Mkulu ameshangaa kuwa Drones zinahusika vipi kuzima moto. Drones ni moja ya technology rahisi kuzima moto kwani.
Zimamoto ndiyo taasisi inayohusika na uokoaji wowote wa raia inapotokea moto au tatizo lolote.
Mkulu kawatimua wataalamu wa zimamoto kwa kununua Drones kwamba ni vitu vya kipumbavu. Drones zinasaidia kupiga live picha eneo la tukio kama ghorofani kuweza kujua kama kuna watu wamekwama sehemu gani na kuweza kuwasaidia zimamoto kuwapa kipaumbele cha kuweza kuwaokoa kwanza.
Pia ikitokea ghorofa kuporomoka, drones zinaweza kutumika kupiga picha za x-ray kujua wapi kuna watu wamekwama na kuwezesha zoezi la uokoaji. Ni vema kama mkulu akiwateua wataalamu awaache wafanye kazi bila kuwaingilia na kuwakosoa kwa utaalamu wao kwani wao ndiyo wataalamu.
Huwezi kumuajiri daktari alafu umkosoe kwa kufanya kazi yake kisa wewe unaona ni ya kipumbavu wakati wewe hujasomea udakitari. Ukweli ni kwamba zimamoto ni taasisi ambayo ina uhaba mkubwa sana wa vitendea kazi japo ni moja ya taasisi ya muhimu sana kwa usalama wa raia.
Ifike wakati taasisi ya zimamoto iwezeshwe ili iwe na uwezo mkubwa wa kuokoa mali na uhai wa raia wote katika kila kona ya nchi yetu.
Trillion 1 ni pesa ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa nchi yetu, jeshi la zimamoto linatakiwa liweze kuwafikia kwa wakati raia wote nchi nzima dakika moja wanapopatwa na tatizo la moto au uokoaji wa aina yoyote ile.
Tuwaache wataalamu tuliowapa majukumu wafanye kazi ya kulijenga Jeshi la Zimamoto bila kuwafedhehesha kisa wamefanya maamuzi mazuri bila kupata sifa za wanasiasa.
Sent using
Jamii Forums mobile app