Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
- Thread starter
- #41
Picha ya chini wakiwa wanaomba kura kwa style ya kupiga magoti.
Jamani nyingine nitaleta kesho. Bado mwahitaji picha?
Mkuu asante kwa kutuwekea habari hii hapa. Nisingeweza kuweka kila kitu mwenyewe. Mungu akubariki.Mkutano wa kihistoria. Pale Uhuru platform pamoja na barabara zote nne zinazozunguka uwanja zilijaa watu. wasillizaji wakubwa walikuwa maaskari polisi waliovalia kininja waliokuwa hata hawataki mtu akohoe.(Baadaye niligundua hawakutaka walikose hata neno moja analosema
Slaa). Dr alimwaga sera akieleza maadui 3 aliowaacha mwl Nyerere hawakuthibitiwa sasa wamejaa mtoto jeuri aitwaye ufisadi sasa si watatu tena bali wanne. Akaeleza kumuenzi mwl ni kuendeleza fikra na matendo aliyoyaanzisha. Suala la utaifa na maandalizi ya vijana wa kitanzania yanapaswa kugharamiwa kwa gharama yoyote. Alieleza jinsi Nyerere alivyowapeleka wahaya kusomea Mtwara na Wanyakyusa akawaleta Ngara. Wakati ule hakuna aliyemwelewa na hasa alipotaifisha mashule na kuitwika serkali mzigo wa kuyaendesha. Kumbe alichokuwa anapambana nacho ni kujenga utaifa. Wachaga wakafanya urafiki na wamakonde na kuoa huko huo ukawa mwisho wa uhasama na vita ya makabila. Isitoshe aliwapeleka vijana wote wa kitanzania jkt wakapikwa na kufundishwa uzalendo kwa nchi yao. Leo sisiem wanapeleka vijana kwenye makambi ya green guards ili wajifunze kumwaga damu ya watanzania wenzao badala ya kulinda usalama wa nchi yao. Akasema ndiyo maana serkali ya Chadema inaamua kubeba mzigo mkubwa sana wa kutoa elimu itakayorejesha utaifa kwa kuondoa matabaka ili wote wasome. Amesema wengi wanahoji atatoa wapi fedha lakini anajua kuwa vx wanazotembelea mawaziri wa jk zimebeba gharama ya shule nzima ya sekondari -200mil au dispensari 4. Yeye amekubali kula mihogo ikulu na kutembelea Landcruiser mkonga ili akomboe hela inayotumiwa kwa kuongeza starehe ikulu kusomesha watoto wa kitanzania. Huku akishangiliwa na kukatishwa mara kadhaa na wazee waliotaka kurudisha kadi za ccm alionyesha kuwa kujenga tu zahanati kila kijiji haitoshi kama watu wanaishi katika mazingira hatarishi. Miaka 49 ya uhuru watanzania wanaishi katika nyumba za kuchimba chini ya ardhi, ziliparatwa kwa tope huku vumbi likitimka na kuathiri afya zao. Hata ungejenga zahanati ngapi afya haiwezi kuboreka wakati watu wanaishi katika viroboto na vumbi. Ndiyo maana serkali ya chadema katika kuboresha maisha ya watanzania wa kawaida ili mwl anayepata 160000 ajenge nyumba na askari anayelipwa 200000 ajenge nyumba itaondoa kodi ya serkali katika vifaa vya ujenzi kama simenti na bati. Dr awali alikuwa ameeleza ubaya na madhara ya rushwa na ufisadi na jinsi Chadema imekuwa ikipambana nayo kurudiha tunu za nchi yetu. Amesema Jk anawakumbatia mafisadi wote na hana utashi wala ubavu wowote wa kuwakemea. Rostam Aziz mmiliki wa Kagoda, Andrew Chenge na vituko vya rada, Basil Mramba, ni Chadema tu iliyowahi kujitokeza kupambana na ufisadi tangu Richmond, benki kuu, Rada nk Dr alikazia kuwa hata zile fedha za kusaidia madhara ya mtikisiko wa kiuchumi ambazo wakulima waliadhirika kwa kukosa bei nzuri ya mazao na makampuni yanayonunua mazao yalipata hasara kwa kukosa soko zuri zimeishia mifukoni mwa maswahiba wa kikwete. Amewaomba usalama wa taifa wasidhubutu kujiigiza katika kuchakachua kura kwani watanzania wamekwisha amua wanachokitaka. Hawahitaji kusemewa na Redet wala Synovet maana wao wana midomo yao. Ndipo akauliza eti wangapi watampa Dr Slaa kura tar 31 uwanja mzima ukanyoosha mikono akasema hebu usalama wa taifa chukueni rekodi hiyo. wanagapi watampa jk wote wakashusha mikono. Mwishoni alitoa tamko la chama chake kuwa Chadema haitaki kuingia ikulu kwa kumwaga damu ya mtu. Je tutawaongoza kina nani ikiwa watu tayari wamekufa? Alidai Chadema ni chama cha amani na hawataki damu ya mtu imwagike. Badala yake akamwonya jk kuwazuia green guards waliosambazwa nchi nzima kufanya fujo kwa vyama tofauti na ccm. kama kila chama kikiweka vijana wake kama ccm wanavyoffanya ili kuwadhibiti green guard patakuwa hapakaliki tena. Na hiyo fujo itakuwa imeanzishwa na ccm. Pia aliwaambia usalama wa taifa wasijaribu kabisa kuchakachua kura maana mipango yao amekwisha inasa. Amesema ataileza wakati ukifika. Saa 12 akafunga mkutano na watu kwa furaha wakaagana naye na wengine kuchangia gharama za mafuta ya helikopta. Wazee wawili waliokaa kando ya msikiti wa uswahilini wakasikika wakisema uwanja huu umekuwa na mikutano mingi lakini huu ni kwanza wa aina yake. Watu wengi, maneno mazuri, asiyempa kura baba huyu ana lake jambo!!!!!!!
:biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1:Mkuu una masihara wewe, nani kasema picha zimetosha? Tunasubiri hiyo kesho:dance:
Tofauti moja ni kwamba Dr pia alipiga magoti mwenyewe.:biggrin1: Lakini wa kijani alikuwa anafanya maigizo kwa kuwaomba watu kwa picha ya mtu aliyeshindwa na asiyejali wananchi wake. Alidiliki kuwambia baadhi kuwa hataki kura zao.Hahahaaa, hii imekaa safi sana.
Pole sana mkuu Omulangi, hilo ndilo sasa hivi wanalofanya Vodacom kwa kukata vipesa vya watu bila idhini yao na kuvipeleka sisi m. kwa kisingizio cha mkoko. Nawatahadhalisha wapenda maendeleo wote jiepusheni na MKOKO ni deal ya sisi m hiyo!Bibi mmoja alipoulizwa kama atapiga kura alisema kwa kihaya BILA SHAKA. Na kura yako utampa nani mwaka huu akasema kwa kihaya huyo wa wote Shilaa (hawezi kusema Slaa). Kwa nini huwapigii ccm chama ulichojiunga tangu zamani? Alijibu hao tumekwisha wapigia siku za nyuma wacha tumpe na huyu kwani naye si mtoto wa watu? Nikaelewa Dr amekwishapigwa kama chapa katika mioyo ya watu. Bibi hakuta sera wala kujua zaidi anavutwa na huruma tu ya uzazi!!!!!! kazi kweli. Bahati nzuri tangu jana nilipogundua nimekatwa fedha zangu bila ridhaa yangu kuchangia ccm nimeamua kumpa Dr Slaa kura yangu anikamatie wezi wanaotuibia wanyonge wakati wao wana mabilioni benki.
Jamani wanasiasa tuwaache walivyo na uwanasiasa wako. Tunaweza kutengeneza tafsiri nyingi saana lakini wote wamepiga magoti. By the way, sio tatizo kama wengi tunavyotaka lionekane, bali desturi za jamii nyingi za Kitanzania hufanya hivyo. Kupiga magoti pia si kupewa kura.Tofauti moja ni kwamba Dr pia alipiga magoti mwenyewe.:biggrin1: Lakini wa kijani alikuwa anafanya maigizo kwa kuwaomba watu kwa picha ya mtu aliyeshindwa na asiyejali wananchi wake. Alidiliki kuwambia baadhi kuwa hataki kura zao.