Dr. Slaa Unayajua Haya? Picha ya Chopa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa Unayajua Haya? Picha ya Chopa

Discussion in 'Jamii Photos' started by MPadmire, Jun 1, 2009.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa napita mitaani nikaona kijitabu kina Title :- Dr. Slaa unayajua haya? Pia kimechorwa picha ya Chopa. Kitabu kilikuwa kinauzwa na wauza magazeti.

  Ndani ya kitabu kuna propaganda zilizoandikwa kuhusu Marehemu Chacha Wangwe, Ruzuku ya chama, Ukabila, matumizi ya chopa, Bilicanas na mengineyo.

  Naomba taarifa zaidi.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kimetungwa na nani?
   
 3. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #3
  Jun 1, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mpadmire,
  Ahsante sana.

  Kijitabu hicho ninakifahamu. Kiliandaliwa kama mkakati maalum wa kumg'oa Dr. Slaa, Karatu na CCM. Kikaangukia mikononi mwa Dr Slaa, kabla haikijawekwa hadharani. Kikapata majibu hapo hapo katika mkutano mkubwa wa Hadhara Karatu mjini. It is no more an issue in Karatu. Kimsingi, no hoja ya watu waliofilisika.

  Hawana jipya, hakuna takwimu zozote-huwezi kuongea ubadhirifu bila takwimu wala data ya aina yeyote ile. Huwezi kuwaeleza watanzania kuhusu Chopper, kwani hoja yenyewe imepitwa na wakati, ccm waliisha kujaribu Chopper Kiteto na Tarime wakaleta mbili. Wananchi hawakusumbuliwa na Chopper. Hii ni tradition ya Chadema na tutaendelea kuitumia. Inaowauma wacha iwaume zaidi, lakini sababu ni dhahiri kwani uchaguzi mdogo una siku 28 tu na kwa mfano wa Busanda kuna vijiji 75 unategemea vipi vyama vyetu visivyo na mtandao wa Dola kufika kwenye vijiji hivyo katika siku 28.

  Wanajenga hoja kwa kuwa inawaumiza sana. Hoja kuhusu Chacha Wangwe nazo ziliisha kupitwa na wakati- Ikiwa hazikuwa na impact Tarime ambako alikuwa Mbunge wanataka kumpotosha nani. Hoja ya Wabunge wa Viti Maalum is no longer an issue ndani ya Chadema, lakini hata kwa Watanzania, na tumeisha kuitolea ufafanuzi mara chungu mbovu.

  Hivyo hakuna hoja yeyote inayotusumbua, kwa kuwa wana fedha za kuchezea zikiwemo za ufisadi, tuwaache tu wazitumie kwa propaganda hizo. Pamoja na yote, ninakushukuru sana.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaah,

  Siku zote tunafahamu kuwa ukitaka kumuua NYOKA basi lazima ulenge kichwani. Tatizo linakuwa wakati nyoka huyo kichwa chake ni kigumu sana kukilenga. Ila wanasema palipo na nia pana njia. Shida kubwa sana ya huyo NYOKA ni kuwa kila siku anazidi kuongeza NGOME/Ngozi katika mwili wake. Leo nimeshangaa kufahamu kuwa hadi Moscow kuna tawi la CCM. Hapo nikaona kuwa kutegemea kuwa siku moja mtashinda na kuwa wengi bungeni, ni kazi ngumu sana. Inabaki kazi moja rahisi ila inahitaji mtu mmoja aende kukilenga hicho kichwa kwa msaada wa wananchi. Mtu huyo lazima awe ni mtu mwenye nia kweli na uchungu wa kuona hicho kichwa kimepondeka na kipotee walau kwa miaka kadhaa kabla hakijazaliwa kingine maana always maovu hurudi duniani.

  Chadema, kuishinda CCM na kuwa wengi kwenye Bunge na hata upinzani kwa ujumla naona ni kazi ngumu sana. Inabaki kulenga KICHWA cha nyoka na KUKIBADILISHA.

  Sitaki kusema sana, ila kama ukiamuwa kuchukua hilo jukumu (hapa sisemi UJARIBU), basi lazima ufahamu kuwa ntakuwa MPAMBE namba 1 Sikonge. Nafikiri itakuwa Rahisi kuanzia juu na kuleta chini mabadiliko hasa ukichukulia Kichwa chetu kina madaraka makubwa ya kufanya MAAJABU nchini kwetu ila tu kama KIKITAKA.

  Ntaendelea KUSUBIRI huo ujumbe ili nianze kazi. Warusi walikuwa Masikini sana miaka 20 iliyopita na wakichekwa. Leo hii wananunua kampuni ya General Motors kweli ni ajabu. Ila kama si UJASIRI wa Putin, pamoja la laana zote anazopata, wazingeliweza kufanya hivyo. Tanzania hata kama tungelikuwa na Mafuta, bado tungeliendelea kuwa omba omba. Na kwa Katiba ya Tanzania, mtu mmoja tu wa kulaumiwa kwa umasikini wetu ingawa na sisi tuna utajiri Mkubwa sana sana.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 5. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Waw! Asante Dk Slaa kwa ufafanuzi maana nilikuwa nimepatwa na mshtuko. Nikafikiri kuwa mngeanza kujibu haraka ili wananchi waelewe.

  Mafisadi maji yamewafika shingoni maana wananchi wengi wako nyuma ya Chadema.

  Watanzania sio Mabwege tena, hata huko vjijini wanakotegemea watakosa kura 2010.

  Aluta continua
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Dr.W.Slaa,
  Hata kama unayajua hayo ndo iweje?
  wanataka kutwambia hayo ya chopper n.k ndo yanafanana na mamilioni ya EPA n.k yaliyotumika kufadhili kampeni za uchaguzi mkuu wa chama cha mafisadi, uliomuweka madarakani JK? mbona hawasemi kuwa pesa chafu ndizo zilizo finance kampeni za chama chao. Waseme kinachowasumbua Dr. ni kuwa unawanyima usingizi, hawapati kutumia mamilioni ya wizi kwa raha.
  L'aluta continua
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Siku huyu mzalendo akiamua kujitosa kugombea uraisi- basi kura yangu na familia yangu anayo!
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hili ndio tamko rasmi la kwanza nalisikia kutoka uongozi wa CHADEMA kuhusu kushindwa Busanda.

  Kumbe tatizo ni kwamba huwa wanashindwa kufika kila pembe za vijiji.

  Sasa kama chama kizima kimelenga jimbo moja tu, kimepewa siku 28, CHADEMA nzima na helikopta juu, na hawakuweza kufika vijijini, ina maana nchi nzima kwenye uchaguzi mkuu ndio wataweza kufika?

  Dr. Slaa anasema wao hawana ``mtandao wa dola.`` Ina maana mwenye dola, yani incumbent administration tu ndio anaweza kushinda uchaguzi. Huna dola hushindi. Upinzani tujizatiti, enough with defeatist excuses.
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Please Dilunga try to be fair - ninavyoelewa mimi hilo halikuwa tamko rasmi la Chadema kuhusu kushindwa Busanda bali ni tamko la Dr.Slaa kuhusu kijarida kinachouzwa mitaani chenye title - Dr. Slaa unayajua haya?
   
 10. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu heshima yako, Hebu jaribu kuelewa jambo kabla ya kukimbilia kukosoakosoa hapa Slaa amesema kua sababu ya kutumia Chopper ni ili kuweza kuvifikia vijiji 75 ndani ya siku 28 wewe umeelewa kinyume chake na badala yake unasema mambo unayofikilia wewe kua hiyo ndo sababu ya kushindwa Busanda come on..!
   
 11. Z

  Zahir Salim Member

  #11
  Jun 1, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dk Slaa hana jipya midhali mama watoto wake ni Diwani wa CCM, kwani sadaka huanza nyumbani au ulingano huwa mwanzo ndani mwako sasa yeye yamemshinda Kwisha hata 2010 hapo KARATU Slaa na CHADEMA yake watapasikia Redioni. Chama cha siasa hakiendeshwi kwa Ukabila wala Ukoo na Udini kama kiendeshavyo CHADEMA kitabakia Kuzurura na CHOPPA nchi Nzima hawataambulia lolote huko mbele twendako kwani Watanzania tuliowengi hatuufurahii UCHAGA wa CHADEMA.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Naombeni namba ya Dr Slaa, mwenye nayo ama mwenyewe aniPM!

  Thanks

  Masa wa Nilo
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Naona na wewe Mgeni hapa. Ila cha ajabu hata KAMBA mguuni huna.

  Karibu tena Wavuni.

  zahir salim [​IMG]
  zahir salim has no status.
  Member
  Join Date: Fri Mar 2009
  Posts: 29
  Thanks: 0
  Thanked 10 Times in 9 Posts
  Rep Power: 0 [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
  Credits: 69,430
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Mkuu Sikonge usipoteze your valuable ATPs kumjibu huyu jamaa!
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pamoja na yote haya naomba kuunganmisha mada hii na swali langu..
  Chadema wameshindwa vipi Busanda?..nini hasa sababu kubwa ya wao kushindwa sehemu ambayo (kama sikosei) walikuwa na hakika ya Ushindi..
  Dr.Slaa unaweza kutupa somo kidogo, umejifunza kitu gani toka uchaguzi wa Busanda!
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Duh! very strong yaani bila kumuangalia usoni, maana ungeweza kumuonea haya, saafi sana Mkulu na wako ni mfano wa kuigwa yaani hoja hujibiwa kwa hoja tu!

  Respect.

  FMEs!
   
 17. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Somo mhimu kwa wapenda demokrasia wote ila nashauri badala ya kusubiria masomo hapa ktk komyuta yako pia uwe unajipa muda kujifunza live- tuache kuatamia komyuta all time and get out to fight and accelerate democrasia tunayoililia siku zote
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wengi wetu tunaelekea kutoelewa kampeni ni nini na lugha, mbinu na mikakati yake ikoje. CHADEMA wanaelekea kumudu sema tu refa mzuri kwenye chaguzi zetu hajapatikana. Wasikate tamaa, Watanzania wanaanza kuwaelewa taratiiibu.
   
 19. N

  NTIRU Member

  #19
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WildCard,
  Asante kwa maneno yako ya kutia moyo. Kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo na uelewa wa watu unavyoimarika juu ya jinsi CCM inavyowafukarisha kishenzi. Ni wazi hata wale mbumbumbu wa vijijini wanaoendelea kuwapa kura hao mafisadi wa CCM kwa kugawiwa t-shirt, khanga na visenti kidogo, baadhi yao wanaanza kuamka gizani. Siku za mafisadi wa CCM kubaki madarakani zinaanza kwisha.
  Dr. Slaa, wapenda mapinduzi tuko nyuma yako. Umejitoa mhanga kuikomboa nchi hii kutoka mdomoni mwa mafisadi, endelea bila kuogopa. Mungu yuko pamoja nawe nasi tunaendelea kukuombea. Ni siri iliyo wazi kuwa CHADEMA ndicho chama makini (serious) ambacho kitaleta mapinduzi chanya katika nchi yetu tuipendayo Tanzania. Dr. Slaa, usijali wasemayo vibaraka wa Chama cha Mafisadi (CCM) na mafisadi wenyewe kwani hata Bwana Yesu angejali wasemayo Mafarisayo na Masadukayo azima yake ya ukombozi isingefanikiwa. Mungu ibariki Tanzania, Mungu tuepushe na mafisadi wa CCM.
   
 20. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtasema sana mwaka huu!!! Busanda tu imekuwa hivi je mwakani ???
   
Loading...