Drones ni muhimu sana kuzima moto

Drones ni muhimu sana kuzima moto

Mkulu ameshangaa kuwa Drones zinahusika vipi kuzima moto. Drones ni moja ya technology rahisi kuzima moto kwani.
Zimamoto ndiyo taasisi inayohusika na uokoaji wowote wa raia inapotokea moto au tatizo lolote.

Mkulu kawatimua wataalamu wa zimamoto kwa kununua Drones kwamba ni vitu vya kipumbavu. Drones zinasaidia kupiga live picha eneo la tukio kama ghorofani kuweza kujua kama kuna watu wamekwama sehemu gani na kuweza kuwasaidia zimamoto kuwapa kipaumbele cha kuweza kuwaokoa kwanza.

Pia ikitokea ghorofa kuporomoka, drones zinaweza kutumika kupiga picha za x-ray kujua wapi kuna watu wamekwama na kuwezesha zoezi la uokoaji. Ni vema kama mkulu akiwateua wataalamu awaache wafanye kazi bila kuwaingilia na kuwakosoa kwa utaalamu wao kwani wao ndiyo wataalamu.

Huwezi kumuajiri daktari alafu umkosoe kwa kufanya kazi yake kisa wewe unaona ni ya kipumbavu wakati wewe hujasomea udakitari. Ukweli ni kwamba zimamoto ni taasisi ambayo ina uhaba mkubwa sana wa vitendea kazi japo ni moja ya taasisi ya muhimu sana kwa usalama wa raia.

Ifike wakati taasisi ya zimamoto iwezeshwe ili iwe na uwezo mkubwa wa kuokoa mali na uhai wa raia wote katika kila kona ya nchi yetu.

Trillion 1 ni pesa ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa nchi yetu, jeshi la zimamoto linatakiwa liweze kuwafikia kwa wakati raia wote nchi nzima dakika moja wanapopatwa na tatizo la moto au uokoaji wa aina yoyote ile.

Tuwaache wataalamu tuliowapa majukumu wafanye kazi ya kulijenga Jeshi la Zimamoto bila kuwafedhehesha kisa wamefanya maamuzi mazuri bila kupata sifa za wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna vitu vingine rais wetu yuko under informed..
 
Mkuu nakubaliana na hoja kwamba drone kwa jeshi Letu ambalo halina magari, vifaa vya kisasa ni upotezaji wa hela tu.Matumizi yake yatakuwa hayana msaada.

Ila drones zinatumika kwa nchi zilizoendelea kusaidia kuzima moto.

Mfano inapiga picha kitaalamu kudect chanzo cha moto na kuuzima kwa haraka, kuangalia watu waliokwama n.k n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo za kupåiga picha zinauzwa rahisi sana. Hata serikali ikimuamua kila wilaya iwe na yake inaweza kununua! Sasa hawa waliotumbuliwa walitaka kutumia zaidi ya trilion moja kununua huu upuuzi wakati gear zenyewe za kuzimia moto kama magari hatuna? Waweke nguvu kwenye magari, mafunzo na vitu vingine vya msingi kwanza.
 
Kwani aliyepinga lift kujengwa kwenye jengo la hospitali ni tofauti au ni yule yule?
 
Hii ina make a lot of sense.

Bwana Mkubwa ameamua tu kutuchanganyia habari ili hali akijua kabisa vichwa vya Watanzania watakavyopokea.

Hao wenye Kampuni husika kuwa entertain Watu ni sehemu tu ya mbinu ya kibiashara, ni sawa na kuingia Duka kubwa ukakaribishwa kahawa au juice huku unatembezwa kuona bidhaa...ni sehemu ya kukuvuta Mteja na sio kosa, ingawa Bw Mkubwa anaiweka ionekane kama ilikuwa ni kosa.

Kuhusu Drones sioni dhambi kutafuta teknolojia mpya kama zinaweza kurahisisha kazi, mbona juzi juzi tumezindua paspoti za kisasa...hivi kulikuwa na emergency yoyote?

Huenda tu Mzee Kangi alikuwa ananing'inia kwenye uzi, ikafika muda.
Hakuna drone zenye uwezo wa kuzima moto in large scale popote duniani hivyo usikariri. Kama unazungumzia hizi za kupiga picha basi zipo nyingi sana madukani na bei yake ni rahisi kabisa.
 
Huyu ni Rais wetu wote kuna mambo anatakiwa kuambiwa ukweli ...hili haliko Sawa
Na narudia tena kama sio fitna ya waliomzunguka ambao kampuni waliyotaka itembelewe imetokea haijapita kwenye vigezo
Basi ni ile ile mbinu ya kutafuta sababu ya KUTOWANUNULIA VIFAA

KATIKA yaliyofanyika hakuna jambo la Ajabu na iko siku mtakumbuka
Huwezi kuwa na Jeshi la wazima moto hawana vifaaa na kutegemea Kila mara watumie michanga

Kuna wanaoongelea drone hiyi ndio technology ya Sasa ya kupiga picha maeneo yenye matukio kama moto ili walio kwenye control vehicle waweze kuona ni wapi moto upo au kuna watu wanahitaji kuokolewa ili kamanda wa operesheni atoe amri sahihi
Umesoma post zangu? Drone za kupiga picha kwa sh trilion? Unataniani wewe! Nimecheza sana na drone tangu zinatoka na nakuhakikishia ni bei rahisi tu. Tafuteni sababu nyingine ya kutetea huo ujinga lakini siyo namna hii!
 
instagram,

Pamoja na Ukomedi wake Kangi kwenye hili kaonewa

Na hata ni aibu kuwa Kamishna General Andengenye na MAJ general Kingu wametakiwa kujiuzulu kwenye hili ; ni uonevu na majungu tu

Kwanza hakuna Memorandum Of Understanding inayohitaji kibali Cha Bunge ; kwenye manunuzi nyeti ya vifaaa vya ki usalama hakuna kampuni inayoweza kukupa tpur kwenye facility zake ikiwemo demonstrations bila mwisho kutaka msaiini MoU.

Hapo haitaongelea uwezekano wa kununua tu bali nao wanajilinda juu ya uwezekano wa kuwatembelea wakawapa taarifa zao na nyie mkazitumia kuwapa washindani wao... kuna mambo mengi.

Kuwa na MoU haikua inawalazimisha kununua bali ni “Nia Njema ya uwezekano wa kununua; intention “
Ni aibu kuwa wanaomzunguka Rais wametuhusu atumie sababu isio na mshiko kufukuza watu kazi
Hii itakua inauwa ubunifu ; moja ya kazi ya majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni kuzunguka duniani kote kutafuta teknelojia mpya na hakuna kampuni au nchi watakayoenda na kuruhusiwa kuonyeshwa technology bila kusainishwa MoU hata kama ni “non disclosures “ bado ziko in the form of bilateral mou ... Sasa kama wanafungwa mikono watakuwa wanasafiri wanarudi hawajaonyeshwa lolote la Maana kwakua wanaogopa kusaini .. na hizo terms huwa zinakuwa shared hata kabla ya Safari

Hadi kuchukua uamuzi wa kununua teknelojia ya Kiulinzi na usalama Timu zilizoenda nchi mbali mbali hufanya presentation kwenye Kamati maalum na ndio huamua kampuni gani ichukuliwe mkataba wa mwisho wa kujadiliana Malipo hapo hujadiliwa na Hazina na lazima Rais ahusike na kama ni pesa nyingi lazima Rais wa nchi yenye kampuni ahusike kama kunahitajiika dhamana ya mikopo.

Pia kuna baadhi ya vifaaa ikiwemo hizo high tech lazima pia kibali Cha kuruhusu technology na mitambo kuuzwa hata kama mnanunua kampuni Binafsi Rais wa nchi inayouza akubalii kwa kusaini na pengine kwa mazungumzo na mwenzake wa nchi inayonunua.

Hiyo hatua waliyowafukuza ni jambo la kawaida mno kwenye sourcing na ni hatua ya awali sana ambayo sio lazima hata Rais kutaarifiwa pengine ingeweza kuchukua hata miaka miwili mbele kabla ya mkataba halisi wa mauziano kufikiwa

Kwenye hili kama ni harufu ya hujuma itakuwa kuna waliomzunguka Rais wana kampuni zao au yao ambayo wangependa itembelewe wakaona haijapewa kioaumbele wakaamua kupotosha

