Dr. Slaa kumjibu askofu Gwajima

Dr. Slaa kumjibu askofu Gwajima

Status
Not open for further replies.
Kuna tetesi kuwa huenda Dr Slaa akaibuka wiki ijayo kumjibu askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima. Dr Slaa anamtuhumu mtumishi huyo wa Mungu kumleta Laigwanan Lowassa ndani ya UKAWA hivyo kumnyima fursa ya kugombea urais kupitia muungano huo wa vyama vya siasa.

Majibu ya Dr Slaa yanakuja baada ya kimya cha muda mrefu tangu askofu Gwajima alipoanika hadharani ukweli kuhusu Dr Slaa kustaafu siasa. Inadaiwa kwamba Dr Slaa amechukua muda mrefu kwa kuwa kwanza alikuwa akitafuta bomu kali la kuja kulipua.

Kwa sasa Dr Slaa yupo nchini Marekani akipumzika na mchumba wake Josephine Mushumbushi.

Awali askofu Gwajima alitahadhalisha kwamba atalipua bomu kali sana endapo Dr Slaa atajitokeza hadharani kumjibu. Haifahamiki mwanasiasa huyo mstaafu amejiandaa kiasi gani kupangua hoja za Gwajima ambazo zina ushahidi wa kutosha. Ni suala la kusubiri na kuona jinsi alivyojiandaa kujibu hoja.

MAONI YANGU
Naomba watanzania wenzangu tutulize mawazo yetu kwenye kampeni; tusiyumbishwe kamwe.

:yield:
Umeandika huu uzi ukionesha tayari kuwa una upande wako kati ya hizi pande mbili.
 
Dr Slaa Akijibu Bishop Atamuumbua Mchana Kweupe

Watakaonufaika na mapambano haya ni wanasiasa tu, lakini kwa upande wa kiimani, Gwajima anaizika huduma yake. Tayari wakristo wa kweli wameshajitenga na mipasho yake.
 
Watu tumeshasahau ya Dr slaa kwa sasa tuko bize kwenda kuwafurusha CCM Ikulu,kama ana taka kumjibu Gwajima amuite chumbani kwake akamjibie huko kwa sasa hatutaki kusikia upuuzi wake.
 
kama una akili za MAITI utatambuaje huo ushahidi?

na kama unadhani ushahidi alioutoa dr gwajima bado haujitoshelezi mwambie dr mihogo ajitokeze hadharani halafu gwajima aje na ushahidi wa kufa mtu ndipo mtajua maana ya ushahidi. unajua nyie maCCM sijui akili zenu zikoje.
Eti Gwajoo naye ni Dr? Hahaha..we lazima utakuwa sista Flora
 
Mpunga wa CCM apige yeye,machicha ndio ana taka atutapikie kama ana nia njema na sisi kwanini asitugawie mpunga kidogo na sisi tupate nauli ya kwenda kumsalimia Obama?.
 
Dr Slaa ameamua kukaa kimya lakini kuna vijana naona wanatumwa kumchokoza ili kupima upepo ....subirini mihemuko ya mabadiliko feki iwatoke baada ya tarehe 25 alafu tuwaanzishie dozi mpoteane humu ...
 
Thubutuuu...hawezi kabisa,kwasababu akifanya hivyo Gwajima atafichua siri zote za ndani za Dr Slaa.
 
Dr Slaa ameamua kukaa kimya lakini kuna vijana naona wanatumwa kumchokoza ili kupima upepo ....subirini mihemuko ya mabadiliko feki iwatoke baada ya tarehe 25 alafu tuwaanzishie dozi mpoteane humu ...

Huo ni mtazamo wako, lakini haya mabadiliko siyo lazima asimame Dr slaa ndo yatokee nyie chagueni maisha mapya siasa hamziwezi.
 
Sidhani kuna mtu atasikiliza kwa umanani zaidi ya kumshangaa. Na kama kweli ataendeleza mipasho yake ile, basi afadhali safari hii avae dera na afunge kibwebwe na matarumbeta pembeni ili tutathmini uwezo wa Josephine kwenye uumbaji!.
 
Hawez kujibu kitu tena dr.mihogo
Hayo mabilion ya ccm ayatumbue tu na akitaka apande kwenye jukwaa la ccm ....tupo nyuma ya wakati tunayawinda mabadiliko ambayo yalitakiwa yafanyike toka 2005
 
tuliambiwa na mh. mmoja hapa kuwa tutaiona nguvu ya dr. Mihongo na UKAWA itapasuka vipande vipande... ninachokiona sasa ni UKAWA kupata nguvu zilizokithiri na watu kuzidi kumchukia yeyote anayeipiga vita UKAWA!!

HIVI HAWA WENZETU WANAISHI DUNIA IPI WANAYOPEANA TAARIFA WASIZOZIJUA?

CCM TUACHIENI NCHI YETU SALAMA
 
Muungwana akivuliwa nguo uchutama.

nitamshangaa na kumuona hana akili kama ataendeleza malumbano.
 
TCRA walishapiga marufuku watu binafsi kwenda kwenye media kuzungumzia siasa. Labda akajibu kwenye mikutano ya ccm...! Huyo Dr.W.Slaa na Humphrey Polepole walishazimwa na hawatasikika tena mpaka uchaguzi upite.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom