Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

uzini hali ilikuwaje?mbona pesa imetumika nyingi lakini kura zimepatikana kidogo tu????
 
Kwani tatizo hapa ni nini. Mtoa hoja amewaomba wana jamvi wanaolijua au yeye mwenyewe ajitokeze kujibu. Kosa la mtoa mada hapa ni lipi? kutujuza au kutaka kuupata ukweli??? maana sijaona katika maelezo yake kuwa anamtuhumu DR. ila ameomba kwa wanaoujua ukweli watujuze. Pili hili suala amelichukua TANURI LA FIKRA na ametuletea akiamini miongoni mwetu kuna watu wanalijua hili fika na watatupatia majibu yanayostahili.
 
Huu use.ge wa Nape sasa unatia kinyaa. Mimi ni Mngoni mamangu, dada yangu na mtoto wangu wametibiwa CCBRT zaidi ya mara kumi hakuna cha usumbufu wala kuonewa na hizo gharama sikuziona. Acheni mambo ya kisen.ge CCM

Sasa wewe MAPURENDE ni mngoni wa wapi? wangoni ninao wafahamu mimi wapo makini kwenye hoja. Hoja iliyotolewa hapa ni tuhuma sasa haya ya Nape na CCM unayatoa wapi. Usitupotoshe tunahitaji kuujua ukweli kuhusu hizo tuhuma.
 
Haya mambo ya kuchukua umbeya na majungu kutoka kwenye mijadara ya watoto na kuyaleta kwenye mijadara ya wakubwa(JF-SIASA) siyo vizuri TO! mnatupotezea muda wa kukata issue za maana bwana! naomba ya FACEBOOK yaishie FACEBOOK na ya JF-SIASA yaishie JF bwana. Mtu akikua automatically atakuja tu hapa JF-SIASA maana ndo kwa waliopevuka lakini akiwa hajakomaa hawezi kuingia JF-SIASA maana hatakuwa na cha kuchangia labda aende chit-chat.
 
Awali ya yote nikulaumu kwa uandishi mbaya usio na mpangilio mzuri na kukosea maneno ambayo inasababisha kutokukuelewa vizuri.,Pili udhaifu wa hali ya juu uliojenga kwenye hoja yako, umeshindwa kuanisha kuwa wagonjwa toka sehemu zingine ambazo sio kaskazini wakienda hapo wananyimwa huduma au nini kinatokea??iunasema wafanyakazi wengi ni kutoka kaskazini bila kuweka takwimu, kama umefanikiwa kujua idadi ya wagonjwa toka kaskazini na sehemu nyingine ambao ni wengi mno umekosaje takwimu za wafanyakazi ambao ni wachache.,umetaja 0.7% ya waajiriwa ndio walemavu bila kutaja kazi ambazo zinaweza kufanywa na walemavu lakini bado zinafanywa na watu wa kawaida zikiwepo za kitaalamu kama upasuaji,. unamtaja diwani wa chadema kukutwa na silaha ya vita AK47 bila kutueleza, ni hatua gani zilchukuliwa dhidi yake huku ukijua chadema sio polisi wala mahakama, je chadema waliendelea kumkubatia kama vile mafisadi wanavokumbatiwa kwenye chama kimojawapo cha siasa?? , na pia huyu mbunge aliyeingiza magari ya wizi na kutokulipa kodi alifanywaje?? sheria ilichukua mkondo wake halafu CUF wakamkumbatia??Pia sidhani kama umefanya survey ya kutosha kuonesha gharama za tiba ukilinganisha na CCBRT, mwisho umetaja vyanzo vingine kama EU IRISH AID na nyingine kuchangia CCBRT lakina hakuna uwazi, sasa wewe mleta tuhuma ulitakiwa ufuatilie vyanzo hivo uje na takwimu kuwa EU walichangia kiasi fulani kuanzia muda x hadi muda y otherwise unaonekana mdaku, mchonganishi na mkurupukaji tu!!
 
Ingekuwa hii ni kesi imeshinda High court halafu imeletwa kwangu Court of Appeal kusikiliza rufaa, ningesema hivi "THE JUDGEMENT WAS TOTALLY DEFECTIVE AS DECIDED NOTHING" .
 
Nadhani kuna maswali yanahitaji majibu ingawa hoja ya mleta mada haikujengwa vizuri. Kwamba wametibiwa Wachagga na Wakasikazini zaidi sijui ametumia kigezo kipi! Je kuna mtu amewahi kwenda kutibiwa akanyimwa huduma kwasababu hatoki kasikazini? Issue ya ajira kuna ushahidi kwamba kigezo kikuu cha kupata ajira ni uchagga na ukasikazini?
 
