Dr. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Sam GM, Oct 6, 2008.

 1. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jf imekuwa ni mahali pa kupashana habari na kuweza pia kuzungumzia mambo ya historia yetu na mwelekeo wa nchi. Kuna Huyu bwana anajulikana kama marehemu Dr Kleruu, mie nimekuwa nikimsikia katika wimbo wa Mbaraka Mwinshehe kuwa alikuwa mwanamapinduzi, Je kuna yeyote anaweza kutupatia taarifa kumhususu huyu Dr Kleruu alikuwa nani hasa na uana mapainduzi wake ulikuwa vipi katika historia na siasa za Tanzania?


  [​IMG]

  Mnara wa kumbukumbu kifo cha Dr. Kleruu kijijini Isimani


  [​IMG]

  Mtoto wa Said Mwamwindi
  === Historia ya Dr. Kleruu kwa ufupi ===​

  -----------------------------


  Habari nyingine inayohusiana na habari hii fuatilia - Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni
   
 2. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Kaka gm,Naona ingekuwa busara kama post hii ungeulizia kule kwenye Thread ya Field Marshall ES inayohusu Historia,kuna Waheshimiwa kule wana kumbukumbu nzuri wangekupa mengi kuhusu huyu Mzee Kreluu.Lakini kwa kifupi tu,na kwa ufahamu wangu,nitakupa maelezo yafuatayo kuhusu Mzee Kreluu.

  Dr Kleruu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Aliuawa siku ya Krismas mwaka 1971.Kifo chake kilizungukwa na utata mkubwa,na kilimtia simanzi nyingi Marehemu Julius Kambarage Nyerere ( Rais wa Jamhuri) ambaye pamoja na Mzee Kawawa (Waziri Mkuu),Dr Kleruu alikuwa rafiki yao mkubwa. Msiba wa Dr Kleruu uliisikitisha Nchi nzima...kwa sababu alikufa kwa kupigwa risasi na mtu maarufu huko Iringa aliyejulikana kwa jina la Alhaj Abdallah Mwamwindi.

  Kisa cha mauaji ya Dr Kleruu hakipo wazi;Serikali ilitoa tamko kuwa Alhaji Mwamwindi alikataa Amri ya serikali ya kuhamia kwenye vijiji vya Ujamaa kwa madai kuwa eneo alilokuwa anaishi lina makaburi na shamba alilorithi,na kwa mila ya huko (Iringa) huwezi kuishi mbali na makaburi ya ndugu zako.Serikali kwa kutumia vyombo vya dola (Polisi) wakatumia nguvu kumuhamisha Alhaji Mwamwindi,hiyo ilimchukiza Mwamwindi na kuishia kumpiga risasi Mkuu wa Mkoa......maelezo hayako wazi kama Dr Kleruu alikuwepo kwenye tukio siku ya Kumuhamisha Mwamwindi na ukizingatia kuwa mauaji yalitokea siku ya Krismas (siku ya mapumziko).

  Kuna Taarifa nyingine ambayo ilikuwa inasema kuwa,kulikuwa kuna chuki,kati ya Mfanyabiashara Mwamwindi na Mkuu wa Mkoa Dr Kleruu,na Mkuu wa Mkoa akaichukulia Amri ya serikali ili kumkomoa Mwamwindi. Mfanyabiashara huyo akamvizia Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa anatoka na mkewe mdogo...alimpiga risasi na kuipeleka maiti ya Mkuu wa Mkoa kituo cha Polisi Iringa mjini.....na kwa dharau akawaambia Polisi "kamchukueni mbwa wenu kwenye buti la gari yangu"......baada ya kuichukua hiyo maiti ya Mkuu wao wa kazi Polisi walimtia kizuizini Alhaj Mwamwindi,alihukumiwa kifo na alinyongwa.

  Kwa mtazamo wangu sikuuona uwanamapinduzi wa Dr Kleruu,labda ni usimamizi imara wa Azimio la Vijiji vya ujamaa.Mkuu gm hiyo ndio historia fupi ya Marehemu Dr Kleruu....ni wazi utapata maelezo zaidi kwa wanaolifahamu hilo.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Oct 6, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Alikuwa daktari wa nini huyu Kleruu? Alikuwa kabila gani?
   