Kwa watu weledi kama MAJ gen Kingu na CGF andengenye wana uzoefu wa kutembelea hizo kampuni kutokana na historia zao na kabla ya kufanya shortlist ya kampuni za kutembelea kutafuta technology fulani lazima tathmini ya awali hufanyika kutokana na mahitaji na wataalamu ndio huamua kampuni ambazo wanadhani zitafaa kwenye Kila category ya vifaaa ( preliminaries)

Pia nadharia nyingine huenda tu hataki kuwanunulia vifaaa hivyo ameamua kudiscourage mchakato ina maana hata CGF atakayekuja hatadhubutu tena kuomba vifaaa... na watabakia zimamoto jina tu.
Tatizo hiyo mikataba mnaificha, mngetuonyesha ili na sisi tujue nini cha kuamini.., maana walioona wanasema mkataba ukianza kutekelezwa ni lazima utekelezwe, sasa hiyo maana yake ulishaanzwa kutekelezwa?
 
Hakuna drone zenye uwezo wa kuzima moto in large scale popote duniani hivyo usikariri. Kama unazungumzia hizi za kupiga picha basi zipo nyingi sana madukani na bei yake ni rahisi kabisa.
Teknolojia inaenda spidi kuliko wewe unavyowaza, acha kukariri.

Wewe umeshaziona hizo Drones? au ukisikia Drone akili inakupeleka tu kwenye hizo za kupigia picha?
 
Teknolojia inaenda spidi kuliko wewe unavyowaza, acha kukariri.

Wewe umeshaziona hizo Drones? au ukisikia Drone akili inakupeleka tu kwenye hizo za kupigia picha?
Siyo tu nimeshaziona ila mimi ni mtumiaji mzuri wa drone. Na aina zote nina ujuzi wa kuzi-operate... multi-rotter, fixed wing. Kama ni picha nimepiga nazo sana. Possibly wewe hata kabla hujajua kuna kitu kinaitwa drone mimi nilikuwa nachezea vile vidogo vya kurusha ndani!
 
Mkulu ameshangaa kuwa Drones zinahusika vipi kuzima moto. Drones ni moja ya technology rahisi kuzima moto kwani.
Zimamoto ndiyo taasisi inayohusika na uokoaji wowote wa raia inapotokea moto au tatizo lolote.

Mkulu kawatimua wataalamu wa zimamoto kwa kununua Drones kwamba ni vitu vya kipumbavu. Drones zinasaidia kupiga live picha eneo la tukio kama ghorofani kuweza kujua kama kuna watu wamekwama sehemu gani na kuweza kuwasaidia zimamoto kuwapa kipaumbele cha kuweza kuwaokoa kwanza.

Pia ikitokea ghorofa kuporomoka, drones zinaweza kutumika kupiga picha za x-ray kujua wapi kuna watu wamekwama na kuwezesha zoezi la uokoaji. Ni vema kama mkulu akiwateua wataalamu awaache wafanye kazi bila kuwaingilia na kuwakosoa kwa utaalamu wao kwani wao ndiyo wataalamu.

Huwezi kumuajiri daktari alafu umkosoe kwa kufanya kazi yake kisa wewe unaona ni ya kipumbavu wakati wewe hujasomea udakitari. Ukweli ni kwamba zimamoto ni taasisi ambayo ina uhaba mkubwa sana wa vitendea kazi japo ni moja ya taasisi ya muhimu sana kwa usalama wa raia.

Ifike wakati taasisi ya zimamoto iwezeshwe ili iwe na uwezo mkubwa wa kuokoa mali na uhai wa raia wote katika kila kona ya nchi yetu.

Trillion 1 ni pesa ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa nchi yetu, jeshi la zimamoto linatakiwa liweze kuwafikia kwa wakati raia wote nchi nzima dakika moja wanapopatwa na tatizo la moto au uokoaji wa aina yoyote ile.

Tuwaache wataalamu tuliowapa majukumu wafanye kazi ya kulijenga Jeshi la Zimamoto bila kuwafedhehesha kisa wamefanya maamuzi mazuri bila kupata sifa za wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lugola tulia dawa ikuingie. Rais amekutumbua kwa sababu hukufuata taratibu za manunuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo fedha zingweza kununua magari mangapi ya zimamoto??
Ni mara ngapi Wananchi+ Askari wa zimamoto wamelalamika kukosekana/ uchakavu wa magari + vifaa vya zimamoto??
 
Back
Top Bottom