Mwacheni Slaa mwenyewe ajibu tuhuma badala ya kuanza kutokwa mapovu kwa niaba yake.
 
Kwani tatizo hapa ni nini. Mtoa hoja amewaomba wana jamvi wanaolijua au yeye mwenyewe ajitokeze kujibu. Kosa la mtoa mada hapa ni lipi? kutujuza au kutaka kuupata ukweli??? maana sijaona katika maelezo yake kuwa anamtuhumu DR. ila ameomba kwa wanaoujua ukweli watujuze. Pili hili suala amelichukua TANURI LA FIKRA na ametuletea akiamini miongoni mwetu kuna watu wanalijua hili fika na watatupatia majibu yanayostahili.
Mkuu hili litakuwa tanuru la vilaza....... Usitoke mapovu.!!
 
Kasome wajibu wa katibu wa Bodi ya wakurenzi, kama ni kuajiri au kupanga bei ya matibabu au kupanaga nani afanyiwe operation na nani asifanyiowe the uje tena na thread nyingine sio hii.
 
Nimepita katika group moja katika facebook nikakuta kuna post ambayo inazungumzia tuhuma za ufisadi uliofanywa na watu mbalimbali kutoka vyama vya upinzani akiwemo Dr Slaa..,si vibaya tuhuma hizi nikizileta hapa jamvini kwa kuwa Dr Slaa yupo na naamini wapo pia watu wenye uelewa katika haya yaliyozungumzwa wanaweza kuchangia ama kusaidia katika kukanusha ama kusahihisha ama kukiri tuhuma hizi..,

TandaleOne,
Una fistila au mdomo sungura?
Kama ndivyo nitumie ujumbe mfupi sasa hivi ukapatiwe matibabu bure bila kujali unatoka sehemu ipi ya Tanzania. Wahamasishe na wenzio!
 
TandaleOne, hizo ni shutuma au majungu na umbea?

hata mi nashangaa, wagonjwa wa kaskazini kuwa wengi ni kwa sababu kuna branch iko kaskazini. Hospitali nyingi za serikali zinapeleka wagonjwa wake mnh hivyo hawaweze kuwa wengi ccbrt hizo ndo protocol. Pia madaktari wa macho wa serikali huwa wanakuwa na outreach nyingi za kwenda kanda ya kati na magharibi hivyo case nyingi za macho zinaishia huko huko ndo maana wanakuwa wachache. Sera ya wizara mara nyingi sehemu yenye prevalence ya ugonjwa fulani mfano matatizo ya macho ddm,huwa inapeleka madaktari mara kwa mara kufanya chek up na kutoa huduma. Suala la wachaga na watu wa kaskazini kuwa wengi ni suala ambalo lipo kila ofisi. Wakati wao wanajenga shule sisi tulikua tunajenga vilabu vya pombe,aafu kwenye ajira tuwe sawa.khaaa!. Nenda mnh ukaone madaktari wa kichaga walivyo wengi. Huwezi ajiri mtu kwa sababu ya distribution, lazima ujali qualification. Hawa jamaa wanazo,mi nawakubali ni kama kampuni za kichina siku hizi zinavyojazana kwenye tenda,huwezi kuwakwepa labda utumie majungu tu. Shida ya sie tuonaouona mwanga jioni ndo hizi ya kupiga majungu na fitina zisizo na faida
 
nimepita katika group moja katika facebook nikakuta kuna post ambayo inazungumzia tuhuma za ufisadi uliofanywa na watu mbalimbali kutoka vyama vya upinzani akiwemo dr slaa..,si vibaya tuhuma hizi nikizileta hapa jamvini kwa kuwa dr slaa yupo na naamini wapo pia watu wenye uelewa katika haya yaliyozungumzwa wanaweza kuchangia ama kusaidia katika kukanusha ama kusahihisha ama kukiri tuhuma hizi..,

