Dr. Vincent Mashinji amesema muda huu mawakala wao wamepewa viapo, tayari kusimamia na kuhakikisha upigaji kura .

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Malisa GJ

Nimeandika na kufuta zaidi ya mara 10. Moyo wangu una huzuni kubwa. Kwanini tutendewe hivi? Ni madaraka tu haya ya kupita?

Hadi leo mawakala wetu walikua hawajapewa viapo, that means kesho wasingeweza kuwepo vituoni, kusimamia kura. Ikumbukwe Kiapo kwa mawakala sio ombi ni haki yao. Lakini Mkurugenzi wa Kinondoni alikatalia viapo vyao. Jana viongozi wa chama walienda Tume ya uchaguzi kujua hatma ya viapo kwa mawakala wetu. Tume nao hawakutoa majibu ya kuridhisha.

Leo imebidi viongozi waambatane na mawakala kwenda kwa Mkurugenzi kudai viapo vyao. Maana bila viapo hivyo kesho kusingekuwa hata na wakala mmoja ambaye angeruhusiwa kituoni. Kwahiyo ilibidi kwenda kufuata viapo vyao leo.

Kumbuka ni muda mrefu sasa Mkurugenzi anazungusha kuwapa viapo mawakala wa CHADEMA lakini mawakala wa CCM wote walishapewa viapo vyao. Hii ni double standard ya kipumbavu mno kutokea. Hakuna kiongozi yeyote aliyejitokeza kukemea uonevu huu. Hata yule ajiitaye "mcha Mungu"

Chadema wametumia njia zote za kidiplomasia kudai haki yao ya kupewa viapo kwa mawakala bila mafanikio. So ilibidi leo kwenda ofisi ya mkurugenzi kudai haki yao wakiongozwa na viongozi wakuu wa chama.

Lakini Polisi wamewapiga risasi mawakala wetu waliokua wanaenda ofisi ya mkurugenzi kudai haki yao ya viapo. Polisi wanatumia silaha za moto kwa watu wasio hata na fimbo mkononi. Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Segerea Gango Kidera ameponea chupuchupu kupigwa risasi na Polisi. Hata hivyo wafuasi kadhaa wa Chadema wamewapiga risasi na baadhi wamelazwa Hospitali ya Mwananyamala (mmoja amekimbizwa Muhimbili usiku huu, hali yake ni mbaya). Kidera ndiye anayeongoza zoezi za kuhakikisha wanapatiwa huduma.

Kidera anaeleza kuwa, polisi wamemuua mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDSM Aqulina Akwilini Baftaha ambaye amepigwa risasi akiwa kwenye daladala. Huyu hakuwa hata mfuasi wa Chadema maskini. Ni abiria tu aliyekua kwenye daladala lakini risasi imemfuata hukohuko, ikampiga kichwani na kufa.

Mbunge wa Tarime vijijini John Heche amekamatwa pamoja na wanachama kadhaa. Hali hii haikubaliki. Uonevu huu hata lini?

Je tumeamua kutafuta madaraka kwa kuua watu? Tumeamua kutafuta madaraka kwa kumwaga damu za watanzania wanyonge tunaojinasibu kila siku kwamba tupo kwa ajili yao? Huyu binti wa UDSM aliyeuawa ana wazazi, ana ndugu zake, ana familia. Hivi wamepokeaje taarifa hizi? Kwamba polisi wamemuua kwa risasi mtoto wao akiwa kwenye daladala. So painful. Hivi CCM wanadhani wao peke yao ndio watu, wengine sio watu? Wanaweza kutuua, kutujeruhi, kutupiga risasi, na kututeka kadri wawezavyo. Is that the case?

Baada ya polisi kuua na kujeruhi ndio mkurugenzi katoa viapo usiku huu. Just imagine. Kwanini hakutoa mapema kuepusha yote haya? Kwanini they normally react instead of being proactive? Hadi muue ndo mtoe viapo? Kwanini? Na sisi ni binadamu kama nyie. Tuna haki ya kuishi kama nyie. Plz treat us like human beings.

Kule Mbweni Bashe alisema Chadema ikiwagusa WANAUA. Nadhani sasa ana furaha maana kiu yake imetimia. Lkn nimwambie Bashe na wanaCCM wenzie kuwa DAMU HIZI HAZITAENDA BURE. Kama MUNGU aishivyo hazitaenda bure.!

=========
Jitokezeni kupiga kura kwani sasa mawakala wamepewa viapo tayari kwa kazi moja tu hapo kesho...kusimamia na kuhakikisha upigaji kura unakwenda kwa mujibu wa sheria! KUWENI WA KWANZA VITUONI KWANI USHINDI NI WETU!.Dr Vicent Mashinji
 
Angesema walipewa viapo lini
Itakuwa tangu siku za nyuma mnataka kudanganya wananchi kutafuta kura za huruma.. ha ha haaaa tumeamka hatupendi kiki

Kwanini wanaficha kuwa mawakala wao walishapata hayo na hata hawataji namba.. leo wanasema eti wamepewa huku wanadai walitawanishwa eeeeeh hivyo wamekutana wapi kukusanywa kwa viapo?

Uongo mwingine bomu kabisa sema mliitea mkawaficha labda kusubiria usiku mjidai walikataliwa.. uongo mtupu ya mauaji yamewashinda ya mwenzenu
 
Ushazoeleka bibi!
 
hii habari watu kama jingalao,yehodaya,cocochannel hawatapendezwa nayo maana walishaanza kusema muda kazi umepita
 
Back
Top Bottom