Licha ya kuchafulia na kubuniwa uwongo wa kila aina, ni wazi kuwa Dr Slaa amejipatia umaarufu mkubwa kisiasa. Anaonekana ni mtu asiyeteteleka katika kusimamia 'principles' zake. Kama anaamini haki haikutendeka ataendelea kuamini haki haikutendeka mapaka pale atakapoona inatendeka na si vinginevyo.
Msimamo kama huu ni muhimu sana na unatoa fundisho muhimu kwa watu vigeugeu. Kinachowavutia wananchi kumwamini Dr Slaa ni ushujaa wake - kutoogopa kuwa matatani wakati akitetea maslahi ya Watanzania. Najua Watanzania tulio wengi ni waoga na pia wanafiki na inapotokea mtu anajitoa kutetea maslahi ya wengi hata kama akinenwa vibaya na washindani wake anakuwa bado hajapoteza umaarufu wake.
Watu wote maarufu duniani walikutana na matatizo mengi sana ya kuundiwa uwongo na kilichowafanya waheshimiwe ni ule moyo wao wa kutoteteleka. Na hili ndilo linalonivutia hata kwa Dr Slaa. Baadhi ya watu wanasema akubali kushindwa - lakini Dr Slaa hajakataa kushindwa bali anachotaka kuonesha ni kwamba ili akubali kushindwa ni lazima ionekane ameshindwa kilalali na siyo ushindi unaotokana na udanganyifu na kupindisha matokeo. Mtu yeyote anayekubali kushindwa pale anapojua mbinu chafu zimetumika kumpata mshindi anakuwa anasaidia kuendeleza vitendo vya udanganyifu na kutotendeka kwa haki.
Naungana na Dr Slaa kutokubali matokeo ya udanganyifu na aenedelee kuyapinga ila kwa kutumia njia za amani (peaceful means). Tunachotaka Watanzania ni kujenga taifa la wawajibikaji na siyo la walaghai. Ulaghai usikubalike kabisa! Nampongeza Dr Slaa kwa msimamo wake na aendelee kutetea maslahi ya Watanzania na kuwafungua macho ili waone yale anaoyoyaamini na kuyasimamia - maendeleo ya Watanzania.
Huu ni mfano mfu kabisa, sikujua kama na wewe una low level ya kufikiria kiasi hicho. Hv unaweza kushabihisha kuibiwa shati na wizi wa kura anao dai slaaa? ni vitu tofauti kabisa.
..........Na mwisho tukitumia vigezo vyote vya elimu Slaa kasoma kuliko Kikwete kawanini ashindwe kuongoza iwapo kichwa maji Kikwete ni Rais, huyu Rais anatutia aibu sana akija America rafiki yangu mmoja mnigeria liniuliza huyu kweli ni Rais? nikamuuliza kwanini? akasema mbona hawezi kujenga hoja na kujieleza kwa kiingereza kasoma kweli nikamjubu sisis Tanzania tunatumia kiswahili, kiingereza si sana akasema lakinii huyu si ana shahada ya uchumi kasoma chuo kikuu kwani alikuwa anatumia kiswahili kuandika paper? Nilikosa jibu lakini nilikuwa na jibu kichwani kuwa rais Kikwete ni mweupe uzuri wa sura tu darasani hakuna kitu, haya yaliwahi kusemwa na Lipumba kuwa walipokuwa shule Kikwete alikuwa mbabaishaji na mtu wa mizaha
Kweli nimeamini JF siku hizi inapoteza mwelekeo na imevamiwa, yaani hata wale wenye elimu ya darasa la pili c kama wewe unaingia humu na kuchangia pumba kiasi hicho..Hizo stori zenu mnazojazwa huko kwenye vijiwe vya kahawa msiwe mnatuletea humu kwani humu twahitaji watu wenye upeo wa kufikiri na kuchambua mambo vya vielelezo sahihi.Ninaadika kwa masikitiko kwasababu mwanzoni nilikuwa nadhani Dr. Slaa ni kiongozi imara, nimegundua kuwa kumbe ni mbabaishaji na anajiharibia kazi yote aliyo ifanya katika kampeni yake. Nilikuwa sikubaliani na sera zake lakini niliona kuwa anakitiia changamoto CCM.
Lakini kwa haya anayo yafanya na kuongea sasa baada ya matokeo inanibidi nibadili muono nilio kuwa nao kwake. Dr. Slaa ana mawazo mufilisi na uchu wa uongozi ndio maana ana lalama kuonewa. Waswahili walisema kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani. Katika uwanja wa siasa, au mahali popote huwezi kutoa malalamiko ya uzushi uzushi tu.
Kura zote zimehesabiwa palepale jimboni na mbele ya wakala wake. Kuna wakala aliye dhihirisha kuwa kura zake zimeibiwa ?
Kwa fikira zake inadhihirisha kuwa Dr. Slaa ni mtu hatari sana na anaonyesha haja wiva kimawazo na anaeta siasa na kuigaiga (toka nchi zajirani) na kuropoka kama vile Lyatonga Mrema alivyo jipotezea umaarufu wake nchini (sikuhizi Lyatonga ni kama "The Comedy " Nobody takes him serious. Dr. Slaa anajiharibia hata sisi wengine tulio mpigia kura tunasikitika. Ninajuta kumpa kura yangu na itabidi hawa wagombea wanao jichomoza chomoza kuwa angalia sana.
Hivi Dr. Slaa alikuwa amechanjia kwamba mwaka huu lazima awe raisi wa jamuhuri ya Tanzania ? Hata kama kura alizopigiwa hazitoshi ? Ni kiumbe gani huyu, alafu eti alikuwa awe raisi ? Sasa hebu imagine mtu kama huyu alivyo na uchu awe raisi... it will be worse than what we complain of what CCM is doing
Mungu ashukuriwe na sala za kuiombea nchi yetu ziendelee kila siku. Tumeepukana na janga la watu kama Dr. Slaa.
Hii inadhihirisha kuwa upinzani unayo kazi kubwa ya kufanya ili kuaminika na wananchi. Jimbo la Mbulu kwenyewe anakotoka Slaa hakupata kura zote, wamegawana na JK. Inaonyesha hata watu jimboni kwake wasivyo muamini.
Mungu ibariki Tanzania
Acha weweeee, hoja ipi ya kujibu hapoo? Huo upupu mliomwaga hapo ndio unasema ni hoja ya kujadili? Kwa hali tuliyonayo sasa Tanzania tukiwa na watu wenye upeo mfupi wa kufikiri kama nyie tutadidimia zaidi. Kama wewe ni mmoja wa hao unaosema ni Great Thinkers basi JF imepoteza thamani yake kabisa.umepata nini sasa?? huo ndio unazi, ungekua wa maana ungejibu hoja kwa hoja na sio kuita wenzio wapumbavu kisa unatafoatiana nao mtazamo..
use ur head bro, dis is JF home of Great Thinkers!!!