Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnthebaptist, May 19, 2017.

 1. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 10,337
  Likes Received: 8,359
  Trophy Points: 280
  ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.


  Jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilisambaa taarifa kwamba mwanasiasa huyo ambaye aliondoka nchini baada ya kujiweka kando na chama chake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, angewasili leo nchini.


  “Dk. Slaa ataingia kesho (leo) nchini na kwamba atazungumza na waandishi wa habari saa tano asubuhi,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


  Kutokana na hilo, MTANZANIA ilimtafuta Dk. Slaa kupitia simu yake ya kiganjani akiwa nchini Canada jana, ambapo alieleza kushangazwa na taarifa hizo akisema watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo.


  “Mmmhh! Ninawashangaa! Unajua watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo tena yasiyo ya maana…naomba mpuuze,”alisema Dk. Slaa.


  Pamoja na hilo, MTANZANIA ilimwuliza ni lini atarejea nchini, alisema kwa kifupi: “Nikiwa tayari nitakujulisha wala usijali lakini hizo taarifa ni za uongo,” alisema.


  Mwishoni mwa Machi, mwaka huu, gazeti hili lilifanya mahojiano na Dk. Slaa akiwa Canada ambapo pamoja na mambo mengine, alisema amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.


  “Ni kweli nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea,”alisema Dk. Slaa.


  Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.


  Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

  “Sina tabia ya kuyumbishwa…sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,”alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

  Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.


  Chanzo: Mtanzania gazeti
   
 2. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2017
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 18,039
  Likes Received: 19,992
  Trophy Points: 280
  Sawa, yeye akae huko atuache sie na minyoo, malaria na taiphodi zetu.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,322
  Likes Received: 12,828
  Trophy Points: 280
  Ana beep!!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 19, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 77,846
  Likes Received: 39,867
  Trophy Points: 280
  Maisha ni popote pale.

  Canada baby....
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,642
  Likes Received: 16,818
  Trophy Points: 280
  Utumwa.
   
 6. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 12,000
  Likes Received: 14,133
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuwa Tanzania ukawa mtumwa wa Magufuli na ukawa Canada na uhuru zaidi.
   
 7. HOPECOMFORT

  HOPECOMFORT JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2017
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 2,900
  Likes Received: 3,648
  Trophy Points: 280
  Atakuja tu kama sio hai basi umauti uta mrudisha.
   
 8. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2017
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 13,079
  Likes Received: 16,760
  Trophy Points: 280
  Wewe ukirudi bongo hutarudi tena usa kwasababu ya ukimbixi


  Swissme
   
 9. balimar

  balimar JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2017
  Joined: Sep 18, 2015
  Messages: 2,836
  Likes Received: 3,367
  Trophy Points: 280
  East-west home is best
   
 10. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2017
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 13,079
  Likes Received: 16,760
  Trophy Points: 280
  Bora jamaa asirudi tu huku bogo  Swissme
   
 11. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 10,337
  Likes Received: 8,359
  Trophy Points: 280
  Amekimbia uhakiki wa vyeti vya madaktari!
   
 12. Mto_Ngono

  Mto_Ngono JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2017
  Joined: Mar 1, 2017
  Messages: 541
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  Kwa elaaliyopewa kipindi cha uchaguzi wacha akae tu huko
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,642
  Likes Received: 16,818
  Trophy Points: 280
  Heri niwe mtumwa ndani ya nchi yangu kuliko kuwa mtumwa kwenye nchi za watu.

  na kushindwa kuishi ndani ya jamii uliyokulia ni udhaifu ni kwamba huna uwezo wa kupambana na changamoto zinazokuzunguka ukaona afadhali kuzikimbia.
   
 14. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 10,337
  Likes Received: 8,359
  Trophy Points: 280
  Anaogopa ULIPUMBA
   
 15. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2017
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,443
  Likes Received: 3,693
  Trophy Points: 280
  msaliti bora usirudi
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2017
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,955
  Likes Received: 5,786
  Trophy Points: 280
  Ngoja abunye mabilioni yake aliyowapiga chama chakavu. Lile lipropesa fala lilipewa mshiko kiduuuuuchu sasa umekata linabaki kufanyishwa kazi chafu.
   
 17. malamsha shao

  malamsha shao Senior Member

  #17
  May 19, 2017
  Joined: Sep 23, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  You can't run away from challenges,as a scollar you have 2face them
   
 18. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2017
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 20,406
  Likes Received: 43,481
  Trophy Points: 280
  Hata ningekuwa mimi nisingerudi huku uswahilini
   
 19. chipaka.com

  chipaka.com JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2017
  Joined: Dec 5, 2015
  Messages: 2,726
  Likes Received: 1,059
  Trophy Points: 280
  Aje aungane na profesa waendeleze mapambano dhidi ya upinzani,
   
 20. M

  Mkwaruu JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2017
  Joined: Mar 13, 2017
  Messages: 2,490
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kuupata uzeeni lazima upumzike kwani ulikuja wenyewe pasipo hodi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...