Elections 2010 Dr Slaa ndani ya Bukoba

Jamani hapa naanza kwa picha tu jinsi mambo yalivyokuwa uwanjani.
IMGP0059.jpg

IMGP0058.jpg

IMGP0060.jpg
Picha hizo zinaonyesha watu walivyokuwa kushoto katikati na kulia wote wakiwa tayari kumsikiliza Dr Slaa.
 
Mkutano wa kihistoria. Pale Uhuru platform pamoja na barabara zote nne zinazozunguka uwanja zilijaa watu. wasillizaji wakubwa walikuwa maaskari polisi waliovalia kininja waliokuwa hata hawataki mtu akohoe.(Baadaye niligundua hawakutaka walikose hata neno moja analosema Slaa).

Dr alimwaga sera akieleza maadui 3 aliowaacha mwl Nyerere hawakuthibitiwa sasa wamejaa mtoto jeuri aitwaye ufisadi sasa si watatu tena bali wanne. Akaeleza kumuenzi mwl ni kuendeleza fikra na matendo aliyoyaanzisha. Suala la utaifa na maandalizi ya vijana wa kitanzania yanapaswa kugharamiwa kwa gharama yoyote. Alieleza jinsi Nyerere alivyowapeleka wahaya kusomea Mtwara na Wanyakyusa akawaleta Ngara. Wakati ule hakuna aliyemwelewa na hasa alipotaifisha mashule na kuitwika serkali mzigo wa kuyaendesha. Kumbe alichokuwa anapambana nacho ni kujenga utaifa.

Wachaga wakafanya urafiki na wamakonde na kuoa huko huo ukawa mwisho wa uhasama na vita ya makabila. Isitoshe aliwapeleka vijana wote wa kitanzania jkt wakapikwa na kufundishwa uzalendo kwa nchi yao. Leo sisiem wanapeleka vijana kwenye makambi ya green guards ili wajifunze kumwaga damu ya watanzania wenzao badala ya kulinda usalama wa nchi yao. Akasema ndiyo maana serkali ya Chadema inaamua kubeba mzigo mkubwa sana wa kutoa elimu itakayorejesha utaifa kwa kuondoa matabaka ili wote wasome.

Amesema wengi wanahoji atatoa wapi fedha lakini anajua kuwa vx wanazotembelea mawaziri wa jk zimebeba gharama ya shule nzima ya sekondari -200mil au dispensari 4. Yeye amekubali kula mihogo ikulu na kutembelea Landcruiser mkonga ili akomboe hela inayotumiwa kwa kuongeza starehe ikulu kusomesha watoto wa kitanzania. Huku akishangiliwa na kukatishwa mara kadhaa na wazee waliotaka kurudisha kadi za ccm alionyesha kuwa kujenga tu zahanati kila kijiji haitoshi kama watu wanaishi katika mazingira hatarishi. Miaka 49 ya uhuru watanzania wanaishi katika nyumba za kuchimba chini ya ardhi, ziliparatwa kwa tope huku vumbi likitimka na kuathiri afya zao. Hata ungejenga zahanati ngapi afya haiwezi kuboreka wakati watu wanaishi katika viroboto na vumbi. Ndiyo maana serkali ya chadema katika kuboresha maisha ya watanzania wa kawaida ili mwl anayepata 160000 ajenge nyumba na askari anayelipwa 200000 ajenge nyumba itaondoa kodi ya serkali katika vifaa vya ujenzi kama simenti na bati.

Dr awali alikuwa ameeleza ubaya na madhara ya rushwa na ufisadi na jinsi Chadema imekuwa ikipambana nayo kurudiha tunu za nchi yetu. Amesema Jk anawakumbatia mafisadi wote na hana utashi wala ubavu wowote wa kuwakemea. Rostam Aziz mmiliki wa Kagoda, Andrew Chenge na vituko vya rada, Basil Mramba, ni Chadema tu iliyowahi kujitokeza kupambana na ufisadi tangu Richmond, benki kuu, Rada nk Dr alikazia kuwa hata zile fedha za kusaidia madhara ya mtikisiko wa kiuchumi ambazo wakulima waliadhirika kwa kukosa bei nzuri ya mazao na makampuni yanayonunua mazao yalipata hasara kwa kukosa soko zuri zimeishia mifukoni mwa maswahiba wa kikwete. Amewaomba usalama wa taifa wasidhubutu kujiigiza katika kuchakachua kura kwani watanzania wamekwisha amua wanachokitaka. Hawahitaji kusemewa na Redet wala Synovet maana wao wana midomo yao.

Ndipo akauliza eti wangapi watampa Dr Slaa kura tar 31 uwanja mzima ukanyoosha mikono akasema hebu usalama wa taifa chukueni rekodi hiyo. wanagapi watampa jk wote wakashusha mikono. Mwishoni alitoa tamko la chama chake kuwa Chadema haitaki kuingia ikulu kwa kumwaga damu ya mtu. Je tutawaongoza kina nani ikiwa watu tayari wamekufa? Alidai Chadema ni chama cha amani na hawataki damu ya mtu imwagike. Badala yake akamwonya jk kuwazuia green guards waliosambazwa nchi nzima kufanya fujo kwa vyama tofauti na ccm. kama kila chama kikiweka vijana wake kama ccm wanavyoffanya ili kuwadhibiti green guard patakuwa hapakaliki tena. Na hiyo fujo itakuwa imeanzishwa na ccm.

Pia aliwaambia usalama wa taifa wasijaribu kabisa kuchakachua kura maana mipango yao amekwisha inasa. Amesema ataileza wakati ukifika. Saa 12 akafunga mkutano na watu kwa furaha wakaagana naye na wengine kuchangia gharama za mafuta ya helikopta. Wazee wawili waliokaa kando ya msikiti wa uswahilini wakasikika wakisema uwanja huu umekuwa na mikutano mingi lakini huu ni kwanza wa aina yake. Watu wengi, maneno mazuri, asiyempa kura baba huyu ana lake jambo!!!!!!!
 
IMGP0115.jpg
IMGP0114.jpg
Dr Slaa akimnadi mgombea ubunge Wilfred Lwakatare. Picha ya chini wakiwa wanaomba kura kwa style ya kupiga magoti.

IMGP0086.jpg
IMGP0091.jpg
IMGP0061.jpg
Dr Slaa akiuza sera na ilani ya Chadema.
 
IMGP0075.jpg
Jamaa huyo alishindwa kujizuia kuendelea kuwa mwanachama wa sisi m kwa hiyo aliamua kurudisha kadi hapo hapo wakati mkutano ukiendelea wakati Dr Slaa akimwaga sera za Chadema.

PICT0491.jpg
Jamaa huyu anaitwa Shemela na anaimba bongo fleva kwa kihaya na kiswahili kama wafanyavyo wakina Chege. Hapa yupo anahamasisha.

IMGP0071.jpg
Mambo ya usalama haya

IMGP0085.jpg
Na huyu baby anafurahia uwepo wa Dr Slaa uwanjani kwa kuangalia picha yake.
 
Mambo ya picha yanaendelea sitaki mkose uhondo wa yale yaliyotokea Bukoba
 
IMGP0095.jpg
IMGP0076.jpg
PICT0522.jpg
Mikono yote iliyonyanyuliwa ilkuwa ikijibu swali la nani yuko tayari kutoa kura yake kwa Rais,mbunge na madiwani wa jimbo la Bukoba mjini alilouliza Dr Slaa.
 
IMGP0102.jpg
PICT0525.jpg
Mgombea ubunge kwa tiketi ya chadema Bukoba mjini akiomba kura kwa ajili yake, madiwani na Rais Dr Slaa.
 
Duh mwaka huu kuna kazi jamaa wameziba pande zote...
Omar ilyas onaona? PIIIIIPOOOOOOZZZZZZZ
 
PICT0508.jpg
IMGP0134.jpg
Mambo ya mabango hayo. Message sent.

PICT0495.jpg

PICT0527.jpg
Picha hizi nyie jazieni wenyewe maana ni mambo ya ushemeji!
 
Bibi mmoja alipoulizwa kama atapiga kura alisema kwa kihaya BILA SHAKA. Na kura yako utampa nani mwaka huu akasema kwa kihaya huyo wa wote Shilaa (hawezi kusema Slaa). Kwa nini huwapigii ccm chama ulichojiunga tangu zamani? Alijibu hao tumekwisha wapigia siku za nyuma wacha tumpe na huyu kwani naye si mtoto wa watu? Nikaelewa Dr amekwishapigwa kama chapa katika mioyo ya watu. Bibi hakuta sera wala kujua zaidi anavutwa na huruma tu ya uzazi!!!!!! kazi kweli. Bahati nzuri tangu jana nilipogundua nimekatwa fedha zangu bila ridhaa yangu kuchangia ccm nimeamua kumpa Dr Slaa kura yangu anikamatie wezi wanaotuibia wanyonge wakati wao wana mabilioni benki.
 
IMGP0139.jpg
IMGP0137.jpg
Hii ni changia Chadema ishinde na usafiri wa Dr Slaa angani. Watu walikuwa wanatoa pesa yao kwa hiari tena hapa mkutano ukiwa umeshafungwa.
Jamani ebu tuichangie chadema. Tuma neno CHADEMA kwenda 15710 utakuwa umeichangia sh. 350 tu. unaweza kutuma mara nyingi uwezavyo.
Ni ushauri wangu badala ya kuchangia ile kitu ambayo inaitwa mkoko ambayo ni wizi mtupu, bora uchangie Chadema kwa mabadiliko na ushindi wa haki.
 
Mkutano wa kihistoria. Pale Uhuru platform pamoja na barabara zote nne zinazozunguka uwanja zilijaa watu. wasillizaji wakubwa walikuwa maaskari polisi waliovalia kininja waliokuwa hata hawataki mtu akohoe.(Baadaye niligundua hawakutaka walikose hata neno moja analosema
Slaa). Dr alimwaga sera akieleza maadui 3 aliowaacha mwl Nyerere hawakuthibitiwa sasa wamejaa mtoto jeuri aitwaye ufisadi sasa si watatu tena bali wanne. Akaeleza kumuenzi mwl ni kuendeleza fikra na matendo aliyoyaanzisha. Suala la utaifa na maandalizi ya vijana wa kitanzania yanapaswa kugharamiwa kwa gharama yoyote. Alieleza jinsi Nyerere alivyowapeleka wahaya kusomea Mtwara na Wanyakyusa akawaleta Ngara. Wakati ule hakuna aliyemwelewa na hasa alipotaifisha mashule na kuitwika serkali mzigo wa kuyaendesha. Kumbe alichokuwa anapambana nacho ni kujenga utaifa. Wachaga wakafanya urafiki na wamakonde na kuoa huko huo ukawa mwisho wa uhasama na vita ya makabila. Isitoshe aliwapeleka vijana wote wa kitanzania jkt wakapikwa na kufundishwa uzalendo kwa nchi yao. Leo sisiem wanapeleka vijana kwenye makambi ya green guards ili wajifunze kumwaga damu ya watanzania wenzao badala ya kulinda usalama wa nchi yao. Akasema ndiyo maana serkali ya Chadema inaamua kubeba mzigo mkubwa sana wa kutoa elimu itakayorejesha utaifa kwa kuondoa matabaka ili wote wasome. Amesema wengi wanahoji atatoa wapi fedha lakini anajua kuwa vx wanazotembelea mawaziri wa jk zimebeba gharama ya shule nzima ya sekondari -200mil au dispensari 4. Yeye amekubali kula mihogo ikulu na kutembelea Landcruiser mkonga ili akomboe hela inayotumiwa kwa kuongeza starehe ikulu kusomesha watoto wa kitanzania. Huku akishangiliwa na kukatishwa mara kadhaa na wazee waliotaka kurudisha kadi za ccm alionyesha kuwa kujenga tu zahanati kila kijiji haitoshi kama watu wanaishi katika mazingira hatarishi. Miaka 49 ya uhuru watanzania wanaishi katika nyumba za kuchimba chini ya ardhi, ziliparatwa kwa tope huku vumbi likitimka na kuathiri afya zao. Hata ungejenga zahanati ngapi afya haiwezi kuboreka wakati watu wanaishi katika viroboto na vumbi. Ndiyo maana serkali ya chadema katika kuboresha maisha ya watanzania wa kawaida ili mwl anayepata 160000 ajenge nyumba na askari anayelipwa 200000 ajenge nyumba itaondoa kodi ya serkali katika vifaa vya ujenzi kama simenti na bati. Dr awali alikuwa ameeleza ubaya na madhara ya rushwa na ufisadi na jinsi Chadema imekuwa ikipambana nayo kurudiha tunu za nchi yetu. Amesema Jk anawakumbatia mafisadi wote na hana utashi wala ubavu wowote wa kuwakemea. Rostam Aziz mmiliki wa Kagoda, Andrew Chenge na vituko vya rada, Basil Mramba, ni Chadema tu iliyowahi kujitokeza kupambana na ufisadi tangu Richmond, benki kuu, Rada nk Dr alikazia kuwa hata zile fedha za kusaidia madhara ya mtikisiko wa kiuchumi ambazo wakulima waliadhirika kwa kukosa bei nzuri ya mazao na makampuni yanayonunua mazao yalipata hasara kwa kukosa soko zuri zimeishia mifukoni mwa maswahiba wa kikwete. Amewaomba usalama wa taifa wasidhubutu kujiigiza katika kuchakachua kura kwani watanzania wamekwisha amua wanachokitaka. Hawahitaji kusemewa na Redet wala Synovet maana wao wana midomo yao. Ndipo akauliza eti wangapi watampa Dr Slaa kura tar 31 uwanja mzima ukanyoosha mikono akasema hebu usalama wa taifa chukueni rekodi hiyo. wanagapi watampa jk wote wakashusha mikono. Mwishoni alitoa tamko la chama chake kuwa Chadema haitaki kuingia ikulu kwa kumwaga damu ya mtu. Je tutawaongoza kina nani ikiwa watu tayari wamekufa? Alidai Chadema ni chama cha amani na hawataki damu ya mtu imwagike. Badala yake akamwonya jk kuwazuia green guards waliosambazwa nchi nzima kufanya fujo kwa vyama tofauti na ccm. kama kila chama kikiweka vijana wake kama ccm wanavyoffanya ili kuwadhibiti green guard patakuwa hapakaliki tena. Na hiyo fujo itakuwa imeanzishwa na ccm. Pia aliwaambia usalama wa taifa wasijaribu kabisa kuchakachua kura maana mipango yao amekwisha inasa. Amesema ataileza wakati ukifika. Saa 12 akafunga mkutano na watu kwa furaha wakaagana naye na wengine kuchangia gharama za mafuta ya helikopta. Wazee wawili waliokaa kando ya msikiti wa uswahilini wakasikika wakisema uwanja huu umekuwa na mikutano mingi lakini huu ni kwanza wa aina yake. Watu wengi, maneno mazuri, asiyempa kura baba huyu ana lake jambo!!!!!!!
Mkuu asante kwa kutuwekea habari hii hapa. Nisingeweza kuweka kila kitu mwenyewe. Mungu akubariki.
 
