Dragon fruits mdogomdogo inaanza ingia sokoni

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
Dragon fruit ni tunda ghari sana ingawa siku zote naamini kitu kikiuzwa ghari sana una exclude kundi kubwa sana kuto kununua.

Majority ya watu ni wa viapato vya chini. Sasa ukiuza tunda sh 10,000/ au 15,000/ au 5000/ kwa mtu wa kawaida hawezi nununua ni bora akanunue tikitiki maji sh 2000/ hio bei inabakia kwa watu wa daraja la juu ndio watanunua tunda sh 15,000/.

Matunda kama haya yanapaswa kuja kuuzwa sh 500/ au 1000/ na hapo ndio consumption itakuwa kubwa sana.

Hapo ni Arusha mitaa ya Rushuda.tunda moja hapo ni sh 5000/ bado ni ghari sana. inapaswa kuja kuwa sh 1000/ au 1500/ basi.

IMG_20240208_102424.jpg
 
Mambo ya sungura wa nyama, mayai ya kware yanajirudia
Dragon fruits ni matunda na ni chakula,

nchi ina wapumbavu wengi sana hii, Mayai ya kware ni chakula unaweza yatumia badala ya mayai ya kuku, mfano mayai ya kware 2 had 3 ni yai moja la kuku. lets say wewe unatumiaga mayai mawili ya kuku, unawexmza tumia mayai 3 ya kware badala ya mayai ya kuku na bado cost za kuzalisha mayai 6 ya kware ziko chini kuliko za kuzalisha mayai 2 ya kuku.

Nikirud kwenye Nyama, Kware wanafugwa kwa ajili ya nyama, nu kitoweo kamili kabisa,yaani ni full kitoweo ukiachana na maya yake binafisi nawapenda sana upande wa nyama.

Sungura- Sungura ukiachana na utamaduni wa wa watu wengi hawali Sungura kwa sababu ya kiimani, Ila Sungura wana kazi zingine ikiwemo kuwafuga na kuuza nyama ya Mbwa kwa wale wanao fuga mbwa na kuwapa matunzo ya ukweli. Sungura analiwa na mbwa raw meat na ni nyama nzuri sana kwa ajili ya mbwa.

Shida tumejawa na ujinga mwingi sana.Mungu saidia.
 
Tulianza na aloe vera,mafuta ya ubuyu, mayai ya kwale, almond,mbegu za maboga,mkojo wa sungura,kilimo cha nyoka, Tikiti elfu 1 kwa eka, ufugaji wa mende na sasa tumefika kwenye Kilimo cha Dragon

Job kweli kweli.
1.Alovera ni biashara kubwa sana Duniani, huonagi products za Alovera? au unataka vipi?

2. Hayo mafuta ya Ubuyu mbona yanauzwa na watu wana wananunua, unacho pondea kuna wenzako wana make pesa sasa endelea kupondea tu.

3.Mayai ya kware ni chakula, unaweza yatumia badala ya maayi ya kuku, yaani kazi zote zinazo fanywa na mayai ya kuku unaweza tumia mayai ya kware kwa usahihi na bado cost za kuzalisha hayo mayai ya kware zinakuwa chini kuliko za kuzalisha mayai ya kuku.Pia nyama yake ni unaweza kula unaweza tumia kama kitoweo na maisha yakaenda na kware wanatumia space ndogo kuliko kuku na hata chakula pia wanatumia kidogo sana.Wale wanafugwa kwa chakula, mayai yake na nyama yake unaweza hata chemsaha supu yake ni tamu usipime.

4.Almond mbona ziko sokoni na ni ghari sana? Kwanza Tanzania hatulimi almond sasa sijui unazungumzia almondi zipi.

5.Mbegu za Maboga mbona ziko sokoni na ni ghari sana? binafisi niliwahi enda sokoni nikashindwa bei yake, ni ghari sana, sijui unazungumzia nini na unataka nini hasa hapo. Nenda sokoni zipo na bei yake sio ya kitoto, sasa endelea kuponda wenzako ndio kazi zao, wewe kama unaona sio passion zako pita hivi waache ambao wao wanaona ndio sehemu wanapatia riziki.

6.Mkojo wa Sungura ni mbolea kuna wanao zalisha kwa kiwango kikubwa na wanasindika kabisa kwenye galloni za lita 5 au 10. ni mbolea Oramganic hilo halina ubishi, sasa sijui unataka nini.

7.Kilimo cha nyoka kama zoo au? Pale Arusha kuna Snake Park wanafuga nyoka na wanaingiza Pesa, sijui unazungumzia ufugaji wa aina gani wa nyoka na kwa ajili gani.Ila wanafugwa na wanao fuga wanapata pesa ndio maana wanafuga.

8.Tikitiki ni kilimo kikubwa sana, ni matunda yanapatikana msimu mzima, ni moja ya matunda ambayo yanapatikana mwaka mzima, inamaana sokoni huyaoni au unaish Mars? Kuna wanao kata kata wanauza sh 500/ ili watu wamudu kununua kuliko kununua zima na wanauza sana.

9.Mende wanafugwa wanao fuga wana make pesa.

10. Dragon fruits ni matunda, ni food,unaweza kula kama chakula labda kwako chakula ni ugari na wali, Dragon fruit ni tunda na tunda maana yake ni chakula so linaliwa kama chakula, ni geni kama ilivyo kiwi au Blueberries, na matunda mengine, ambayo ni yana kuwa imported. so tunda kama Dragon linalimika Bongo so tunapata chakula. Kuna aina zingine za matunda kwa nature hazilimwi Bongo so zinaendelea kuagizwa kutoka Nje.
 
Back
Top Bottom