extracted from tanuri la fikra

kuchukua tuhuma za mwanachama na kuivesha tuhuma hiyo kwa chama ni makosa na hili linafanywa makusudi na wapinzani ili waendelee kichafua ccm.,haiwezekani ufisadi unasibishwe na ccm hali ya kuwa katika kila chama watu wa aina hiyo wapo; nikianza moja kwa moja na katibu mkuu na mgombea urais wa chadema bwana wilbrod slaa ambaye ni kiongozi mkuu wa taasisi ya ccbrt (katibu wa bodi ya wakurugenzi) ambayo inapatiwa ruzuku ya shilingi za kitanzania; 1,000,000,000/= kutoka kwa serikali kila mwaka kwa kuiendeleza taasisi hiyo kwa manufaa ya watanzania wote na taifa kwa ujumla na pia inapata misaada na harambee mbalimbali kutoka kwa watu binafsi na mashirika makubwa ndani na nje ya tanzania kama european union,irish aid, austrarian gvt, ausaid, cbm, johnson&johnson nk, ili kuwaendeleza watanzania katika nyanja ya afya,.tofauti na malengo hayo taasisi hii chini ya dr slaa imekuwa ikitoa huduma za jamii kwa ubaguzi mkubwa na kukosekana kwa usawa; nitabainisha kama ifuatavyo;
a) wagonjwa wanaotibiwa kwa mwaka wanakadiriwa kufika 1,080,000 katika hawa zaidi ya nusu ni kutoka katika mikoa ya kasikazini ikiongozwa na moshi na arusha.(branch ya ccbrt iko moshi)
b) operesheni zilizofanywa kati ya mwaka 2003-2007 ni kama ifuatavyo.,macho 31,200 napo pia zaidi ya nusu ya wagonjwa walitoka maeneo hayo. Mimi sidhani kuwa moshi kuna watu wenye matatizo ya macho zaidi ya dodoma, singida na sehemu nyingine za tanzania ya kati.
c) operesheni za orthopaedic&plastic surgery kati ya 2003-2007 ni 6,520 bado wagonjwa wengi walitokea kaskazini
d) na waathirika waliokuwa wakihudumiwa na ccbrt kati ya 2003-2007 zaidi ya 60% ni kutoka mikoa ya arusha na kilimanjaro (ripoti ya tom varnneste 24 jully 2008)
e) taasisi hii pia inakadiriwa kuwa na waajiriwa 320 napo hapa ni uchaga, na ukaskazini umetawala, mchakato wa uajiri ukisaidiwa na jacqueline kweka(advocacy officer) uliona kuwa hakuna watu waliosoma na kustahili kufanya kazi ccbrt ila ni wachaga na watu wa kanda ya kaskazini. Katika utafiti uliosimamiwa na ccbrt, radar development pamoja na disability aid abroad umeonyesha kuwa ni asilimia 0.7% ya waajiriwa ndio watu wenye ulemavu(ccbrt ikiwemo kwa kutoajiri walemavu ingawa ni taasisi ya kusimamia walemavu nchini)
f) lakini kama hilo halitoshi gharama za matibabu ni za juu sana katika hospitali zilizo chini ya ccbrt, takwimu zipo; gharama ya matibabu kwa ccbrt mtu binafsi anatakiwa kulipa kati ya dola 400-714 sawa na 600,000-1,071,000/= gharama hii ni kubwa ajabu kulingana na pato la kawaida la mtanzania na pia ni gharama ya juu hata kuzidi hospitali zingine hapa nchini ambazo hazipati msaada serikali wala mashirika makubwa ya nje na pia hazifanyiwi harambee kama ccbrt.,mfano cataract surgery hindu mandal 400,000/=, aga khan 315,000/= regency 300,000/= mission mikocheni 180,000 wakati ccbrt 680,000(tom venneste appendix iii-nov 2008)

pia ccbrt imekuwa haiko tayari kuwa wawazi juu ya kiasi cha mapato kinachochangiwa kutoka katika taasisi hizi kubwa duniani (dalili kubwa ya kuwepo ufisadi ndani yake)

ama ukiacha hayo ambayo yanamgusa moja kwa moja dr slaa, pia kuna yanayowahusu viongozi wengine wa chadema kama vile diwani wa kata ya serengeti,mkoani mara kukamatwa akimiliki ak47 kinyume cha sheria kiuhalisia huu pia ni ufisadi na hata yule mbunge wa cuf aliyeshutumiwa kuingiza nchini magari ya wizi na kisha kukwepa kodi huu pia ni ufisadi ila inapotokea mambo kama haya yakifanywa na viongozi au wanachama wa ccm yatatangazwa vyombo vyote vya habari na pia suala hilo litabebeshwa kwa chama badala ya mtu binafsi.

sasa hapa dr slaa yeye binafsi kama dr slaa hana tuhuma gani za kujibu? Kama unaona kuajiri na kutibu wachaga na watu wa kaskazini basi ni tuhuma basi nenda kwa utawala wa hiyo hospitali. Dr slaa anahusika vipi na uendeshaji wa kila siku wa hospital?

hii hoja ya wachaga kila wakati ni vipi jamani? Mimi kila nikisiliza matangazo ya vifo radio one, matangazo mengi yanakuwa ya watu kutoka uchagani, au kaskazini( kilimanjaro, arusha) sasa hapa nako kuna upendeleo kwa hawa watu???
 
