Dr. Slaa na Septemba Mosi: ‘Siasa ni sayansi’

Dr. Slaa na Septemba Mosi: ‘Siasa ni sayansi’

Maudhui ya Mletamada kwamba ukawa /chadema wamechafuka Na Ccm ni wasafi kwa kisi gizio cha mleta madam ni uchaguzi uliopita :
Jibu maswali haya :

Nitajie msafi katika wagombea wa Urais mwaka Jana Kama yupo ?

Kama Issue ni Uchafu mbona miaka yote mmeshindwa kumpeleka mahakamani kama mujibu wa sheria !

Mimi nilikuwepo mwembeyanga siku ambayo Dr Slaa alitaja Watuhumiwa wa ufisadi:

Jina la Lowasa lilikuwa
NamBa 13 kuhusu LA j Richmond
ambayo walio chini yake walisababisha .

Jina LA jakaya likuwa LA 14

Watuhumiwa wengoine Namba 1
Mpaka
12 wakashfa nzito zilizotajwa
pale hajashughulikiwa

Wengi tunawaona wanapishana ;Na hata Jana kwenye Jubilee wamekutana na lowasa !!

Kama mnachukia Ufisadi
uliotendwa Na ccm Na Magufuli akiwemo.. mbona Dr Slaa hamjampa kura ?

Nakujulisha tu Vita ya ufisadi haijapata mwenyewe hapa ni mbwe mbwe tu !

Hebu nikuulize !!!

Jakaya alisamehe baadhi ya wezi wa Epa wakarudisha pesa basi:hAkua kesi

Magufuli akasamehe wale wa kodi ya makontena !
Hakuna aliyeshitakiwa baada ya kulipa walichoiba ,,,,,

Sijasahau bado !
Siasa ni sayansi.....kutokana na tabia ya chadema ya kushupaza shingo kutuhumu kila mtu hovyo hovyo kila hoja ikija mnalialia badala ya kutoa hoja....mbona list of shame mmeiondoa kwenye wavuti....au ilikuwa hoja ya Dr.Slaa?
 
Baada ya miaka 9 sasa unaulizia kwanini haionekani kwenye Website!

Kwa nini usiifanyie KAzi so unayo ?

Vyombo vyote vya Habari si wanayo ?

Je Ikiwekwa tena kwenye website ndo ntaifanyia KAzi ?

Kwa ninimnadai chadema ndo
wa kwanza kumchafua badala
Ya cmm Nikuulize 1995ya Richmond yaa 207 ilikiwepo ?

Operesheni kuvua Magamba ni ya chadema?!

Hoja sio kuiondoa hoja hapa ni kupinga Lila vitendo vya aibu Na kwa watu wote !

Ufisadi Maana yake ni mambo ya aibu !

Mbna hao watunu.iwa wengine hamuwasemi mnao tiuiiiiuu
Ninaelewa kwa kuwa umevurugwa.
 
Akija mtu na kachupa. Akakuambia "Hiyo uliyoshika sio dhahabu. Dhahabu ni hii hapa. Naye akakupa" kachupa " ukiamini ni dhahabu nawe ukaitupa dhahabu ya kweli na kuchekelea kama zuzu na kachupa kako. Utakuwa umeliwa.
Mbowe alimtupa Dr slaa (dhahabu) na kushangilia na EL (kachupa) .Alishangilia kama zuzu.
Hakika falsafa uliyonena ni ya uwezo wa juu katika dhana ya 'siasa ni sayansi'
 
Baada ya miaka 9 sasa unaulizia kwanini haionekani kwenye Website!

Kwa nini usiifanyie KAzi so unayo ?

Vyombo vyote vya Habari si wanayo ?

Je Ikiwekwa tena kwenye website ndo ntaifanyia KAzi ?

Kwa ninimnadai chadema ndo
wa kwanza kumchafua badala
Ya cmm Nikuulize 1995ya Richmond yaa 207 ilikiwepo ?

Operesheni kuvua Magamba ni ya chadema?!

Hoja sio kuiondoa hoja hapa ni kupinga Lila vitendo vya aibu Na kwa watu wote !

Ufisadi Maana yake ni mambo ya aibu !

