laki si pesa.
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 9,983
- 9,760
Slaa ameshikiliwa mateka na Josephin mpaka uchaguzi upite October ndio ataachiliwa.
Dr. Slaa na Watanzania wote salaam kwenu,
Ni weekend njema hapa jijini bongo kwani uandikishaji unaendelea vema katika vituo vingi. Watanzania wengi tumepata "vikatio" vyetu tayari kwa kupeleka msiba huko magambani ifikapo octoba 25.
Baada ya utangulizi huo, ninaomba sasa nijikite kwenye kichwa cha habari hapo juu. Kumekuwepo sintofahamu na uzushi mwingi tangu Mh. Lowasa ahamie CHADEMA na kukabidhiwa jukumu la kupeperusha bendera ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla katika mbio za urais. Dr. Slaa hujaonekana katika matukio yote hayo japo tumeambiwa na wasemaji wa chama kuwa hakuna tatizo ila ni mgawanyo wa majukumu tu. Nimesoma pia bandiko lako leo ukimkana Yeriko Nyerere kijana aliyejitolea mhanga kuinadi CHADEMA kwa hali na mali. Niliposoma nikagundua kuwa kuna jambo haliko sawa kwa upande wako na CHADEMA. Wapinzani wa CHADEMA hasa CCM wanasambaza propaganda katika vyombo mbali mbali vya habari ya kuwa umeamua "kubwaga manyanga" Kisa! eti kwa nini CHADEMA imemkaribisha Lowasa. Kama hivyo ndivyo ilivyo basi Watanzania wengi wenye mapenzi mema na wewe na pia kwa nchi yetu tutaendelea kusikitikia umauzi huo.
Dr. Slaa, wewe unapendwa na watanzania wengi sana sio walioko CHADEMA pekee bali na sisi wengi ambao hatuna vyama. Wengi wetu tunakerwa na mfumo kandamizi wa CCM na kila siku tunaomba Mungu atuondolee "dubwana hili". Tulipata matumaini baada ya UKAWA kuundwa na kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja kwa kila ngazi za kisiasa. Ghafla tuliingiwa na simanzi baada ya kuona mivutano inaendelea katika kufikia hitimisho la mgombea urais. Hali ilikuwa mbaya zaidi hadi baadhi ya vyama ilisemekana vilitaka kujitoa UKAWA. Mimi binafsi nilihisi mgogoro huo hadi nikatoa pendekezo kuwa isingekuwa busara kuendelea kulumbana baina ya CHADEMA na CUF. hIvyo nikapendekeza kupitia hapa jamii forum kuwa wewe Dr. Slaa kubali ukagombee ubunge na CUF wamsimamishe Prof. Lipumba katika urais. Nilishauri hivyo ili CHADEMA chenye ushawishi mkubwa bara kingepata nafasi ya kusimamisha wagombea wengi na hivyo kupata viti vingi vya ubunge na pengine kutoa Waziri Mkuu. Hayo yakiendelea, ghafla ulienea uvumi na hatimaye ukweli kuwa Lowasa anahamia CHADEMA. Kusema ukweli siasa za nchi zimebadirika mara baada ya ujio wa Lowasa. Magufuri aliyekuwa anakuja kwa kasi hivi sasa hasikiki kabisa. Gumzo limebaki kwako Dr. Slaa na Lowasa. Hata magazeti ya CCM yamejikita hapo!
Ushauri wangu kwako mpendwa Dr. Slaa ni huu; Pitia vizuri uchambuzi wa Dr. Lweitama ameeleza vizuri sana umuhimu wa Lowasa kuhamia upinzani. Katika maelezo yake ameeleza kwa ushahidi mwingi jinsi "mahasimu wa kisiasa" wanvyoweza kusahau tofauti zao na kutimiza kusudi kuu. Tumaini la watanzania wengi ni mabadiliko ya kuuondoa utawala ulioshindwa wa CCM na kung'oa mifumo yote kandamizi. Kwa sasa naweza kusema imetokea "bahati ya mtende" silaha ya kuliondoa hili "dubwana" linalotusumbua imepatikana japo hiyo silaha imetelekezwa na adui. Cha msingi ni kuangalia hiyo silaha kama inafaa kwa mapambano na kuitumia kumwangamiza adui ambaye ndiye alikuwa mmiliki wa hiyo silaha ya maangamizi. Kwa maoni yangu na watanzania wengi, Lowasa ni silaha iliyotelekezwa na adui kwa ulevi tu na kushindwa kutunza vema silaha zake. Ikiwa hiyo silaha imeangukia mikononi mwako hutaitumia? eti kwa kuwa ilimilikiwa na dui? hapana Dr. wewe ni mtu makini sana huwezi kufanya hivyo. Usiwape nafasi CCM ya kuwagawa na kundelea kueneza propaganda za kuwachonganisha na viongozi wenzako.
Dr. Slaa kaza buti, inuka jitokeze msitari wa mbele kama kawaida yako uongoze mashambulizi upande wa adui. hakuna kipindi kizuri cha kuwaondoa CCM madarakani kirahisi kama sasa.Dr. usikubali hii nafasi ipite.
Asante kwa kuwa naamini utazingatia ushauri huu.
Mkuu ubarikiwe sana kwa hekima hii,nimefurahi sana kukutana na uzi huuKutokana na watanzania kunyonywa,kikandamizwa na kutothaminiwa na Nduli ccm kwa takribani miaka 50 sasa ni wakati wa kueaondoa kwenye dola na kusimika dola mpya yenye matumaini.
Ni kweli Baba na mpendwa wetu Dr slaa tunajua msinamo wako hasa unapotetea maslahi ya watanzania huna mzaha hata chembe na hurudi nyuma kamwe.
Ombi kwako Dr Slaa.
Tunaomba utusamehe (kama hukuwa umeridhia ujio wa Mh Lowasa na hatimae kupeperusha bendera ya ukawa ktk uchaguzi mkuu ujao) tuendelee na umoja wetu kama ukawa maana muda huu tunahitaji Tembo afe bila kujali ameuawa kwa silaha gani iwe riffle sawa,iwe Ak43 sawa,Rpg sawa halafu baaada ya ukombozi tutachagua silaha sahihi kwa tembo atakaejitokeza.
Dr Slaa usione Lowasa tunamuunga mkono ni shauku ya mabadiliko lakini wewe umo mioyoni mwa mamilioni ya watanzania na wana mabadiliko,wewe ndiye umekuwa kiongozi shupavu na shujaa katika siasa za vyama vya siasa Afrika usiyetetereka.
Rudisha roho nyuma,uwe nasi.
Nashangaa, wasiojua (kwa kutojua au umbumbumbu) ni wengi hapa JF.
Lowasa hakuja CHADEMA kwa kuwa anakubaliana na na chama, ametumia utajiri wakw kuwanunua wenye CHADEMA kuhitimisha mradi wake wa kuingia ikulu. Hili Mwalimu alilliona mapema. Kwamba CCM ilimzima, ni plus kwao. CHADENA imejichafua isivyosemeka.
Mwishoni, wanahisa wa CHADEMA walilipwa ngapi?
Dr. Slaa Mwanamapinduzi. Wengi wetu tupo nyuma yake kwa uamuzi wake sahii.
Lowasa atashinda tu hata bila kupigiwa debe na mtu yoyote kutoka Ukawa..
Dr. Slaa na Watanzania wote salaam kwenu,
Ni weekend njema hapa jijini bongo kwani uandikishaji unaendelea vema katika vituo vingi. Watanzania wengi tumepata "vikatio" vyetu tayari kwa kupeleka msiba huko magambani ifikapo octoba 25.
Baada ya utangulizi huo, ninaomba sasa nijikite kwenye kichwa cha habari hapo juu. Kumekuwepo sintofahamu na uzushi mwingi tangu Mh. Lowasa ahamie CHADEMA na kukabidhiwa jukumu la kupeperusha bendera ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla katika mbio za urais. Dr. Slaa hujaonekana katika matukio yote hayo japo tumeambiwa na wasemaji wa chama kuwa hakuna tatizo ila ni mgawanyo wa majukumu tu. Nimesoma pia bandiko lako leo ukimkana Yeriko Nyerere kijana aliyejitolea mhanga kuinadi CHADEMA kwa hali na mali. Niliposoma nikagundua kuwa kuna jambo haliko sawa kwa upande wako na CHADEMA. Wapinzani wa CHADEMA hasa CCM wanasambaza propaganda katika vyombo mbali mbali vya habari ya kuwa umeamua "kubwaga manyanga" Kisa! eti kwa nini CHADEMA imemkaribisha Lowasa. Kama hivyo ndivyo ilivyo basi Watanzania wengi wenye mapenzi mema na wewe na pia kwa nchi yetu tutaendelea kusikitikia umauzi huo.
Dr. Slaa, wewe unapendwa na watanzania wengi sana sio walioko CHADEMA pekee bali na sisi wengi ambao hatuna vyama. Wengi wetu tunakerwa na mfumo kandamizi wa CCM na kila siku tunaomba Mungu atuondolee "dubwana hili". Tulipata matumaini baada ya UKAWA kuundwa na kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja kwa kila ngazi za kisiasa. Ghafla tuliingiwa na simanzi baada ya kuona mivutano inaendelea katika kufikia hitimisho la mgombea urais. Hali ilikuwa mbaya zaidi hadi baadhi ya vyama ilisemekana vilitaka kujitoa UKAWA. Mimi binafsi nilihisi mgogoro huo hadi nikatoa pendekezo kuwa isingekuwa busara kuendelea kulumbana baina ya CHADEMA na CUF. hIvyo nikapendekeza kupitia hapa jamii forum kuwa wewe Dr. Slaa kubali ukagombee ubunge na CUF wamsimamishe Prof. Lipumba katika urais. Nilishauri hivyo ili CHADEMA chenye ushawishi mkubwa bara kingepata nafasi ya kusimamisha wagombea wengi na hivyo kupata viti vingi vya ubunge na pengine kutoa Waziri Mkuu. Hayo yakiendelea, ghafla ulienea uvumi na hatimaye ukweli kuwa Lowasa anahamia CHADEMA. Kusema ukweli siasa za nchi zimebadirika mara baada ya ujio wa Lowasa. Magufuri aliyekuwa anakuja kwa kasi hivi sasa hasikiki kabisa. Gumzo limebaki kwako Dr. Slaa na Lowasa. Hata magazeti ya CCM yamejikita hapo!
Ushauri wangu kwako mpendwa Dr. Slaa ni huu; Pitia vizuri uchambuzi wa Dr. Lweitama ameeleza vizuri sana umuhimu wa Lowasa kuhamia upinzani. Katika maelezo yake ameeleza kwa ushahidi mwingi jinsi "mahasimu wa kisiasa" wanvyoweza kusahau tofauti zao na kutimiza kusudi kuu. Tumaini la watanzania wengi ni mabadiliko ya kuuondoa utawala ulioshindwa wa CCM na kung'oa mifumo yote kandamizi. Kwa sasa naweza kusema imetokea "bahati ya mtende" silaha ya kuliondoa hili "dubwana" linalotusumbua imepatikana japo hiyo silaha imetelekezwa na adui. Cha msingi ni kuangalia hiyo silaha kama inafaa kwa mapambano na kuitumia kumwangamiza adui ambaye ndiye alikuwa mmiliki wa hiyo silaha ya maangamizi. Kwa maoni yangu na watanzania wengi, Lowasa ni silaha iliyotelekezwa na adui kwa ulevi tu na kushindwa kutunza vema silaha zake. Ikiwa hiyo silaha imeangukia mikononi mwako hutaitumia? eti kwa kuwa ilimilikiwa na dui? hapana Dr. wewe ni mtu makini sana huwezi kufanya hivyo. Usiwape nafasi CCM ya kuwagawa na kundelea kueneza propaganda za kuwachonganisha na viongozi wenzako.
Dr. Slaa kaza buti, inuka jitokeze msitari wa mbele kama kawaida yako uongoze mashambulizi upande wa adui. hakuna kipindi kizuri cha kuwaondoa CCM madarakani kirahisi kama sasa.Dr. usikubali hii nafasi ipite.
Asante kwa kuwa naamini utazingatia ushauri huu.
Kutokana na watanzania kunyonywa,kikandamizwa na kutothaminiwa na Nduli ccm kwa takribani miaka 50 sasa ni wakati wa kueaondoa kwenye dola na kusimika dola mpya yenye matumaini.
Ni kweli Baba na mpendwa wetu Dr slaa tunajua msinamo wako hasa unapotetea maslahi ya watanzania huna mzaha hata chembe na hurudi nyuma kamwe.
Ombi kwako Dr Slaa.
Tunaomba utusamehe (kama hukuwa umeridhia ujio wa Mh Lowasa na hatimae kupeperusha bendera ya ukawa ktk uchaguzi mkuu ujao) tuendelee na umoja wetu kama ukawa maana muda huu tunahitaji Tembo afe bila kujali ameuawa kwa silaha gani iwe riffle sawa,iwe Ak43 sawa,Rpg sawa halafu baaada ya ukombozi tutachagua silaha sahihi kwa tembo atakaejitokeza.
Dr Slaa usione Lowasa tunamuunga mkono ni shauku ya mabadiliko lakini wewe umo mioyoni mwa mamilioni ya watanzania na wana mabadiliko,wewe ndiye umekuwa kiongozi shupavu na shujaa katika siasa za vyama vya siasa Afrika usiyetetereka.
Rudisha roho nyuma,uwe nasi.
Ukisema hvyo unaharib jarb ku comment fair kwan ni ngum lowassa kushinda bila Muungano wa ukawa pls msilewe sifa kias hicho.
Tatizo Slaa anataka kututoa kwenye mood sasa hivi... Tumpotezee tu