Dr. Slaa na Septemba Mosi: ‘Siasa ni sayansi’

Dr. Slaa na Septemba Mosi: ‘Siasa ni sayansi’

NI makosa kwa sababu ni WAPINZANI wako sahihi kwa sababu ni watawala hivyo tu basi ama kweli akili ni nywele sote tunazo
 
Tatizo unadanganywa kuwa bila kuonyeshwa live ndio wabunge wamezibwa....hata wakiedit mambo hayazuiliki...kule bungeni ni hoja kwa hoja...hata bila ya TV bunge liliwaka moto...G55...,Skandali za Prof.Mbilinyi,Mzondakaya nk....ni watanzania wachache sana hufuatilia bunge na kwa namna yoyote haijawahikuzuia bunge kufanya kazi yake.
Niliona wabunge wa upinzani wakihoji kua kuna mtu aliuliza swali. Ile ya ku edit usiku wa manane, hawakumuonyesha., bali wachangiaji wengine walionyeshwa.

Pili Sababu za SIRI-kali kuzuia live hazina mashiko na zimekua zikibadilika badilika.
Visingizio vinapobadilika vinatuongezea maswali sisi walaji taarifa.

Bunge Live lina faida kulingana na maswala ya transparency katika governance.

Wananchi wanakua active member kujua nia njema ya serikali yao kupitia wabunge wao. Ikiwemo kuwahoji mitazamo yao ikiwa watachangia pumba. Kama yule muheshimiwa mwenye uchungu mwingi.
 
Ooh that's right! Siasa ni sayansi.. bila kubuni sera, mikakati ya kuendesha nchi na wananchi kuwaelewa mtaishiaga ccm wezi, mbona wabunge wa upinzani wanashinda wanapitia wapi? Ccm inajivunia baraka alizoxiacha Nyerere.
 
Umesema vyema kabisa Kobe_Mzee. Matatizo yapo kwenye chama tawala, na yapo pia kwenye vyama vya upinzani. La muhimu kwa maendeleo ya tsifa hili ni vyama kujitafakari. Kwetu sisi kama wananchi wa kawaida (sio makada wa vyama) si sahihi kuguna kwa makosa ya upinzani tu huku tukipigia makofi makosa ya chama tawala. Mwishowe hayo yatatuathiri wrote bila kubagua.
Swadakta Zikomo Songea
 
Dr. Slaa na Septemba Mosi, 2016 ‘Siasa ni sayansi’ - Kuelekea mwaka mmoja tangu aachane na CHADEMA (Septemba,1 2015).

‘Siasa ni sayansi’ ni msemo wenye maneno machache ambao ulinenwa na Dr.Wilbod Slaa Septemba, mosi mwaka 2015 wakati anatangaza rasmi sababu zake kuachia ngazi CHADEMA na kujivua unanachama na kujiuzulu siasa.

Takribani mwaka mmoja baadaye Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anaitangaza Septemba Mosi mwaka 2016 kama siku ya kuanza maandamano ya kupinga kile walichokiita ‘udikteta’.. UKUTA.

Ikumbukwe Dr.Slaa alijitokeza septemba,mosi 2015 ili kuzima uzushi/propaganda wa kuwa yupo likizo uliyoenezwa kwa kipindi cha takribani miezi miwili na sasa imepita takribani miezi miwili toka Mbowe atangaze UKUTA kuelekea Septemba mosi 2016….. Hakika ni mgongano wa ajabu!....ni propaganda nzito zilizochukuwa miezi miwili kuwaaminisha watanzania mambo yasiyokuwepo/uongo…lakini Septemba mosi 2015 Dr. Slaa alikanusha na kuwaacha mdomo wazi..ya septemba mosi 2016 yanafurahisha…tusubiri!

Siasa ni sayansi ina maana kubwa, sasa ni dhahiri sasa CHADEMA haina wanasayansi katika siasa bali kuna wapiga propaganda wenye hadaa nyingi..! Prof. Baregu anautetea utafiti wa TADIP?

Siasa ni sayansi ina maana ya kupanga mipango halisi na yenye kuetekelezeka na sio kujipaka mate machoni ili kuhadaa kuwa unatiririka na machozi!...Ni ngumu kuaminika.

Siasa ni sayansi ina maana ya kuetengeneza ajenda/hoja endelevu ambazo zitadumu misimu yote iwe utawala wa kiongozi yeyote…!

Siasa ni sayansi ina maana ya kuunganisha fikra za wananchi katika hoja zinazoibuliwa….inahitajika sayansi ya hali ya juu kujua kuwa wananchi wanahitaji nini kwa sasa na sio tu kuja na ‘’hoja maarufu’’ isiyogusa maisha yao…hoja ya udikteta haiwaingii wananchi kwani wanauhuru wote wanaouhitaji…hakukuwa na sayansi katika kutafakari.

Siasa ni sayansi inamaanish kuweza kuchambua madhara ya kushirikiana na baadhi ya watu katika kujenga imani ya wananchi ya muda mrefu….kushirikiana na mtu tuliyemdhihaki na kumfanya kuwa kinara?
Tutamwamini vipi? Je, waweza kumpa urithi motto wa jirani yako sababu tu anafaulu darasani na kumnyima mwanao?

Siasa ni sayansi ni pamoja na kuwa na kiongozi ambaye hata akijumuika na viongozi wa vyama vingine/hasimu haitaharibu taswira ya ajenda yetu kwani wafuasi hawatahoji au kuwepo kwake..na sio kuwa na kinara ambaye akipiga tu picha na viongozi wa vyama vingine inabadilisha mtazamo na dhamira ya chama na wanachama.

