Dr. Slaa: Waandishi wa habari someni mjue mikutano inahusu nini kabla hamjaenda kwenye mikutano

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Dr. Slaa awaambia Waandishi wa habari wafanye uchunguzi kujua mikutano wanayoenda kuhudhuria kutazungumzwa nini kabla ya siku ya tukio ili wasiende kuwa watu ambao hawana maana kwa kushindwa kupeleka ujumbe unaotakiwa kwa wananchi.

Dr. Silaa alisema hayo baada ya mwandishi wa habari kumwambia amekuwa akijihusisha na mambo ya siasa na kuvalia njuga suala la DP World wakati mwaka 2015 alitangaza kuachana na CHADEMA japokuwa alisema ataendelea kubaki kuwa mwanasiasa.

Dr. Slaa aliendelea kusema kuwa, kwa mujibu wa katiba akiacha kuwa mwanachama hazuiwi kutoa maoni yake na kwamba kama mwandishi angejiandaa na mkutano huu kabla, angekuwa anajua maana ya mtu kuwa kwenye chama na lini anaacha kuwa kwenye chama, lakini pia angejua kwa mujibu wa katiba, ibara ya 27 (1) inayosema ni wajibu wa kila mwananchi kulinda rasilimali za nchi haijalishi kama ana chama au la.
 
Asisahau posho Tu Kwa waandishi....
Karamagi katoa mzigo wa kutosha
 
Paskali Mayalla anakuja sasa hivi na yale mapost yake marefu ya kusimamisha shilingi ili aonekane hata yeye alisema, lakini ukifuatilia hayana uhalisia wa hivyo. Sasa hivi akina mayalla wanatumia zaidi utumbo mpana kufikiri kuliko akili zao.
 
Back
Top Bottom