G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,654
- 8,708
Sisi tunakupenda sana, na tunajua umeifanyia CHADEMA makubwa na tunajua ulishinda uchaguzi ila walikuibia kura zako. Tunajua hata sasa ungegombea ungeshinda.
Nia ya CHADEMA nini? Jibu ni kuondoa mfumo wa CCM na kama uko tayari basi tunakuomba uwe mvumilivu ili tutumie hii Silaha tuliyoiokota ikiwa imetupwa na maadui zetu CCM tuwauwe wenyewe maana tunajua nia yako ni kutosikia CCM. Tusaidie sisi waja wako tuko nyuma yenu. Mwache EL agombee na tunaomba umsaidie katika kampeni.
Tunajua Ruto wa Kenya alikuwa maarufu sana lakini kaamua kumwachia Kenyata na mwisho wa siku wakashinda kwa kishindo. MUNGU AKUBARIKI UWE NA HEKIMA KATIKA HILI.
Mtoto alihama nyumbani kwa ugomvi wake na baba yake ndani ya wiki moja unaweza amini anaweza kwenda kumuua baba yake eti tu umemwambia baba yako hafai??