Dr. Wilibrod P. Slaa: Special Thread

Dr. Wilibrod P. Slaa: Special Thread

Ana wakati mgumu,sio Rahisi kihivyo,tusubiri atakaeteuliwa na CCM,Kama ni Membe,kazi ni nyepesi,kama magufuli,kazi ni pevu.
 
Habari Wakuu.Ninaleta kwenu Dr.W.P Slaa The Special Thread.Uzi huu una malengo makubwa mawili
  1. Kumshawishi Dr.Slaa aone umuhimu wa kuomba ridhaa ya kugombea urais kupitia UKAWA.Na vilevile kuwashawishi UKAWA waone busara ya kumptisha Dr.Slaa kupeperusha bendera ya UKAWA.
  2. Kuweka pamoja katika JF harakati za Dr.Slaa(kama atapitishwa) kuanzia kuchukua fomu,harakati zote za kipindi cha kampeni mpaka kusimikwa na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
View attachment 258204View attachment 258206
Dr.W.P Slaa

View attachment 258227
Mama Maria Nyerere akimsihi jambo Dr.Slaa
Mambo 10 Kuhusu Dr.Wilbroad Slaa
1. Anachokisimamia

Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, umakini na uwajubikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.
Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

3. Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.


4. Mafanikio ya Dk . Slaa kikazi na kitaalamu

Dk. Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:
Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Wasioona Tanzania, 1992 – 1998
Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985 – 1991
Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 19977 – 1979 na 1982 – 1985
Padri wa Kanisa Katoliki kuanzia 1977 hadi 1991

5. Vitabu alivyoandika

Utimilifu wa Msichana (1977) na Utimilifu wa Mvulana (1977)
Expediency and Exigency Liturgical Legislation (1981)

6. Ufasaha katika lugha nane (8)

Dk. Slaa anajua kuzungumza na kuandika lugha nane za kimataifa zifuatazo:
Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

7. Uzoefu wa Dk. Slaa Kisiasa

Dk. Slaa ana uzoefu wa musa mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni hizi zifuatazo.

Mbunge wa karatu kwa miaka 15 kutoka 1995 hadi 2010

Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa
Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998 – 2002

Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

8. Uzoefu wa Dk. Slaa KItaifa na Kimataifa

Dk. Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo.

Mjumbe w akuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika,Carribean na Pcific-FU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996 – 2000.

Mjumbe kamati ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)

Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998 hadi 2010

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la SADC(Inter Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010.

Nibu kiongozi wa kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010

Mwenyekiti Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Bunge la Tanzania 2008-2010

9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji

Dk. Slaa amekuwa mbunge wa karatu kwa miaka 15 mfululizo.
Karatu ni moja ya wilaya hapa nchini zenye maafanikio makubwa ikiwamo miundo mbinu bora, maji na huduma nyingine za kijamii, Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka 15 ya ubunge wa Karatu na uongozi madhubuti wa ukatibu mkuu CHADEMA, kwa ajili ya taifa zima.

Ndiye katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA kwa kushirikiana na viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.

Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kafsha za ufisadi mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini kutoroka nchini.

10.Zaidi ya yote Dr.Slaa anajua maisha ya watanzania wa kawaida na mateso yao ya kila siku


Kuhusu List of Shame


Karibuni



Tanzania haiongozwi na Shahada za DINI.
 
Ana wakati mgumu,sio Rahisi kihivyo,tusubiri atakaeteuliwa na CCM,Kama ni Membe,kazi ni nyepesi,kama magufuli,kazi ni pevu.

..hata Magufuli ni mwepesi kutokana na kashfa inayomkabili ya kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa.

..pia ana kashfa nyingine ya kukaidi ushauri wa wanasheria na kuamuru kuvunjwa kwa kituo cha mafuta mwanza. Kesi ilipopelekwa mahakamani ikaamuliwa serikali ilipe sh. Billion 14.

..tatizo lake lingine ni mropokaji. Kwa mfano aliwahi kwenda Kenya na kumpigia kampeni Raila Odinga. Magufuli alidai angekuwa na uwezo angemuachia Raila aongoze jimbo la Chato!!
 
Sipati picha siku J.M. Kikwewe anatoka kwenye kiti na kukaa .Dr. W. P. Slaa
 
[h=3][/h]



Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa wa twitter wa Dr Slaa kathibitisha kuteuliwa na UKAWA.
CREDIT:MILLARDAYO
habari njema kwa watanzania
 
Last edited by a moderator:
Mambo gani yameiva mkuu; fafanua.
niliogopa ku-pre empty hii kitu
[h=3][/h]



Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa wa twitter wa Dr Slaa kathibitisha kuteuliwa na UKAWA.
CREDIT:MILLARDAYO
 
Last edited by a moderator:
Mbona CV imeacha mambo kadhaa tuanyoyajua

1. Alifukuzwa seminari

2. Aliingilia ndoa ya mtu, na huyo mke wake alitelekeza watoto wake mwenyewe akahamia kwa huyu mzee. Kesi ilikuwa ifunguliwe mahakamani ikazimwa kwa mazingira ya kumalizana wao kimya kimya?
 
Dr Slaa ndiye rais wetu ajaye.Nimefurahi sana mnara wa babeli kuanguka
 
Maesabu ya UKAWA yameenda vizuri sana kwani imewaondolea uwezekano wa watu wa LUMUMBA kuwapenyezea virusi wakati wa mchakato wa kutafuta Mwali wao, kweli walikua makuni.
 
Mmmmmmmmmmm CCM wamecheza karata dume kumuweka Magufuli pale. Ni vigumu kwa upinzani kutwaa uraisi.
 
Hata wapinzani watampa Magufuli uraisi jamani si kwelieeee
 
Wapinzani tupooooooo. CCM wameshamaliza game. Jamani wametuuuwa Ila kwa kuwa Tanzania ni moja basi si shida kama tukapata magufuli
 
Ccm imeshapasuka hata kama wamefany reconciliation na kumuangusha Membe ili Lowassa apate ahueni ukawa pigeni haya magamba
 
Frankly speaking 2015, UKAWA watapita kwa asilimia 71 urais, asilimia 68 ubunge na udiwani.
 
Back
Top Bottom