Mbna hao watunu.iwa wengine hamuwasemi mnao tiuiiiiuu
Kijana hii orodha ya mafisadi imeondolewa septemba mosi 2015....wimbo wa chadema katika kampeni uliimba ''tuwapige chini mafisadi'' sasa ni wapi?...moja ya gamba alikuwa ni Lowassa kwa hiyo mmeamua kulivaa gamba....Lema aliwahi kusema kwenye kampeni huko Arumeru....'ni heshima kubwa kwa Mungu kumuita Lowassa fisadi''...embu waulize hao 'makamanda'
 
nilishaeleza swala sio kwamba yeye sio mtuhumiwa

kama walivyo
MNA Maana
Nyinyi mna serikali mpelekeni mahakamani kama pamoja nanyi !

Kwani kutoweka inazuia nini ?

Hivi kama wewe unapinga ufisadi mbona mmemchagua

mtuhumiwa Kule Bungeni?
Kuondokelewa, kunapunguza tuhuma ?

Acheni hiZo ;Mmekwama
 
Siasa ni sayansi!??Inawezekana, lakini sio hizi za chadema bhana, hizi ni arts aka usanii
 
nilishaeleza swala sio kwamba yeye sio mtuhumiwa

kama walivyo
MNA Maana
Nyinyi mna serikali mpelekeni mahakamani kama pamoja nanyi !

Kwani kutoweka inazuia nini ?

Hivi kama wewe unapinga ufisadi mbona mmemchagua

mtuhumiwa Kule Bungeni?
Kuondokelewa, kunapunguza tuhuma ?

Acheni hiZo ;Mmekwama
Unatumia nguvu nyingi kuupinga ukweli.
 
Vyama vyetu vya siasa katika Dunia ya Tatu vina haja ya kujitathmin upya. Hapo namaanisha vyama tawala na vile pinzani. Siasa zetu bado zina walakini mkubwa.
Umesema vyema kabisa Kobe_Mzee. Matatizo yapo kwenye chama tawala, na yapo pia kwenye vyama vya upinzani. La muhimu kwa maendeleo ya tsifa hili ni vyama kujitafakari. Kwetu sisi kama wananchi wa kawaida (sio makada wa vyama) si sahihi kuguna kwa makosa ya upinzani tu huku tukipigia makofi makosa ya chama tawala. Mwishowe hayo yatatuathiri wrote bila kubagua.
 
Watu wengi sana hupenda kulaumu wakati huo wao huwa hawana mchango hata kidogo zaidi ya kulaumu Na kusifia upande huu au ule! Kufanya siasa ya vyama vingi kwenye nchi ambazo majeshi Na dola yote Kwa ujumla huwa watesi Na watetezi WA chama cha kilichopo madarakani! Akina mbowe mnaowasema wanamsimamo thabiti sana!
Kuhusu ukuta hata wasipoandamana wamefanikiwa maana mwezi mmoja mzima watu wameiba juu ya ukuta Na kusema ukuta. Wafanya mazoezi wamefanya Na wengi wameongea Kwa hakika wamefanikiwa! Kila wakati jiulize mchango wako nini ambao una haki ndani yake!
Unaelewa kipimo cha mafanikio? Ni pale lengo lako linapotimia. Je unajua lengo la UKUTA? Unaweza kuwaeleza wananchi udikteta umeishaje?
 
Ni vizuri tukatumia jukwaa letu kwa kuelimishana kuliko kulaumu, kuchocheana na kudanganyana.

UKUTA ina lengo la kufikisha ujumbe kwamba nchi hii inatawaliwa kidikteta na madai mengine ya CHADEMA unayosema ni halali. Unaenda mbali zaidi na kutujengea hofu kwamba kutakuwa na machafuko, kiasi titajuta, mh!
1) Mdai gani ya CHADEMA ni halali na kwa misingi ipi!
2) Kutakuwa machafuko yapi kwa nini, njia zipi na kwa kiwango gani!
3) Hatua gani zichukuliwe, bila kulaumu mtu, kikundi, taasisi au chombo chochote!

TUSIFICHE LENGO BAYA NYUMA YA PAZIA LA KATIBA

Mkuu, sijatoa unabii kua nchi itaingia kwenye machafuko.
Binafsi ni muumini wa Taifa bila upinzank Imara, tunaweza tusipige hatua ya maana.

Watanzania wengi waliamini zamu hii, Bunge litakua Moto sana kwakua wabunge wa upinzani wameongezeka. Lakini hali ni tofauti sana. Upinzani umedhohofu sana bila kujali wingi wao. Kwangu hii ni dalili ya kudumaa.

