Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Huku Hatuna Umeme,
nakosa mambo ya maana kutoka kwa m2 wa maana
 
Sijajua tatizo ni uelewa wetu au ni dhamira ya kutotaka kuelewa. Mtanzania wa caliber yako kutojua kosa la Muhongo kama afisa wa serikali na maadili ya uongozi tunayotumia kama kigezo cha kudhibiti nidhamu katika utumishi wa umma. Hata kama tunapofushwa na rushwa wanazozitoa wahusika, basi tuandike kama ni watu wenye akili pia.

kumbe muhongo amekiuka maadili,ok,sasa hebu twambie sasa hayo maadili aliyokiuka huyu jamaa
 
basi kama hamna wasomi huko tuleeteni hata lisu si mnasemaga anajua sana mambo ya sheria aje hapa atwambie makosa ya mhongo,step by step ili watu waelewe,maana sasa tushachoka na hizi bla blaa.

aje pia aseme huyo ngalimi ni nani na anahusika vipi na pap ama escrow

Nimefuatilia mjadala na namna unavyojibizana na wana forum humu, nimekuja na hitimisho hili juu yako na wote mnaotetea upande wa serikali kwa maana ya huyu jamaa Rais wetu kwa "bahati mbaya sana" (najua kwa statement hii utang'aka pia) Jakaya Kikwete;

Mosi, Hufahamu chochote lakini uko "so obssesed" na ujinga wa kudhani kuwa unajua kumbe hujui

Pili, Kwa sababu hiyo hapo juu hata ungetembelewa na Mungu mwenyewe aliyekuumba kamwe hutaelewa kwa sababu hiyo "obssession" ya ujinga wako utakwenda nayo kaburini hivyohivyo. Yaani "Wagalatia" wa enzi za mtume Paul wana afadhali kuliko wewe!

Mwisho chukua clip ya hotuba ya "Rais wako" Kikwete ya tarehe 21/12 na chukua clip ya uchambuzi wa Dr Slaa halafu watazame vizuri "facial expression" ya kila mmoja utagundua haya hata bila kupata kitabu cha ziada kilicho na facts za skandali ya Tegeta Escrow Account;

Mosi, Rais wako Jakaya Kikwete ni mshiriki mkuu wa wizi huo na inathibitishwa na kutojiamini kwake ktk hotuba yake (ambayo hadhira ya Tz ilitrajia iwe ni ya Rais mwenye maamuzi na aliye tayari kuitetea nchi yake na wananchi wake) kinyume chake akajiumauma na kujikanganya kwingi katika maelezo yake kwa kuwa wakili na mtetezi wa IPTL na washirika wake PAP na VIP Engeneering - wawekezaji wezi na matapeli katika nchi yetu. Dr Slaa kwa upande wake ukimtazama na kumsikiliza unatambua mara moja kuwa anamjua Kikwete na tabia yake ya wizi ambaye "in return and in his own deffensive manner" huumiza wenzake ktk serikali yake kuliko anavyojijua yeye!!

Pili, utagundua mara moja kuwa aidha Rais wako alijipanga kwa makusudi kuja kuwahadaa na kuwadanganya wananchi wake mwenyewe kwa kudhani kuwa yeye kwa kuwa ndiye aliye juu pale kwenye ofisi kuu ya nchi yetu, basi ndiye pia mwenye akili na ufahamu mwingi zaidi ya watz 45ml anaowaongoza na waliojadili jambo hilohilo na kuliona kuwa haliko sawa na limezingirwa na wingu zito la ufisadi au amedanganyika na pasipokujua naye akakurupuka kuja kutudanganya sisi!!

Bro, Mungu kakupa akili ili uitumie kupambanua mambo wewe mwenyewe pasipo kumtegemea Kikwete au Dr Slaa au huyo Muhongo unayemtetea. Muhimu ni kuwasikiliza lakini hitimisho unalitoa wewe pasipo akili yako kushikiliwa na mtu!
 
Babu anajidai Eti kageuka Sumaku (magnet)ya kunasa mawasiliano. Kila mtu anajua kuwa unaweza kuanzisha Email mbili tofauti kwa kutumia majina unayotaka then ukarusha email ukaenda kutangaza umenasa mawasiliano.mfano fmbowe@yahoo.com na nyingine drslaa@Gmail.com then ukarusha any sms kutoka one account kwenda nyingine ukajitokeza kujifanya Sumaku ya kudaka mawasiliano.

email hii imeanza kuzungumzwa wiki iliyopita ikulu haijaikanusha licha ya kulijua hilo wamekaa kimya tumwamini nani sasa offcourse Dr.SLaa otherwise ikulu ingeshakanusha kwani kufoji email ya mawasiliano ya rais ni kosa la jinai
 
kumbe muhongo amekiuka maadili,ok,sasa hebu twambie sasa hayo maadili aliyokiuka huyu jamaa

Usidhani kila anaechangia uzi wako anapungukiwa kama wewe. Hayo yameimbwa kuanzia bungeni mpaka hotuba ya JK juzi. Tupe nafasi tujipange kuangalia mstakabali wa nchi yetu na sio upuuzi wa njaa zenu. Hata Tibaijuka mlijaribu kutumia lugha kama hiyohiyo hata pale mlipoambiwa kuwa viongozi wetu wamesaini kulinda na kutoenda kinyume na maadili ya utumishi wao.
 
Babu anajidai Eti kageuka Sumaku (magnet)ya kunasa mawasiliano. Kila mtu anajua kuwa unaweza kuanzisha Email mbili tofauti kwa kutumia majina unayotaka then ukarusha email ukaenda kutangaza umenasa mawasiliano.mfano fmbowe@yahoo.com na nyingine drslaa@Gmail.com then ukarusha any sms kutoka one account kwenda nyingine ukajitokeza kujifanya Sumaku ya kudaka mawasiliano.

Umemaliza kaka!
 
mnyampaa kitaturu mbona kama hujajibu swali?.
umesema jk ana facial expression,hajiamini,amejiuma uma na kujikanyaga kwingi,ukimtazama na kumsikiliza tu unambua tabia yake ya wizi ,SASA MKUU mbona sioni point zaidi unamtukana jk?
ndo kusema hata mahakamani utatumia facial expression kama ushahidi?.

wewe usiwe na wasiwasi eti hata ukisema jinsi mhongo alivyokwapua escrow sitaamini,kwani hata nisipoamini mimi si wengine wataamini bana?.
sasa mnapoficha wizi ndo maanake nini,wewe weka hapa jinsi muhongo alivyoiba escrow hizi habari za facial expression hazina mantiki
 
Wewe umeangushwa nini wewe? kama kweli una uzalendo acha kutumia umeme, ulitaka umeme wa bure? maana Habinder anazalisha umeme mpaka dakika hii, na michuzi inaingia.

Babu kapiga porojo, sikuona alipoonesha nani kaiba na nini kimeibiwa. Au wewe umesikia hilo?
haa haa, kweli nakuhurumia sana. Jk ni janga kubwa!
 
Utamchaguwa wewe, sisi hatumchaguwi. Hilo ni wazi. 90% ya wapiga kura Waislam hawatathubutu kumchaguwa, hilo kumbuka.

Hatuwezi kuchaguwa mtu asiye na maadili hata kidogo, awe padri asiwe padri. Unamuona nyoka kaingia kwenye tundu halafu unapeleka mkono? mawee!
images.jpgHuyu hapa ambaye aligongana na uhusika wa "urais" bila kujua, anachofanya ni kutafuta kujinusuru huku sisi tusiojua tukishangilia eti jamaa ana mbinu kali....wapi!
 
siasa za namna hii ccm walidhani zinaweza kuwasaidia watz wakasema noo tumechoka na uhuni wenu..... Zamani vijana walikuwa wanaandaliwa wawe na hoja za kujibu matatizo wa watz siku hizi sifa kubwa ya kupewa uongozi ni UWEZO WAKO WA KUTUKANA UPINZANI NA KUWATUKANA WAZEE NA WAASISI WA TAIFA KM WARIOBA TENA MATUSI YA NGUONI. ccm hawana tofauti na mbwa
mkuu huo ndo ukweli, ccm imepoteza misingi yake yote ya asili.
 
email hii imeanza kuzungumzwa wiki iliyopita ikulu haijaikanusha licha ya kulijua hilo wamekaa kimya tumwamini nani sasa offcourse Dr.SLaa otherwise ikulu ingeshakanusha kwani kufoji email ya mawasiliano ya rais ni kosa la jinai

kama kila linaloandikwa hapa jf kuhusi ikulu inabidi wakanushe then hawatakua na kazi ingine ila kukunusha tu usiku na mchana
 
anaongea pumba HUYU MZEE ANACHOONGEA HAKIELEWEKI..UCHUNGUZI UNAENDELEA ANACHO JADILI NINI?

bora nimuanglie marin hassan TBC 1

Kuna bingwa wa kufanya UCHUNGUZI anayeaminika na kutegemewa na SERIKALI kuliko CAG? Tumia akili kama msomi.
 
Dr Slaa anatumia empirical data zilizopo meza ambazo ziliapata barak za RAIS wa nchi hadi kuwasilishwa bungeni. Tumia uweledi, usomi na uchambuzi bila kutumia ushabiki wala itikadi za chama.
 
mwenyekiti ameridhia serikali isijiuzulu
katibu ijiuzulu
what kind of people ?

tatizo mnakurupuka na neno "kujiuzulu" tu bila kujua km dr kasema ingekuwa ni nchi nyingine rais angejiuzulu bt hajasema rais ajiuzulu.. Msimamo wake ni kuwajibishwa kwa wez.. Hata deo filikunjombe alimnukuu mwl kuwa huwez kumwajibisha rais bila nchi kutikisika..... Mnajua hiyo nukuu ina maana gani mnaomshambulia dr.?
 
Usidhani kila anaechangia uzi wako anapungukiwa kama wewe. Hayo yameimbwa kuanzia bungeni mpaka hotuba ya JK juzi. Tupe nafasi tujipange kuangalia mstakabali wa nchi yetu na sio upuuzi wa njaa zenu. Hata Tibaijuka mlijaribu kutumia lugha kama hiyohiyo hata pale mlipoambiwa kuwa viongozi wetu wamesaini kulinda na kutoenda kinyume na maadili ya utumishi wao.

kwahiyo muhongo ameenda kinyume na maadili yapi?
 
Dr Slaa anatumia empirical data zilizopo meza ambazo ziliapata barak za RAIS wa nchi hadi kuwasilishwa bungeni. Tumia uweledi, usomi na uchambuzi bila kutumia ushabiki wala itikadi za chama.

slaa anamtaja mtu na kusema kwamba ameshiriki na jk kupora escrow,hiyo data katoa wapi na kwanini hasemi huyo anaemtaja kashiriki vipi.

anadai singa anajuana siku nyingi na jk,hasemi tangu lini na kwavipi kujuana nae iwe ishu
 
Back
Top Bottom