Dr. Slaa ni mbabaishaji na hafai kuwa kiongozi ?

venividivici

Member
Dec 30, 2006
19
0
Ninaadika kwa masikitiko kwasababu mwanzoni nilikuwa nadhani Dr. Slaa ni kiongozi imara, nimegundua kuwa kumbe ni mbabaishaji na anajiharibia kazi yote aliyo ifanya katika kampeni yake. Nilikuwa sikubaliani na sera zake lakini niliona kuwa anakitiia changamoto CCM.

Lakini kwa haya anayo yafanya na kuongea sasa baada ya matokeo inanibidi nibadili muono nilio kuwa nao kwake. Dr. Slaa ana mawazo mufilisi na uchu wa uongozi ndio maana ana lalama kuonewa. Waswahili walisema kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani. Katika uwanja wa siasa, au mahali popote huwezi kutoa malalamiko ya uzushi uzushi tu.

Kura zote zimehesabiwa palepale jimboni na mbele ya wakala wake. Kuna wakala aliye dhihirisha kuwa kura zake zimeibiwa ?

Kwa fikira zake inadhihirisha kuwa Dr. Slaa ni mtu hatari sana na anaonyesha haja wiva kimawazo na anaeta siasa na kuigaiga (toka nchi zajirani) na kuropoka kama vile Lyatonga Mrema alivyo jipotezea umaarufu wake nchini (sikuhizi Lyatonga ni kama "The Comedy " Nobody takes him serious. Dr. Slaa anajiharibia hata sisi wengine tulio mpigia kura tunasikitika. Ninajuta kumpa kura yangu na itabidi hawa wagombea wanao jichomoza chomoza kuwa angalia sana.

Hivi Dr. Slaa alikuwa amechanjia kwamba mwaka huu lazima awe raisi wa jamuhuri ya Tanzania ? Hata kama kura alizopigiwa hazitoshi ? Ni kiumbe gani huyu, alafu eti alikuwa awe raisi ? Sasa hebu imagine mtu kama huyu alivyo na uchu awe raisi... it will be worse than what we complain of what CCM is doing

Mungu ashukuriwe na sala za kuiombea nchi yetu ziendelee kila siku. Tumeepukana na janga la watu kama Dr. Slaa.

Hii inadhihirisha kuwa upinzani unayo kazi kubwa ya kufanya ili kuaminika na wananchi. Jimbo la Mbulu kwenyewe anakotoka Slaa hakupata kura zote, wamegawana na JK. Inaonyesha hata watu jimboni kwake wasivyo muamini.

Mungu ibariki Tanzania
 
Nafurahi sana kujua km kuna watu wanaona ujinga wa huyu Dr Silaha. Kususa kwa kwenda kwenye matokeo ya mwisho ni ushamba, tangu lini wanaume wanasusa. ? na tangu lini mtu anataka ushindani wakati hataki kushindwa.? kama kweli yeye ni mwanaume wa kweli akubari matokeo, na ingetokea jamaa akashinda Dr. Slaa angekuwa Rais wa milele.
 
Wewe ni mshirika wa dini ya mashetani nini? Hiyo avatar yako , mhhhh!
 
:A S cry:nadhani unamawazo finyu na mtazamo hasi kwa kupenda chama chako cha ccm. ndo maana unachangia na kutoa mawazo finyu yasio na maana juu ya Dr slaa.
 
Hivi hili neno kukimbilia madaraka mnalichambuaje kati ya Kikwete na Slaa nani ni mkimbilia madaraka? Kikwete alikuwa mbunge wa miaka tisa tayari akajitosa kuwania urais wa Tanzania wakati Dk Slaa alikuwa mbunge wa miaka kumi na tano akajitosa kuwania urais kati ya hawa yupi aliwahi mapema? Msiwe mnaongea kwa kutumia maongezi ya kwenye kahawa mwaga data si maneno.

Nani kakwambia kura za Urais zilikuwa zinatundikwa jimboni? Unaona mnaorukia hoja ambazo si zenu kura za rais NEC ilikataa toka mwazo kuwa hazitawekwa kwenye jimbo la uchaguzi isipokuwa zitasomwa makao makuu huo ndio uchakachuaji wa kura zenyewe pili mawakala wa CHADEMA na vyama vingine kule Mbozi, Kilombero, Shinyanga Mjini, Tarime, Geita, Busanda, Kigoma Mjini, Sumbawanga mjini, Mpanda,Segerea, Kigamboni, Kishapu, Karagwe, Mbeya vijijini na maeneo mengine mengi hawakusaini matokeo na bado tume ya uchaguzi imetangaza wabunge wale wameshinda, swali ni kwamba iwapo wameshinda kihalali kwanini wanalindwa na polisi? kama si uchakachuaji ni nini?

