instagram,
Pamoja na Ukomedi wake Kangi kwenye hili kaonewa
Na hata ni aibu kuwa Kamishna General Andengenye na MAJ general Kingu wametakiwa kujiuzulu kwenye hili ; ni uonevu na majungu tu
Kwanza hakuna Memorandum Of Understanding inayohitaji kibali Cha Bunge ; kwenye manunuzi nyeti ya vifaaa vya ki usalama hakuna kampuni inayoweza kukupa tpur kwenye facility zake ikiwemo demonstrations bila mwisho kutaka msaiini MoU.
Hapo haitaongelea uwezekano wa kununua tu bali nao wanajilinda juu ya uwezekano wa kuwatembelea wakawapa taarifa zao na nyie mkazitumia kuwapa washindani wao... kuna mambo mengi.
Kuwa na MoU haikua inawalazimisha kununua bali ni “Nia Njema ya uwezekano wa kununua; intention “
Ni aibu kuwa wanaomzunguka Rais wametuhusu atumie sababu isio na mshiko kufukuza watu kazi
Hii itakua inauwa ubunifu ; moja ya kazi ya majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni kuzunguka duniani kote kutafuta teknelojia mpya na hakuna kampuni au nchi watakayoenda na kuruhusiwa kuonyeshwa technology bila kusainishwa MoU hata kama ni “non disclosures “ bado ziko in the form of bilateral mou ... Sasa kama wanafungwa mikono watakuwa wanasafiri wanarudi hawajaonyeshwa lolote la Maana kwakua wanaogopa kusaini .. na hizo terms huwa zinakuwa shared hata kabla ya Safari
Hadi kuchukua uamuzi wa kununua teknelojia ya Kiulinzi na usalama Timu zilizoenda nchi mbali mbali hufanya presentation kwenye Kamati maalum na ndio huamua kampuni gani ichukuliwe mkataba wa mwisho wa kujadiliana Malipo hapo hujadiliwa na Hazina na lazima Rais ahusike na kama ni pesa nyingi lazima Rais wa nchi yenye kampuni ahusike kama kunahitajiika dhamana ya mikopo.
Pia kuna baadhi ya vifaaa ikiwemo hizo high tech lazima pia kibali Cha kuruhusu technology na mitambo kuuzwa hata kama mnanunua kampuni Binafsi Rais wa nchi inayouza akubalii kwa kusaini na pengine kwa mazungumzo na mwenzake wa nchi inayonunua.
Hiyo hatua waliyowafukuza ni jambo la kawaida mno kwenye sourcing na ni hatua ya awali sana ambayo sio lazima hata Rais kutaarifiwa pengine ingeweza kuchukua hata miaka miwili mbele kabla ya mkataba halisi wa mauziano kufikiwa
Kwenye hili kama ni harufu ya hujuma itakuwa kuna waliomzunguka Rais wana kampuni zao au yao ambayo wangependa itembelewe wakaona haijapewa kioaumbele wakaamua kupotosha
Kwa watu weledi kama MAJ gen Kingu na CGF andengenye wana uzoefu wa kutembelea hizo kampuni kutokana na historia zao na kabla ya kufanya shortlist ya kampuni za kutembelea kutafuta technology fulani lazima tathmini ya awali hufanyika kutokana na mahitaji na wataalamu ndio huamua kampuni ambazo wanadhani zitafaa kwenye Kila category ya vifaaa ( preliminaries)
Pia nadharia nyingine huenda tu hataki kuwanunulia vifaaa hivyo ameamua kudiscourage mchakato ina maana hata CGF atakayekuja hatadhubutu tena kuomba vifaaa... na watabakia zimamoto jina tu.