Biashara tatu za mtaji mdogo: Mayai, Miwa na Matunda

Biashara tatu za mtaji mdogo: Mayai, Miwa na Matunda

demarine

Member
Joined
Dec 6, 2020
Posts
18
Reaction score
29
1. MAYAI YA KUCHEMSHA
mchanganuo wake uko ivi - ukiwa na mtaji wa elfu kumi 10000/= unatosha kuanza biashara hii ambapo trey ya mayai moja inauzwa 7500/= mpaka 8000/= , pia waweza nunua trey zile za boksi ambayo moja ni 500 au kama wajiweza unaweza nunua ya plastic kwa 2000/= , pia utanunua na packet ya chumvi ndogo 400/=

LOCATION: biashara yoyote inategemea mzunguko wa watu akikisha unapata mazingira ambayo yanawatu wa kutosha mfano standi ya mabasi au daladala, masokoni na kwenye minada.

FAIDA: ukifanikiwa kuuza trey moja ya mayai utakua umeingiza 15,000/= KO ukitoa bei ya mayai apo utabaki na 7000/= faida. Ambao kwa mwezi ni sawa na 210000/=

Lakini pia unaweza kujiongeza kwa kutafuta madogo wawe wanakuuzia kwa trey unaweza walipa 2000 ww ukabaki na 5000 so ukiwa nao wa3 kwa mtaji wa 30000 means kwa siku unaweza tengeneza 15000/= ikiwa wote wakauza trey moja moja ambapo kwa mwezi ni sawa na 450,000/=.

2. BIASHARA YA MIWA
hii biashara inaitaji mtaji mdogo nauzuli ni kwamba unaweza fanyia kokote, ila maeneo mazuri ni barabarani ambapo watu wanapita kwa wingi

MAITAJI: ili ufanye hii biashara unaitajika kuwa na meza kwaajili ya kuwekea miwa yako, kisu cha kukatia miwa, vifungashio vinauzwa 2000/= ,pia uwe na kisado cha kukatia miwa na kiti au benchi la kukalia .

Kuhusu bei ya miwa inategemea na eneo lakini sehemu nyingi wanauza mua mmoja 300 ambapo ww waweza uuza kwa 500 so unaweza anza na miwa ya 10000 au kulingana na bajeti yako mwenyewe.

NB: Bei ya kuuza na kununua miwa inategemea mkoa so kabla ujataka kuuza fanya utafiti wa eneo ulilopo wanauzaje na wanapimaje ndo ufanye ila kwa mkoa kama morogoro kila mua mmoja unauzwa kwa 500 eiza umeumenya na kuufunga kwenye kipackti au bila kumenywa kwaiyo kwa kila mua unapata faida ya 200/=.

Lakini kwa watu wa dar hii biashar inalipa sana mana vipande vi5 unauziwa kwa 200 so katika mua mmoja unaweza toa vipande vingi mno na ukapiga pesa ya kutosha.

BIASHARA YA MATUNDA
Ili kufanya biashara hii unaitajika kuwa na meza,sahani,kisu,pia uwe na maji ya kuoshea matunda yako na benchi la kukalia, pamoja na matunda.

JINSI YA KUFANYA: nunua matunda yako mchanganyiko lakini sio lazima kila tunda liwepo ila matunda haya ndo muimu na sehemu nyingi ukipita unakuta matunda haya (embe-kama ni msimu wa maembe, papai, ndizi,tikiti, palachichi, nanasi-kama ni msimu wa nanasi, tango).

So unachotakiwa kufanya unaandaa sahani yako zen akikisha ayo matunda unakata kipande kimoja kisha unakatia katia kwenye sahani yako . au unaweza usikate mteja mwenyewe akaja kuchagua tunda analo taka unamkatia.

BEI : inategemea na eneo kuna wengine sahani wanauza 500 na wengine 1000 ila sehemu nyingi kwa dar sahani ni 1000. Pia waweza uza kwa kipande mfano palachichi kipande 200 ambapo kwa palachichi moja la mia 300 unaweza toa vipande vi 5 so ukapata faida ya 700, pia papai kipande 200 tikiti kipande mia kwa 500. Pia waweza uza tunda zima zima ingawa uwezi pata faida kubwa kama ukiuza kipande.

MDA WA BIASHARA : kuanzia mchana unaweza uza matunda yako lakini mda mzuri ni kuanzia jioni mda ambao watu wanaludi kutoka makazini.

NB: ni vema matunda ukafata mwenyewe sokoni uchukue kwa bei nafuu. Pia akikisha unapata sehemu ya barabarani ambapo kuna mzunguko mkubwa wa watu.

MWISHO
Karibuni kwa nyongeza na marekebisho.
 
Hivi wabongo faida huwa tunaicalculate vp?
Jamaa anaongelea faida ya mayai utadhani atauza bila kuyachemsha, hana habari na mkaa au gas, haongelei habari ya nauli au mengine kama kula. Faida (ghafi) kaitengeneza ya siku 30 isiyo na matumizi.
 
Mtaji ni Pesa, na Nguvu kazi pia ni Mtaji... Kwahio unapoongelea udogo ongelea pia ni manpower kiasi gani unaweka..., Unaweza kulima hekari moja bila kuweka hata shilingi, ila uka-burn calories za kufa mtu kwa kutumia jembe la mkono au hata ukitumia pilau ukatumia nguvu kumlisha huo ng'ombe

Pili, biashara yoyote ambayo ina mtaji mdogo, barrier of entry ni ndogo..., unasema utafute madogo wakuuzie trays, ndio watauza ila sababu wenyewe ndio wanakutaka na wateja ana kwa ana ni rahisi sana wakaona unawazingua wakaamua kukupindua na kufanya kile unachowatuma wakifanye ila kwa faida yao (be their own boss).

In short Kinachokunufaisha wewe huenda kisimnufaisha huyu au yule..., sio kwamba hakifai..., its just the way it is.....
 
Mtaji ni Pesa, na Nguvu kazi pia ni Mtaji... Kwahio unapoongelea udogo ongelea pia ni manpower kiasi gani unaweka..., Unaweza kulima hekari moja bila kuweka hata shilingi, ila uka-burn calories za kufa mtu kwa kutumia jembe la mkono au hata ukitumia pilau ukatumia nguvu kumlisha huo ng'ombe

Pili, biashara yoyote ambayo ina mtaji mdogo, barrier of entry ni ndogo..., unasema utafute madogo wakuuzie trays, ndio watauza ila sababu wenyewe ndio wanakutaka na wateja ana kwa ana ni rahisi sana wakaona unawazingua wakaamua kukupindua na kufanya kile unachowatuma wakifanye ila kwa faida yao (be their own boss).

In short Kinachokunufaisha wewe huenda kisimnufaisha huyu au yule..., sio kwamba hakifai..., its just the way it is.....
Hao madogo wa kuwalipa elf2 kwa siku labda wawe watoto wake
 
Back
Top Bottom