Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnthebaptist, May 19, 2017 at 8:16 AM.

 1. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017 at 8:16 AM
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 3,941
  Likes Received: 2,169
  Trophy Points: 280
  ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.


  Jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilisambaa taarifa kwamba mwanasiasa huyo ambaye aliondoka nchini baada ya kujiweka kando na chama chake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, angewasili leo nchini.


  “Dk. Slaa ataingia kesho (leo) nchini na kwamba atazungumza na waandishi wa habari saa tano asubuhi,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


  Kutokana na hilo, MTANZANIA ilimtafuta Dk. Slaa kupitia simu yake ya kiganjani akiwa nchini Canada jana, ambapo alieleza kushangazwa na taarifa hizo akisema watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo.


  “Mmmhh! Ninawashangaa! Unajua watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo tena yasiyo ya maana…naomba mpuuze,”alisema Dk. Slaa.


  Pamoja na hilo, MTANZANIA ilimwuliza ni lini atarejea nchini, alisema kwa kifupi: “Nikiwa tayari nitakujulisha wala usijali lakini hizo taarifa ni za uongo,” alisema.


  Mwishoni mwa Machi, mwaka huu, gazeti hili lilifanya mahojiano na Dk. Slaa akiwa Canada ambapo pamoja na mambo mengine, alisema amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.


  “Ni kweli nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea,”alisema Dk. Slaa.


  Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.


  Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

  “Sina tabia ya kuyumbishwa…sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,”alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

  Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.


  Chanzo: Mtanzania gazeti
   
 2. reactionmechanism

  reactionmechanism Member

  #21
  May 19, 2017 at 8:45 AM
  Joined: May 8, 2017
  Messages: 21
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  Hii taarifa n ya kweli jmn....mm Nina mashaka
   
 3. Cannibal OX

  Cannibal OX JF-Expert Member

  #22
  May 19, 2017 at 8:55 AM
  Joined: Aug 27, 2014
  Messages: 885
  Likes Received: 924
  Trophy Points: 180
  Bora asirudi atapata hasira bure maana ile vita dhidi ya ufisadi aliyoiasisi mwenzake wamegeuka na kuanza kukumbatia na kutetea ufisadi kwa nguvu na gharama zote.
   
 4. A

  Al-Watan JF-Expert Member

  #23
  May 19, 2017 at 8:55 AM
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 2,105
  Likes Received: 2,083
  Trophy Points: 280
  Utumwa ni nini?

  Kwa nini mtu akubali kuwa mtumwa popote?

  Kama wananchi wa Arusha wanashindwa kukaa kikao cha msiba na kuwapa rambirambi wenzao bila kuingiliwa na kukamatwa na serikali, huo si utumwa?

  Kwa nini unafikiri mtu akiwa "nchi za watu" , whatever that means, ni lazima kuwa mtumwa?

  Kwa nini kutotaka kuishi katika jamii uliyokulia iwe lazima ni kushindwa?

  Kuna wengine hatushindwi kuishi huko, tumeamua tu.

  Watu wa Syria wanakimbia walipozaliwa.Kuna mauaji. Watu wanauana left, right and center.

  Kukimbia walikokulia ni udhaifu?

  Kuna watu wamesoma na wamezidi level ya challenges zilizopo Tanzania, wametafuta sehemu zenye challenges za level zao.

  Hawa hawajaondoka kwa sababu wameshindwa kuzikabili challenges za Tanzania, hawa wameondoka kwa sababu Tanzania haina challenges za kuufikia uwezo wao.

  Usitake ku simplify mambo kwa akili nyembamba, ukifikiri hivyo hata hii internet utashindwa kuitumia kwa sababu utataka internet iliyogunduliwa na Watanzania.

  Utarudi kuishi mapangoni uishi kama mnyama.
   
 5. b

  bizoheddy Member

  #24
  May 19, 2017 at 8:56 AM
  Joined: May 13, 2017
  Messages: 20
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 5
  Hivi bado yuko na Josephine hahahaha huu ushilawadu sasa
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #25
  May 19, 2017 at 8:57 AM
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 11,718
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana na hilo limbukeni la USA limebakia kupiga picha nyumba na barabara zilizojengwa na wanaume
   
 7. m

  mwakibete JF-Expert Member

  #26
  May 19, 2017 at 9:00 AM
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,079
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Mkuu unamuogopa Mwakyembe nini?? Mbona na wewe kichwa cha habari tu??
   
 8. A

  Akasankara JF-Expert Member

  #27
  May 19, 2017 at 9:00 AM
  Joined: Feb 28, 2015
  Messages: 1,179
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Dr. Mihogo kwenye ubora wake
   
 9. dripu

  dripu Senior Member

  #28
  May 19, 2017 at 9:01 AM
  Joined: Jan 30, 2017
  Messages: 112
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Kaa huko huko huku namba za kirumi ndio tunazisoma tu
   
 10. D

  DomieLe JF-Expert Member

  #29
  May 19, 2017 at 9:02 AM
  Joined: Sep 1, 2016
  Messages: 311
  Likes Received: 269
  Trophy Points: 80
  Wazungu wana msemo unaosema " CHOICE IS A LUXURY"......1. Je Dr Slaa ana makazi decent kwa sasa ya kuishi Tanzania 2.Je Dr Slaa ana cha kufanya hapanchini hata akiurudi?
   
 11. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #30
  May 19, 2017 at 9:06 AM
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 3,941
  Likes Received: 2,169
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa anaona MBALI
   
 12. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #31
  May 19, 2017 at 9:08 AM
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,210
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Chief negotiator wa deal lile la kumng'oa Slaa, alikuwa Josephine Mushumbusi, ndo maana Slaa akapata fungu kubwa.. Tofauti na huyu Lipumba, yeye sisiem wameshamfanya kama mole wao, yuko kwenye payroll yao.. So hana ujanja anytym wakimtuma inabidi akatende tu hicho alichotumwa..
   
 13. M

  Muite JF-Expert Member

  #32
  May 19, 2017 at 9:10 AM
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 481
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Una akili sana. Anasikilizia
   
 14. kashesho

  kashesho JF-Expert Member

  #33
  May 19, 2017 at 9:10 AM
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 4,396
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Duh
   
 15. banned do

  banned do JF-Expert Member

  #34
  May 19, 2017 at 9:11 AM
  Joined: Apr 27, 2017
  Messages: 218
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  Usimtukane Mamba kabla haujavuka mto.
   
 16. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #35
  May 19, 2017 at 9:30 AM
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,335
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Mwanzo alisema hana mpango wa kurejea chadema baadae akasema hana mpango wa kurudi kwenye siasa sasa hivi anasema hana mpango wa kurejea tanzania, sijui mwisho atasema hana mpango wa kurejea wapi.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #36
  May 19, 2017 at 9:40 AM
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 68,840
  Likes Received: 24,169
  Trophy Points: 280
  Watu hata hawajui utumwa ni nini.

  Mtu aliyeenda sehemu kwa hiari yake mwenyewe na ambaye yuko huru atakuwaje mtumwa?

  It doesn't even make sense!
   
 18. Dr. Msafiri

  Dr. Msafiri JF-Expert Member

  #37
  May 19, 2017 at 9:43 AM
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Pengine huyu alipata fedha za kutosha kuendelea kukaa huko kwa muda mrefu ikilinganishwa na aliyerudia Kigali baada ya kukaa kwa siku kadhaa!
   
 19. A

  Al-Watan JF-Expert Member

  #38
  May 19, 2017 at 9:43 AM
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 2,105
  Likes Received: 2,083
  Trophy Points: 280
  Wanakariri sana wakati mambo yanataka kuelewa sana.
   
 20. m

  mwasu JF-Expert Member

  #39
  May 19, 2017 at 9:44 AM
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 7,614
  Likes Received: 5,248
  Trophy Points: 280
  Amejua kabisa upuuzi wa lipumba cuf, hawezi kurudi kuufanya chadema, acha ale hela za wana ccm.
   
 21. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #40
  May 19, 2017 at 9:50 AM
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 68,840
  Likes Received: 24,169
  Trophy Points: 280
  Kumwita Dr. Slaa kuwa ni mtumwa kisa yupo huko alipo kwa hiari yake mwenyewe tena akiwa mtu huru ni kuwatusi wote waliokuwa utumwani!

  Mtu aliyeelimika vizuri kuhusu historia hawezi kutoa kauli za kijinga namna hiyo.

  I mean, watu walipoteza maisha yao wakiwa utumwani, waliobaki wakavuliwa utu wao, wakatumikishwa na mijeledi juu, leo hii eti Dr. Slaa ndo analinganishwa nao?

  With these type of simpletons it will be hard to make any kind of meaningful progress....sad!
   
Loading...