Dr Slaa na Mbowe,Chadema kauli zenu zina Utata! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa na Mbowe,Chadema kauli zenu zina Utata!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mlengo wa Kati, May 11, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kauli za viongozi wa Chadema lazima ziangaliwe kwa Umakini mkubwa lasivyo Watanzania watazizoea na kushindwa kujua lipi ni kweli lisemwalo na viongozi hao!
  Mbowe akiwa Kyela alisema kuna taasisi moja ya utafiti ya nje(hata jina hakuitaja) kuwa imegundua asilimia 35 ya bajeti ya Tanzania inaliwa na Viongozi kila Mwaka kwa kujenga magorofa na majumba!
  Dr Slaa nae akiwa Tunduma amesema Biilioni 200 zimeliwa na Viongozi wa serikali zilikua kwa ajiri ya kulipa deni la Taifa
  Mheshimiwa Sugu(Mr Two) akiwa kyela amekaliliwa akisema ameamua kua Mbunge wa. Kyela!
  Regia Mtema akiwa Tunduma amekaliliwa akisema kuna watoto wanakosa ada wakati wabunge wakilipana hela kubwa na kuishi maisha ya kifahari!

  My take:
  Mbowe anajua kweli asilimia 35 ya bajeti ni kiasi gani?
  Dr Slaa tumehangaika sana na 94 Bilioni zisilipwe kwa Dowans kwa 200 Bilioni anazisema kimzaha tu kweli au ni siasa?
  Mh Sugu hivi jimbo unalichukulia kama kijiji au mtaa? Kero za mbeya mjini zimeisha na sasa unataka umalize za Kyela
  Mh Regia Mtema una amaanisha Wabunge gani? Wabunge Wachadema hawalipwi hizo hela?
  Chadema jipangeni kwa Kauli zenu Watanzania wana wasikiliza na Kuzipima!
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Yep! Angalizo muhimu hili.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hizo sehemu nilizokuwekea RED NI KAZI YA SERIKALI KUKANUSHA NA KUTUELEZA UKWELI NI UPI, KAMA WALIVYOELEKEZWA NA BOSI WAO KWENYE SEMINA ELEKEZI. OTHERWISE DR SLAA ANAYO REKODI SAFI YA KUTUAMBIA UKWELI WATANZANIA.
  kuhusu Sugu na Regia Mtema hao bado wanajifunza siasa, tuwape muda kwanza unajuwa siasa nazo zina mbwembwe zake, lakini all in all hoja yako ni nzuri.
   
 4. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndio maana wana siasa watz siwahamini hata kidogo wawe wa ccm au cdm, wote wezi tu na wanasumbuliwa na njaa. Kwa style hii napata picha mbaya sana kwa CDM chama ambacho nilikiamini na kudhani kina watu makini kumbe sivyo ndivyo.

  Hii ni dalili mbaya kwa CDM tena ambayo imeanza kuonekana asubuhi yote hii.
   
 5. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Ww Tundu la kati usitafute pa kuhemea, embu tutajie asilimia 35 ya bajeti ni kiasi gani? Tatizo lako ni dharau kwa viongozi wasio wa CCM na upumbavu huo ni HULKA ya wanachama na vigogo wa nchi hii na mashoga na malaya wengi wanaonufaika na mfumo nyonyaji na kandamiz km huu. Suala la Sugu usichoelewa wewe ni nini? Ama ni propaganda kama kawaida kutafuta vi phrase vidogovidogo kukidh kiu yako ya propaganda. Ni bora niamini takwimu na komitment ya upinzani kuliko ya wale mafisi wenye matumbo makubwa na maumbile makubwa nyuma sababu ya unyonyaji.
   
 6. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Next time lete hoja sio maswali ...
   
 7. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Hakuna uhalali wowote wa kufanya ukwapuaji kwenye Mali za Umma, hATA Kama ni sh 5 mali ya umma, somebody anaweza kusema mia Tano, then huyu mwizi anasema hapana niliiba mia tano Tu!! Then tuna pa kuanzia sasa!! Hivyo kwenye siasa kama wizi upo your free to say any figure then Wezi wenyewe wanarekebisha figure!!
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbowe akiwa Kyela alisema kuna taasisi moja ya utafiti ya nje(hata jina hakuitaja) kuwa imegundua asilimia 35 ya bajeti ya Tanzania inaliwa na Viongozi kila Mwaka kwa kujenga magorofa na majumba!
  Dr Slaa nae akiwa Tunduma amesema Biilioni 200 zimeliwa na Viongozi wa serikali zilikua kwa ajiri ya kulipa deni la Taifa
  Mheshimiwa Sugu(Mr Two) akiwa kyela amekaliliwa akisema ameamua kua Mbunge wa. Kyela!
  Regia Mtema akiwa Tunduma amekaliliwa akisema kuna watoto wanakosa ada wakati wabunge wakilipana hela kubwa na kuishi maisha ya kifahari!

  My take:
  Mbowe anajua kweli asilimia 35 ya bajeti ni kiasi gani?
  Dr Slaa tumehangaika sana na 94 Bilioni zisilipwe kwa Dowans kwa 200 Bilioni anazisema kimzaha tu kweli au ni siasa?
  Mh Sugu hivi jimbo unalichukulia kama kijiji au mtaa? Kero za mbeya mjini zimeisha na sasa unataka umalize za Kyela
  Mh Regia Mtema una amaanisha Wabunge gani? Wabunge Wachadema hawalipwi hizo hela?
  Chadema jipangeni kwa Kauli zenu Watanzania wana wasikiliza na Kuzipima![/QUOTE]

  Mbowe anajua kweli asilimia 35 ya bajeti ni kiasi gani?
  Kikwete mwenyewe alisema kuwa 30% ya fedha za Umma zinaliwa na viongozi wabovu serikalini kabla ya uchaguzi sikumbuki tarehe na mwezi. Sasa kwanini unashangaa 35% ya mbowe haushangai 30% ya Kikwete mwenyewe? Inawezekana kabisa JK amepunguza 5% kwa kuona aibu.

  Pili, kikwete hakutaja reference yo yote, alijiongelea mwenyewe, wakati Mbowe ana reference. Je kati ya hawa tumwamini nani? Mimi nitamwamini mbowe ambaye ana kitu cha kurejea hata kama hakutaja jina lake kwa kuwa historia ya kufanya mzaha ktk masuala yanayohusu taifa.
  Dr Slaa nae akiwa Tunduma amesema Biilioni 200 zimeliwa na Viongozi wa serikali zilikua kwa ajiri ya kulipa deni la Taifa
  Tangu lini Dr Slaa akawa mfanya mzaha? Yaani azunguke nchi kutania au kusema uwongo? Ingekuwa hivyo, kwa kauli zake zote alizotoa dhidi ya viongozi wakubwa akiwahusisha na ufisadi akiwepo kikwete wangeshampeleka jela - Yuko makini. Baraza kuu lilipitisha maandamano hayo ili wakawaeleze watz ukweli tu. Hawakutumwa kwenda kufanya mzaha. Hiyo sivyo Dr Slaa binafsi alivyo, na siyo nmaazimio ya baraza kuu la Chadema lililowatuma. Kumbuka hawajiendei, wametumwa.

  Mheshimiwa Sugu(Mr Two) akiwa kyela amekaliliwa akisema ameamua kua Mbunge wa. Kyela!
  Hivi kweli kuwasemea watu wa kyela bungeni ni mpaka umalize matatizo ya mbeya mjini? Hivi wabunge ambao ni mawaziri wanapotumikia nchi nzima kama mawaziri wamemaliza matatizo katika majimbo yao? Kama kipimo cha kuwatatulia matatatizo watu wa majimbo mengine ni kumaliza matatizo ya jimbo lako?, Kama ndivyo, mbona pinda jimboni kwake watu hawana umeme wala nyumba za maana? Sembuse mr two kuwasemea majirani zake wa kyela bungeni? I don't see a problem, kama nimezidiwa na partisanship au uchadema nikosolewe kwa hoja.

  Mh Regia Mtema una amaanisha Wabunge gani? Wabunge Wachadema hawalipwi hizo hela?
  Chadema tuna deal na sera ya nchi (national policy) -not petty issues. Ndiyo maana Dr Slaa wakati anagombea hakuahidi bajaji, au kuwalipia watu madeni ya SACCOS, wala ujenzi wa vijibarabara vya hapa na pale aili apate kura. Yeye alijadili sera ya kodi, mfumo wa elimu, sera za ujenzi kwa ujumla, ukubwa wa serikali, anahoja kazi wakuu wa wilaya na mikoa wakati kikwete ana deal na kazi za wenyeviti wa Halmashauri na manispaa via mabajaji.
  Regia kama mkuu wake wa kazi anajadili sera ya malipo ya wabunge kuwa ni kubwa na haiendani na ukuaji wa uchumi wetu wala haitendi haki kwa wafanyakza wengine nchini. Yeye na wenzake kususia mishahara yao ubunge kwa kuwa wanalalamika kuwa ni mikubwa siyo utatuzi, ni sawa na kumsusia mlevi pombe. Si ndo atafurahi?.
  Pili, itawapunguzia watanzania umaskini kwa asilimia ngapi? Si, bora akachukua halafu akatumia kwenye maandamano kuwaelimisha watanzania kama anavyofanya sasa?
  Hitimisho langu, kauli za viongozi wa Chadema ni hazina hata kidogo kwa mujibu wa thread hii.
   
