Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

Sasa na mimi naomba kuuliza maswali yangu:
1. Je Dr. Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi anashughulika na shughuli za kila siku za kiofisi?
2. Je Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi anafanya kazi za idara ya utumishi?
Baada ya hapo nataka kukuuliza mbona tuhuma zako zimeegemea upande mmoja tu ambao ni wa CCBRT?
Hivi kabla ya kuja kwenye jukwaa ulijaribu kutafuta wahusika ambao ni CCBRT ili wakujibu?
Naomba tuache majungu na fitina...tuegemee ukweli
HIVI KWANINI WATANZANIA TUNAFIKIRIA UCHAGUZI WA 2015,BADALA YA KUFIKIRIA MAENDELEO YA TAIFA LETU NA HATMA YA WATOTO WETU NA WADOGO ZETU?
 
Rejao bwana unachekesha kweli we hujui kama dr.slaa alishinda urais 2010 sema faulo tu za zzm.

Athari za kuamini dhahania huathiri ubongo pia. Ubongo ukisha athiriwa na dhahania haurekebishiki tena na utabaki kuwa uleule unaotumikia dhahania. Sawa na mlokole mwenye imani kali, akiamini dhana ya kuwa maombi huponya basi atataka na mgonjwa wa kipindupindu aponywe kwa maombi ya imani yake. Kutokana na athari ya dhahania katika ubongo wako huwezi amini kuwa Dr Slaa hakushinda mwaka 2010 bari unamini kuwa alishinda kwa dhana na athari zilizoota mizizi katika imani yako.
 
Kaka ushapiga kura tayari.Mi najua uchaguzi bado.Huyo slaa iwaje tena?
hivi nyie magamba nani aliyewaroga unajua iko siku njaa zenu za kumtumikia lowassa na kumlamba miguu zitawatokea puani! Hapo ccbrt slaa ana sahihi ngapi zisizo sawa weka tuone
 
Taabu kubwa ya Serikali yetu ni kushindwa kutofautisha Siasa na mambo mengine ya msingi wao kila kitu lazima waingize Siasa vivyo hivyo humu Jukwaani pameshavamiwa na wimbi la kuchanganya Hoja na Itikadi za Vyama na mapenzi yetu kwa viongozi wetu wa Vyama jambo ambalo kamwe halitaleta suluhu juu ya hoja ziletwazo humu; kidogo napata taabu kwa kuwa mleta hoja katoa na references ikiwamo hiyo anayooita "Tom Vatrnneste Report" na kaandika na kurasa zaidi katoa mchanganuo wa tofauti za bei za Kitabibu kati ya hiyo CCBRT na Hospitali zingine wengi wameomba Slaa ajibu hizi tuhumu kama ambavyo amekuwa akijitokeza na kujibu zingine kushindwa kwake ndiko huko kunakozidi kumpa mtoa hoja nguvu ya kuendelea kushinikiza yale yeye anayoyaamini.

Si mbaya ile list of shame nayo inaweza ikafanyiwa review majina mengine yakaongezwa kama hivi vdivyo........
 
Hivi shirika si huwa lina identify project location?kama waliamua kuanzia Kaskazini kutekeleza miradi yake kuna tatizo gani?Mbona World Vision shirika lenye makao yake makuu Marekani na makao yake makuu hapa TZ yako Arusha je ni la watu wa kaskazini?lakini je kwa sasa mbona limesambaa kanda ya ziwa na ya kati?ku-extend project location inategemea na shirika limelenga nini,kuchagua mahali pa kutekeleza miradi ya shirika fulani inategemea na walichokikusudia,wakati CCBRT inaanza Dr Slaa alikuwa bado ni mtumishi wa Mungu(Padre) na alikuwa jimbo la mbulu kama sijasahau(mwenye uhakika atanisahihisha) hivyo basi kuelekeza miradi hiyo huko na kwa vile yaliyokuwa yamekusudiwa na CCBRT wananchi wa huko yanawakumba ni vipi leo tuseme kuna ukanda?je wakati CCRBT ikiendesha mradi wa ukimwi mashule yote ya DAR miaka ya 2001/2002 ni vipi hamkusema ukanda?mbona mradi wa huduma ya wgonjwa nyumbani uliendeshwa DAR hamkusema ukanda?na je mbona kuna wagonjwa wengi tu ambao hawajiwezi wamewahi kutibiwa CCBRT na hawakuwa na pesa za kutosha kiasi kwamba wengine wamewahi kusaidiwa nauli hapo,na kwa bahati nzuri mgonjwa huyo alikuwa refered na mimi ambae natoka Usukumani?naye ni wa kusini?na je vipi mdogo wangu alitibiwa macho miaka ya 2006 sikuona ukanda wowote?
Kama kuna ufisadi wa fedha zinazotolewa kama ruzuku inamaana hakuna audit yeyote iliyokwisha fanyika na kugundua haya?je mnajua jisi CCRBT ilivyona namahusiano mazuri na wafadhili wanaochangia pesa za kuendesha shughuli za CCBRT? kama kuna ufisadi wa kiwango unachotaka kutuaminsha nao hawauoni?na je serikali iko tayari kuteswa na Dr Slaa wakati taasisi anayoingoza yeye ni ya kifisadi?let us think twice
 
Usitupandkizie chuki,Mm hapa wa Singida nilshaenda sna kutibiwa macho tena kwa bei nafuu tu na miwani,alaf watu wa kanda ya kati ha2na matatzo macho sna kama wa kaskzn,Dr. ni MUIRAQ,Ofcourse wachaga wanaji2na na walitangulie kusoma wakiwemo na baadh ya makabila.
 
Kama hawa wagogo na wazaramo wanaumwa wanaogopa kwenda hospital unataka watu wa kaskazini wasiende kisa idadi yao kubwa? Kwa kuajiriwa waliotangulia kusoma ni akinanai? Wamakonde wazaramo au wakwere? Ajira zinatolewa kwa kuangalia taaluma.hakuna taasisi yoyote kubwa utakayo ingia umkose mchaga,
 
Taabu kubwa ya Serikali yetu ni kushindwa kutofautisha Siasa na mambo mengine ya msingi wao kila kitu lazima waingize Siasa vivyo hivyo humu Jukwaani pameshavamiwa na wimbi la kuchanganya Hoja na Itikadi za Vyama na mapenzi yetu kwa viongozi wetu wa Vyama jambo ambalo kamwe halitaleta suluhu juu ya hoja ziletwazo humu; kidogo napata taabu kwa kuwa mleta hoja katoa na references ikiwamo hiyo anayooita "Tom Vatrnneste Report" na kaandika na kurasa zaidi katoa mchanganuo wa tofauti za bei za Kitabibu kati ya hiyo CCBRT na Hospitali zingine wengi wameomba Slaa ajibu hizi tuhumu kama ambavyo amekuwa akijitokeza na kujibu zingine kushindwa kwake ndiko huko kunakozidi kumpa mtoa hoja nguvu ya kuendelea kushinikiza yale yeye anayoyaamini.

Si mbaya ile list of shame nayo inaweza ikafanyiwa review majina mengine yakaongezwa kama hivi vdivyo........

kwenye RED kaka unamaanisha kuwa tuongeze jina la Daktari Slaa au vipi..,naomba ufafanuzi...!
 
watu wamekuwa katika utata mkubwa na sintofahamu juu ya madai haya dhidi ya taasisi hii ambayo DR slaa amekuwa ni mwenyekiti wake kwa muda mrefu sasa. Ni wazi kuwa wengi katika watu hawana ufahamu wa kutosha juu ya ukweli halisi wa takwimu hizi ambazo kulingana na mtoa mada hazina utata na zinaushahidi wa kutosha lakini pia watu hawafahamu kiunaga ubaga mfumo kamili na hali ya kiutendaji ya taasisi hii. Ili ni kwa sababu watu ambao wako answerable kusemea taasisi hii hawako tayari kufanya hivyo, kwani naamini kuwa taarifa hii tayari imewafikia, ila wameamua kuipuuza ama kuidharau. lakini madhara ya kupuuza tuhuma ambazo mtu zinamkabili ni kuwa unazalisha uelewa wenye kukinzana katika vichwa vya watu. Wapo wataopuuza na kudharau tuhuma hizo wakiamini kuwa ni uzushi na uongo mkuu, lakini wapo watakaoamini na kuchukua tuhuma hizo kuwa ni ukweli juu ya mtuhumiwa. Lakin wapo ambao hawatadharau lakini pia hawatokuwa tayari kukubali moja kwa moja hivyo wao hujikuta katika hali ya utata na kutaka kujua zaidi. Makundi haya yote matatu ambayo yanazaliwa kutokana na ukimya huu ni hatari kwa afya ya kisiasa ya Daktari slaa ama juu ya credibility ya CCBRT.

ushauri wangu;

i) kwa kuwa ripoti iliyotumika kama ushahidi iko either online or offline.,wanajf hasa wapenzi na wakereketwa wa DAKTARI wangelijaribu kuhakikisha kuwa inapatikana na kuja kuletwa hapa jamviniili watu waone kwa macho yao kuwa data juu ya ripoti hiyo haziko sawa.

ii) lakini hata ushahidi wa kimazingira unaweza kutosha katika hili, kwani hizo hospitali zilizotajwa hapo juu ni hospitali ambazo zipo mjini na zinafikika na watu wanaweza kupata kiwango sahihi cha bei za matibabu ya magonjwa tajwa.

iii) LINGINE AMBALO NI LA MSINGI ni kuwa kwa kuwa suala hili linamtaja DAKTARI moja kwa moja kama yeye na si kama chadema, basi ni busara jambo hili likabebwa kuwa ni la Slaa na wala uchadema na uccm usipewe nafasi katika mjadala huu. Na pia Slaa amekuwa akijibu tuhuma nyingi humu katika JF kwanini hili lidumu muda wote huu na bila kulitolea majibu ama kwa kulikanusha na kulipinga, kulikubali na kulitolea ufafanuzi ama kwa kutolipinga wala kulikubali lakini ilimradi aseme kitu juu ya hili, naona siku zinavyozidi linazidi kupata sura mpya na mitazamo tata zaidi.

TAFADHARI DAKTARI...!
 
tusipumbazwe akili na siasa kupita kiasi!
ameleta mada km zilivo mada nyngne either ni kuchangia na kuangalia ukwel uliomo kuliko kukashifiana!
kwani uyo dr.slaa kazaliwa bethelehem awe msafi kupita wengne?tucpende kushabikia uchama kwa kila jambo hata km mambo mengne yana umuhimu ndan yake!
tuwe na fikra chanya kwa uchambuz wa mambo ushabiki wa vyama kwa mambo ya msingi utatumaliza!
 
watu wamekuwa katika utata mkubwa na sintofahamu juu ya madai haya dhidi ya taasisi hii ambayo DR slaa amekuwa ni mwenyekiti wake kwa muda mrefu sasa. Ni wazi kuwa wengi katika watu hawana ufahamu wa kutosha juu ya ukweli halisi wa takwimu hizi ambazo kulingana na mtoa mada hazina utata na zinaushahidi wa kutosha lakini pia watu hawafahamu kiunaga ubaga mfumo kamili na hali ya kiutendaji ya taasisi hii. Ili ni kwa sababu watu ambao wako answerable kusemea taasisi hii hawako tayari kufanya hivyo, kwani naamini kuwa taarifa hii tayari imewafikia, ila wameamua kuipuuza ama kuidharau. lakini madhara ya kupuuza tuhuma ambazo mtu zinamkabili ni kuwa unazalisha uelewa wenye kukinzana katika vichwa vya watu. Wapo wataopuuza na kudharau tuhuma hizo wakiamini kuwa ni uzushi na uongo mkuu, lakini wapo watakaoamini na kuchukua tuhuma hizo kuwa ni ukweli juu ya mtuhumiwa. Lakin wapo ambao hawatadharau lakini pia hawatokuwa tayari kukubali moja kwa moja hivyo wao hujikuta katika hali ya utata na kutaka kujua zaidi. Makundi haya yote matatu ambayo yanazaliwa kutokana na ukimya huu ni hatari kwa afya ya kisiasa ya Daktari slaa ama juu ya credibility ya CCBRT.

ushauri wangu;

i) kwa kuwa ripoti iliyotumika kama ushahidi iko either online or offline.,wanajf hasa wapenzi na wakereketwa wa DAKTARI wangelijaribu kuhakikisha kuwa inapatikana na kuja kuletwa hapa jamviniili watu waone kwa macho yao kuwa data juu ya ripoti hiyo haziko sawa.

ii) lakini hata ushahidi wa kimazingira unaweza kutosha katika hili, kwani hizo hospitali zilizotajwa hapo juu ni hospitali ambazo zipo mjini na zinafikika na watu wanaweza kupata kiwango sahihi cha bei za matibabu ya magonjwa tajwa.

iii) LINGINE AMBALO NI LA MSINGI ni kuwa kwa kuwa suala hili linamtaja DAKTARI moja kwa moja kama yeye na si kama chadema, basi ni busara jambo hili likabebwa kuwa ni la Slaa na wala uchadema na uccm usipewe nafasi katika mjadala huu. Na pia Slaa amekuwa akijibu tuhuma nyingi humu katika JF kwanini hili lidumu muda wote huu na bila kulitolea majibu ama kwa kulikanusha na kulipinga, kulikubali na kulitolea ufafanuzi ama kwa kutolipinga wala kulikubali lakini ilimradi aseme kitu juu ya hili, naona siku zinavyozidi linazidi kupata sura mpya na mitazamo tata zaidi.

TAFADHARI DAKTARI...!

AISEEE..,hii kitu sijaona majibu yake...! Napenda hapo kwenye red papewe kipaumbele...!
 
Uhalifu wowote huanza na tuhuma...tusibishe kwa sababu tu ni DR.SLAA ametajwa.
Mkuu Kengemumaji na wakuu wangu GT wa JF! Taasisi kama CCBRT ni kubwa na mambo mengi inayoyafanya hapa nchini kila mtu anaweza aka-google na kujisomea. Dr. Slaa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Shughuli za kila siku zinasimamiwa na Mtendaji Mkuu ambaye ni mzungu. Wanaandika ktk mtandao wao kwamba wanatibu wagonjwa 120,000 kwa mwaka. Ukisoma zaidi unaona wengi kati ya wagonjwa wa Fistula ambao wanatibiwa bure wanatokea mikoa ya Nyanda za Juu Kusini huko Njombe,Ludewa na Songea. Sikufanikiwa kupata gharama zao kwa huduma nyingine. Lakini mtu yeyote anaweza akaingia ktk wavuti yao ambayo ni; www.ccrbt.or.tz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom