Dr. Slaa na Septemba Mosi: ‘Siasa ni sayansi’

Dr. Slaa na Septemba Mosi: ‘Siasa ni sayansi’

chadema imebadili ajenda...walioyapinga wanayafurahia.
Mbona dr. Slaa aligombea Urais hamkumpa Kura?.
Kama mlikubaliana na ajenda yake.?/
Dunia nzima ikishuhudia jk akijiuma uma kwenye mdahalo wa urais kwa kushindwa kujibu hoja. Lakini mkampa urais. Dr. Slaa aliongea hoja za kisayansi hakupata.
Leo mnailaumu cdm kwa kutompendekeza..?

Tanzania ni nchi ya ajabu..unashinda bila kujenga hoja makini. Kule USA huwezi shinda kamwe.

Shule za kata kweli zimegeuka mzigo kwa Taifa.

Wenye hoja makini kwakua wanatoka upinzani wanaitwa wataleta vita.

Ukitaka kushinda we vaa nguo ya kijani tu ..ukiwa jukwaani imba wimbo wa mtaisoma namba. Kisha kakae. Wanakupa kura tu. Mfsssss
 
Watu wengi sana hupenda kulaumu wakati huo wao huwa hawana mchango hata kidogo zaidi ya kulaumu Na kusifia upande huu au ule! Kufanya siasa ya vyama vingi kwenye nchi ambazo majeshi Na dola yote Kwa ujumla huwa watesi Na watetezi WA chama cha kilichopo madarakani! Akina mbowe mnaowasema wanamsimamo thabiti sana!
Kuhusu ukuta hata wasipoandamana wamefanikiwa maana mwezi mmoja mzima watu wameiba juu ya ukuta Na kusema ukuta. Wafanya mazoezi wamefanya Na wengi wameongea Kwa hakika wamefanikiwa! Kila wakati jiulize mchango wako nini ambao una haki ndani yake!
 
Vyama vyetu vya siasa katika Dunia ya Tatu vina haja ya kujitathmin upya. Hapo namaanisha vyama tawala na vile pinzani. Siasa zetu bado zina walakini mkubwa.
Tatizo siyo siasa ni wanasiasa tulionao.

Wengi hawakupitia wala hawaoni umhimu wa kusoma elimu ya "sayansi ya siasa"(political science).

Hivyo hivyo watu wengi, kwenye makundi ya fani mbalimbali za maisha, hawaoni umhimu wa kujielimisha katika fani zao (sanaa, kilimo, ufugaji, uvuvi, michezo, nk)· Wengi wetu ni 'bora liende'.

Hata walio na elimu katika fani zao wanafanya shughuli hizo kwa mazoea kana kwamba hawana elimu yake! Kwa mfano mwanasheria nguri anayetoa maneno ya matusi hadharani ni makusudi au ujuha!
 
Watu wengi sana hupenda kulaumu wakati huo wao huwa hawana mchango hata kidogo zaidi ya kulaumu Na kusifia upande huu au ule! Kufanya siasa ya vyama vingi kwenye nchi ambazo majeshi Na dola yote Kwa ujumla huwa watesi Na watetezi WA chama cha kilichopo madarakani! Akina mbowe mnaowasema wanamsimamo thabiti sana!
Kuhusu ukuta hata wasipoandamana wamefanikiwa maana mwezi mmoja mzima watu wameiba juu ya ukuta Na kusema ukuta. Wafanya mazoezi wamefanya Na wengi wameongea Kwa hakika wamefanikiwa! Kila wakati jiulize mchango wako nini ambao una haki ndani yake!
Mara kutoka ''lazima tuandamane'' hadi kujifariji eti ''mwezi mmoja wameimba juu ya ukuta''...sidhani kama siasa ni maandamano pekee kama una sera utachaguliwa tu...ndio maana wameshinda ubunge...na kama kuna mgombea uraisi mwenye sifa na tija atashinda.
 
Tatizo siyo siasa ni wanasiasa tulionao.

Wengi hawakupitia wala hawaoni umhimu wa kusoma elimu ya "sayansi ya siasa"(political science).

Hivyo hivyo watu wengi, kwenye makundi ya fani mbalimbali za maisha, hawaoni umhimu wa kujielimisha katika fani zao (sanaa, kilimo, ufugaji, uvuvi, michezo, nk)· Wengi wetu ni 'bora liende'.

Hata walio na elimu katika fani zao wanafanya shughuli hizo kwa mazoea kana kwamba hawana elimu yake! Kwa mfano mwanasheria nguri anayetoa maneno ya matusi hadharani ni makusudi au ujuha!
Hakika!
 
Siasa ni art. Ina depends very much ni context ipi naelezea.

Mleta mada watanzania wenye Akili wanajua fika Madai ya cdm ni valid na solid.

Mliokalia ile "colonialism mentality ya mighty is always right."
. Mtamsifu mfalme.

But ukweli utakuja kutuhukumu siku moja.
Ni vizuri tukatumia jukwaa letu kwa kuelimishana kuliko kulaumu, kuchocheana na kudanganyana.

UKUTA ina lengo la kufikisha ujumbe kwamba nchi hii inatawaliwa kidikteta na madai mengine ya CHADEMA unayosema ni halali. Unaenda mbali zaidi na kutujengea hofu kwamba kutakuwa na machafuko, kiasi titajuta, mh!
1) Mdai gani ya CHADEMA ni halali na kwa misingi ipi!
2) Kutakuwa machafuko yapi kwa nini, njia zipi na kwa kiwango gani!
3) Hatua gani zichukuliwe, bila kulaumu mtu, kikundi, taasisi au chombo chochote!

TUSIFICHE LENGO BAYA NYUMA YA PAZIA LA KATIBA
 
Siasa ni sayansi ina maana pana zaidi kubwa ya yote ilkiwa ni kubuni na kuchambua na mipango,sera ambazo zitaleta
Nakubaliana wewe kuwa Siasa ni sayansi na ina maana pana zaidi kubwa ya yote ikiwa ni kubuni na kuchambua na mipango,sera za chama tawala ambazo zitaleta mivurugano/mipasuko na kutoelewana kwenye vyama vya upinzani kama alivyofanya kwa kutumiwa na akina Dr.Slaa na sasa Pro.Lipumba.

Tafsiri yangu mimi ni kuwa Siasa inajumuisha vitendo na harakati zote za maelewano na ushirikiano katika jamii pamoja na mizozo.
 
Umedadavua kwa mapana zaidi.....yah ni maoni kuntu.
 
Dr. Slaa na Septemba Mosi, 2016 ‘Siasa ni sayansi’ - Kuelekea mwaka mmoja tangu aachane na CHADEMA (Septemba,1 2015).

‘Siasa ni sayansi’ ni msemo wenye maneno machache ambao ulinenwa na Dr.Wilbod Slaa Septemba, mosi mwaka 2015 wakati anatangaza rasmi sababu zake kuachia ngazi CHADEMA na kujivua unanachama na kujiuzulu siasa.

Takribani mwaka mmoja baadaye Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anaitangaza Septemba Mosi mwaka 2016 kama siku ya kuanza maandamano ya kupinga kile walichokiita ‘udikteta’.. UKUTA.

Ikumbukwe Dr.Slaa alijitokeza septemba,mosi 2015 ili kuzima uzushi/propaganda wa kuwa yupo likizo uliyoenezwa kwa kipindi cha takribani miezi miwili na sasa imepita takribani miezi miwili toka Mbowe atangaze UKUTA kuelekea Septemba mosi 2016….. Hakika ni mgongano wa ajabu!....ni propaganda nzito zilizochukuwa miezi miwili kuwaaminisha watanzania mambo yasiyokuwepo/uongo…lakini Septemba mosi 2015 Dr. Slaa alikanusha na kuwaacha mdomo wazi..ya septemba mosi 2016 yanafurahisha…tusubiri!

Siasa ni sayansi ina maana kubwa, sasa ni dhahiri sasa CHADEMA haina wanasayansi katika siasa bali kuna wapiga propaganda wenye hadaa nyingi..! Prof. Baregu anautetea utafiti wa TADIP?

Siasa ni sayansi ina maana ya kupanga mipango halisi na yenye kuetekelezeka na sio kujipaka mate machoni ili kuhadaa kuwa unatiririka na machozi!...Ni ngumu kuaminika.

Siasa ni sayansi ina maana ya kuetengeneza ajenda/hoja endelevu ambazo zitadumu misimu yote iwe utawala wa kiongozi yeyote…!

Siasa ni sayansi ina maana ya kuunganisha fikra za wananchi katika hoja zinazoibuliwa….inahitajika sayansi ya hali ya juu kujua kuwa wananchi wanahitaji nini kwa sasa na sio tu kuja na ‘’hoja maarufu’’ isiyogusa maisha yao…hoja ya udikteta haiwaingii wananchi kwani wanauhuru wote wanaouhitaji…hakukuwa na sayansi katika kutafakari.

Siasa ni sayansi inamaanish kuweza kuchambua madhara ya kushirikiana na baadhi ya watu katika kujenga imani ya wananchi ya muda mrefu….kushirikiana na mtu tuliyemdhihaki na kumfanya kuwa kinara?
Tutamwamini vipi? Je, waweza kumpa urithi motto wa jirani yako sababu tu anafaulu darasani na kumnyima mwanao?

Siasa ni sayansi ni pamoja na kuwa na kiongozi ambaye hata akijumuika na viongozi wa vyama vingine/hasimu haitaharibu taswira ya ajenda yetu kwani wafuasi hawatahoji au kuwepo kwake..na sio kuwa na kinara ambaye akipiga tu picha na viongozi wa vyama vingine inabadilisha mtazamo na dhamira ya chama na wanachama.

Siasa ni sayansi inamaanisha kuwa kiongozi unayempa dhamana ni yule mwenye sifa ya kusaidia wananchi...sasa kituko cha mwaka katika moja ya vibwagizo ambavyo CHADEMA walimsifia kwa furaha ni pamoja na kuinadi sifa mbaya kuwa alikuwa kinara wa mgomo wa madaktari nchini ulioacha maelfu vilema na vifo kuwa Katibu Mkuu wa chama..Dr.Mashinji....eti Mbowe na wananchedema wakamsifia kuwa kwa uzoefu huo wa kufanikisha mgomo wa madaktari dhidi ya serikali na wananchi kuwa ni mtu sahihi kuongoza mapambano....lo lo lo...eti hata UKUTA wananchi wakifa itakuwa ni moja ya mafanikio yake....'siasa ni sayansi'.

Siasa ni sayansi ina maana pana zaidi kubwa ya yote ilkiwa ni kubuni na kuchambua na mipango,sera ambazo zitaleta maendeleo kwa wananchi bila kuzingatia chama kipo madarakani au upinzani.

Mada hii ni maalum kuelekea septemba mosi ambapo ni siku Dr. Slaa anatimiza mwaka mmoja tangu ajitoe CHADEMA.
Nimekuelewa vizuri sana, wataendelea kubisha kwa kuwa wana sifa ya ubishi, mchango wa Dr Slaa ndani ya hiki chama ni mkubwa, na bado wanatembelea "viatu" vyake, hadi 2020 itakuwa historia!
 
Akija mtu na kachupa. Akakuambia "Hiyo uliyoshika sio dhahabu. Dhahabu ni hii hapa. Naye akakupa" kachupa " ukiamini ni dhahabu nawe ukaitupa dhahabu ya kweli na kuchekelea kama zuzu na kachupa kako. Utakuwa umeliwa.
Mbowe alimtupa Dr slaa (dhahabu) na kushangilia na EL (kachupa) .Alishangilia kama zuzu.
 
Maudhui ya Mletamada kwamba ukawa /chadema wamechafuka Na Ccm ni wasafi kwa kisi gizio cha mleta madam ni uchaguzi uliopita :
Jibu maswali haya :

Nitajie msafi katika wagombea wa Urais mwaka Jana Kama yupo ?

Kama Issue ni Uchafu mbona miaka yote mmeshindwa kumpeleka mahakamani kama mujibu wa sheria !

Mimi nilikuwepo mwembeyanga siku ambayo Dr Slaa alitaja Watuhumiwa wa ufisadi:

Jina la Lowasa lilikuwa
NamBa 13 kuhusu LA j Richmond
ambayo walio chini yake walisababisha .

Jina LA jakaya likuwa LA 14

Watuhumiwa wengoine Namba 1
Mpaka
12 wakashfa nzito zilizotajwa
pale hajashughulikiwa

Wengi tunawaona wanapishana ;Na hata Jana kwenye Jubilee wamekutana na lowasa !!

Kama mnachukia Ufisadi
uliotendwa Na ccm Na Magufuli akiwemo.. mbona Dr Slaa hamjampa kura ?

Nakujulisha tu Vita ya ufisadi haijapata mwenyewe hapa ni mbwe mbwe tu !

Hebu nikuulize !!!

Jakaya alisamehe baadhi ya wezi wa Epa wakarudisha pesa basi:hAkua kesi

Magufuli akasamehe wale wa kodi ya makontena !
Hakuna aliyeshitakiwa baada ya kulipa walichoiba ,,,,,

Sijasahau bado !
 
Umejielekeza upande mmoja-- "siasa ni sayansi", ila kumbuka kuna " sayansi ya siasa". Wakati wote binadamu anatakiwa kuwa mpevu wa kulielewa duara anamozunguka. Wewe unaonekana kuangalia mzunguko wa duara pale ambapo limesimama na wakati huna namna ya kulianzishia mwendo kwa sababu tu uko ndani yake. Akili yako inakutuma kuwa waweza kulianzishia mwendo ukiwa nje tu. Kimsingi mawazo ya mtu mmoja hugota pahali lakini asitambue kwamba mawazo yake yamegota. Siasa haitawaliwi na sayansi ila siasa huitawala sayansi. Kwa mawazo yako, unaamini sayansi inapaswa kuiongoza siasa na miundo yake. Hapana. Siasa ndiyo huongoza sayansi na miundo yake. Wenye mawazo kama yako, wakipata madaraka ndiyo huibua mtanziko kama tulio nao. Kuwepo wanasayansi na wanasiasa ni kwa sababu kuna sayansi na siasa. Wanasayansi hawatumii misingi ya siasa, lakini wasiasa hutumia misingi ya sayansi, ila siasa siyo sayansi, bali kuna sayansi ya siasa.
Kama anao ufahamu basi atakua amekuelewa vizuri sana.
 
Nimekuelewa vizuri sana, wataendelea kubisha kwa kuwa wana sifa ya ubishi, mchango wa Dr Slaa ndani ya hiki chama ni mkubwa, na bado wanatembelea "viatu" vyake, hadi 2020 itakuwa historia!
Hakika mkuu.
 
Back
Top Bottom