Kilimo cha Dragons na matunda mengine kama Kiwi

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
Watanzania ni bahati mbaya huwa tunapokea furusa mwishoni kabisa au hadi tuone kwenye TV au tutangaziwe na kiongozi.

Matunda kama Dragon fruits ni moja ya matunda ambayo ni commercial na pia nayaweka katika kundi la mimea yenye gharama ndogo sana za kuwekeza ukilinganisha na aina nyingine zote zote za miti.

Dragon inafanya vyema maeneo yenye jua jingi sana na mvua za wastani, maeneo kama kanda ya kati ni mazuri zaidi kwa Dragon, na pia maeneo kama kanda ya ziwa na pwani yote, ingawa pia bado maeneo yenye baridi inafanya vyema pia kama Arusha na au Iringa na Mbeya.

Dragon uoteshaji wake ni kwa kutumia vipando au cuttings ambapo ukitumia cuttings au kipando itakuchukua mwaka mmoja na nusu kuanza kula matunda. Ukitumia mbegu za ndani ya tunda ni miaka 6 hadi 7.

Na hizo vipando ndio utakavyo vitumia kupanua shamba lako huhitaji kununua mbegu wala vipando tena.

MATUNZO
Dragon inahitaji maji kidogo sana make adui wake mkuu ni maji mengi na hata ukiotesha vipando utamwagilia kwa wiki labda mara 1. Haitaki maji yanyo tuama hii ndio adui wake.

Dragon ni kama zabibu lazima uiwekee sapoti ya nguzo la sivyo itavunjika, nguzo za zege uu miti ilio wekewa dawa kama nguzo za Tanesco.

Haihitaji parizi, hailiwi na wanyama wala mifuho, kitu cha kufanya ni prooning tu.

MATUNDA
Tunda lake laweza kufikia kilo 1 na yapo ya nusu kilo na chini ya robo pia.

Tunda lake lazima liivie juu ya mti, haliwezi chumwa bichi na likaiva.

SOKO
Hadi sasa haya matunda unaweza yapata kwenye soko kama.kisutu kwa wazunhu na wahindi na pia Super Market kubwa pekeee Tanzania hii, na Mahoteli pia.

Zinatoka South Africa ingawa kwa sasa zimeanza kutoka Kenya pia kwa kiasi fulani.

Bei yake bado iko juu sana kuanzia Tsh 30,000\ hadi 10,000\ kulingana na size ya tunda. Ila hii sio ishu bali matunda yanapaswa kuwepo menhi na friend peice ambayo kila mtu atamudu.

Haya matunda ni matamu sana ukionjeshwa kesho utauatafuta shida bado ni Supply na wanayo yajua au kuyala ni watu wale wa Daraja la juu sana hawa wa daraja la chini ni kwa bahati sana ni kwa nadra mno.

ASILI YAKE
Ni mexco na kusambaa Asia sana na Marekani ya kusini na kati, na Africa, Ulaya hawalimi kwa sababu ya baridi ila ni walaji wakuu kutoka Asia.

Marekani pia ni kama majimbo 2 ndio yanalima kwa sababu ya Climate.

MATUMIZI YAKE
Juice, kukiwa freshi, Jam, wine, Ice cream na Lipstic pia.

Yanafaida nyingi sana mwilini na hii ndio sababu ya kuuzwa ghari.

NB: Kama una mashamba yako yamekaa unaweza lima uzuri hii unaaanza mdogo mdogo sana una enda una expand na gharama zake labda ni kwenye nguzo.

Nguzo imara ni muhimu kwa sababu linakaa miaka 40.

Kiwi kuna Red, Purple, white na yellow.

KIWI
Kiwi pia ni.moja wapo ya tunda la kigeni na ghari sana pia na pia linafanya vyema maeneo yenye jua la kutosha wakati wote.

Tofauti ya Dragon na kiwi iko kwenye matunzo Kiwi inahitaji matunzo kaisi.

Kiwi pia ni kama Zababu kwenye kulima na kutunza.

Kiwi pia lazima uoteshe Dume na Jike yaani kiwi ni mmoja ya plants ambazo zina Jike na Duke so lazima uoteshe both plants.

Dume mmoja anaweza chavusha majike 10.

Kiwi poa ina last kwa miaka zaidi ya 30.

Kiwi ni imported kutoka South Africa, Egypt na Nchi kama Italy.

Kiwi pia unaotesha kijijiti chake, ni kama zababu kuotesha.

FB_IMG_1692456169077.jpg

View attachment 2721742
 
Kwa kweli wenzetu wamechukua mbegu kutoka tropical countries kwa miaka mingi sana hata wanyama wetu na wadudu, ila sisi tumelala sana
Inabidi tunahakikisha tunarudi na mbegu kutoka nje au tunaagiza
Wao mpaka mende wanabeba
 
Aina ipi na matokeo gan hupati? Dragon kuna varieties zaidi ya 100
Ninayo za matunda ya red na white, infact mbegu za mwanzo kabisa nilichukua kwako na nyingine nilinunua kwa Anthony KINOTI kutoka kenya

matokeo ambayo siyapati ni matunda kipindi cha joto kali na jua siambulii kitu kipindi kingine napata matunda machace saana ....nafikiria niweke green house ila bado sija figure out
 
Jaman na mbegu za kiwi zinapatikana wapi. Halafu Kuna mtu aliniambia kiwi zinastawi mahala pa baridi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom