Elungata, wewe ni mdau wa siku nyingi humu JF. Michango yako mingi huwa ni very constructive kiasi kwamba nachelea kusema labda Id yako imeibwa na kutumiwa vibaya.
Hivi inawezekanaje CAG na PCCB wakatoa ripoti fake Bungeni? Imewahi kutokea wapi na lini? Mbona unajifanya hamnazo na kujitoa ufahamu kiasi cha kutetea upuuzi ambao hata zuzu inamwia vigumu kutetea? Hushangai kuwa pamoja na jitihada Rais amefanya na kuchukua hatua dhidi ya Prof Tiba na Maswi bado umma haujaridhika?
ooh,kumbe hukunielewa,nadhani umeona hapa kuna mmoja nimmchallenge aweke japo kipande cha riport ya CAG ikionyesha wizi umetokea,mpaka sasa kimya.
nikasema huko nyuma riport ya PAC imedai zimeibiwa bilion 321 toka escrow wakati kumbe hakukua hata na pesa hiyo.
kwa ufupi zito na watu wake wamechomekea kitu ambacho hakipo kwani katika account ya escrow zilikuwepo bilioni 202 tu,sasa hesabu ya bilioni 321 kina zito wametoa wapi?
kama wewe una maelezo yakueleweka hebu sasa fafanua hapo.