 9. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Report ya Mkaguzi mkuu wa serikali iko nje, imetoa taarifa juu ya wizi wa mabilioni mengi tu yaliyoibiwa
  na serikali katika kipindi cha mwaka mmoja ulioisha. hatujasikia kiongozi hata mmoja wa serikali
  akijitokeza na kuijadiri report hiyo, wananchofanya chadema ni kuitumia report hiyo hiyo kufanya analysis
  na kuwaeleza wananchi.

  Jakaya ameishasema mawaziri wake wafanye hivyo hivyo, of course wataeleza mafanikio yao, kama
  wataweza kutuelezea juu ya ujambazi ulio kwenye report hizo pia, tusubiri tuone watatumia style gani.

  Billion 200 anazozingumzia DR SLAA, Hajasema zimeibiwa katika muda gani, what if anazungumia pesa
  za EPA, sababu ndio hasa zinahusika na deni la nje, utabisha? na kwa mtazamo wake hapo ndio
  wamemuelewa vizuri utabisha? jiongeze kwa matamshi ya mbowe pia.

  Ufisadi umewafanya hata wasomi wakubwa kabisa katika nchi hii kuwa na akili kama za matope,
  hawawezi kujibu hoja kwa hoja wamekuwa kama wanawake wa uswailini majibu yao mapesi tu,
  uo uongo uo ungo, what is the truth...

  Chadema wanafanya siasa ambazo ni mpya kabisa nchini mwetu, singai gap lililopo kati yake
  na vyama vingine vyote vya siasa pamoja na serikali.
   
 10. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu sikubaliani na wewe kwa sababu zifuatazo.
  Mbowe anajua kweli asilimia 35 ya bajeti ni kiasi gani?
  Kikwete mwenyewe alisema kuwa 30% ya fedha za Umma zinaliwa na viongozi wabovu serikalini kabla ya uchaguzi sikumbuki tarehe na mwezi. Sasa kwanini unashangaa 35% ya mbowe haushangai 30% ya Kikwete mwenyewe? Inawezekana kabisa JK amepunguza 5% kwa kuona aibu.

  Pili, kikwete hakutaja reference yo yote, alijiongelea mwenyewe, wakati Mbowe ana reference. Je kati ya hawa tumwamini nani? Mimi nitamwamini mbowe ambaye ana kitu cha kurejea hata kama hakutaja jina lake kwa kuwa historia ya kufanya mzaha ktk masuala yanayohusu taifa.
  Dr Slaa nae akiwa Tunduma amesema Biilioni 200 zimeliwa na Viongozi wa serikali zilikua kwa ajiri ya kulipa deni la Taifa
  Tangu lini Dr Slaa akawa mfanya mzaha? Yaani azunguke nchi kutania au kusema uwongo? Ingekuwa hivyo, kwa kauli zake zote alizotoa dhidi ya viongozi wakubwa akiwahusisha na ufisadi akiwepo kikwete wangeshampeleka jela - Yuko makini. Baraza kuu lilipitisha maandamano hayo ili wakawaeleze watz ukweli tu. Hawakutumwa kwenda kufanya mzaha. Hiyo sivyo Dr Slaa binafsi alivyo, na siyo nmaazimio ya baraza kuu la Chadema lililowatuma. Kumbuka hawajiendei, wametumwa.

  Mheshimiwa Sugu(Mr Two) akiwa kyela amekaliliwa akisema ameamua kua Mbunge wa. Kyela!
  Hivi kweli kuwasemea watu wa kyela bungeni ni mpaka umalize matatizo ya mbeya mjini? Hivi wabunge ambao ni mawaziri wanapotumikia nchi nzima kama mawaziri wamemaliza matatizo katika majimbo yao? Kama kipimo cha kuwatatulia matatatizo watu wa majimbo mengine ni kumaliza matatizo ya jimbo lako?, Kama ndivyo, mbona pinda jimboni kwake watu hawana umeme wala nyumba za maana? Sembuse mr two kuwasemea majirani zake wa kyela bungeni? I don't see a problem, kama nimezidiwa na partisanship au uchadema nikosolewe kwa hoja.

  Mh Regia Mtema una amaanisha Wabunge gani? Wabunge Wachadema hawalipwi hizo hela?
  Chadema tuna deal na sera ya nchi (national policy) -not petty issues. Ndiyo maana Dr Slaa wakati anagombea hakuahidi bajaji, au kuwalipia watu madeni ya SACCOS, wala ujenzi wa vijibarabara vya hapa na pale aili apate kura. Yeye alijadili sera ya kodi, mfumo wa elimu, sera za ujenzi kwa ujumla, ukubwa wa serikali, anahoja kazi wakuu wa wilaya na mikoa wakati kikwete ana deal na kazi za wenyeviti wa Halmashauri na manispaa via mabajaji.
  Regia kama mkuu wake wa kazi anajadili sera ya malipo ya wabunge kuwa ni kubwa na haiendani na ukuaji wa uchumi wetu wala haitendi haki kwa wafanyakza wengine nchini. Yeye na wenzake kususia mishahara yao ubunge kwa kuwa wanalalamika kuwa ni mikubwa siyo utatuzi, ni sawa na kumsusia mlevi pombe. Si ndo atafurahi?.
  Pili, itawapunguzia watanzania umaskini kwa asilimia ngapi? Si, bora akachukua halafu akatumia kwenye maandamano kuwaelimisha watanzania kama anavyofanya sasa?
  Hitimisho langu, kauli za viongozi wa Chadema ni hazina hata kidogo kwa mujibu wa thread hii.
   
 11. M

  Makupa JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  siku zote cdm huwa hawaimanishi wanachokuwa wanaongea ila kadri siku zinvyoyoyoma watanzania wameanza kuwaelewa na sitashangaa mwaka 2015 wakawa hawapo
   
 12. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio utapotea sio Chadema
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Great thinkers huwa wanatoa mifano halisi ili ujibiwe. Sasa hii generalization yako tutakusaidiaje?
  Siku zote chadema huwa wanamaanisha wanachosema. Mifano hai, walitaja mafisadi kumi na moja, Leo ndo wanatolewa magamba baada ya kukana kwa miaka na kusema chadema waongo. Sasa wanaumbuka kimya kimya.
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukiisha ona viongozi wana kauli nyingi nyingi kiasi hiki :
  1. Hawakujipanga na hawako organised
  2. Ni alama ya mtu / watu wanafiki
  3. Tujiepushe nao
   
 15. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  He he he eheeee, ununuzi wa magari chakavu ya mbowe wakati wao ndio wanaopinga, vp hapo mkuu? Slaa kula matapishi yake mwenyewe kwa kusema mishahara ya wabunge ni mikubwa , wakati yeye amelazimisha baraza kuu limlipe kama mbunge, hapo vp mkuu? . Ni kweli wanachosema sicho wanacho tenda. Kama data ndizo hizo
   
 16. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watu wengine mnatokea wapi mnakurupuka tu na , hoja nahisi ulitoka usingizini, sina uhakika huyu mtoa hoja ya wabunge wa chadema kuziangalia kauli zao kabla hawajatamka kama kweli ana darasa la kutosha kichwani mwake,

  In your own thinking , are you convinced with all the natural resources we have, the country like Tanzania to continue being among the poorest country in the world, tunaambiwa kila siku deni la taifa linaongezeka, inflation rate ndo hivyo tena,

  Kwa nini tusiamini kuwa fedha zinaliwa na wajanja wachache, na mind you mwanasiasa yoyote awe wa ccm, cdm, au vyama vingine anachoweza kutamka jukwaani ni ukweli au kinakaribiana na ukweli therefore is your responsibility kufuatilia na kujua, sio kukurupuka na hoja za kijinga hizo
   
 17. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Kweli Magamba mmebanwa mmezoea kula bila kunawa!! Mmeshutukiwa sasa naona mtaipata fresh!! Piga kote kote Docta wa Ukweli, Tutasikia mengi na semina elekezi kila kukicha!! Duh Aibu
   
 18. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  We ndo hujajipanga kajipange sasa kabla hujachelewa
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hebu nikumbushe umejiunga lini JF vile
   
 20. kimpango

  kimpango JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 515
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 80
  this is jf ambapo wa2 hawana haja ya kujadili nusu upembuzi sasa tuelewe kwamba anachokisema slaa na wenzake ni nusu tu ya ukweli lakini mdau jua nchi hii inaliwa na wewe umeshaanza kuliwa kama hujielewi wake up
   
Loading...