Mimi ni mfuasi wako ingawa simo kwenye chama chako. Tangu nikiwa masomoni,nilikuwa nakufuatilia na umekuwa ukinifunza mambo mengi ingawa nilijifunza bila ridhaa yako. Nimekuwa 'nikikuibia' busara zako, uelewa wako,maono yako na ndoto zako juu ya mustakabali wa Tanzania yetu. Kwakuwa umekuwa ukinivutia kimtazamo katika harakati zako za kisiasa,nimekuwa sijifichi kama mfuasi wako hata kutokea nje ya CHADEMA.
Dr. Slaa, tafadhali fanya kila uwezalo ili uwepo kwenye Mhimili mmojawapo wa nchi hii kati ya Serikali au Bunge. Kama uamuzi wako wa busara kuu utakuongoza kutogombea Urais kupitia CHADEMA/UKAWA mwaka huu, tafadhali gombea Ubunge katika jimbo mojawapo hapa Tanzania. Tangu ulipokoma kuwa Mbunge mwaka 2010, pengo lako ndani ya Bunge letu limekuwa wazi na gumu kuzibika.
Bunge lijalo lapaswa kuwa Bunge la kimabadiliko na lenye kuhitaji Wabunge wa aina yako. Litahitaji Wabunge wanaofikiri vyema,kutafiti na kujenga hoja kwa maslahi ya Tanzania yetu. Sifa hizo zote pamoja na nyinginezo unazo na inakupasa ujiunge na Bunge la kiabadiliko. Umeshajenga CHADEMA yenu kwa kiasi cha kutosha na utaendelea kujenga hata ukiwa Bungeni. Bunge lijalo linakuhiaji kwakuwa litakuwa la kitaifa zaidi kuliko la kichama. Tafdhali nisikie.
Aisome: Dr.W.Slaa, Tumaini Makene kwa kumfikishia ujumbe huu Dr. Slaa
Mimi ni mfuasi wako ingawa simo kwenye chama chako. Tangu nikiwa masomoni,nilikuwa nakufuatilia na umekuwa ukinifunza mambo mengi ingawa nilijifunza bila ridhaa yako. Nimekuwa 'nikikuibia' busara zako, uelewa wako,maono yako na ndoto zako juu ya mustakabali wa Tanzania yetu. Kwakuwa umekuwa ukinivutia kimtazamo katika harakati zako za kisiasa,nimekuwa sijifichi kama mfuasi wako hata kutokea nje ya CHADEMA.
Dr. Slaa, tafadhali fanya kila uwezalo ili uwepo kwenye Mhimili mmojawapo wa nchi hii kati ya Serikali au Bunge. Kama uamuzi wako wa busara kuu utakuongoza kutogombea Urais kupitia CHADEMA/UKAWA mwaka huu, tafadhali gombea Ubunge katika jimbo mojawapo hapa Tanzania. Tangu ulipokoma kuwa Mbunge mwaka 2010, pengo lako ndani ya Bunge letu limekuwa wazi na gumu kuzibika.
Bunge lijalo lapaswa kuwa Bunge la kimabadiliko na lenye kuhitaji Wabunge wa aina yako. Litahitaji Wabunge wanaofikiri vyema,kutafiti na kujenga hoja kwa maslahi ya Tanzania yetu. Sifa hizo zote pamoja na nyinginezo unazo na inakupasa ujiunge na Bunge la kiabadiliko. Umeshajenga CHADEMA yenu kwa kiasi cha kutosha na utaendelea kujenga hata ukiwa Bungeni. Bunge lijalo linakuhiaji kwakuwa litakuwa la kitaifa zaidi kuliko la kichama. Tafadhali nisikie.
Aisome: Dr.W.Slaa, Tumaini Makene kwa kumfikishia ujumbe huu Dr. Slaa
Isije kuwa wameisha mdhuru? ili watimize malengo yaoMkuu huu waraka wako ni kama unawakilisha walio wengi. Ikumbukwe kuwa kuna sintofahamu kuhusu shughuli zake ktk chama chao cha CHADEMA. Labda kwa kuongezea ni kwamba, inabidi atueleza yuko wapi maana kwa watu ambao wamekuwa wanamfuatilia inakuwa vigumu kutuliza mioyo bila kujua huyu kipenzi wetu yuko wapi!
tusubiri kimya kingi kina mshindo.. muda rafiki.. tutajua hata dr slaa soon.. porojo nyingi zimesemwa..
Isije kuwa wameisha mdhuru? ili watimize malengo yao
Mkuu nafikiri the same!! sioni UKAWA wakiingia madrakani bila DR.Slaa na watu kukata tamaa!!Bila Slaa tuna kazi ya kujenga upya upinzani....