Dr. Slaa tafadhali sana baba, tumeyaona uliyoyafanya

mzalendoalltz

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
828
709
Sisi tunakupenda sana, na tunajua umeifanyia CHADEMA makubwa na tunajua ulishinda uchaguzi ila walikuibia kura zako. Tunajua hata sasa ungegombea ungeshinda.

Nia ya CHADEMA nini? Jibu ni kuondoa mfumo wa CCM na kama uko tayari basi tunakuomba uwe mvumilivu ili tutumie hii Silaha tuliyoiokota ikiwa imetupwa na maadui zetu CCM tuwauwe wenyewe maana tunajua nia yako ni kutosikia CCM. Tusaidie sisi waja wako tuko nyuma yenu. Mwache EL agombee na tunaomba umsaidie katika kampeni.

Tunajua Ruto wa Kenya alikuwa maarufu sana lakini kaamua kumwachia Kenyata na mwisho wa siku wakashinda kwa kishindo. MUNGU AKUBARIKI UWE NA HEKIMA KATIKA HILI.

Mimi ni mfuasi wako ingawa simo kwenye chama chako. Tangu nikiwa masomoni,nilikuwa nakufuatilia na umekuwa ukinifunza mambo mengi ingawa nilijifunza bila ridhaa yako. Nimekuwa 'nikikuibia' busara zako, uelewa wako,maono yako na ndoto zako juu ya mustakabali wa Tanzania yetu. Kwakuwa umekuwa ukinivutia kimtazamo katika harakati zako za kisiasa,nimekuwa sijifichi kama mfuasi wako hata kutokea nje ya CHADEMA.

Dr. Slaa, tafadhali fanya kila uwezalo ili uwepo kwenye Mhimili mmojawapo wa nchi hii kati ya Serikali au Bunge. Kama uamuzi wako wa busara kuu utakuongoza kutogombea Urais kupitia CHADEMA/UKAWA mwaka huu, tafadhali gombea Ubunge katika jimbo mojawapo hapa Tanzania. Tangu ulipokoma kuwa Mbunge mwaka 2010, pengo lako ndani ya Bunge letu limekuwa wazi na gumu kuzibika.

Bunge lijalo lapaswa kuwa Bunge la kimabadiliko na lenye kuhitaji Wabunge wa aina yako. Litahitaji Wabunge wanaofikiri vyema,kutafiti na kujenga hoja kwa maslahi ya Tanzania yetu. Sifa hizo zote pamoja na nyinginezo unazo na inakupasa ujiunge na Bunge la kiabadiliko. Umeshajenga CHADEMA yenu kwa kiasi cha kutosha na utaendelea kujenga hata ukiwa Bungeni. Bunge lijalo linakuhiaji kwakuwa litakuwa la kitaifa zaidi kuliko la kichama. Tafadhali nisikie.

Aisome: Dr.W.Slaa, Tumaini Makene kwa kumfikishia ujumbe huu Dr. Slaa
Pengine hii ni njia pekee nayoweza kuwasiliana nawe.

Tanzania inakuhitaj sana katka nyakat hiz, sio kwa wana chadema tu bal pia ccm kwn hata wao wamechoka na chama chao. Ninakuheshm sana, na pia mchango wko ktk taifa. Kwa sasa sio mda wa kurud nyuma, let's keep the focus, Naamin unalinda utu na kile unachokiamin, ila ccm ni adui zaid! Ninakuhitaj chadema, tunakuhitaj Tanzania, tunakuhitaj chadema!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibark ukawa!
Kutokana na watanzania kunyonywa,kikandamizwa na kutothaminiwa na Nduli CCM kwa takribani miaka 50 sasa ni wakati wa kuiondoa kwenye dola na kusimika dola mpya yenye matumaini.

Ni kweli Baba na mpendwa wetu Dr. Slaa tunajua msinamo wako hasa unapotetea maslahi ya watanzania huna mzaha hata chembe na hurudi nyuma kamwe.

Ombi kwako Dr. Slaa

Tunaomba utusamehe (kama hukuwa umeridhia ujio wa Lowassa na hatimae kupeperusha bendera ya UKAWA ktk uchaguzi mkuu ujao) tuendelee na umoja wetu kama UKAWA maana muda huu tunahitaji Tembo afe bila kujali ameuawa kwa silaha gani iwe riffle sawa,iwe Ak43 sawa,Rpg sawa halafu baaada ya ukombozi tutachagua silaha sahihi kwa tembo atakaejitokeza.

Dr Slaa usione Lowassa tunamuunga mkono ni shauku ya mabadiliko lakini wewe umo mioyoni mwa mamilioni ya watanzania na wana mabadiliko,wewe ndiye umekuwa kiongozi shupavu na shujaa katika siasa za vyama vya siasa Afrika usiyetetereka.

Rudisha roho nyuma,uwe nasi.
 
Mmeanza kumbembeleza. Hayo maneno alipaswa kuongea mwenyekiti wako.mtatizo yule ni DJ Zero
 
nasikia mnataka kumchukua kwa kumhonga bilioni 10, tafadhali hata akiondoka hatakuwa na madhara kwa ukawa kama lowasa alivyoleta madhara kwenu.
 
Yaani kapi la CCM mnaita kifaa? Kweli machadema yamechanganyikiwa na yameishiwa

EL ni silaha haramu lakini ni kali iliyotupwa na jambazi katika kurupushani na wananzengo. Sasa kuna ubaya gani wananzengo kuitumia kummalizia jambazi mwenyewe? Polisi ukiwaita wanachukua masaa kufika kwa sababu wamekula dili na jambazi. Ngoja tumalize jambazi ndipo mambo mengine yafuate.
 
Mada nyingine bhana, eti ungegombea ungeshinda ila tatizo ni kuondoa mfumo, mfumo gani huo? Labda mfumo mpya wa utawala wa Kanda ya kaskazini
 
Acheni unafiki mmemtumia huyu mzee mmetimiza haja yenu kisiasa leo mnaanza kumbembeleza kinafki dr ni muadilifu hawezi kuungana na genge la mafisadi mnaojitahidi kuwapigia magoti kwa tamaa za fedha zao hakika Dr yako pamoja na mungu atamuongoza na hakika mungu atamlipa kadri ya haki yako, hakika chadema haina maisha tena ktk safari ya kisiasa
 
asante mkuu,nami naungana na nyie wote nnao penda limfumo hili lililo feli liondoke! MUNGU akutangulie dr.wetu mzee slaa uwe na hekima km kaweida yk.hivo bc tunaomba muwe wamoja.
 
Sisi tunakupenda sana, na tunajua umeifanyia chadema makubwa na tunajua ulishinda uchaguzi ila walikuibia kura zako. Tunajua hata sasa ungegombea ungeshinda.
Nia ya chadema nini? Jibu ni kuondoa mfumo wa ccm na kama uko tayari basi tunakuomba uwe mvumilivu ili tutumie hii Silaha tuliyoiokota ikiwa imetupwa na maadui zetu ccm tuwauwe wenyewe maana tunajua nia yako ni kutosikia ccm. Tusaidie sisi waja wako tuko nyuma yenu. Mwache EL agombee na tunaomba umsaidie ktk kampeni. Tunajua Ruto wa kenya alikuwa maarufu sana lakini kaamua kumwachia kenyata na mwisho wa siku wakashinda kwa kishindo. MUMGU AKUBARIKI UWE NA HEKIMA KATIKA HILI.



CCM Ni Chama Dola kwa maana halisi ya neno Dola!

 
asante mkuu,nami naungana na nyie wote nnao penda limfumo hili lililo feli liondoke! MUNGU akutangulie dr.wetu mzee slaa uwe na hekima km kaweida yk.hivo bc tunaomba muwe wamoja.

Mtamaliza sala zote, ndiyo Muelewe wanaposema Chama Dola wanamaanisha nini!
 
Hapo ndo mtajua ni kwa nini ccm walimtema lowasa.
Yule ni mroho wa madaraka. Hapo kafuta urais tu na wala hana mapenzi na chadema
 
Back
Top Bottom