Siasa ni sayansi inamaanisha kuwa kiongozi unayempa dhamana ni yule mwenye sifa ya kusaidia wananchi...sasa kituko cha mwaka katika moja ya vibwagizo ambavyo CHADEMA walimsifia kwa furaha ni pamoja na kuinadi sifa mbaya kuwa alikuwa kinara wa mgomo wa madaktari nchini ulioacha maelfu vilema na vifo kuwa Katibu Mkuu wa chama..Dr.Mashinji....eti Mbowe na wananchedema wakamsifia kuwa kwa uzoefu huo wa kufanikisha mgomo wa madaktari dhidi ya serikali na wananchi kuwa ni mtu sahihi kuongoza mapambano....lo lo lo...eti hata UKUTA wananchi wakifa itakuwa ni moja ya mafanikio yake....'siasa ni sayansi'.

Siasa ni sayansi ina maana pana zaidi kubwa ya yote ilkiwa ni kubuni na kuchambua na mipango,sera ambazo zitaleta maendeleo kwa wananchi bila kuzingatia chama kipo madarakani au upinzani.

Mada hii ni maalum kuelekea septemba mosi ambapo ni siku Dr. Slaa anatimiza mwaka mmoja tangu ajitoe CHADEMA.
Mtu akikubishia mkuu,
Jua ni Tahira level one...
Well said mkuu...
Bravo!!!!!
 
Watu wengi sana hupenda kulaumu wakati huo wao huwa hawana mchango hata kidogo zaidi ya kulaumu Na kusifia upande huu au ule! Kufanya siasa ya vyama vingi kwenye nchi ambazo majeshi Na dola yote Kwa ujumla huwa watesi Na watetezi WA chama cha kilichopo madarakani! Akina mbowe mnaowasema wanamsimamo thabiti sana!
Kuhusu ukuta hata wasipoandamana wamefanikiwa maana mwezi mmoja mzima watu wameiba juu ya ukuta Na kusema ukuta. Wafanya mazoezi wamefanya Na wengi wameongea Kwa hakika wamefanikiwa! Kila wakati jiulize mchango wako nini ambao una haki ndani yake!
Kumbe lengo ni kupiga makelele ili msikike mpo au kutoa hoja zenye mashiko kwa lengo la kujenga maana toa tafsiri ya Udicteta uone kama haya siyo yale tulikuwa tunaambiwa Dr yupo mapunziko ya siasa. Kubadili gia ya ndege angani
 
nilishaeleza swala sio kwamba yeye sio mtuhumiwa

kama walivyo
MNA Maana
Nyinyi mna serikali mpelekeni mahakamani kama pamoja nanyi !

Kwani kutoweka inazuia nini ?

Hivi kama wewe unapinga ufisadi mbona mmemchagua

mtuhumiwa Kule Bungeni?
Kuondokelewa, kunapunguza tuhuma ?

Acheni hiZo ;Mmekwama
wewe shule yako mashaka sana, maana hata kuandika kiswahili ni issue. he Lema sijui Lema gani 😱😱 yule mwingine kagoma kula naye shule ilimshinda nasikia alikuwa mwizi wa magari lakini anajiita mkombozi wa Arusha 😳😳😵 issue pole go back to school usilete ujinga hapa.😛
 
Dr Slaa angekuwepo tayari angelikuwa amepeleka mapato na matumizi ya CDM kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

Hawa waliopo wametia pamba masikioni, hii inaonesha kuwa hata wakitwaa nchi watafanya mambo kiholela.

Dr Slaa alikuwa rais wa mioyo yetu.....Sultan Mbowe alimfukuza kwa sababu ya pesa.
Mbowe alimfukuza Dr Slaa!? You are so incredible.
 
Mkuu, sijatoa unabii kua nchi itaingia kwenye machafuko.
Binafsi ni muumini wa Taifa bila upinzank Imara, tunaweza tusipige hatua ya maana.

Watanzania wengi waliamini zamu hii, Bunge litakua Moto sana kwakua wabunge wa upinzani wameongezeka. Lakini hali ni tofauti sana. Upinzani umedhohofu sana bila kujali wingi wao. Kwangu hii ni dalili ya kudumaa.

Pia Bunge limekua controlled:-wana edit kwanza ndio wanatupa mrejesho kile kilichojiri. Kwangu Hii si sawa kabisa.

Naunga mkono UKUTA.
Kwasababu mpaka sasa sijajua sababu gani serikali inauogopa.
Siamini katika Blatant arguments kua "ukuta" unaleta vurugu au vita.

Zzk aliongea mkutanoni, kuhusu wao kutimuliwa bungeni, kupanda kwa bei ya sukari, uchumi na mambo mengine. Serikali ikaja na zuio la mikutano ya siasa.

Ukiwa mpinzani na ukawa Tajiri unakua katika wakati mgumu sana.

Africa is the same.
Ha ha ha msome Kipanya.

14063731_10154471553309339_5595812698222202422_n.jpg


Ukuta ni sehemu.muhimu
Hata hivyo kuna kila dalili kua.mkakati wowote wa upinzani utakua hijacked na kua blocked na mfumo dola.
Hatua madhubuti ni kuujadili ukuta every single day. Ili kila mtanzanja aelewe. Wako.wengi hawana habari yoyote
 
September mosi Tutakua kwenye sayansi ya kutunza mazngira kwa kufanya usafi
Na tutahakikisha uchafu wowote tutakao uona tunauweka kwenye gari la taka, na hakika tutauchoma moto.
 
Back
Top Bottom