Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnthebaptist, May 19, 2017.

 1. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 4,012
  Likes Received: 2,266
  Trophy Points: 280
  ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.


  Jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilisambaa taarifa kwamba mwanasiasa huyo ambaye aliondoka nchini baada ya kujiweka kando na chama chake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, angewasili leo nchini.


  “Dk. Slaa ataingia kesho (leo) nchini na kwamba atazungumza na waandishi wa habari saa tano asubuhi,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


  Kutokana na hilo, MTANZANIA ilimtafuta Dk. Slaa kupitia simu yake ya kiganjani akiwa nchini Canada jana, ambapo alieleza kushangazwa na taarifa hizo akisema watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo.


  “Mmmhh! Ninawashangaa! Unajua watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo tena yasiyo ya maana…naomba mpuuze,”alisema Dk. Slaa.


  Pamoja na hilo, MTANZANIA ilimwuliza ni lini atarejea nchini, alisema kwa kifupi: “Nikiwa tayari nitakujulisha wala usijali lakini hizo taarifa ni za uongo,” alisema.


  Mwishoni mwa Machi, mwaka huu, gazeti hili lilifanya mahojiano na Dk. Slaa akiwa Canada ambapo pamoja na mambo mengine, alisema amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.


  “Ni kweli nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea,”alisema Dk. Slaa.


  Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.


  Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

  “Sina tabia ya kuyumbishwa…sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,”alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

  Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.


  Chanzo: Mtanzania gazeti
   
 2. boaz mwalwayo

  boaz mwalwayo JF-Expert Member

  #61
  May 19, 2017
  Joined: Jan 27, 2015
  Messages: 2,912
  Likes Received: 1,688
  Trophy Points: 280
  Utumwa ni Utumwa tu
   
 3. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #62
  May 19, 2017
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 13,067
  Likes Received: 19,897
  Trophy Points: 280
  Uyu mzee na yeye haeleweki kama rafiki yake Lipumbav.
   
 4. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #63
  May 19, 2017
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 10,878
  Likes Received: 10,289
  Trophy Points: 280
  Tetetetetete halina peper

  Swissme
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #64
  May 19, 2017
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 10,357
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Dr. rudi tu maana Prof anakutafuta huku mje muijenge KAFU mpya.
   
 6. R

  Robinhomtoto JF-Expert Member

  #65
  May 19, 2017
  Joined: May 17, 2017
  Messages: 240
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  Mzee huyu alisaliti Manisa katoliki , Alisakiti ndoa yake, Alisaliti Upinzani sasa sijui atasaliti nini
   
 7. Blood of Jesus

  Blood of Jesus JF-Expert Member

  #66
  May 19, 2017
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 620
  Likes Received: 963
  Trophy Points: 180
  Sasa anamwambia nani
   
 8. A

  Al-Watan JF-Expert Member

  #67
  May 19, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 3,576
  Likes Received: 3,486
  Trophy Points: 280
  Umauti utamrudishaje Tanzania?

  Una hakika kwamba hatataka kuzikwa huko nje pia?
   
 9. N'yadikwa

  N'yadikwa JF-Expert Member

  #68
  May 19, 2017
  Joined: Aug 10, 2014
  Messages: 2,360
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  Msaliti mkubwa wa wenzake huyo mzee a baki hukohuko
   
 10. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #69
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 4,012
  Likes Received: 2,266
  Trophy Points: 280
  Atamsaliti Lipumba
   
 11. stranger man

  stranger man JF-Expert Member

  #70
  May 19, 2017
  Joined: Nov 19, 2014
  Messages: 201
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 60
  We a live confortable kamwe hatutishiki its life
   
 12. IROKOS

  IROKOS JF-Expert Member

  #71
  May 19, 2017
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 3,668
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  ....Hata umauti siyo tiketi ya kurudi, wamkumbuka yule gavana wetu mpendwa?
   
 13. mbalizi1

  mbalizi1 JF-Expert Member

  #72
  May 19, 2017
  Joined: Dec 16, 2015
  Messages: 2,704
  Likes Received: 1,446
  Trophy Points: 280
  Mamluki tu nae, hana tofauti na prof bwana yule
   
 14. kipara kipya

  kipara kipya JF-Expert Member

  #73
  May 19, 2017
  Joined: May 2, 2016
  Messages: 1,499
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kifupi unazingua hata ukirudi maisha yapo kasi uliowaacha sio wale tena
   
 15. chishango

  chishango JF-Expert Member

  #74
  May 19, 2017
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 811
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Arudi tuna jambo la kuteta nae...
   
 16. kiumbe kipya

  kiumbe kipya JF-Expert Member

  #75
  May 19, 2017
  Joined: Sep 30, 2016
  Messages: 1,192
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  Yuko sahihi sana na namkubali sana kwa sbb anajua ni nini ataka kifanyike
   
 17. MLA PANYA SWANGA

  MLA PANYA SWANGA JF-Expert Member

  #76
  May 19, 2017
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 867
  Likes Received: 887
  Trophy Points: 180
  Mnafiki huyo.
   
 18. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #77
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 5,796
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Waliompigia simu.
   
 19. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #78
  May 20, 2017
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 1,785
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  His marriage to Josephine wa Watu has been his weakest link in his life...the rest is history
   
Loading...