venividivici
Member
- Dec 30, 2006
- 19
- 0
Nafurahi sana kujua km kuna watu wanaona ujinga wa huyu Dr Silaha. Kususa kwa kwenda kwenye matokeo ya mwisho ni ushamba, tangu lini wanaume wanasusa. ? na tangu lini mtu anataka ushindani wakati hataki kushindwa.? kama kweli yeye ni mwanaume wa kweli akubari matokeo, na ingetokea jamaa akashinda Dr. Slaa angekuwa Rais wa milele.
Hivi hili neno kukimbilia madaraka mnalichambuaje kati ya Kikwete na Slaa nani ni mkimbilia madaraka? Kikwete alikuwa mbunge wa miaka tisa tayari akajitosa kuwania urais wa Tanzania wakati Dk Slaa alikuwa mbunge wa miaka kumi na tano akajitosa kuwania urais kati ya hawa yupi aliwahi mapema? Msiwe mnaongea kwa kutumia maongezi ya kwenye kahawa mwaga data si maneno.
Nani kakwambia kura za Urais zilikuwa zinatundikwa jimboni? Unaona mnaorukia hoja ambazo si zenu kura za rais NEC ilikataa toka mwazo kuwa hazitawekwa kwenye jimbo la uchaguzi isipokuwa zitasomwa makao makuu huo ndio uchakachuaji wa kura zenyewe pili mawakala wa CHADEMA na vyama vingine kule Mbozi, Kilombero, Shinyanga Mjini, Tarime, Geita, Busanda, Kigoma Mjini, Sumbawanga mjini, Mpanda,Segerea, Kigamboni, Kishapu, Karagwe, Mbeya vijijini na maeneo mengine mengi hawakusaini matokeo na bado tume ya uchaguzi imetangaza wabunge wale wameshinda, swali ni kwamba iwapo wameshinda kihalali kwanini wanalindwa na polisi? kama si uchakachuaji ni nini?
Tatu inakuwaje NEC watangaze kwanza matokeo ya Urais katika majimbo ambayo CCM imefanya vizuri kwanza na kuruka maeneo ambayo tayari yalishatangaza wabunge hata kama ni ya wa upinzani kwa mfano by tarehe 2 mwezi wa kumi na moja tayari Mwanza walishatangaza wabunge wao lakini kura za urais kutoka Mwanza zilitangazwa tarehe 4 wakati Mtwara walitangaza kura za ubunge tarehe 4 na kura za urais siku hiyohiyo kwa sababu tu mgombea aliyeshinda mtwara ni wa CCM na walioshinda Mwanza ni wa Upinzani CHADEMA.
Na mwisho tukitumia vigezo vyote vya elimu Slaa kasoma kuliko Kikwete kawanini ashindwe kuongoza iwapo kichwa maji Kikwete ni Rais, huyu Rais anatutia aibu sana akija America rafiki yangu mmoja mnigeria liniuliza huyu kweli ni Rais? nikamuuliza kwanini? akasema mbona hawezi kujenga hoja na kujieleza kwa kiingereza kasoma kweli nikamjubu sisis Tanzania tunatumia kiswahili, kiingereza si sana akasema lakinii huyu si ana shahada ya uchumi kasoma chuo kikuu kwani alikuwa anatumia kiswahili kuandika paper? Nilikosa jibu lakini nilikuwa na jibu kichwani kuwa rais Kikwete ni mweupe uzuri wa sura tu darasani hakuna kitu, haya yaliwahi kusemwa na Lipumba kuwa walipokuwa shule Kikwete alikuwa mbabaishaji na mtu wa mizaha
Shame on you!1) Hakuna ushahidi wa kura kuibiwa (ndio maana nasema huu ni ubabaishaji na uzushi). Tatizo ni kwamba watanzania tunapenda sana majungu, uzushi, umbeya baseless. Just because he was met by big crowds in campagn meeting haimaanishi kuwa zile ni kura - Unajuaje watu walikuja kusikiliza anachosema alafu wameamua vinginevyo 2) Nani kasema ukisoma sana ndio unakuwa kiongozi mzuri - Going to school is necessary but not a sufficient condition/qualification kuwa kiongozi bora. Hata mimi nataka CCM waondoke lakini Dr. Slaa is using a wrong strategy - He is being overzealous about kuwa Raisi. Nimekuwa disappointed sana na huyu jamaa ana mambo ya kuiga. That is why I am taking this position.
Ninaadika kwa masikitiko kwasababu mwanzoni nilikuwa nadhani Dr. Slaa ni kiongozi imara, nimegundua kuwa kumbe ni mbabaishaji na anajiharibia kazi yote aliyo ifanya katika kampeni yake. Nilikuwa sikubaliani na sera zake lakini niliona kuwa anakitiia changamoto CCM.
Kura zote zimehesabiwa palepale jimboni na mbele ya wakala wake. Kuna wakala aliye dhihirisha kuwa kura zake zimeibiwa
Hivi Dr. Slaa alikuwa amechanjia kwamba mwaka huu lazima awe raisi wa jamuhuri ya Tanzania ? Hata kama kura alizopigiwa hazitoshi ? Ni kiumbe gani huyu, alafu eti alikuwa awe raisi ? Sasa hebu imagine mtu kama huyu alivyo na uchu awe raisi... it will be worse than what we complain of what CCM is doing
Mungu ashukuriwe na sala za kuiombea nchi yetu ziendelee kila siku. Tumeepukana na janga la watu kama Dr. Slaa.
Hii inadhihirisha kuwa upinzani unayo kazi kubwa ya kufanya ili kuaminika na wananchi. Jimbo la Mbulu kwenyewe anakotoka Slaa hakupata kura zote, wamegawana na JK. Inaonyesha hata watu jimboni kwake wasivyo muamini.
Mungu ibariki Tanzania
Ninaadika kwa masikitiko kwasababu mwanzoni nilikuwa nadhani Dr. Slaa ni kiongozi imara, nimegundua kuwa kumbe ni mbabaishaji na anajiharibia kazi yote aliyo ifanya katika kampeni yake. Nilikuwa sikubaliani na sera zake lakini niliona kuwa anakitiia changamoto CCM.
Lakini kwa haya anayo yafanya na kuongea sasa baada ya matokeo inanibidi nibadili muono nilio kuwa nao kwake. Dr. Slaa ana mawazo mufilisi na uchu wa uongozi ndio maana ana lalama kuonewa. Waswahili walisema kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani. Katika uwanja wa siasa, au mahali popote huwezi kutoa malalamiko ya uzushi uzushi tu.
Kura zote zimehesabiwa palepale jimboni na mbele ya wakala wake. Kuna wakala aliye dhihirisha kuwa kura zake zimeibiwa ?
Kwa fikira zake inadhihirisha kuwa Dr. Slaa ni mtu hatari sana na anaonyesha haja wiva kimawazo na anaeta siasa na kuigaiga (toka nchi zajirani) na kuropoka kama vile Lyatonga Mrema alivyo jipotezea umaarufu wake nchini (sikuhizi Lyatonga ni kama "The Comedy " Nobody takes him serious. Dr. Slaa anajiharibia hata sisi wengine tulio mpigia kura tunasikitika. Ninajuta kumpa kura yangu na itabidi hawa wagombea wanao jichomoza chomoza kuwa angalia sana.
Hivi Dr. Slaa alikuwa amechanjia kwamba mwaka huu lazima awe raisi wa jamuhuri ya Tanzania ? Hata kama kura alizopigiwa hazitoshi ? Ni kiumbe gani huyu, alafu eti alikuwa awe raisi ? Sasa hebu imagine mtu kama huyu alivyo na uchu awe raisi... it will be worse than what we complain of what CCM is doing
Mungu ashukuriwe na sala za kuiombea nchi yetu ziendelee kila siku. Tumeepukana na janga la watu kama Dr. Slaa.
Hii inadhihirisha kuwa upinzani unayo kazi kubwa ya kufanya ili kuaminika na wananchi. Jimbo la Mbulu kwenyewe anakotoka Slaa hakupata kura zote, wamegawana na JK. Inaonyesha hata watu jimboni kwake wasivyo muamini.
Mungu ibariki Tanzania