Mkuu una masihara wewe, nani kasema picha zimetosha? Tunasubiri hiyo kesho:dance:
:biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1:
Hamna noma
 
Hahahaaa, hii imekaa safi sana.
Tofauti moja ni kwamba Dr pia alipiga magoti mwenyewe.:biggrin1: Lakini wa kijani alikuwa anafanya maigizo kwa kuwaomba watu kwa picha ya mtu aliyeshindwa na asiyejali wananchi wake. Alidiliki kuwambia baadhi kuwa hataki kura zao.
 
Bibi mmoja alipoulizwa kama atapiga kura alisema kwa kihaya BILA SHAKA. Na kura yako utampa nani mwaka huu akasema kwa kihaya huyo wa wote Shilaa (hawezi kusema Slaa). Kwa nini huwapigii ccm chama ulichojiunga tangu zamani? Alijibu hao tumekwisha wapigia siku za nyuma wacha tumpe na huyu kwani naye si mtoto wa watu? Nikaelewa Dr amekwishapigwa kama chapa katika mioyo ya watu. Bibi hakuta sera wala kujua zaidi anavutwa na huruma tu ya uzazi!!!!!! kazi kweli. Bahati nzuri tangu jana nilipogundua nimekatwa fedha zangu bila ridhaa yangu kuchangia ccm nimeamua kumpa Dr Slaa kura yangu anikamatie wezi wanaotuibia wanyonge wakati wao wana mabilioni benki.
Pole sana mkuu Omulangi, hilo ndilo sasa hivi wanalofanya Vodacom kwa kukata vipesa vya watu bila idhini yao na kuvipeleka sisi m. kwa kisingizio cha mkoko. Nawatahadhalisha wapenda maendeleo wote jiepusheni na MKOKO ni deal ya sisi m hiyo!
 
My president, usikose kufika Kamachumu walimu wanalia kukuona, pita pia kata ya Buganguzi kwa Tibaigana wakulima wa Vanilla na jatrofa wanakusubiri,pia walioibiwa ardhi na miti pale Ahakona na waujumu waliojiita TASAF wana malalamiko yao. MR President kachukue kula zetu izo.
 
Tofauti moja ni kwamba Dr pia alipiga magoti mwenyewe.:biggrin1: Lakini wa kijani alikuwa anafanya maigizo kwa kuwaomba watu kwa picha ya mtu aliyeshindwa na asiyejali wananchi wake. Alidiliki kuwambia baadhi kuwa hataki kura zao.
Jamani wanasiasa tuwaache walivyo na uwanasiasa wako. Tunaweza kutengeneza tafsiri nyingi saana lakini wote wamepiga magoti. By the way, sio tatizo kama wengi tunavyotaka lionekane, bali desturi za jamii nyingi za Kitanzania hufanya hivyo. Kupiga magoti pia si kupewa kura.
 
Back
Top Bottom