutembelea kutafuta technology fulani lazima tathmini ya awali hufanyika kutokana na mahitaji na wataalamu ndio huamua kampuni ambazo wanadhani zitafaa kwenye Kila category ya vifaaa ( preliminaries)

Pia nadharia nyingine huenda tu hataki kuwanunulia vifaaa hivyo ameamua kudiscourage mchakato ina maana hata CGF atakayekuja hatadhubutu tena kuomba vifaaa... na watabakia zimamoto jina tu.
Tatizo siyo kununua hivyo vifaa bali matatizo yako kwenye utaratibu wa manunuzi hayo ulivyotumika. Kwanza huwezi kuingia MoU ya kununua vifaa vya 1+ Trillion bila kulihusisha Baraza la Mawaziri. Halafu vifaa vya fire siyo nyeti kiasi hicho kiasi NW kufichwa na kufanywa kuwa siri. Kwanini waziri wa fedha hakuhusishwa kwenye huo mchakazo wa mkopo? Kwanini supplier awanunulie Laptop na kuwalipa perdiem wahusika wa mchakato wa mkopo huo? Hiyo si rushwa?? Mimi kwa maoni yangu mchakato wote huo uligubikwa na rushwa!
 
U-mjini nao mzigo zaidi! Kwa haya haya mazingira ya Tanzania, nyumba inawaka moto, badala ya kuzima unatuma drone kupiga picha? Hebu tutumie walau robo ya ubongo wetu tunapoelezea vitu kama hivi. Hayo magari ya kuzimia yapo? Akili zako za 'ki-mjini'' zinakutuma kuwa tukimbilie kununua drone badala ya magari? Katika mikasa yote ya nyumba kuungua eg jiji la Dar, ni mara ngapi umeshasikia kuwa majanga yametokea kwa sababu wazimamoto walishindwa kujua kama ndani kuna watu au la na wako wapi? Ndugu, kuna vitu vya msingi na lazima kufanya kabla huja-complicate kununua vitu visivyo na umuhimu wowote kwenye mazingira yetu.
Hivi walisema kwenye iyo trillion 1 hawatanunua magari au umeng'ang'ania drones tu? Hivi unajua magnitude ya 1 trillion? Hoja hapa ni kwamba drones zimetolewa kama kitu cha kipumbavu huenda hatA bajeti yake haikuzidi 500 million na utakuta iyo bajeti mostly ni magari ila ndo mazwazwa mkiamua kujitoa ufahamu mmejiaminisha kwamba zinaletwa drones za 1 trillion.

Drone ya nini kwenye moto kwa haya mazingira yetu? Drone ya nini? Nyumba zetu hizi zilivyo drone itatumika wapi? Visa vyote vya nyumba kuungua Dar au sehemu nyingine ni tukio gani unaweza kusema hili kama drone ingekuwepo ingesaidia? Hoja yangu ni kuwa hatuzihitaji kwenye moto. Ingekuwa kupigana na uhalifu hapo ni jambo jingine lakini siyo kwa zimamoto! Kama uzwazwa ni kukataa jambo lisilo la maana basi acha niendelee kubaki zwazwa!
 
Kwaiyo wewe unajua zimamoto ni kuzima moto nyumba za uswahili tu. Hujui kuwa zimamoto hufanya shughuli zote za uokoaji? Anyway wewe ndo unajua zaidi kuliko wataalamu wenyewe wa zimamoto walio request izo drones? Kwaiyo wewe wataalamu wa jiolojia waki request vifaa yao vya kazi mkemia akisema vya kipumbavu na wewe utashadadia tuu. Daktari akiagiza vifaa vya robotic kufanya operations kwa video, mkemia akisema vya kipumbavu wewe utashobokea na mi knowledge yako kupiga video za harusini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
karibu wilaya zote hazina magari ya zimamoto na baadhi ya mikoa na viwanja vya ndege , unanunua Drone ya Nini ? wilaya zaidi ya 40 hazina kabisa magari ya zimamoto.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nisawa kuvaa na kununua suti wakati watoto karibu wote hawana viatu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
U-mjini nao mzigo zaidi! Kwa haya haya mazingira ya Tanzania, nyumba inawaka moto, badala ya kuzima unatuma drone kupiga picha? Hebu tutumie walau robo ya ubongo wetu tunapoelezea vitu kama hivi. Hayo magari ya kuzimia yapo? Akili zako za 'ki-mjini'' zinakutuma kuwa tukimbilie kununua drone badala ya magari? Katika mikasa yote ya nyumba kuungua eg jiji la Dar, ni mara ngapi umeshasikia kuwa majanga yametokea kwa sababu wazimamoto walishindwa kujua kama ndani kuna watu au la na wako wapi? Ndugu, kuna vitu vya msingi na lazima kufanya kabla huja-complicate kununua vitu visivyo na umuhimu wowote kwenye mazingira yetu.

Kwenye manunuzi kulikua na list ndefu ya vifaaa ; kuanzia
mavazi
Magari ya kuzima moto
Magari ya operesheni ( Utawala)
Ambulance
vifaaa mbali mbali ie Ngazi maalum etc
Vifaaa vya Mafunzo
Na hizo Drones ni sehemu tu ya vifaaa
Hatua ya kuchagua item moja tu kati ya list ndefu hiyo “drone” na kuitumia hiyo tu kama Fimbo ya kuwachapa wahusika inaonyesha kabisa ni sababu tu wametafutiwa

Hivi wewe kabisa kwa akili yako ; unadhani maafisa wenye uweledi kama Maj Gen Kingu ; Commissioner Andengenye na wasaidizi wao woote kabisa wangeweza kununua kamera za Trilion Moja wakati Kila mtu anajua kuwa jeshi la zimamoto simply ni jina tu wana Uhaba mkubwa sana wa Vifaaa
Hata Sare zao tu ni shida na ndio maana kazi wanayobakiwa nayo ni kukagua tu fire extinguishers mitaani na kutumika kama watoza ushuru

Hili suala hata ukitafuta reports za wazi na Ndani “ malalamiko ya vijana “ ni makubwa Sana kwa ujumla kwenye suala zima la Vitendea kazi na isifanywe Siasa hapa

Siku matatizo yakitokea tunaanza kukimbilia kuomba misaada nje
Pale Rusumo Mpakani moto uliunguza magari hao zimamoto na vyombo vingine Walibaki kukodoa macho hadi Zimamoto ya Rwanda wakaja na Helicopter

Moto wa SONGAS SERIKALI baada ya kuona hauzimiki waliruhusu dola milioni 3 zitumike kuagiza ikodishwe ndege maalum kuzima bahati ukazimika ikiwa haijafika ; Kila mtu alishakata tamaaa na kama matanki yangelipuka Eneo la square km 5 toka pale lingeungua

Leo hiii watu wanatafuta vifaa ( sio kununua ) mnawasingizia walitaka kununua “drone” as If ndio the only item

Haya mshawafukuza je hiyo inaondoa ukweli kuwa kuna tatizo la vifaaaa ? tatizo limeisha au ni njia tu ya kuahirisha Tatizo maana atakayekuja hapo hata kuulizia tu au kuwa pro active kuendelea kutafuta vifaaa ataogopa
 
Tatizo siyo kununua hivyo vifaa bali matatizo yako kwenye utaratibu wa manunuzi hayo ulivyotumika. Kwanza huwezi kuingia MoU ya kununua vifaa vya 1+ Trillion bila kulihusisha Baraza la Mawaziri. Halafu vifaa vya fire siyo nyeti kiasi hicho kiasi NW kufichwa na kufanywa kuwa siri. Kwanini waziri wa fedha hakuhusishwa kwenye huo mchakazo wa mkopo? Kwanini supplier awanunulie Laptop na kuwalipa perdiem wahusika wa mchakato wa mkopo huo? Hiyo si rushwa?? Mimi kwa maoni yangu mchakato wote huo uligubikwa na rushwa!

Kwa uelewa wako makampuni yote yanayouza vifaaa vya category ya “usalama” duniani wakialika majeshi au maafisa wa nchi yeyote kwenda kuona vifaaa huwa wanagharamia wao Kila kitu kuanzia ticket ; malazi hadi gharama za kujikimu that is a normal practice iwe mtanunua au hamnunui
Mfano leo hii AIRBUS wanazindua aina mpya ya Helicopter wataalika maafisa wa Kijeshi au waambata wa Kijeshi kwa gharama zao ( na kawaida anayealika hulipa standard rate kadiri ya nchi husika )

Ila ikitokea mnaenda kutafuta vifaaa “sourcing” bila mualiko basi hapo serikali inatakiwa inagharamia

Kuna nchi zingine zina pesa ambazo hata wakialikwa aidha huwalipa waliotumwa stahiki zao mbali ya zile wanazolipwa na hayo makampuni au Hukataaa kugharamiwa
Sasa tujiulize kama wanasema supplier aliwalipa perdiem ; je yeye aliwalipia ( na kuwagiza wakatae Malipo ya aliyewaalika)
Aliwalipia nauli ? malazi ?
Iwapo haya yalifanyika basi ana haki kualalamika na kama hayakufanyika basi iwe kimya
 
Back
Top Bottom