Dr. Slaa tafadhali sana baba, tumeyaona uliyoyafanya

Dr. Slaa tafadhali sana baba, tumeyaona uliyoyafanya

Naamini dr slaa ni mtu makn na haya yanayotokea ameshiriki ila tabia ya wanajami na wandishi wa habari wanachokoza tu.
 
Hakuna kitu kitakachonikatisha tamaa kama Dr W P Slaa kuondoka Chadema...
 
Dr. Hotuba zako ndizo zinazotakiwa kwenye Siasa. CCC zimewazingua, wamempoteza, tumeongeza mtaji. Dr. toa kauli MZEE! We are in a dalema.
 
kweli baba slaa tunaomba sana urudi sasa utufungue mioyo ukweli lowasa anakuja kama messenger na mimi ktk hilo nimeelewa hakuna mizengwe tunaomba utuokoe kizazi hiki na kizazi kijacho; muachie lowasa na muunge mkono atutoe miaka 5 tu baada ya hapo nchi itakuwa iko chini ya katiba ambayo wewe ni muasisi wake; fungua moyo baba mwana haramu apite ila mzigo ufike ng'ambo
 
Dr. hajaondoka ila hawezi kushiriki dhambi ya kuwalaghai Watanzania kwa tamaa ya kwenda ikulu. Tanzania ni zaidi ya urais au uwaziri mkuu kwa Dr. Slaa

Wacha wenye tamaa ya ukuu watumie njia hata za kutapeli watu wao waende ikulu, lakini Dr ni mtu wa Mungu, hawezi...
 
Edo akamwaangukie dr ili kuunganisha nguvu ya pa1 na Dr kinyume na hivo cdm kamgogoro kanafukuta na si kazuri kwa faida ya taifa.
 
Dr Slaa tunaomjua vizuri hawezi kurudi. Ameshaamua. Mbona hamkumtetea kabla? Wengine mnaendelea kumsimanga na kumtukana ye na mke wake. Ambao tuko nae tumesimama nae tokea awali na tulionya atafutwe mapema .. now it's too late. ..
Best case scenario aendelee kukaa kimya ..
 
Dr. Slaa you are my hero always you shall be my hero and forever please stay with us as the hope of our family and unit without you we lost please Dr. Slaa my hero wherever you are right now hear my request and have mercy on us your participants in the redemption of this nation don't and never leave us alone and abandoned.

I love you my hero Dr. Willbroad Slaa forever to the ground.
 
Dk kiukwel tunaumia sana moyon mwetu tumekuwa ka makinda ya ndege yasiyo kuwa na wazaz hatujui ukwel wa yale yanayosemwa mioyo yetu imepondeka huzun imetujaa baba yetu na shujaa wa taifa letu tunakuomba angalau utuckie cc tunaokulilia tunakuhitaj kwa dhamira ya dhat toka moyon daah chakula hakipit hamuwez kuamin ila ukwel ndo huo inauma sana yan najuta kuifaham siasa pls dk ucondoke tunakuhitaj mno dah
 
Hakika Dr watanzania tunakuhitaji kama umekwazika kwa namna yeyote ile tunakuomba samehe tusonge wote mbele kwa pamoja, siku zote umesimamia umoja ili kuiondoa ccm. Mama Josephine tunakuomba wana mageuzi ongea na Dr maana wewe pekee ndo muhimu zaidi kwake maana kimsingi tunasema familia kwanza hivyo ushawishi wako kwa mzee ni muhimu sana. Tafadhari Mama
 
Binafsi nimeudhiwa sana na Tundu Lissu ,Mungi na Yericko kwa kumnanga.Labda wana nia njema ila njia walikosea.
Ila tunaomba Dr atumie hekima yake na kusamehe ili tuendelee mbele.
Dr Slaa tunaomjua vizuri hawezi kurudi. Ameshaamua. Mbona hamkumtetea kabla? Wengine mnaendelea kumsimanga na kumtukana ye na mke wake. Ambao tuko nae tumesimama nae tokea awali na tulionya atafutwe mapema .. now it's too late. ..
Best case scenario aendelee kukaa kimya ..
 
Dr. Slaa na Watanzania wote salaam kwenu,

Ni weekend njema hapa jijini bongo kwani uandikishaji unaendelea vema katika vituo vingi. Watanzania wengi tumepata "vikatio" vyetu tayari kwa kupeleka msiba huko magambani ifikapo octoba 25.

Baada ya utangulizi huo, ninaomba sasa nijikite kwenye kichwa cha habari hapo juu. Kumekuwepo sintofahamu na uzushi mwingi tangu Mh. Lowasa ahamie CHADEMA na kukabidhiwa jukumu la kupeperusha bendera ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla katika mbio za urais. Dr. Slaa hujaonekana katika matukio yote hayo japo tumeambiwa na wasemaji wa chama kuwa hakuna tatizo ila ni mgawanyo wa majukumu tu. Nimesoma pia bandiko lako leo ukimkana Yeriko Nyerere kijana aliyejitolea mhanga kuinadi CHADEMA kwa hali na mali. Niliposoma nikagundua kuwa kuna jambo haliko sawa kwa upande wako na CHADEMA. Wapinzani wa CHADEMA hasa CCM wanasambaza propaganda katika vyombo mbali mbali vya habari ya kuwa umeamua "kubwaga manyanga" Kisa! eti kwa nini CHADEMA imemkaribisha Lowasa. Kama hivyo ndivyo ilivyo basi Watanzania wengi wenye mapenzi mema na wewe na pia kwa nchi yetu tutaendelea kusikitikia umauzi huo.

Dr. Slaa, wewe unapendwa na watanzania wengi sana sio walioko CHADEMA pekee bali na sisi wengi ambao hatuna vyama. Wengi wetu tunakerwa na mfumo kandamizi wa CCM na kila siku tunaomba Mungu atuondolee "dubwana hili". Tulipata matumaini baada ya UKAWA kuundwa na kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja kwa kila ngazi za kisiasa. Ghafla tuliingiwa na simanzi baada ya kuona mivutano inaendelea katika kufikia hitimisho la mgombea urais. Hali ilikuwa mbaya zaidi hadi baadhi ya vyama ilisemekana vilitaka kujitoa UKAWA. Mimi binafsi nilihisi mgogoro huo hadi nikatoa pendekezo kuwa isingekuwa busara kuendelea kulumbana baina ya CHADEMA na CUF. hIvyo nikapendekeza kupitia hapa jamii forum kuwa wewe Dr. Slaa kubali ukagombee ubunge na CUF wamsimamishe Prof. Lipumba katika urais. Nilishauri hivyo ili CHADEMA chenye ushawishi mkubwa bara kingepata nafasi ya kusimamisha wagombea wengi na hivyo kupata viti vingi vya ubunge na pengine kutoa Waziri Mkuu. Hayo yakiendelea, ghafla ulienea uvumi na hatimaye ukweli kuwa Lowasa anahamia CHADEMA. Kusema ukweli siasa za nchi zimebadirika mara baada ya ujio wa Lowasa. Magufuri aliyekuwa anakuja kwa kasi hivi sasa hasikiki kabisa. Gumzo limebaki kwako Dr. Slaa na Lowasa. Hata magazeti ya CCM yamejikita hapo!

Ushauri wangu kwako mpendwa Dr. Slaa ni huu; Pitia vizuri uchambuzi wa Dr. Lweitama ameeleza vizuri sana umuhimu wa Lowasa kuhamia upinzani. Katika maelezo yake ameeleza kwa ushahidi mwingi jinsi "mahasimu wa kisiasa" wanvyoweza kusahau tofauti zao na kutimiza kusudi kuu. Tumaini la watanzania wengi ni mabadiliko ya kuuondoa utawala ulioshindwa wa CCM na kung'oa mifumo yote kandamizi. Kwa sasa naweza kusema imetokea "bahati ya mtende" silaha ya kuliondoa hili "dubwana" linalotusumbua imepatikana japo hiyo silaha imetelekezwa na adui. Cha msingi ni kuangalia hiyo silaha kama inafaa kwa mapambano na kuitumia kumwangamiza adui ambaye ndiye alikuwa mmiliki wa hiyo silaha ya maangamizi. Kwa maoni yangu na watanzania wengi, Lowasa ni silaha iliyotelekezwa na adui kwa ulevi tu na kushindwa kutunza vema silaha zake. Ikiwa hiyo silaha imeangukia mikononi mwako hutaitumia? eti kwa kuwa ilimilikiwa na dui? hapana Dr. wewe ni mtu makini sana huwezi kufanya hivyo. Usiwape nafasi CCM ya kuwagawa na kundelea kueneza propaganda za kuwachonganisha na viongozi wenzako.

Dr. Slaa kaza buti, inuka jitokeze msitari wa mbele kama kawaida yako uongoze mashambulizi upande wa adui. hakuna kipindi kizuri cha kuwaondoa CCM madarakani kirahisi kama sasa.Dr. usikubali hii nafasi ipite.

Asante kwa kuwa naamini utazingatia ushauri huu.
 
Kusamehe ni jambo jema. Watu wanataka mabadiriko tafadhali dr. Usituache msituni
 
Back
Top Bottom