Sasa mnaposema CUF chama cha waarabu hivi Lipumba ni muarabu ?
Yaani wengine hamjui kabisa kuzungumza siasa ,siasa haina dini wala rangi ni kugandamiza tu.
Zitto kama mtamuangalia siku hizi picha haziendani na Chadema kwa kuwa alichokigundua Chadema ni kuwa hawana muelekeo wana matatizo ya ndani kwa ndani ,na wasemaji wa kubwa Chadena ni Slaa na Mbowe ,Zitto alikuwa mmoja wao lakini wameanza kumueka pembeni na amesikika kuwa hagombei tena ubunge kwa maana hagombei tena Chadema .
Unajua Chadema kinaonekana ni Chama cha watu wawili tu ,Mbowe na Slaa bila ya wao hakuna anaeweza kuzungumza na kuvutia wateja au wananchi ,mkutano unakuwa hovyo kabisa hauna kichwa wala miguu ni kama mkutano wa CCM kukosa TOT.
Zitto hawezi kuusema ukweli wake kwa sasa lakini kwa tuonavyo kuna tofauti kubwa imeanza kujitokeza ambazo zinaonyesha kuwa sio wanalindana bali wanawindana kila mmoja anataka aonekane yeye ni top kuliko mwenziwe hawana umoja kama tuonavyo katika CUF ,maana katika CUF kila mmoja ni kivutio kumshinda mwenziwe ,awepo jukwaani na ni jambo ambalo linawafanya wananchi wawe kwenye msimamo mzuri sana ,kwa kuwa atakaewahutubia basi anawatosheleza kabisa ,hilo halina ubishi kwa ushahidi kuwa inawezzekana miezi kupita humuoni mwenyekiti wala katibu kupanda majukwaani ,ni vijjana tu wanasema na kurapu kuliko wakubwa zao ,ila kwenye Chadema ni Mbowe na Slaa ,sio nawazarau hapana kinachihitajika ni kuwapisha wengine na kuwapa elimu ya uzungumzaji katika majukwaa ya kisiasa ,yapo memngi ya kuwavutia wananchi na si kuhusu mafisadi jambo ambalo limeanza kuchujuka na kuondoa mvuto,siku zinakwenda tumebakishwa na mafisadi yaani CCM wametuachia pelemende ya kijiti tumungunye katika mikutano hatuna jipya ,au uongo Chadema hawana jipya zaidi ya kusakama fisadi mmoja mmoja.
Sasa kama unavyoona wamejikita ndani ya UCCM upinzani unamtetea kada wa CCM how comes ,siasa za upinzani kila siku mnaambiwa
usijaribu kujiweka hata dakika moja kwenye Chama Tawala ,naweza kusema Zitto alifanikiwa kuchonganisha ndani ya CCM na kuzidisha matatizo akiigawa CCM mapande mawili ,alikuwa amefanikiwa kabisa lakini akina Slaa na Mbowe wamempiga na chini kweli au uongo ? Wao wapo na Mwakiembe wakimkandamiza Rostam wakati Mwakiyembe nae ana lake limemkaa shingoni na lilikuwa limeanza kushika kasi ,Mbowe na Slaa wamekuwa watetezi ,hivi kuna upinzani hapo ?
Zitto alikuwa ,naamini kabisa akijua gemu aliyokuwa akiicheza na kwa kweli ilianza kushika kasi ,CCM ilikwisha gawika ,serikali bunge mvutano mtupu ,sasa tujiulize yote yamekwenda wapi ?
Serikali ingenunua kwa wakati ule ingewezekana baadae kuibana kwa kuzitazama sheria za bunge ,tayari kungekuwepo na mtafaruku mwengine ,upinzani ungerudi kwa wananchi na kuwambia mnaona serikali yetu haifuati sheria ,kwani sheria hii na hii inasema hivi ,hapo ingewezekana kubambikiza mambu kibao ,kwa sasa ni vigumu kwani gemu imeshavurugika. Siasa sii mchezo mchafu ila unachezwa kwa triki na mitego ya uangalifu kabisa ,maana ilikuwa tayari Kikwete ameshatoa agizo kuwa panunuliwe ,kuna kitu alisema ambacho kiliashiria kuwa sheria zikiukwe au zisizuie kitu kama hivyo ,Na sita nae akajibu kuwa kama wapo wenye ubavu na wanunue lakini tusije tukaonana maadui hapa Bungeni kitu kama hivyo,ila kwa sasa mtego umeshateguliwa na imebaki makelele tu ,kubadilisha upepo.