Kiongozi Mkuu wa Upinzani Nchini ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Peter Slaa anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Hedaru-Same Jumanne tarehe 15 January 2013.
Mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara Dr Slaa anatarajiwa pia kupokea wanachama wapya wa Chadema,kufungua ofisi za Chadema kata ya Hedaru na kuzindua matawi ya Chadema maeneo ya Hedaru,Makanya na Same.
Tayari mji wote wa Same na vitongoji vyake kuna gumzo kubwa kuhusu Ujio huo wa Dr Slaa ambaye anaonekana kama kiongozi aliyevuka vizingiti vingi vya mahasimu wake huku nyota yake ikizidi kung'aa kila siku kuelekea mwaka 2015
Kwa sasa Katibu Mkuu huyo amejichimbia mkoani Kilimanjaro akiongoza vikao vizito vya Sekretariati yake ikiwa ni maandalizi ya operesheni kubwa ya kuimarisha chama chake kwa mwaka huu.