Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

Kuna watu humu JF wanamwona Slaa kama mungu mtu!

Sasa ww una muona wa kawaida? pale paramiho alihamia ili aje kusoma seminary. Hajakaa sana akawa raisi wa serikali ya wanafunzi. Kila mahala lazma mumpe cheo ndio maana kila eneo yy ni katibu. Akaja akashinda ubunge bila hata diwani mmoja wa chama chake wala mwenyekiti. miaka mitano badae anatwaa ngome yote yaan halmashauri. Huyu jamaa anashinda uongozi kama ananawa vile. Ww unadhani humu watu tusimpende mteule huyu??? Rejao naomba urejee nafsi
 
Aisee..ngoja nisiongee maana nitatukana halafu nitapigwa ban bure..hivi hapo tuhuma zinazomgusa Dr Slaa ni zipi? Hivi wewe mleta uzi,kweli umekosa akili za kawaida kabisa kufanya upembuzi yakinifu ya hii habari kabla ujaileta hapa JF? Kwanini tunapenda kujidhalilisha mbele za watu bila hata kutafakari madhara yake? Mke wako na watoto wako wanajua kuwa uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo kiasi hiki? Kwamba unabeba habari kichwa kichwa bila hata kuchuja? Nadhani unapaswa kujifunza namna ya kusoma mambo na angalau kufanya uchambuzi kabla ya kuleta hapa kwenye jukwaa makini.
 
Nimepita katika group moja katika facebook nikakuta kuna post ambayo inazungumzia tuhuma za ufisadi uliofanywa na watu mbalimbali kutoka vyama vya upinzani akiwemo Dr Slaa..,si vibaya tuhuma hizi nikizileta hapa jamvini kwa kuwa Dr Slaa yupo na naamini wapo pia watu wenye uelewa katika haya yaliyozungumzwa wanaweza kuchangia ama kusaidia katika kukanusha ama kusahihisha ama kukiri tuhuma hizi..,

extracted from TANURI LA FIKRA

Kuchukua tuhuma za mwanachama na kuivesha tuhuma hiyo kwa chama ni makosa na hili linafanywa makusudi na wapinzani ili waendelee kichafua CCM.,haiwezekani ufisadi unasibishwe na CCM hali ya kuwa katika kila chama watu wa AINA hiyo wapo; Nikianza moja kwa moja na katibu mkuu na mgombea URAIS wa chadema Bwana WILBROD SLAA ambaye ni kiongozi mkuu wa taasisi ya CCBRT (katibu wa bodi ya wakurugenzi) ambayo inapatiwa ruzuku ya shilingi za kitanzania; 1,000,000,000/= kutoka kwa serikali kila mwaka kwa kuiendeleza taasisi hiyo kwa manufaa ya watanzania wote na taifa kwa ujumla na pia inapata misaada na harambee mbalimbali kutoka kwa watu binafsi na mashirika makubwa ndani na nje ya TANZANIA kama EUROPEAN UNION,IRISH AID, AUSTRARIAN GVT, AusAID, CBM, JOHNSON&JOHNSON nk, ili kuwaendeleza watanzania katika nyanja ya afya,.tofauti na malengo hayo taasisi hii chini ya Dr Slaa imekuwa ikitoa huduma za jamii kwa ubaguzi mkubwa na kukosekana kwa usawa; nitabainisha kama ifuatavyo;
a) Wagonjwa wanaotibiwa kwa mwaka wanakadiriwa kufika 1,080,000 katika hawa zaidi ya nusu ni kutoka katika mikoa ya kasikazini ikiongozwa na moshi na arusha.(branch ya CCBRT iko moshi)
b) Operesheni zilizofanywa kati ya mwaka 2003-2007 ni kama ifuatavyo.,macho 31,200 napo pia zaidi ya nusu ya wagonjwa walitoka maeneo hayo. Mimi sidhani kuwa moshi kuna watu wenye matatizo ya macho zaidi ya Dodoma, Singida na sehemu nyingine za tanzania ya kati.
c) Operesheni za orthopaedic&plastic surgery kati ya 2003-2007 ni 6,520 bado wagonjwa wengi walitokea kaskazini
d) Na waathirika waliokuwa wakihudumiwa na CCBRT kati ya 2003-2007 zaidi ya 60% ni kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro (ripoti ya Tom Varnneste 24 jully 2008)
e) Taasisi hii pia inakadiriwa kuwa na waajiriwa 320 napo hapa ni uchaga, na ukaskazini umetawala, mchakato wa uajiri ukisaidiwa na Jacqueline Kweka(Advocacy Officer) uliona kuwa hakuna watu waliosoma na kustahili kufanya kazi CCBRT ila ni wachaga na watu wa kanda ya kaskazini. Katika utafiti uliosimamiwa na CCBRT, Radar development pamoja na DISABILITY AID ABROAD umeonyesha kuwa ni asilimia 0.7% ya waajiriwa ndio watu wenye ulemavu(CCBRT ikiwemo kwa kutoajiri walemavu ingawa ni taasisi ya kusimamia walemavu nchini)
f) Lakini kama hilo halitoshi gharama za matibabu ni za juu sana katika hospitali zilizo chini ya CCBRT, takwimu zipo; Gharama ya matibabu kwa CCBRT mtu binafsi anatakiwa kulipa kati ya dola 400-714 sawa na 600,000-1,071,000/= gharama hii ni kubwa ajabu kulingana na pato la kawaida la mtanzania na pia ni gharama ya juu hata kuzidi hospitali zingine hapa nchini ambazo hazipati msaada serikali wala mashirika makubwa ya nje na pia hazifanyiwi harambee kama CCBRT.,mfano CATARACT SURGERY HINDU MANDAL 400,000/=, AGA KHAN 315,000/= REGENCY 300,000/= MISSION MIKOCHENI 180,000 WAKATI CCBRT 680,000(Tom Venneste Appendix iii-nov 2008)

Pia CCBRT imekuwa haiko tayari kuwa wawazi juu ya kiasi cha mapato kinachochangiwa kutoka katika taasisi hizi kubwa duniani (dalili kubwa ya kuwepo ufisadi ndani yake)

Ama ukiacha hayo ambayo yanamgusa moja kwa moja Dr Slaa, pia kuna yanayowahusu viongozi wengine wa CHADEMA kama vile DIWANI WA KATA YA SERENGETI,MKOANI MARA KUKAMATWA AKIMILIKI AK47 KINYUME CHA SHERIA kiuhalisia huu pia ni ufisadi na hata yule MBUNGE WA CUF ALIYESHUTUMIWA KUINGIZA NCHINI MAGARI YA WIZI NA KISHA KUKWEPA KODI huu pia ni ufisadi ila inapotokea mambo kama haya yakifanywa na viongozi au wanachama wa CCM yatatangazwa vyombo vyote vya habari na pia suala hilo litabebeshwa kwa chama badala ya mtu binafsi.

mbona hiyo haimgusi dr.slaa moja kwa moja,maana hayuko peke yake kwny utendaji,na kingine yeye sio mtendaji mkuu,hili ilibidi lielekezwe kwa mtendaji mkuu,halafu eti anasema CCBRT chini ya Dr Slaa,bogus.
 
Nimejaribu kusoma na kurudia rudia mwisho nimegundua CCM wako sharp safari hii hawalazi dammu wanashambulia ndege hata kabla haijaondoka ardhini! Arumeru itakuja na mengi kweli. Ndani ya wiki moja tumeona viongozi mbalimbali wa CDM wanavyoshambuliwa bila kupepesa macho. Natarajia hili litaendelea hadi viongozi wa CDM watakapotambua nilichosema karibu mwaka mmoja uliopita siyo maslahi ya CDM kuwasaidia CCM watawale vizuri! Lengo la CDM linatakiwa kuidhoofisha CCM na kuifanya ionenake mbovu! Bahati mbaya sidhani kama hili linaeleweka bado!
 
Sasa ww una muona wa kawaida? pale paramiho alihamia ili aje kusoma seminary. Hajakaa sana akawa raisi wa serikali ya wanafunzi. Kila mahala lazma mumpe cheo ndio maana kila eneo yy ni katibu. Akaja akashinda ubunge bila hata diwani mmoja wa chama chake wala mwenyekiti. miaka mitano badae anatwaa ngome yote yaan halmashauri. Huyu jamaa anashinda uongozi kama ananawa vile. Ww unadhani humu watu tusimpende mteule huyu??? Rejao naomba urejee nafsi

Nilimsikiliza alipoongea kwny ule mdahalo wa ITV wkt wa election campaigns and i was like,this is the president speaking.
 
Hivi taasisi kubwa kama CCBRT haifanyiwi year auditing na reputable consultancies? au wanafikiri international organs zinapoisaidia CCBRT huwa hazipitii account books zake!?
 
Sasa ww una muona wa kawaida? pale paramiho alihamia ili aje kusoma seminary. Hajakaa sana akawa raisi wa serikali ya wanafunzi. Kila mahala lazma mumpe cheo ndio maana kila eneo yy ni katibu. Akaja akashinda ubunge bila hata diwani mmoja wa chama chake wala mwenyekiti. miaka mitano badae anatwaa ngome yote yaan halmashauri. Huyu jamaa anashinda uongozi kama ananawa vile. Ww unadhani humu watu tusimpende mteule huyu??? Rejao naomba urejee nafsi
Kama anasjhinda kila mahali..kwanini hakushinda urais 2010?
Jaribu kufikiri kwanza kabla hujaandika chochote hapa!!
 
Kwani tatizo hapa ni nini. Mtoa hoja amewaomba wana jamvi wanaolijua au yeye mwenyewe ajitokeze kujibu. Kosa la mtoa mada hapa ni lipi? kutujuza au kutaka kuupata ukweli??? maana sijaona katika maelezo yake kuwa anamtuhumu DR. ila ameomba kwa wanaoujua ukweli watujuze. Pili hili suala amelichukua TANURI LA FIKRA na ametuletea akiamini miongoni mwetu kuna watu wanalijua hili fika na watatupatia majibu yanayostahili.

majibu ya humu bora hata ya Fb,watu wakipenda kitu hawataki kiguswe
 
Hivi taasisi kubwa kama CCBRT haifanyiwi year auditing na reputable consultancies? au wanafikiri international organs zinapoisaidia CCBRT huwa hazipitii account books zake!?
Mkuu mimi hayo mambo ya ufisadi huko CCBRT siyajui lakini nikuambie jambo moja kwamba kazi ya auditing siyo kugundua wizi ama ufisadi ndani ya kampuni ama shirika ila kuna uwezekano (nasema uwezekano si lazima) auditing ikagundua wizi ama ufisadi.
 
Kama anasjhinda kila mahali..kwanini hakushinda urais 2010?
Jaribu kufikiri kwanza kabla hujaandika chochote hapa!!

Kwa taarifa yako Dr. Slaa alishinda urais,ila nyie kwa utapeli wenu usio na aibu mkamtangaza baba mwanaasha,sisi rais wetu ni Dr. Slaa.
 
Hivi Dr Slaa ni mchagga? Huo ukaskazini as if kuna kabila linaitwa kaskazini unatoka wapi? Watanzania tuache uchochezi
 
Chagga people are leading for nepotism and favouritism among African societies, study suggests. Famous research conducted and compiled by the late Zimbabwean professor Julius Mambubwa on 'the effects of nepotism to the economic growth of Africa' documented that 50 percent of the employed Chagga people have had their current jobs through the influence of their fellow Chagga relatives.

Additionally, it went on showing that in nearly each of the public office which is headed by a Chagga, 45 percent of the workers are coming from Chagga tribe apparently getting their employment after someone at the top had pulled strings for them.
those concerned will move on checking the reliability of the study done...!
 
ccbrt.jpg
Rais wa CCBRT Mhe Anne Makinda na viongozi wengine wa CCBRT wakati wa ufunguzi wa Hospotali ya Baobab
[source: website ya CCBRT]
 
Aisee..ngoja nisiongee maana nitatukana halafu nitapigwa ban bure..hivi hapo tuhuma zinazomgusa Dr Slaa ni zipi? Hivi wewe mleta uzi,kweli umekosa akili za kawaida kabisa kufanya upembuzi yakinifu ya hii habari kabla ujaileta hapa JF? Kwanini tunapenda kujidhalilisha mbele za watu bila hata kutafakari madhara yake? Mke wako na watoto wako wanajua kuwa uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo kiasi hiki? Kwamba unabeba habari kichwa kichwa bila hata kuchuja? Nadhani unapaswa kujifunza namna ya kusoma mambo na angalau kufanya uchambuzi kabla ya kuleta hapa kwenye jukwaa makini.

Mke anahusiana nini na yeye.Mlenge yeye.
 
Kwa taarifa yako Dr. Slaa alishinda urais,ila nyie kwa utapeli wenu usio na aibu mkamtangaza baba mwanaasha,sisi rais wetu ni Dr. Slaa.

Kaka ushapiga kura tayari.Mi najua uchaguzi bado.Huyo slaa iwaje tena?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom