Drones ni muhimu sana kuzima moto

Drones ni muhimu sana kuzima moto

Sawa Drones zina umuhimu sana,Lakini kwa nini usiombe ushauri kwa kuagiza hizo Drones?Siyo unaagiza tu kama unanunua Maandazi.
 
Watu wakiwa trapped kwenye kufusi au jengo lililoungua Ni vp mtajua location yao
Hizo changamoto hata ulaya bado zipo, sembuse hii nchi ambayo watoto, shuleni bado wana kaa chini? Sasa hata ukiwa nazo ukajua walipo vifaa vya kuwafukua huna, inasaidia nini? Yaani kwenye majanga bado tuko ZEROOOO!! majanga mangapi yametokea na kutuacha uchi hapa? Hata waokoaji tu shida!!
 
Zina kazi nyingi kwenye majanga kubeba damu,madawa,maboya ya uokozi,utumika kufukuza wanyama wahalibifu mashambani na kuwarudisha mbugani,mfano tembo akiona drones ukimbia balaa kushinda gari,
Mtu anajua drones ni camera tuu ya harmonize na hanscana au kwenye harusi, kumbe application nzima ya drones ina wigo mpana mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo changamoto hata ulaya bado zipo, sembuse hii nchi ambayo watoto, shuleni bado wana kaa chini? Sasa hata ukiwa nazo ukajua walipo vifaa vya kuwafukua huna, inasaidia nini? Yaani kwenye majanga bado tuko ZEROOOO!! majanga mangapi yametokea na kutuacha uchi hapa? Hata waokoaji tu shida!!
Kwaiyo tu subiri kwanza ulaya viwepo kwanza miaka 100 ndo tinunue? Mimi sijaongelea vifaa vingine vya kufukulia nimeongelea drones. Kwani wewe una hakika kuwa hawakua na mpango wa kununua vifaa vya kufukulia. Haya majitu ndo utakuta likianguka jengo la yanakuja na hoja za ajabu ohh zimamoto yetu haina vifaa, ooh jeshi linaendeshwa kizamani, ooh tuite wazungu watusaidie. Mtakaa hadi lini majanga mnasubiri waokoaji kutoka south na ulaya waje? Imezama boti juzi hapo watu 700 wamekufa mita chache toka nchi kavu mmetoa lawama kibao kwa waokoaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
instagram,

Pamoja na Ukomedi wake Kangi kwenye hili kaonewa

Na hata ni aibu kuwa Kamishna General Andengenye na MAJ general Kingu wametakiwa kujiuzulu kwenye hili ; ni uonevu na majungu tu

Kwanza hakuna Memorandum Of Understanding inayohitaji kibali Cha Bunge ; kwenye manunuzi nyeti ya vifaaa vya ki usalama hakuna kampuni inayoweza kukupa tpur kwenye facility zake ikiwemo demonstrations bila mwisho kutaka msaiini MoU.

Hapo haitaongelea uwezekano wa kununua tu bali nao wanajilinda juu ya uwezekano wa kuwatembelea wakawapa taarifa zao na nyie mkazitumia kuwapa washindani wao... kuna mambo mengi.

Kuwa na MoU haikua inawalazimisha kununua bali ni “Nia Njema ya uwezekano wa kununua; intention “
Ni aibu kuwa wanaomzunguka Rais wametuhusu atumie sababu isio na mshiko kufukuza watu kazi
Hii itakua inauwa ubunifu ; moja ya kazi ya majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni kuzunguka duniani kote kutafuta teknelojia mpya na hakuna kampuni au nchi watakayoenda na kuruhusiwa kuonyeshwa technology bila kusainishwa MoU hata kama ni “non disclosures “ bado ziko in the form of bilateral mou ... Sasa kama wanafungwa mikono watakuwa wanasafiri wanarudi hawajaonyeshwa lolote la Maana kwakua wanaogopa kusaini .. na hizo terms huwa zinakuwa shared hata kabla ya Safari

Hadi kuchukua uamuzi wa kununua teknelojia ya Kiulinzi na usalama Timu zilizoenda nchi mbali mbali hufanya presentation kwenye Kamati maalum na ndio huamua kampuni gani ichukuliwe mkataba wa mwisho wa kujadiliana Malipo hapo hujadiliwa na Hazina na lazima Rais ahusike na kama ni pesa nyingi lazima Rais wa nchi yenye kampuni ahusike kama kunahitajiika dhamana ya mikopo.

Pia kuna baadhi ya vifaaa ikiwemo hizo high tech lazima pia kibali Cha kuruhusu technology na mitambo kuuzwa hata kama mnanunua kampuni Binafsi Rais wa nchi inayouza akubalii kwa kusaini na pengine kwa mazungumzo na mwenzake wa nchi inayonunua.

Hiyo hatua waliyowafukuza ni jambo la kawaida mno kwenye sourcing na ni hatua ya awali sana ambayo sio lazima hata Rais kutaarifiwa pengine ingeweza kuchukua hata miaka miwili mbele kabla ya mkataba halisi wa mauziano kufikiwa

Kwenye hili kama ni harufu ya hujuma itakuwa kuna waliomzunguka Rais wana kampuni zao au yao ambayo wangependa itembelewe wakaona haijapewa kioaumbele wakaamua kupotosha

Kwa watu weledi kama MAJ gen Kingu na CGF andengenye wana uzoefu wa kutembelea hizo kampuni kutokana na historia zao na kabla ya kufanya shortlist ya kampuni za kutembelea kutafuta technology fulani lazima tathmini ya awali hufanyika kutokana na mahitaji na wataalamu ndio huamua kampuni ambazo wanadhani zitafaa kwenye Kila category ya vifaaa ( preliminaries)

Pia nadharia nyingine huenda tu hataki kuwanunulia vifaaa hivyo ameamua kudiscourage mchakato ina maana hata CGF atakayekuja hatadhubutu tena kuomba vifaaa... na watabakia zimamoto jina tu.
Uelewa wako kwenye mambo ya mikataba ukoje? Nani kakuambia MOU haiwezi kumbana mtu wa upande wa pili? Nakushauri ujaribu kufanya research zaidi utagundua siyo MOU zote zimefanana!
 
Trilion moja Parefu sana, tusibeze. Hata ningekuwa mimi Rais ningemtimua mtu, Yaani unaiingiza inchi kwenye ishu ya shilingi Trilioni kimya kimya eti sio lazima Rais ajue, hiyo akili pumba. PATO LA NCHI LA MWEZI MZIMA.
 
Kwaiyo tu subiri kwanza ulaya viwepo kwanza miaka 100 ndo tinunue? Mimi sijaongelea vifaa vingine vya kufukulia nimeongelea drones. Kwani wewe una hakika kuwa hawakua na mpango wa kununua vifaa vya kufukulia. Haya majitu ndo utakuta likianguka jengo la yanakuja na hoja za ajabu ohh zimamoto yetu haina vifaa, ooh jeshi linaendeshwa kizamani, ooh tuite wazungu watusaidie. Mtakaa hadi lini majanga mnasubiri waokoaji kutoka south na ulaya waje? Imezama boti juzi hapo watu 700 wamekufa mita chache toka nchi kavu mmetoa lawama kibao kwa waokoaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ulishaona drone ikizima moto wapi? Kwangu mimi nimetembea sehemu nyingi duniani na nimeona idara za Zimamoto nchi mbali mbali hakuna wanaotumia drone!
 
Kwa jeshi la zimamoto Tz, kwa sasa ni ujinga kuwa na kipaumbele cha drones, wakati kuna vifaa vya msingi tena vyenye umuhimu sana, kuliko hata hizo drones, mtoto akitumbukia kwenye shimo la choo tu, ni shida, kisa vifaa hawana!!
 
Mazee wacha kukoroga tumbaku hapa. Mpaka sasa hakuna drone zenye uwezo wa kukabiliana na moto mkubwa! Umeshaona jengo limeshika moto kweli wewe? Unajua uwezo wa drones kwenye kubeba chemicals zinazotumika kuzima moto? Itazima moto gani drone? Uwezo wake ni mdogo kabisa. Tangu wengine msikie hile neno drone basi mmekariri tu bila hata kujua ni chombo cha aina gani hasa! Ghorofa limepemba moto haswa halafu uzime na drone? Hii biashara waliotaka kuifanya haina tofauti na ile ya Lowassa alitotaka kuleta kutoka Thailand ya kutengeneza mvua. Na kama ni drone za kupiga picha basi kwa taarifa yako madukani zimejea! Bei zake ni rahisi na hazifiki miliona tatu. Na hapa nazungumzia ile drone nzuri kabisa ya kupuiga picha!
 
Kwa jeshi la zimamoto Tz, kwa sasa ni ujinga kuwa na kipaumbele cha drones, wakati kuna vifaa vya msingi tena vyenye umuhimu sana, kuliko hata hizo drones, mtoto akitumbukia kwenye shimo la choo tu, ni shida, kisa vifaa hawana!!
Asante sana mkuu kwa kuliona hili. Watu wengine utafikiri wana vichwa vya plastic. Mtu huna gari la kuzimamoto linaloeleweka halafu unakimbilia kununua drone ambayo haiwezi kuzima moto. Na anaposema hizo drones zitapiga picha ndiyo iweje sasa? Ikishapiga picha na huku hatuna uwezo wa kuokoa hao waliopigwa picah si ni uendawazimu mtupu? Tuanze kwanza na yale muhimu.
 
Wewe ulishaona drone ikizima moto wapi? Kwangu mimi nimetembea sehemu nyingi duniani na nimeona idara za Zimamoto nchi mbali mbali hakuna wanaotumia drone!
Mkuu nakubaliana na hoja kwamba drone kwa jeshi Letu ambalo halina magari, vifaa vya kisasa ni upotezaji wa hela tu.Matumizi yake yatakuwa hayana msaada.

Ila drones zinatumika kwa nchi zilizoendelea kusaidia kuzima moto.

Mfano inapiga picha kitaalamu kudect chanzo cha moto na kuuzima kwa haraka, kuangalia watu waliokwama n.k n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Rais amesema wamesaini mkataba? Amewaagiza mawaziri waangalie namna ya kuuvunja?!

Pitia hotuba Kasema ; “ wamsaini MoU” ; sio Contract
MOU sio mkataba bali ni makubaliano tu ya kawaida kama sehemu ya hatua ya kuelekea mkataba rasmi
Kuvunja MOU ni tofauti na mkataba
 
Nadhani hujamuelewa anko katika suala hili nyeti hadi awe na hasira na aweze kuchukua hatua hyo :-
Kwanza analoshtuka ni jinsi mtu unaetaka kufanya nae mazungumzo ya biashara, akulipie hela ya allowance, usafiri, na malazi wakati wewe umeshafanyiwa hayo yote na serikali yko, je hapo hakuna mchezo mchafu? Huyo mtu anatoa hela hizo yeye atazirudishaje?

Pili, anashangaa hata yeye analetewa summary tu ya dondoo ya Mambo yanavyoenda na anaambiwa asaini, kuna nini nyuma ya pazia?

Tatu, mfumo wa kila kitu katika masuala ya mikopo ya nchi inahusu wizara ya fedha, lakini haikupitia huko, kwa nini kuna trespass katika procedure?

Nne, kuna ishu ya drones km Rais anavyopesema, ni sawa, lakini sisi km nchi ndo vipaumbele vyetu? Wakati tunahitaji magari ya zima moto ambayo yanaweza fika hata ghorofa 10, yapo Tanzania? Kuhusu nguo zao zile zisizoshika moto? Na mengineyo?

Tano, kuna vipengele vya mkopo wakati hatujui hizo banks za nje zinatoza riba kiasi gani, kwa nini tufichwe?

Yapo mengi ya kujiuliza hivyo tusubir takukuru huenda tutajua ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app

Kampuni zinazoalika nchi mbali mbali kutembelea facilities zao huwa zinagharamia Idadi fulani ya watu maana wao ndio wanataka mkaone mfumo wao ... hii sio hapa tu ni kote na hulazimiki kununua

Ila kuna scenerio ambapo Nchi inatumia gharama kutafuta vifaaa bila kusubiri mualiko wa wazalishaji ... hapo inajigharamia Kila kitu

Hii hata kampuni binafsi kuna wakati zinapata mialiko ya wazalishaji wanawagharamia Kila kitu
 
Hali ni mbaya sana ila tuliomo ndani ya zimmoto tunasubiri muujiza, huwezi amini baadhi ya maeneo hata ukitaja neno firesuit au horse tu wanaweza kukuuliza ndio toleo la kampuni gani hilo la simu? Kumbe ni moja ya vitendea kazi muhimu.

Huyu ni Rais wetu wote kuna mambo anatakiwa kuambiwa ukweli ...hili haliko Sawa
Na narudia tena kama sio fitna ya waliomzunguka ambao kampuni waliyotaka itembelewe imetokea haijapita kwenye vigezo
Basi ni ile ile mbinu ya kutafuta sababu ya KUTOWANUNULIA VIFAA

KATIKA yaliyofanyika hakuna jambo la Ajabu na iko siku mtakumbuka
Huwezi kuwa na Jeshi la wazima moto hawana vifaaa na kutegemea Kila mara watumie michanga

Kuna wanaoongelea drone hiyi ndio technology ya Sasa ya kupiga picha maeneo yenye matukio kama moto ili walio kwenye control vehicle waweze kuona ni wapi moto upo au kuna watu wanahitaji kuokolewa ili kamanda wa operesheni atoe amri sahihi
 
Hii ina make a lot of sense.

Bwana Mkubwa ameamua tu kutuchanganyia habari ili hali akijua kabisa vichwa vya Watanzania watakavyopokea.

Hao wenye Kampuni husika kuwa entertain Watu ni sehemu tu ya mbinu ya kibiashara, ni sawa na kuingia Duka kubwa ukakaribishwa kahawa au juice huku unatembezwa kuona bidhaa...ni sehemu ya kukuvuta Mteja na sio kosa, ingawa Bw Mkubwa anaiweka ionekane kama ilikuwa ni kosa.

Kuhusu Drones sioni dhambi kutafuta teknolojia mpya kama zinaweza kurahisisha kazi, mbona juzi juzi tumezindua paspoti za kisasa...hivi kulikuwa na emergency yoyote?

Huenda tu Mzee Kangi alikuwa ananing'inia kwenye uzi, ikafika muda.
 
Back
Top Bottom