Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Sina mpango wa kurudi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnthebaptist, May 19, 2017.

 1. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 9,590
  Likes Received: 7,577
  Trophy Points: 280
  ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.


  Jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilisambaa taarifa kwamba mwanasiasa huyo ambaye aliondoka nchini baada ya kujiweka kando na chama chake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, angewasili leo nchini.


  “Dk. Slaa ataingia kesho (leo) nchini na kwamba atazungumza na waandishi wa habari saa tano asubuhi,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


  Kutokana na hilo, MTANZANIA ilimtafuta Dk. Slaa kupitia simu yake ya kiganjani akiwa nchini Canada jana, ambapo alieleza kushangazwa na taarifa hizo akisema watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo.


  “Mmmhh! Ninawashangaa! Unajua watu wakikosa ajenda hubaki kutunga mambo tena yasiyo ya maana…naomba mpuuze,”alisema Dk. Slaa.


  Pamoja na hilo, MTANZANIA ilimwuliza ni lini atarejea nchini, alisema kwa kifupi: “Nikiwa tayari nitakujulisha wala usijali lakini hizo taarifa ni za uongo,” alisema.


  Mwishoni mwa Machi, mwaka huu, gazeti hili lilifanya mahojiano na Dk. Slaa akiwa Canada ambapo pamoja na mambo mengine, alisema amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.


  “Ni kweli nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea,”alisema Dk. Slaa.


  Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.


  Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

  “Sina tabia ya kuyumbishwa…sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,”alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

  Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.


  Chanzo: Mtanzania gazeti
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #41
  May 19, 2017
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,737
  Trophy Points: 280
  Ana PhD ya Kanoni, amepata shavu la kufundisha Chuo kikuu huko 'kwao'
   
 3. Kadhi Mkuu 1

  Kadhi Mkuu 1 JF-Expert Member

  #42
  May 19, 2017
  Joined: Feb 4, 2015
  Messages: 5,945
  Likes Received: 4,340
  Trophy Points: 280
  Siyo mtumishi wa umma. Unaishi wapi ww??
   
 4. Maoni ya Mzalendo

  Maoni ya Mzalendo Member

  #43
  May 19, 2017
  Joined: Feb 19, 2017
  Messages: 89
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 25
  Ndio mfano mzuri kwa taswira ya ndani ya mioyo ya wanasiasa waliowengi. Watatuchochea kuwa na mihemuko ila wao hawana uwezo wa overcome stress na challenge kubwa. Kila siku wana update visa na kuhakikisha passport ziko vizuri muda wote ili kikinuka watotoroke. Ule upendo kwa watanzania nani kauchukua? Je sie walalahoi ambao hata rangi ya passport hatijui ila kuwa mnatujaza maneno tuwaeleweje wanasiasa?
   
 5. L

  Luggy JF-Expert Member

  #44
  May 19, 2017
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 2,362
  Likes Received: 812
  Trophy Points: 280
  mweee...kwa hiyo zile harakati ilikuwa nguvu ya Fanta?
   
 6. k

  kenyamanyori JF-Expert Member

  #45
  May 19, 2017
  Joined: Feb 9, 2014
  Messages: 722
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 60
  Jamana ni Dr Slaa kasema hayo au mama?
   
 7. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #46
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 9,590
  Likes Received: 7,577
  Trophy Points: 280
  Wewe uko HURU?
   
 8. R

  Rwemiko Member

  #47
  May 19, 2017
  Joined: Oct 3, 2016
  Messages: 16
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 5
  ****** ww kama pumbu za baba yako usije mtaja raisi wetu mpendwa kwa maneno yako ya dharau
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #48
  May 19, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 77,847
  Likes Received: 39,838
  Trophy Points: 280
  Huru kufanya nini?
   
 10. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #49
  May 19, 2017
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,449
  Likes Received: 3,351
  Trophy Points: 280
  Hata maiti yake isirudi ikibidi, alaaa!? Yaani unakubali kupangiwa chumba sheraton na magamba ili uchane chane nguvu ya mabadiliko chanya nchini!! Nilikuchukia na naendelea hivyo
   
 11. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #50
  May 19, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,981
  Likes Received: 14,080
  Trophy Points: 280
  Kuwa huru ni nini?
   
 12. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #51
  May 19, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,981
  Likes Received: 14,080
  Trophy Points: 280
  Matusi ni dalili ya mtu asiye na uwezo wa kiakili kushindea kujieleza vizuri kwa hoja.
   
 13. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #52
  May 19, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 9,590
  Likes Received: 7,577
  Trophy Points: 280
  Kujitegemea kimwilii na KIAKILI
   
 14. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #53
  May 19, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,981
  Likes Received: 14,080
  Trophy Points: 280
  Anayejitegemea kimwili hali.

  Ukishakula tu hujajitegemea kimwili kwa sababu mwili wako umetegemea nishati kutoka nje ya mwili wako.

  Kwa tafsiri yako hiyo, hakuna mtu aliye huru.

  Scientia non domus.
   
 15. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #54
  May 19, 2017
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,458
  Likes Received: 7,383
  Trophy Points: 280
  Maneno ya mkosaji
   
 16. Kelvin X

  Kelvin X JF-Expert Member

  #55
  May 19, 2017
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 899
  Likes Received: 671
  Trophy Points: 180
  Coward
   
 17. Hydrazin

  Hydrazin JF-Expert Member

  #56
  May 19, 2017
  Joined: Oct 3, 2015
  Messages: 231
  Likes Received: 294
  Trophy Points: 80
  survive for fitness, Only strong will exist.
   
 18. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #57
  May 19, 2017
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,978
  Likes Received: 3,519
  Trophy Points: 280
  Dokta ?
   
 19. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #58
  May 19, 2017
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,442
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Amekinai mihogo?
   
 20. T

  Tanzania Njema Yaja JF-Expert Member

  #59
  May 19, 2017
  Joined: Jul 15, 2015
  Messages: 3,059
  Likes Received: 2,121
  Trophy Points: 280
  Aliisha chukua chake mapema *ccm* hy Dr Mihogo aje kufanya nn......
   
 21. m

  mshumbue-soi JF-Expert Member

  #60
  May 19, 2017
  Joined: Aug 28, 2013
  Messages: 1,840
  Likes Received: 786
  Trophy Points: 280
  Mihogo haji kweli kuila tena??
   
Loading...