Dr. Ulimboka apelekwa nje kwa matibabu zaidi...

Tunamuombe apone ..ili aje atoe ushuhuda ni jinsi gani kifo kilivyo..mana wenyewe wana ona raha sisi ndugu zetu kufa kwa migomo yao isiyo kuwa na tija kwetu wananchi, zaidi ya faida yao ya fedha na siasa zao za chadema .

mbona una akili fupi we gamba ............
 
Hivi kwa nini kila mtu na kaugonjwa kake lazima apelekwe India? Hawa madokta waliogoma wameshindwa kweli kumsaidia mwenzao? na kama wameshindwa kumtibu mtu aliyejeruhiwa na kipigo, kuna haki gani kwao kugoma kama matatizo kama hayo tu lazima watu wapelekwe nje ya nchi. Ni wakati sasa sisi wananchi tuanze kuuliza hawa madokta wetu wanatibu nini sasa kama kila mtu mwenye kauwezo kidogo tu, anaenda India. Tuliwasomesha ili watusaidie na kama wako kwenye mgomo sasa ina maana hawako busy ya vile, basi wamtibu mwenzao kuonyesha uwezo wao na ili kuhalalisha waongezewe posho, kwa nini apelekwe nje?

Suala siyo uwezo ni vifaa. Kama priority ya wakuu ni kusafiri na siyo kuwekeza katika afya lazima waende huko walikowekeza katika tiba. Zipo njia nyingi za kumaliza mgomo lakini hii ya kuteka, kutesa na kuua ni mbaya sana wanaoshabikia hilo waache maana hujui atakayefuata kutekwa ni nani.
 
JK Nyerere muda mfupi uliopita,,,Dr. ndio anasepa to IndiaView attachment 57775

Hallo JF ni kiboko. Hii picha imepigwa at 14:53 yaani dakika 32 zilizopita.

Kumbe Usalama wa Taifa inabidi wabwage manyanga yao kama ni kuichukia au kuwatafuta wanachama wa JF. Hapa maana yake at least mwanaJF mmoja yuko pale airport. Lazima watu kama mama Lwakatare aogope na kuuliza Bungeni JF inamilikiwa na nani!!
 
Hadha Min Fadhil Rhabi.

Lakini hatuna imani na Madaktari watakaomuhudumia huko nje ya nchi maana wanaweza kupewa maagizo na TISS wasimtibu vizuri ili afie huko na hatimae kupoteza ushahidi wa tuhuma za mauaji zinazowang'ang'ania!
mkuu tumbiri.
india inaitwa(km anaenda huko) ni medical tourist destination ambayo hata wamarekani huwa wanakwenda huko kutibiwa. sidhani kama wanaweza kuharibu credibility yao in that field kwa ajili ya udhaifu wa sirkali ya tz eti wamuhujumu dr uli. ht hivyo kila nchi watu wa fitna wapo. kikubwa tumwombee mungu.
 
Mungu wetu aliye mwaminifu akutangulie katika safari yako, na neema yake ya uponyaji ikawe juu yako!
Upanga wake ukawe juu ya wale waliotenda yale ambayo yapo kinyume na mapenzi yake!
Kuuwa ni kazi yake mola! si vyema kuingilia kazi ya Mungu!
Get well soon Dr. Ulimboka.
 
Tunamuombe apone ..ili aje atoe ushuhuda ni jinsi gani kifo kilivyo..mana wenyewe wana ona raha sisi ndugu zetu kufa kwa migomo yao isiyo kuwa na tija kwetu wananchi, zaidi ya faida yao ya fedha na siasa zao za chadema .

Huna nidhamu kbs. Hv unajua maana ya kudai haki? Mgomo wa madaktari unahusianaje na Chadema kama si prejudice zako tu! Waza km aliyeenda shule bhana.
 
Jamani Dr Ulimboka! Mungu akupe uwezo zaidi, afya zaidi na urudi nchini ukiwa mwenye afya bora. Nina amini Drs wenzako wanaendelea kuungana na kushikamana bila kuyumbishwa serikali hii dharimu hadi madai yenu yatimizwe. Amina!
 
Hivi kwa nini kila mtu na kaugonjwa kake lazima apelekwe India? Hawa madokta waliogoma wameshindwa kweli kumsaidia mwenzao? na kama wameshindwa kumtibu mtu aliyejeruhiwa na kipigo, kuna haki gani kwao kugoma kama matatizo kama hayo tu lazima watu wapelekwe nje ya nchi. Ni wakati sasa sisi wananchi tuanze kuuliza hawa madokta wetu wanatibu nini sasa kama kila mtu mwenye kauwezo kidogo tu, anaenda India. Tuliwasomesha ili watusaidie na kama wako kwenye mgomo sasa ina maana hawako busy ya vile, basi wamtibu mwenzao kuonyesha uwezo wao na ili kuhalalisha waongezewe posho, kwa nini apelekwe nje?

Pole. Hujui usemalo!
 
Tunamuombe apone ..ili aje atoe ushuhuda ni jinsi gani kifo kilivyo..mana wenyewe wana ona raha sisi ndugu zetu kufa kwa migomo yao isiyo kuwa na tija kwetu wananchi, zaidi ya faida yao ya fedha na siasa zao za chadema .

Migomo iwe na tija kwako au haina, iko pale pale. Utajaza. Mpaka kieleweke!! We ni mchawi tu. Ushindwe, huli hiyo nyama.
 
Hivi kwa nini kila mtu na kaugonjwa kake lazima apelekwe India? Hawa madokta waliogoma wameshindwa kweli kumsaidia mwenzao? na kama wameshindwa kumtibu mtu aliyejeruhiwa na kipigo, kuna haki gani kwao kugoma kama matatizo kama hayo tu lazima watu wapelekwe nje ya nchi. Ni wakati sasa sisi wananchi tuanze kuuliza hawa madokta wetu wanatibu nini sasa kama kila mtu mwenye kauwezo kidogo tu, anaenda India. Tuliwasomesha ili watusaidie na kama wako kwenye mgomo sasa ina maana hawako busy ya vile, basi wamtibu mwenzao kuonyesha uwezo wao na ili kuhalalisha waongezewe posho, kwa nini apelekwe nje?

Mpaka unamaliza comment ulikuwa huoni ulivyo mfinyu wa uelewa.majibu unayo mwenyewe!mbaf..!
 
Kuna watu wamekuwa wanatumia nguvu kubwa sana kupindisha madai ya madaktari ili ionekane kama wanachodai ni mishahara minono peke yake. Sasa waone, madaktari wameshindwa kumtibu daktari mwenzio kwa sababu they simply do not have the right equipment. Kwa siku mbili wananchi wakiongozwa na madaktari wenyewe wamekuwa wanachanga ili Dr Ulimboka akatibiwe kwenye taifa jingine! Hicho ndicho kilelezo cha hali ya hospitali zetu.

Madaktari wamegeuzwa kuwa mashuhuda wa wagonjwa wanaokufa kwa kukosa dawa, au huduma mbovu kwa sababu ya ukosefu wa vitendea kazi, na wanapopiga kelele wanaokotwa Mabwepande. Miaka 50 ya uhuru.
 
Back
Top Bottom