Tatu inakuwaje NEC watangaze kwanza matokeo ya Urais katika majimbo ambayo CCM imefanya vizuri kwanza na kuruka maeneo ambayo tayari yalishatangaza wabunge hata kama ni ya wa upinzani kwa mfano by tarehe 2 mwezi wa kumi na moja tayari Mwanza walishatangaza wabunge wao lakini kura za urais kutoka Mwanza zilitangazwa tarehe 4 wakati Mtwara walitangaza kura za ubunge tarehe 4 na kura za urais siku hiyohiyo kwa sababu tu mgombea aliyeshinda mtwara ni wa CCM na walioshinda Mwanza ni wa Upinzani CHADEMA.

Na mwisho tukitumia vigezo vyote vya elimu Slaa kasoma kuliko Kikwete kawanini ashindwe kuongoza iwapo kichwa maji Kikwete ni Rais, huyu Rais anatutia aibu sana akija America rafiki yangu mmoja mnigeria liniuliza huyu kweli ni Rais? nikamuuliza kwanini? akasema mbona hawezi kujenga hoja na kujieleza kwa kiingereza kasoma kweli nikamjubu sisis Tanzania tunatumia kiswahili, kiingereza si sana akasema lakinii huyu si ana shahada ya uchumi kasoma chuo kikuu kwani alikuwa anatumia kiswahili kuandika paper? Nilikosa jibu lakini nilikuwa na jibu kichwani kuwa rais Kikwete ni mweupe uzuri wa sura tu darasani hakuna kitu, haya yaliwahi kusemwa na Lipumba kuwa walipokuwa shule Kikwete alikuwa mbabaishaji na mtu wa mizaha
 
Humtendei haki Dr. Slaa. umekuja kupiga propaganda tu. Kura rais hazikuhesabiwa jimboni. kama hujui kilichokuwa kinafanyika uwaulize wahusika. Kama yaliyokuwa yanatukia ulikuwa unayasikia kwenye vyombo basi tunakupa pole
 
Duu watu wa ccm hamtarithi kingine ktk ulimwengu huu bali ni MIPASHO TU kama mkwere mwenzenu. Hivi mnaelewa kilichokuwa nyuma ya pazia ktk uchaguzi huu? Hamjui kuwa upinzani walikuwa wameshinda pote (Tanganyika na Zanzibar) kama sio hujuma na uchakachuaji?! Nyerere alipigania Watanzania waondoe ujinga na umasikini lakin leo hii mpo nyie ambao hamjaelimika kila kitu kwenu ndio mzee!!! Ccm wamechakachua na Dk. Slaa ni mtu makini na hakurupuki kama wewe, viongozi wenu wa ccm wanaaibu coz chama kinawafia mikononi mwao.
 
1) Hakuna ushahidi wa kura kuibiwa (ndio maana nasema huu ni ubabaishaji na uzushi). Tatizo ni kwamba watanzania tunapenda sana majungu, uzushi, umbeya baseless. Just because he was met by big crowds in campagn meeting haimaanishi kuwa zile ni kura - Unajuaje watu walikuja kusikiliza anachosema alafu wameamua vinginevyo
2) Nani kasema ukisoma sana ndio unakuwa kiongozi mzuri - Going to school is necessary but not a sufficient condition/qualification kuwa kiongozi bora. Hata mimi nataka CCM waondoke lakini Dr. Slaa is using a wrong strategy - He is being overzealous about kuwa Raisi. Nimekuwa disappointed sana na huyu jamaa ana mambo ya kuiga. That is why I am taking this position.
 
Kura zote zimehesabiwa palepale jimboni na mbele ya wakala wake. Kuna wakala aliyedhihirisha kuwa kura zake zimeibiwa.

Hapo ndo ulipoteleza mkuu kwa upande wangu na unapaswa uache ushabiki wa chama kuwa objective bse Slaa kasema ataongea kesho na ataenda mahakamani sasa unadhani ni ushaidi gani ataupeleka kama sio wa kutoka kwa mawakala.

Kura za NEC na Majimboni hazi-tally na mawakala ndo mashaidi.

Muache unazi jamani jaribu kuwa objective na je kama kura zimehesabiwa jimboni kwa nini zitangazwe na NEC tena zingine zikiwa zimebadilishwaaaaaaaaaaaa
 
We unamuona Slaa janga! Subiri janga lenyewe! Yaani kuna watu wanaandikaga mapovu humu ndani yaani wananichosha! Wazembe wa kufikiri na hii miaka mitano mtakula jeuri yenu!
 
Napenda sana Mtu asiye na UNAFIKI.

Kama wewe umeniibia Shati langu na ninajua kuwa umeniibia na wewe unajua kama umeniibia, sina haja ya kujigonga gonga kwako na kushikana na kukumbatiana wakati Moyoni najua umeniibia kitu changu. Huo ni Unafiki.

Kama nimechukia kwa kuwa umeniibia nitafanya kila njia ujue kuwa kweli nimechukia.

Tuone kama Hilo Shati langu uliloniibia utakaa nali kwa Amani kwa miaka mitano!

Nakuambia kila saa utakuwa unageuka nyuma kwa wasiwasi kwamba ninapanga mkakati fulani dhidi yako na hutakuwa na amani kamwe.

Nimeipenda hii ya Dk Slaa ya kutojigonga gonga kwa mtu.

Kama mbwai, mmbwai tu. Dr Slaa Uzi huo huo. Hakuna kushikana Mikono na Vibaka wa Kijani eti kwa kisingizio cha kudumisha Amani yetu. IPI??????????????
 
Hivi hili neno kukimbilia madaraka mnalichambuaje kati ya Kikwete na Slaa nani ni mkimbilia madaraka? Kikwete alikuwa mbunge wa miaka tisa tayari akajitosa kuwania urais wa Tanzania wakati Dk Slaa alikuwa mbunge wa miaka kumi na tano akajitosa kuwania urais kati ya hawa yupi aliwahi mapema? Msiwe mnaongea kwa kutumia maongezi ya kwenye kahawa mwaga data si maneno.

Nani kakwambia kura za Urais zilikuwa zinatundikwa jimboni? Unaona mnaorukia hoja ambazo si zenu kura za rais NEC ilikataa toka mwazo kuwa hazitawekwa kwenye jimbo la uchaguzi isipokuwa zitasomwa makao makuu huo ndio uchakachuaji wa kura zenyewe pili mawakala wa CHADEMA na vyama vingine kule Mbozi, Kilombero, Shinyanga Mjini, Tarime, Geita, Busanda, Kigoma Mjini, Sumbawanga mjini, Mpanda,Segerea, Kigamboni, Kishapu, Karagwe, Mbeya vijijini na maeneo mengine mengi hawakusaini matokeo na bado tume ya uchaguzi imetangaza wabunge wale wameshinda, swali ni kwamba iwapo wameshinda kihalali kwanini wanalindwa na polisi? kama si uchakachuaji ni nini?

Tatu inakuwaje NEC watangaze kwanza matokeo ya Urais katika majimbo ambayo CCM imefanya vizuri kwanza na kuruka maeneo ambayo tayari yalishatangaza wabunge hata kama ni ya wa upinzani kwa mfano by tarehe 2 mwezi wa kumi na moja tayari Mwanza walishatangaza wabunge wao lakini kura za urais kutoka Mwanza zilitangazwa tarehe 4 wakati Mtwara walitangaza kura za ubunge tarehe 4 na kura za urais siku hiyohiyo kwa sababu tu mgombea aliyeshinda mtwara ni wa CCM na walioshinda Mwanza ni wa Upinzani CHADEMA.

Na mwisho tukitumia vigezo vyote vya elimu Slaa kasoma kuliko Kikwete kawanini ashindwe kuongoza iwapo kichwa maji Kikwete ni Rais, huyu Rais anatutia aibu sana akija America rafiki yangu mmoja mnigeria liniuliza huyu kweli ni Rais? nikamuuliza kwanini? akasema mbona hawezi kujenga hoja na kujieleza kwa kiingereza kasoma kweli nikamjubu sisis Tanzania tunatumia kiswahili, kiingereza si sana akasema lakinii huyu si ana shahada ya uchumi kasoma chuo kikuu kwani alikuwa anatumia kiswahili kuandika paper? Nilikosa jibu lakini nilikuwa na jibu kichwani kuwa rais Kikwete ni mweupe uzuri wa sura tu darasani hakuna kitu, haya yaliwahi kusemwa na Lipumba kuwa walipokuwa shule Kikwete alikuwa mbabaishaji na mtu wa mizaha

tz inawataka watu wenye akili km wewe unayefatilia mambo.co m2 amekurupuka2 kaanza kumponda dr slaa.mi nadhan huyu mtoa hoja ni mwanamke mnafik,yan we uibiwe na ufaham uibiwe halaf uende ukampongeze aliyekuibia! Dr angeenda kumpongeza mkwere jana,mim na ukoo wangu wote tungejutia kumpgia kura,na automaticaly wangekua wamekosa kura zetu 2015
 
Waungwana;

Kwa nini kwanza msimpe nafasi Dr. Slaa kesho atoe maelezo yake ndiyo tujadadili? Kuna mahali hapa JF nimesoma kuwa eti hata Karatu ambayo ni ngome ya Dr. Slaa amepata kura 47 tu wakati JK kapata zaidi ya 20,000. Cha ajabu zaidi Mbunge alyechaguliwa ni wa CHADEMA. Mziray na Lipumba wote wamepata kura zaidi kuliko Dr. Slaa. Unless kama Mwananchi ambao ndiyo source ya hiyo habari walikosea.
 
Inasikitisha sana. Yani sijui nionyeshe vipi kusikitishwa kwangu.

Dk slaa, wewe ni rais ndani ya URT ambaye huhitaji vyombo vya dola bali people's power! Waache majuha na wafitini wajipongeze kwani wakati utafika. Eti jk kaapa atailinda katiba na kutawala bila chuki... Wakati utafika tu
 
Wanamapinduzi, hoja kama hizi hakuna haja ya kuhangaika nazo. Ni taaHira tu au fisadi au asiyejua mbele na nyuma anamchagua JK na CCM.

Leo bei zinapaa na mtajua Dr. Slaa alikuwa anasema nini. Mafuta ya kula ndani ya wiki 2 yamepanda toka elf 2 hadi 3 kwa lita. Na bado mtajuta. Haya ni maafa. Dr anachosema ni kwamba matokeo ya NEC hayana uhusiano na kura zilizopigwa.

Amefanya vyema kutohalalisha huu uhuni na mzaha wa JK na watu wake.
 
1) Hakuna ushahidi wa kura kuibiwa (ndio maana nasema huu ni ubabaishaji na uzushi). Tatizo ni kwamba watanzania tunapenda sana majungu, uzushi, umbeya baseless. Just because he was met by big crowds in campagn meeting haimaanishi kuwa zile ni kura - Unajuaje watu walikuja kusikiliza anachosema alafu wameamua vinginevyo 2) Nani kasema ukisoma sana ndio unakuwa kiongozi mzuri - Going to school is necessary but not a sufficient condition/qualification kuwa kiongozi bora. Hata mimi nataka CCM waondoke lakini Dr. Slaa is using a wrong strategy - He is being overzealous about kuwa Raisi. Nimekuwa disappointed sana na huyu jamaa ana mambo ya kuiga. That is why I am taking this position.
Shame on you!
 
Ninaadika kwa masikitiko kwasababu mwanzoni nilikuwa nadhani Dr. Slaa ni kiongozi imara, nimegundua kuwa kumbe ni mbabaishaji na anajiharibia kazi yote aliyo ifanya katika kampeni yake. Nilikuwa sikubaliani na sera zake lakini niliona kuwa anakitiia changamoto CCM.
Kura zote zimehesabiwa palepale jimboni na mbele ya wakala wake. Kuna wakala aliye dhihirisha kuwa kura zake zimeibiwa

Hivi Dr. Slaa alikuwa amechanjia kwamba mwaka huu lazima awe raisi wa jamuhuri ya Tanzania ? Hata kama kura alizopigiwa hazitoshi ? Ni kiumbe gani huyu, alafu eti alikuwa awe raisi ? Sasa hebu imagine mtu kama huyu alivyo na uchu awe raisi... it will be worse than what we complain of what CCM is doing

Mungu ashukuriwe na sala za kuiombea nchi yetu ziendelee kila siku. Tumeepukana na janga la watu kama Dr. Slaa.

Hii inadhihirisha kuwa upinzani unayo kazi kubwa ya kufanya ili kuaminika na wananchi. Jimbo la Mbulu kwenyewe anakotoka Slaa hakupata kura zote, wamegawana na JK. Inaonyesha hata watu jimboni kwake wasivyo muamini.

Mungu ibariki Tanzania

Mr. Veni Vidi Vici
To prove what and who you are.Repeat reading your rubbish marked in red mark!!!!
I can gues or predict that you must be one of those CCM VIHIYO elect MPs or SHUSHUSHU/UWT if not a CCM fan. mhe. umeongea pumba kiasi kwamba unaonyesha wewe ni wale jamaa huwa tunasema wana IQ ya kuku!

Waandishi wa habari wana msemo:NO FACTS,NO RIGHT TO SPEAK!!!
Hivi ni lini Dr.Slaa alikuwa mbunge wa Mbulu???Dr. Slaa amekuwa Mbunge wa Karatu for 15 solid years na Karatu sasa hivi imechululiwa na CHADEMA na MB Mteule Mch.Israel Yohana aliyepata KURA 41,132 zidi ya CCM waliopata 26,281. Je, unategemea hapa Kikwete apate kura ngapi na Dr. Slaa apate ngapi????Kusema Dr. Slaa hawamwamini jimboni kwake ni umbeya na uzushi wa kike!!!

Ukija jimbo la Mbulu ulilompachika Dr. Slaa CHADEMA imelichukua kupitia MB Mteule Mustapha Akoonay kura 48,428 dhidi ya CCM kura 26,281 alizopata Philip Marmo ambaye nasikia amelazwa kwa BP! Kwa hiyo hapa kwa uchakachuaji wako na CCM unategemea Dr.Slaa alipata ngapi na Kiwete wako mlimpa ngapi??
 
Ninaadika kwa masikitiko kwasababu mwanzoni nilikuwa nadhani Dr. Slaa ni kiongozi imara, nimegundua kuwa kumbe ni mbabaishaji na anajiharibia kazi yote aliyo ifanya katika kampeni yake. Nilikuwa sikubaliani na sera zake lakini niliona kuwa anakitiia changamoto CCM.

Lakini kwa haya anayo yafanya na kuongea sasa baada ya matokeo inanibidi nibadili muono nilio kuwa nao kwake. Dr. Slaa ana mawazo mufilisi na uchu wa uongozi ndio maana ana lalama kuonewa. Waswahili walisema kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani. Katika uwanja wa siasa, au mahali popote huwezi kutoa malalamiko ya uzushi uzushi tu.

Kura zote zimehesabiwa palepale jimboni na mbele ya wakala wake. Kuna wakala aliye dhihirisha kuwa kura zake zimeibiwa ?

Kwa fikira zake inadhihirisha kuwa Dr. Slaa ni mtu hatari sana na anaonyesha haja wiva kimawazo na anaeta siasa na kuigaiga (toka nchi zajirani) na kuropoka kama vile Lyatonga Mrema alivyo jipotezea umaarufu wake nchini (sikuhizi Lyatonga ni kama "The Comedy " Nobody takes him serious. Dr. Slaa anajiharibia hata sisi wengine tulio mpigia kura tunasikitika. Ninajuta kumpa kura yangu na itabidi hawa wagombea wanao jichomoza chomoza kuwa angalia sana.

Hivi Dr. Slaa alikuwa amechanjia kwamba mwaka huu lazima awe raisi wa jamuhuri ya Tanzania ? Hata kama kura alizopigiwa hazitoshi ? Ni kiumbe gani huyu, alafu eti alikuwa awe raisi ? Sasa hebu imagine mtu kama huyu alivyo na uchu awe raisi... it will be worse than what we complain of what CCM is doing

Mungu ashukuriwe na sala za kuiombea nchi yetu ziendelee kila siku. Tumeepukana na janga la watu kama Dr. Slaa.

Hii inadhihirisha kuwa upinzani unayo kazi kubwa ya kufanya ili kuaminika na wananchi. Jimbo la Mbulu kwenyewe anakotoka Slaa hakupata kura zote, wamegawana na JK. Inaonyesha hata watu jimboni kwake wasivyo muamini.

Mungu ibariki Tanzania

Ni maneno ya busara na hekima, hongera sana . Wewe ni mmoja wa GOODTHINKER AISEE !
 
If you think you are big tree we are small to cut you down.

DR.SLAA ni makini kuliko hoa mafisadi unaowanadi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom