Dr. Slaa kuzungumza na Vyombo vya Habari, Serena Hotel - Septemba 1, 2015

Status
Not open for further replies.
Leo hii kamamda si uvute subra unajua anongea nini kesho kama anataka kuanza kampeni na Lowassa?

Hii si habari nzuri. kama hadi nyie leo mnajipongeza kwa press conference ya Dr Slaa kesho? hapa lazima kuna kitu. Ila kama Dr Slaa ameamua kubwaga manyanga na iwe hivyo sisi tunaendeleza mapambano hakuna kugeuka nyuma tutakuwa jiwe la chumvi.
 
...vyovyote itakavyokuwa nitabaki tumaini langu litabaki kwa ukawa...

Trust me hakuna kitakacho harbika kwa sasa, watu wamesha muweka kwenye kund la lipumba kitambo tu, tulimpenda sana tukaumia sana kwa kukaa kwake kimya na sasa tunamchukia sana
 
Acheni kumsemea Dr. tusubiri tumsikilize. tuyaheshimu maamuzi take. yeye ni binadamu kama binadamu wengine. anamaamuzi yake.
 
HIVI KARIBUNI KUMEZUKA TENDENCY YA WATU WANAOJIITA TEAM LOWASSA KUWAKEBEHI NA KUWAKEJELI WALE WANACHADEMA ASILIA WANAOWAPINGA MITAZAMO YAOHUU NI MTIZAMO YAO.
Wengi miongoni mwa chadema asilia ni kama wamesusa hivi na wanahisi kupuuzwa na chama, chadema maslahi kwasasa ndo kila kitu, wanajifanya wao ndo chadema sanaaaaa!

WAKATI AKINA DR SLAA WANAHENYA KUKIJENGA CHAMA WAO WALIKUWA CCM WANAKULA BATA. Baada ya chama kunawiri na kupendeza,wamekivamia, wamekinunua na wanaanza kuleta jeuri. Kwanini wasingeenda kukinunua TADEA AU UMD? ACHENI DHARAU KWA WALE WALIOKIJENGA CHAMA. LEO MMEMTUKANA SANA DR SLAA BAADA YA KUSIKA KUWA ATAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI

1441058581661.jpg tunakaa mbali na mtu kama wewe
 
I never trusted him honestly,kuisaliti nadhiri na kiapo kwa Mungu.
mimi nilipomuona yule mzee ni opportunist na si mtu mwenye wito wa kutumikia watu ni pale niliposikia masharti aliyowapa chadema kwa yeye kuacha kugombea ubunge jimbo la karatu na kuwa mgombea urais wa chadema 2010. mzee aliweka sharti ili awe mgombea ni lazima ahikikishiwe maslahi yake endapo angekosa Urais. akata mshahara alipwe kama wa mbunge kila mwezi na marupurupu kibao toka kipindi hicho hajawi kunivutia na hata huwa sielewi watu wanamwonaje ni mkombozi and yet na yeye ni opportunist tu
 
Tunamwombea mzee wetu hawezi kukaa na Magamba kiti kimoja hata mara moja.Ni mzee smart na makini.Dr tunakuombea ,haya mabadiloko wewe una heshima kubwa sana sana.kwani wewe umekuwa injini ya hizi mbio ambazo sasa zimefikia mwisho.Tunakushukuru na kukuheshimu mzee wetu.

Haiwezekani mzee huyu akae kimya muda wote huu halafu aje aite waandishi wa habari lazima kuna kitu.
 
Itakuwa hatari nchi hii na sintokuja kumwamini mtu kama Dr Slaa atarudi ccm

Chiku, binafsi sitoshangaa sana kwani sasa CCM itaonekana ndio chama safi wakati CDM - details zitakapowekwa wazi - kitaonekana kimenunulika. Lakini sidhani kama kuhamia CCM ni jambo lililoko kwenye ajenda; anaweza kwa mfano kuamua kustaafu siasa tu moja kwa moja lakini on his own terms. Binafsi ninaamini harakati za mabadiliko zimepata jeraha kubwa sana kwa kumkumbatia Lowassa kama alama ya mabadiliko tunayoyataka.

Hata hivyo ni lazima tuwe na aina ya kukubali au kutokubali kwa heshima. Kama watu wamempokea Lowassa na wamefurahia maamuzi yake na hawataki hata watu wahoji uwezo wake au sifa zake kama kiongozi wa mageuzi iweje leo watu hao hao wasiwe hata na heshima (courtesy) ya kumpa nafasi ya kumsikiliza mtu ambaye alikuwa alama ya upinzani kwa karibu miaka kumi sasa?

Nilivyosema awali - ninasimama na watu waliosimama kwenye misimamo ambayo nakubaliana nayo. Mtu ukitoka kwenye msimamo huo au msimamo ambao ulituaminisha basi uwe na maelezo ya kushawishi akili badala ya kutuambia tukuamini tu!
 
Nani kakuambia Nyumbu huwa wanageuka nyuma na kurudi kule walikotoka? Sasa kwa taarifa yako, Dr Slaa akiongea negative kuhusu UKAWA mjue mmekwisha. Huyu sio mwanasiasa wa kumdharau hata kidogo. Wewe omba Mungu wako Slaa awe upande wenu, vinginevyo kuanzia kesho mnasambaratika.

Kwa sababu saa hizi ni usiku endelea kuota, Juma Duni Haji anaizika ccm mikos ya kusini huko na Lowasa ndio hakdmatiki kabisaaaa.
 
Bila shaka inawezekana mda huu ukawa umeshalala au bado una peruzi peruzi huko na huko kwenye mitandao ya kijamii mbali mbali Dr.Slaa tumesikia na kuaminishwa kwamba hapo kesho nikimaainisha badae maana ni siku nyingine sasa mda huu ninavyoandika hapa ni 12:57 usiku... utaenda kuzungumza na waandishi wa habari na kuweka wazi msimamo wako Dr.Slaa mimi binafsi ninachokuomba Dr.Ujue chochote utakachoenda kuzungumza kama kwa lengo la kuharibu harakati hizi za mabadiliko Dr.Utakuwa hujatutendea haki kabisa kabisa wanabadiliko..mimi ni mmoja wapo niliyetokea kukuamini na kukupenda sana sababu ya kupambana kwa ajili ya mabiliko lengo kubwa ilikuwa ni kubadili mfumo mzima wa chama tawala wakae pembeni sasa kama kuna njia nyingine ambayo inaweza ikarahisisha hawa jamaa waondoke Dr.Slaa kwa nini unataka utuvunje mioyo yetu kisa ni Urais tu Dr.? nakuomba mzee wangu Slaa utusaidie afadhari kukaa kimya kuliko kwenda kuongea tena lengo ni kusamaratisha UKAWA taarifa zilizopo ni kwamba utaenda kuzungumza kwa udhamini wa ccm...Nina mengi kwako Dr.Slaa lakini lengo kubwa ni kukuomba kutofanya lolote ambalo linaweza likaharibu utaratibu mzima wa mabadiliko haya..Natumaini Mungu atakuongoza Dr.Katika hilo.
wako mtiifu mwanachama hai wa CHAUMA.
 
Hatimaye katibu mkuu wa Cham cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbrod Slaa ameamua rasmi kuachana na siasa baada ya tafakari ya muda mrefu.

Kesho Slaa anatarajiwa kutangaza uamuzi wake huo ndani ya 'Dar es Salaam Serena hotel' ambao utakuwa ni pigo kubwa kwa vyama vinavyounda UKAWA.

Katika hatua nyingine mwanachama wa CHADEMA anayeamini katika siasa za Dr. Slaa, G Sam ameamua kumuunga mkono kutokana na mizengwe ya uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama hicho.

"Nitapiga kura kwa Halima Mdee na mgombea udiwani wa Chadema ila siyo kwa Edward Lowassa" anasema G Sam.

G Sam anamuonea Edward Lowassa kama mgombea dhaifu sana asiyeweza kwenda sambamba na kasi ya chama hicho. Aidha G Sam anakiri kuwa hana tatizo na Edward Lowassa kuhusu mambo ya ufisadi bali ni kutokana na udhaifu unaoonekana waziwazi juu ya mgombea huyo.

Atakula wapi akiacha siasa? Thubutu... Ninachoona atakamilisha mzunguko wa kwanza kwa kurudi alikotoka.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom