Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
Dr. Slaa na Septemba Mosi, 2016 ‘Siasa ni sayansi’ - Kuelekea mwaka mmoja tangu aachane na CHADEMA (Septemba,1 2015).
‘Siasa ni sayansi’ ni msemo wenye maneno machache ambao ulinenwa na Dr.Wilbod Slaa Septemba, mosi mwaka 2015 wakati anatangaza rasmi sababu zake kuachia ngazi CHADEMA na kujivua unanachama na kujiuzulu siasa.
Takribani mwaka mmoja baadaye Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anaitangaza Septemba Mosi mwaka 2016 kama siku ya kuanza maandamano ya kupinga kile walichokiita ‘udikteta’.. UKUTA.
Ikumbukwe Dr.Slaa alijitokeza septemba,mosi 2015 ili kuzima uzushi/propaganda wa kuwa yupo likizo uliyoenezwa kwa kipindi cha takribani miezi miwili na sasa imepita takribani miezi miwili toka Mbowe atangaze UKUTA kuelekea Septemba mosi 2016….. Hakika ni mgongano wa ajabu!....ni propaganda nzito zilizochukuwa miezi miwili kuwaaminisha watanzania mambo yasiyokuwepo/uongo…lakini Septemba mosi 2015 Dr. Slaa alikanusha na kuwaacha mdomo wazi..ya septemba mosi 2016 yanafurahisha…tusubiri!
Siasa ni sayansi ina maana kubwa, sasa ni dhahiri sasa CHADEMA haina wanasayansi katika siasa bali kuna wapiga propaganda wenye hadaa nyingi..! Prof. Baregu anautetea utafiti wa TADIP?
Siasa ni sayansi ina maana ya kupanga mipango halisi na yenye kuetekelezeka na sio kujipaka mate machoni ili kuhadaa kuwa unatiririka na machozi!...Ni ngumu kuaminika.
Siasa ni sayansi ina maana ya kuetengeneza ajenda/hoja endelevu ambazo zitadumu misimu yote iwe utawala wa kiongozi yeyote…!
Siasa ni sayansi ina maana ya kuunganisha fikra za wananchi katika hoja zinazoibuliwa….inahitajika sayansi ya hali ya juu kujua kuwa wananchi wanahitaji nini kwa sasa na sio tu kuja na ‘’hoja maarufu’’ isiyogusa maisha yao…hoja ya udikteta haiwaingii wananchi kwani wanauhuru wote wanaouhitaji…hakukuwa na sayansi katika kutafakari.
Siasa ni sayansi inamaanish kuweza kuchambua madhara ya kushirikiana na baadhi ya watu katika kujenga imani ya wananchi ya muda mrefu….kushirikiana na mtu tuliyemdhihaki na kumfanya kuwa kinara?
Tutamwamini vipi? Je, waweza kumpa urithi motto wa jirani yako sababu tu anafaulu darasani na kumnyima mwanao?
Siasa ni sayansi ni pamoja na kuwa na kiongozi ambaye hata akijumuika na viongozi wa vyama vingine/hasimu haitaharibu taswira ya ajenda yetu kwani wafuasi hawatahoji au kuwepo kwake..na sio kuwa na kinara ambaye akipiga tu picha na viongozi wa vyama vingine inabadilisha mtazamo na dhamira ya chama na wanachama.
Siasa ni sayansi inamaanisha kuwa kiongozi unayempa dhamana ni yule mwenye sifa ya kusaidia wananchi...sasa kituko cha mwaka katika moja ya vibwagizo ambavyo CHADEMA walimsifia kwa furaha ni pamoja na kuinadi sifa mbaya kuwa alikuwa kinara wa mgomo wa madaktari nchini ulioacha maelfu vilema na vifo kuwa Katibu Mkuu wa chama..Dr.Mashinji....eti Mbowe na wananchedema wakamsifia kuwa kwa uzoefu huo wa kufanikisha mgomo wa madaktari dhidi ya serikali na wananchi kuwa ni mtu sahihi kuongoza mapambano....lo lo lo...eti hata UKUTA wananchi wakifa itakuwa ni moja ya mafanikio yake....'siasa ni sayansi'.
Siasa ni sayansi ina maana pana zaidi kubwa ya yote ilkiwa ni kubuni na kuchambua na mipango,sera ambazo zitaleta maendeleo kwa wananchi bila kuzingatia chama kipo madarakani au upinzani.
Mada hii ni maalum kuelekea septemba mosi ambapo ni siku Dr. Slaa anatimiza mwaka mmoja tangu ajitoe CHADEMA.