 4. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Dr Wilbert Kleruu alikuwa mzaliwa wa mkoa wa Kilimanjaro sehemu iitwayo Mamba (au Mwika), Moshi vijijini ambako siku hizi kunaitwa Vunjo. Alisomea uchumi wa kijamaa hadi ngazi ya PhD, na hasa alikuwa agricultural economist.

  Alifanya kazi kwa karibu sana na Mwl Nyerere ambaye alimpenda sana, maana alimwona ni muumini wa siasa yake ya ujamaa na kujitegemea. Alijituma na kuiamini kwa moyo wake itikadi hiyo, kwamba ukombozi wa nchi utapatikana kwa mapinduzi ya kilimo cha kijamaa (ndio uanamapinduzi anaozungumziwa).

  Alijitahidi pia kutekeleza itikadi hiyo kwa vitendo, na ndiyo iliyomgharimu maisha yake mwaka 1971 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Iringa. Siku moja ya jumapili (hakuwa na jumapili huyu mjamaa) alikwenda kwenye shamba la mkulima mmoja aliyeitwa Saidi Mwamwindi, ambaye alikuwa na shamba kubwa sana, kwa lengo la kufuatilia maagizo yake aliyokuwa ametoa kuhusu shamba hilo, ndipo alipokorofishana na mkulima huyo maana yeye hakuzikubali hata kidogo hizo sera za kijamaa. Mwamwindi alikwenda nyumbani kwake akachukua gobore lake, akamfuata Dr Kleruu alipokuwa akampiga risasi na kumwua, kisha akapakia mwili wake kwenye Land Rover yake (pick up short chassis) na kupeleka kwenye kituo cha polisi ambako pia alijisalimisha.

  Nyerere alihuzunishwa sana na kifo hicho, na hata kesi ya Saidi Mwamwindi ilipoisha na kupewa hukumu ya kifo, Nyerere hakusita kusaini, na ni mojawapo ya hukumu tatu tu za kifo zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Mwl Nyerere.

  Wengine wataongezea, lakini kama hapo ulipo unaweza kupata vitabu, tafuta kitabu kiitwacho "The Egalitarian Moment: Asia and Africa 1950-1980" kilichoandikwa na Donald Anthony Low (1995), habari hii ya Dr Kleruu iko kwenye ukurasa wa 52-53, kwenye chapter yenye heading "Richer Peasants and the State".

  Unaweza pia kusoma journal article iliyoandikwa na Phillip Raikes mwaka 1979: Agrarian Crisis and Economical Liberalisation in Tanzania kwenye jarida la Journal of Modern African Studies Vol 17(no.2) pg 309-316, ambayo nimejaribu kukuwekea link yake hapa chini. Kifo cha Dr Kleruu kiliwahuzunisha watu wengi hasa wakulima wadogowadogo wa huko Iringa ambao walikuwa wakifurahia alivyokuwa ananyang'anya mashamba kwa wakulima wakubwa ili yalimwe kijamaa. Pia alikuwa ana tabia ya kuwafokea watumishi wa serikali hata wakurugenzi kwenye mikutano ya hadhara, pale alipoona sera zake za kijamaa hazijafuatwa kama alivyotaka, yaani alikuwa na ule ujamaa wa kibabe hasa uliokuwa Urusi (ajabu ni kwamba huyu alisomea Marekani!). Kwa namna fulani (ama kiasi kikubwa) alikuwa na 'ukali' kama ule wa Marehemu Sokoine. Raikes (1979) anaandika hivi kuhusu kifo cha Dr Kleruu kwenye rejea niliyotaja:

  "...the emergence of the assassin of the Regional Commissioner as a 'folk hero', seems to me a misreading. Dr Wilbert Kleruu had achieved a certain local popularity largely because of his habit of abusing civil servants in public. His expro- priation of the 'rich' peasants also seems to have been quite popular, especially of course with those who received the land. As for the various stories which went the rounds in the aftermath of the murder, I can only go by second hand gossip...." (uk 315).
  Anaendelea:

  "The point stressed was that Mwinyi killed Kleruu for calling him a dog (said to be an unallowable insult among the Hehe) in front of his wife (which made it the more unforgivable). In short, it was seen by Mwinyi as a means to preserve his honour, and this would help to explain why he gave himself up immediately" (uk 316). Mwamwindi alijulikana pia kama "Mwinyi" kwa maana ya "Lord"
   
 5. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kuna siku nilisafiri na mmoja wa wakwe wa huyu Alhaj Abdallah Mwamwindi, hadithi aliyonipa ni kwamba Dr Kleruu siku hiyo ya Christmas alienda shambani kwa Mwamwindi na siku hiyo Mwamwindi alikuwa akilima. Alifika akapaki gari lake uwanjani katika nyumba ya Mwamwindi akamuita Mwamwindi ambaye alikuwa shambani mbali kidogo na pale alipopaki gari. Mwamwindi alipofika mkuu wa mkoa akamuuliza kwanini hataki kuahama na kwanini alikuwa analima siku kuu. Mkuu wa Mkoa alipiga kofi Mwamwindi mbele ya wake zake. Mwamwindi akasema unanipiga kofi mbele ya wake zangu. Akaingia ndani akachukua shortgun na kumpiga mkono wa kulia. Mkuu wa Mkoa akasema nimalize kwa sababu umenikata mkono sina sababu ya kuishi. Ndipo Mwamwindia akammalizia akapakia kwenye buti ya gari na kupeleka polisi. Alipofika pale Polisi walijua ni Mkuu wa Mkoa wakajipanga na kupiga salute kisha Mwamwindi akateremka katika gari ile na kuwaendea pilosi akawaambia kachukueni nguruwe wenu kwenye gari.
   
 6. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Jina lake sio Abdallah, ni Saidi. Mwaka 2004 nilikwenda Iringa kwa shughuli zangu na nilibahatika kukutana na meya wa manispaa wakati ule, Amani Saidi Mwamwindi ambaye ni mtoto wa huyo mzee. Sijawahi kumhoji huyo mstahiki meya kuhusu baba yake, lakini kama ulivyoona kwenye article niliyotoa kwenye post yangu hapo juu, yalisemwa mengi sana kuhusu mazingira ya kifo cha Dr Kleruu. Hata hivyo Mwamwindi alijisalimisha polisi na alimwaga ukweli wote mahakamani wakati wa kesi yake, na utetezi wake mkubwa ulikuwa kwamba alipatwa na hasira kali akashindwa kujizuia. Lakini ukisoma kesi yake kama ilivyoripotiwa kwenye Law Reports, Jaji alikataa kigezo cha hasira kwa maelezo kuwa mshitakiwa alipata nafasi ya kwenda nyumbani kuchukua gobole, na kurudi kumuua marehemu, kwa hiyo malicious intent ilikuwako na si hasira peke yake (najua kuna wanasheria humu wanaweza kutuongezea).
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Unajua si wakati wote ushahidi wa daktari unachukuliwa uzito, inategemea anavyoutetea mahakamani. Katika ile kesi maarufu ya fundi cherehani Ali Maumba aliyelawiti watoto wengi Dar miaka ya 1986-7(nadhani, sikumbuki mwaka kwa usahihi), watoto wale waliolawitiwa walipelekwa hospitali ya Muhimbili kupimwa, na daktari alithibitisha kuwa walilawitiwa, lakini ushahidi wake mahakamani ulitupiliwa mbali wakati wa rufaa, alishindwa kuutetea ule ushahidi ukaonekana hauna uzito. Ninavyofahamu ushahidi wa kutokuwa na akili timamu unaweza kumfaa mtu iwapo itathibitishwa kuwa wakati wa tendo husika hakuwa na akili timamu. Hilo sidhani kama Dr Pendaeli aliweza kulithibitisha na kulitetea mahakamani, pengine mawakili wa Jamhuri walimshinda kwa hoja.
  BTW wakati baba yangu akifanya kazi Mamlaka ya Kahawa kule Moshi mid 70's to mid 80's (sisi pia tuliishi Moshi wakati huo), huyu Dr W.S. Pendaeli alikuwa na kliniki yake kwenye ground floor ya jengo la KNCU (ile yenye KNCU hotel), ilikuwa ya private na general (sio psychiatry), ingawa mwenyewe alikuwa psychiatrist. Ndipo tulipokuwa tunaenda kutibiwa (kukwepa foleni Mawenzi maana kule dawa zilikuwa za bure, lakini foleni yake ndio ilikuwa balaa!). Basi ilikuwa babu ukimkuta na akijua unasoma sekondari basi anakusemesha kiingereza. Natamani kujua aliko huyu mzee, alini-influence sana na kile kiingereza chake miaka ile.
   
 8. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwawando,

  Shukrani sana kwa maelezo na historia ya Dr Kleruu, at least umetoa mwanga hasa wa huyu Dr. kwa watu ambao hatukuwa tunamfahamu kabisa.

  Thanks
   
 9. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kithuku,

  Maelezo mazuri sana na nashukuru pia kwa PDF na maelezo mengine ambayo yanatoka katika journal. Thanks
   
 10. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nyani McCain,

  Sina uhakika alikuwa kabila gani lakini kwa maelezo ya Kithuku ni kuwa alikuwa mzaliwa wa Kilimanjaro na alikuwa daktari wa uchumi.

   
 11. K

  Kinyikani Member

  #11
  Oct 6, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Alhaji Mwamwindi huyu ndio shujaa wa kweli hakukubali siasa mbovu za Nyerere za kunyanganya watu mali zao. Mungu amlaze pahali mema Shujaa wa Tanganyika Alhaji Mwamwindi
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,622
  Trophy Points: 280
  Marehemu Dr. Kleruu ameacha mtoto mmoja wa kiume anaitwa Edwin Kleruu. Mara ya mwisho alisoma Ilboru High School 'HGL' mwenye taarifa za alipo sasa naomba anisaidie.
   
 13. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  kleruu alikuwa pia na binti tulikaa naye mitaa ya daimond jubilee,upanga nakumbuka tulikuwa tunamwita mama twambi,unfortunately binti wa huyu mama,TWAMBI,perished in the fire iliyotokea katika boarding school kilimanjaro some years ago
   
 14. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #14
  Oct 6, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Taarifa zingine zinasema kuwa Kleruu alimkuta Mwamwindi akilima shamba lake na Trekta lake Isimani siku ya 25/12/1971.Alipomkuta akamuuliza kwa nini analima kwenye shamba lake na siyo kwenye shamba la kijiji cha ujamaa?

  Mwamwindi akajibu kuwa kuna tatizo gani kwani siku hiyo ilikuwa ni sikukuu hivyo hakuwa na sababu ya kuwa kwenye shamba la kijiji cha ujamaa kulima kwani watu walikuwa nyumbani wakisherehekea sikukuu.

  Taarifa zinasema kuwa Mkuu wa mkoa akakasirika akamtukana Mwamwindi akamwambia “KUMAMAYO”.Alipotukanwa tusi hilo Mwamwindi akaja juu akamwambia utanitukanaje KUMAMAYO wakati mama yangu alishakufa siku nyingi na kaburi lake lile pale ? Akalionyesha kwa Mkuu wa Mkoa.

  Mkuu wa mkoa Kleruu akazidi kukasirika akasema kaburi ndio nini? akaenda juu ya kaburi na kuanza kupiga mateke lile kaburi.(Hakujua kuwa wahehe kimila huwezi kumtukania mzazi aliyekufa na huwezi chezea kaburi la marehemu sababu makaburi kwa wahehe ni maeneo matakatifu na huyajengea na kuyaenzi na kuyatumia kwa ibada za matambiko.)

  Baada ya Kleruu kupiga mateke kaburi alimwona Mwamwindi anakimbia mbio kwenda nyumbani kwake.Kleruu alipoona anakimbia akaanza kumfukuza nyuma akijua anamkimbia. Hakujua mila za wahehe wenye hasira kuwa ukigombana naye hutakiwi umfukuze ila ukimbie haraka sababu huko aendako anaenda kuita watu wakutandike au anaenda kufuata silaha au anaenda kujinyonga kwa hasira.

  Kleruu akawa anamfukuza kuelekea nyumbani kwa Mwamwindi .Mheshimiwa Kleruu hakujua mila ingine ya wahehe isemayo kuwa mhehe huwa “hapigwi nyumbani kwake na yuko tayari kujiua au kuua mtu kuliko kupigwa nyumbani mbele ya mke,watoto au dada zake”.Kitendo cha Kleruu kumfuata mhehe yule akampige nyumbani kilikuwa hatarishi kwa Kleruu.

  Basi alipofika nyumbani Mwamwindi akaingia ndani akachukua bunduki akawa anatoka nayo mbio akamtandika Risasi Kleruu aliyekuwa anakuja nyumbani kwa Mwamwindi kisha akapakia maiti kwenye gari ya mkuu wa mkoa na kuipeleka Iringa mjini kituo cha polisi ambako hata polisi walishikwa butwaa maana hawakujua ilikuwaje mkuu wa mkoa atoke peke yake kiziara ya kikazi bila wao kutaarifiwa hadi auawe huko.Ilikuwa kizaazaa.Hawakujua maskini polisi,usalama wa taifa n.k watajieleza nini kwa Raisi Julius Nyerere.

  Kwa wahehe Mwamwindi anaheshimika kama shujaa na mtetezi wa makaburi na marehemu wa wahehe ndiyo maana alikuwa na ujasiri wa ajabu hata kujipeleka mwenyewe polisi akijua kuwa kitendo chake kimila kilikuwa sahihi kabisa.Pia ukichukulia kuwa siku hiyo ilikuwa sikukuu ambayo Kleruu kama mchaga alitakiwa awe Moshi akila Krismasi na wachaga wenzie badala ya kwenda kuchokoza wahehe vijijini ambao hawana cha kula Krismasi.

  Wahehe hawana kinyongo na familia yake ndiyo maana waliweza kumchagua hata mwanae kuwa meya wa manispaa ya Iringa na wanaona fahari kuwa na meya mtoto wa mwamwindi.

  Kleruu kama Mkuu wa Mkoa alienda na gari ya serikali akijiendesha mwenyewe na hakuwa na mlinzi kitu ambacho pia hakikuwa sahihi katika matumizi ya mali za umma.Na ki-protokali ziara za mkuu wa mkoa ilibidi serikali ya tarafa,kata na kijiji wataarifiwe ujio wake lakini hawakutaarifiwa.Aliingia tu yeye kama yeye! Ndio maana hata Mwamwindi alimwona kama mhuni aliyekuja kumfuata kwa visa vyake anavyojua yeye.

  Pia ingalikuwa ni ziara ya kiserikali huko kijijini angeambatana na viongozi wa wilaya polisi,n.k Hakufanya hivyo. Ningekuwa jaji nadhani nisingemnyonga Mwamwindi hadi nipate majibu ya kueleweka.

  Kesi ya Mwamwindi ni moja ya kesi ambazo wanasheria wanapaswa kuzipitia upya hukumu zake kuona kama alitendewa haki kunyongwa na pia ni fundisho kwa wataalamu wa saikolojia za kisheria na kivita na uendeshaji wa utawala bora.
   
 15. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Du inaonekana hii issue inachanganya kidogo, kwa mtizamo wa haraka haraka unaweza kusema kuwa Mwamwindi ndiye alikuwa mwana mapinduzi hapa lakini ukiangalia pia issue ya mada sina uhakika wana sheria watasemaje, ni dhahiri kuwa hata kama angekuwa ameuwa kwa kutokukusudia mwelekeo wa siasa wa kipindi hicho kwa vyevyote ungemhukumu tu kwa kumuondoa mkuu wa Mkoa ( I am only speculating though). Pia ukifuatilia hizi post za wana JF waliochangia na kutoa maelezo ya huyu Dr Kleruu, kwa upande mwingine inaonekana kama hasa alikuwa mkereketwa wa ujamaa au alikuwa anatumia madaraka yake vibaya. Nafikiri angeweza kuwa na compromising solution ya kudeal na watu ambao walikuwa na mashamba makubwa zaidi ya hivo alivofanya kama maelezo ya Kithuku yanavyosema hapa:

   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Dr kleruu alikuwa mzaliwa wa mamba, na kaburi lake liko kando ya barabara inayoanzia himo-kilacha hadi mwika, niliona valuation report kwa ajili ya compensation ya watu wanaoathiriwa na ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami,kwenye jalada kabisa wameweka kaburi lake, kwani nalo linapaswa kuhamishwa, hivyo ni mchaga wa marangu
   
 17. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Netanyahu,

  Shukrani kwa maelezo yako!

  Je waweza fafanua kidogo unamaana gani unaposema "Mwamwindi anaheshimika kama shujaa na mtetezi wa makaburi na marehemu wa wahehe" Natanguliza shukrani.
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Oct 6, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  ..silaha inabidi zitumike kwa ajili ya kujihami tu.