Pia Bunge limekua controlled:-wana edit kwanza ndio wanatupa mrejesho kile kilichojiri. Kwangu Hii si sawa kabisa.

Naunga mkono UKUTA.
Kwasababu mpaka sasa sijajua sababu gani serikali inauogopa.
Siamini katika Blatant arguments kua "ukuta" unaleta vurugu au vita.

Zzk aliongea mkutanoni, kuhusu wao kutimuliwa bungeni, kupanda kwa bei ya sukari, uchumi na mambo mengine. Serikali ikaja na zuio la mikutano ya siasa.

Ukiwa mpinzani na ukawa Tajiri unakua katika wakati mgumu sana.

Africa is the same.

Ukuta ni sehemu.muhimu
Hata hivyo kuna kila dalili kua.mkakati wowote wa upinzani utakua hijacked na kua blocked na mfumo dola.
Hatua madhubuti ni kuujadili ukuta every single day. Ili kila mtanzanja aelewe. Wako.wengi hawana habari yoyote
 
Dr. Slaa na Septemba Mosi, 2016 ‘Siasa ni sayansi’ - Kuelekea mwaka mmoja tangu aachane na CHADEMA (Septemba,1 2015).

‘Siasa ni sayansi’ ni msemo wenye maneno machache ambao ulinenwa na Dr.Wilbod Slaa Septemba, mosi mwaka 2015 wakati anatangaza rasmi sababu zake kuachia ngazi CHADEMA na kujivua unanachama na kujiuzulu siasa.

Takribani mwaka mmoja baadaye Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anaitangaza Septemba Mosi mwaka 2016 kama siku ya kuanza maandamano ya kupinga kile walichokiita ‘udikteta’.. UKUTA.

Ikumbukwe Dr.Slaa alijitokeza septemba,mosi 2015 ili kuzima uzushi/propaganda wa kuwa yupo likizo uliyoenezwa kwa kipindi cha takribani miezi miwili na sasa imepita takribani miezi miwili toka Mbowe atangaze UKUTA kuelekea Septemba mosi 2016….. Hakika ni mgongano wa ajabu!....ni propaganda nzito zilizochukuwa miezi miwili kuwaaminisha watanzania mambo yasiyokuwepo/uongo…lakini Septemba mosi 2015 Dr. Slaa alikanusha na kuwaacha mdomo wazi..ya septemba mosi 2016 yanafurahisha…tusubiri!

Siasa ni sayansi ina maana kubwa, sasa ni dhahiri sasa CHADEMA haina wanasayansi katika siasa bali kuna wapiga propaganda wenye hadaa nyingi..! Prof. Baregu anautetea utafiti wa TADIP?

Siasa ni sayansi ina maana ya kupanga mipango halisi na yenye kuetekelezeka na sio kujipaka mate machoni ili kuhadaa kuwa unatiririka na machozi!...Ni ngumu kuaminika.

Siasa ni sayansi ina maana ya kuetengeneza ajenda/hoja endelevu ambazo zitadumu misimu yote iwe utawala wa kiongozi yeyote…!

Siasa ni sayansi ina maana ya kuunganisha fikra za wananchi katika hoja zinazoibuliwa….inahitajika sayansi ya hali ya juu kujua kuwa wananchi wanahitaji nini kwa sasa na sio tu kuja na ‘’hoja maarufu’’ isiyogusa maisha yao…hoja ya udikteta haiwaingii wananchi kwani wanauhuru wote wanaouhitaji…hakukuwa na sayansi katika kutafakari.

Siasa ni sayansi inamaanish kuweza kuchambua madhara ya kushirikiana na baadhi ya watu katika kujenga imani ya wananchi ya muda mrefu….kushirikiana na mtu tuliyemdhihaki na kumfanya kuwa kinara?
Tutamwamini vipi? Je, waweza kumpa urithi motto wa jirani yako sababu tu anafaulu darasani na kumnyima mwanao?

Siasa ni sayansi ni pamoja na kuwa na kiongozi ambaye hata akijumuika na viongozi wa vyama vingine/hasimu haitaharibu taswira ya ajenda yetu kwani wafuasi hawatahoji au kuwepo kwake..na sio kuwa na kinara ambaye akipiga tu picha na viongozi wa vyama vingine inabadilisha mtazamo na dhamira ya chama na wanachama.

Siasa ni sayansi inamaanisha kuwa kiongozi unayempa dhamana ni yule mwenye sifa ya kusaidia wananchi...sasa kituko cha mwaka katika moja ya vibwagizo ambavyo CHADEMA walimsifia kwa furaha ni pamoja na kuinadi sifa mbaya kuwa alikuwa kinara wa mgomo wa madaktari nchini ulioacha maelfu vilema na vifo kuwa Katibu Mkuu wa chama..Dr.Mashinji....eti Mbowe na wananchedema wakamsifia kuwa kwa uzoefu huo wa kufanikisha mgomo wa madaktari dhidi ya serikali na wananchi kuwa ni mtu sahihi kuongoza mapambano....lo lo lo...eti hata UKUTA wananchi wakifa itakuwa ni moja ya mafanikio yake....'siasa ni sayansi'.

Siasa ni sayansi ina maana pana zaidi kubwa ya yote ilkiwa ni kubuni na kuchambua na mipango,sera ambazo zitaleta maendeleo kwa wananchi bila kuzingatia chama kipo madarakani au upinzani.

Mada hii ni maalum kuelekea septemba mosi ambapo ni siku Dr. Slaa anatimiza mwaka mmoja tangu ajitoe CHADEMA.
Sayansi ya siasa .ulichotakiwa kukidadavua hapa ni sayansi .lakini tena na wewe umelete siasa pekee nikama vile ujaelewe sayansi inavyotumika kwenye siasa.na laiti ungejua maana ya Dr slaa kutoa kauli ili ilikuwa kuwasimanga au kuwaumbua waletaa siasa kavu kama wewe .usingeleta Mada hii hapa jf .nambaya zaidi kupingia jambo linalofanyika kutumia sayansi ya siasa
 
Mkuu, sijatoa unabii kua nchi itaingia kwenye machafuko.
Binafsi ni muumini wa Taifa bila upinzank Imara, tunaweza tusipige hatua ya maana.

Watanzania wengi waliamini zamu hii, Bunge litakua Moto sana kwakua wabunge wa upinzani wameongezeka. Lakini hali ni tofauti sana. Upinzani umedhohofu sana bila kujali wingi wao. Kwangu hii ni dalili ya kudumaa.

Pia Bunge limekua controlled:-wana edit kwanza ndio wanatupa mrejesho kile kilichojiri. Kwangu Hii si sawa kabisa.

Naunga mkono UKUTA.
Kwasababu mpaka sasa sijajua sababu gani serikali inauogopa.
Siamini katika Blatant arguments kua "ukuta" unaleta vurugu au vita.

Zzk aliongea mkutanoni, kuhusu wao kutimuliwa bungeni, kupanda kwa bei ya sukari, uchumi na mambo mengine. Serikali ikaja na zuio la mikutano ya siasa.

Ukiwa mpinzani na ukawa Tajiri unakua katika wakati mgumu sana.

Africa is the same.

Ukuta ni sehemu.muhimu
Hata hivyo kuna kila dalili kua.mkakati wowote wa upinzani utakua hijacked na kua blocked na mfumo dola.
Hatua madhubuti ni kuujadili ukuta every single day. Ili kila mtanzanja aelewe. Wako.wengi hawana habari yoyote
Tatizo unadanganywa kuwa bila kuonyeshwa live ndio wabunge wamezibwa....hata wakiedit mambo hayazuiliki...kule bungeni ni hoja kwa hoja...hata bila ya TV bunge liliwaka moto...G55...,Skandali za Prof.Mbilinyi,Mzondakaya nk....ni watanzania wachache sana hufuatilia bunge na kwa namna yoyote haijawahikuzuia bunge kufanya kazi yake.
 
Sayansi ya siasa .ulichotakiwa kukidadavua hapa ni sayansi .lakini tena na wewe umelete siasa pekee nikama vile ujaelewe sayansi inavyotumika kwenye siasa.na laiti ungejua maana ya Dr slaa kutoa kauli ili ilikuwa kuwasimanga au kuwaumbua waletaa siasa kavu kama wewe .usingeleta Mada hii hapa jf .nambaya zaidi kupingia jambo linalofanyika kutumia sayansi ya siasa
Umepanik..badala ya kutoa joja.
 
Back
Top Bottom