  ..naamini siyo watoto wa Dr.Kleruu peke yao walioathirika[kisaikolojia,kiuchumi,..] kutokana na kifo cha mzee wao.

  ..watoto wa Alhaji Mwawindi nao lazima waliishi kwa taabu kutokana na matendo ya mzee wao.

  ..kwa wale ambao tuna familia, kabla ya kuchukua uamuzi wowote mkubwa, hujiuliza uamuzi huo utakuwa na athari gani kwa wanetu.
   
 19. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Hivi nani anaweza kutoa maelezo sahihi "Ni kwa nini Mwalimu alitia saini kifo cha Mwamwindi, wakati ripoti ya Madaktari wakiongozwa na Dr.Pendaeli waliithibitishia Mahakama kwamba Mtuhumiwa alikuwa na Ugonjwa wa Akili?".

  Alhaj Mwamwindi aliua Desemba/1971 na mapema June/1972 kesi ilikuwa imekwishamalizika...Ni vipi kesi hii ya mauaji iliyohitaji uchunguzi wa muda mrefu iliendeshwa kihara haraka namna hiyo?Ni kweli kwamba Mwalimu alitia saini adhabu ya kifo kwa sababu tu kifo kilimuhusu rafiki yake?Mbona alikawia na hatimaye kumuacha huru Mama Liundi ambaye aliuawa watoto wake wawili kwa kuwatilia sumu kwenye chakula?(wakati hukumu ya mahakama ilikuwa ni adhabu ya kifo?)..

  Kama mtakumbuka Mwalimu alikataa kuonana na watu kutoka England ambao walifuatilia kesi ya Mwamwindi....Mwl aliwaambia anafikiri waondoke tu...kwa sababu walikuja mwezi April/1972 siku ambayo karume nae alipigwa risasi Zanzibar....mara baada ya mazishi ya Karume Mwalimu alirudi Butiama kwa siku 7 na kusema wazi kwa kiingereza kwamba inabidi afanye "re-evaluation ya behaviour yake".Ni kwa nini alisema maneno hayo? unafikiri hiyo iliharakisha kusaini kifo cha Mwamwindi? au aliona yaliyomtokea Karume yanaweza kutokea kwake pia?Wakulu mnaolifahamu hili tunaliombea maelezo...
   
 20. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nadhani katika kusaini hukumu ile Mwl Nyerere alikuwa katika capacities mbili: Ya kwanza kama Rais wa nchi ambaye sheria inasema ndiye atakayeridhia utekelezwaji wa hukumu ya kifo inapotamkwa na mahakama, lakini ya pili ni capacity ya kibinadamu ya kutaka kumlipia rafikiye kisasi, ambayo hii inaelekea ilimzidi. Imagine katika miaka 23 ya uongozi wake, ni watu wengi sana walihukumiwa adhabu za kifo, lakini aliridhia 3 tu, mojawapo ikiwa hii ya Mwamwindi. Labda zingeletwa na hizo hukumu nyingine alizosamehe tukaona hazikumgusa binafsi naweza kufuta maneno yangu, lakini nahisi kutekelezwa kwa hukumu hii haraka haraka kulichangiwa pia na ukweli kwamba kosa lililotendwa lilimuumiza Nyerere binafsi. Hivi kwa mfano ukipigana na mtu mtaani ukamuumiza halafu ukakamatwa ukashitakiwa mahakamani, na huko ukakuta hakimu ni baba mzazi wa mlalamikaji, unatarajia nini? Sisemi ilikuwa sawa Nyerere kuendeshwa na hisia binafsi, lakini tunapaswa kuangalia pia namna ya kudhibiti hali kama hii. Katika mahakama zetu kuna utaratibu (sijui kama umeandikwa au la) kuwa hakimu akiona kesi husika ana maslahi nayo, huwa anajitoa na kuomba ipangiwe hakimu mwingine. Kwa rais wa nchi hali ikoje? Hivi mtu akihukumiwa kunyongwa kutokana na kutenda jambo ambalo liligusa maslahi binafsi ya rais (rafiki yake, familia yake nk), rais anaweza kusema kuwa 'anajitoa' katika suala la kuridhia utekelezwaji wa hukumu hiyo?
   
Loading...