Huyu jamaa hana hoja...zaidi naona majungu ndo yametawala...hawa wafadhili uliowataja ukichezea pesa zao huwezi pewa tena awamu nyingine coz wanafatilia kila senti inayotumika..Iweje CCBRT iendelee kupewa fedha miaka nenda rudi...ACHA UNAZI WEWE...wanajamii mi naona huyu mleta USHUZI anataka kubadiri attention za watu kuacha kujadili mambo ya msingi.
 
Nadhani Dr. Slaa hapa anawajibika kujibu yale ya kisera pekee kutokana na role ya Bodi ya Wakurugenzi. Lakini yale mengine ambayo yameambatanishwa humu ni muhimu yakawa directed to Managing Director (i hope the Centre has a person like that) kama Mtendaji Mkuu wa shughuli za kila siku na mtoa taarifa kwa Bodi. Taarifa za MD ndizo uchangia kutoa maamuzi na wakati mwingine kuona umuhimu wa kuwa na sera fulani fulani kwa manufaa ya jamii,sasa kama anadanganya, hili nalo ni tatizo lingine. Mfano anaweza kuonyesha katika takwimu walemavu ni asilimia 0.2% improvement ikawa 0.7% na Bodi ikaona kazi imefanyika.

Vilevile tafsiri ya kusimamia walemavu si katika lengo la kutoa ajira kwa walemavu zaidi ila kuwapata watu wa kuwahudumia walemavu.Mtu anayemuhudumia mlemavu automatically anapaswa awe mzima.Hapa sijaona tatizo.

Hilo la ajira nyingi kutoka ukanda fulani, majibu yake huwa ni mepesi tu WANAUWEZO,VYETI VIZURI NA WAMESHINDA USAHILI (INTERVIEW) na haya yote hayazingatii ukanda ila wanajikuta wanatokea sehemu moja by COINCIDENCE tu.Teeeeh....teeeeh.

Ni mtazamo tu.
 
Mimi huwa naamini kuwa anayezungumzia na kuchambua masuala ya ubaguzi wa kikabila kama mtoa mada hii, yeye ndiye mwenye kasumba za ubaguzi.

Back to the mada, Mimi nadhan proper way ya kuassess ubaguzi hapo ingekuwa ni kujua idadi ya watu waliokataliwa kupewa huduma na CCBRT na sio kuangalia watu waliopewa huduma CCBRT. Hiki kingekuwa ndiyo kipimo sahihi, mana tungeenda hatua ya mbele zaidi ya kutaka kujua ni kwa nini wamekataliwa, then kama tungekuta kuwa ni makabila yao ndiyo yamewaponza wasipewe huduma then tungesema CCBRT kuna ukabila.

Kigezo ulichokitumia kupima ukabila, hasa kwa idadi ya wagonjwa waliotibiwa mimi nadhan si sahihi kwa sababu zifuatazo: -

1. Inawezekana watu wengi wa kaskazini ndio wenye uwezo wa kumudu gharama hizo kubwa kama ulivyotuambia AU

2. Inawezekana watu wa kaskazini ndio wenye information za kutosha kuhusu huduma zitolewazo na CCBRT.

3. Mtandao wa huduma za CCBRT upoje?? umefika Kigoma??umefika Ruvuma??upo kila Mkoa???

4. Takwimu zako zimebase kwenye study area gani??usije kuwa ulifanya utafiti huu Mikoa ya kaskazini then ukaja kulalama JF kwa matokeo hayo. Sample size ni ngap??je inatosha kisayansi kugeneralize matokeo ya utafiti huo kwa Tanzania nzima???

5. Kuhusu ubaguzi wa ajira kwa walemavu, huu utafiti ni Tanzania nzima au?? hiyo 0.7% ni watu wangap?, Je katika hiyo 0.7% CCBRT ina ngap ambayo ni sawa na watu wangap???

6. Kuhusu kuajiri wachaga, Hapa pia ilibidi uainishe mchakato mzima wa kupata waajiriwa wapya lakin pia ungechanganua walioapply, shortlisted na waliofika kwenye intervw na waliopata kazi pia ungetuambiwa composition ya interview panelists kimakabila then tungeweza kupata hints za nn kimetokea. Kudeal na ishu ya ukabila ni kazi, so mtoa mada ulibd uzame kote huko.

Kimsingi ulichotaka kusema ni kwamba ukiona duka la bidhaa linafwatwa na jamii fulani, basi hapo kuna ukabila. Hii si sahihi, ni wangap hatuend kununua nguo Woolworth??Nani katubagua???Ni wangap hatutumii usafiri wa Ndege??nani katubagua??je iwapo ikaonyesha Precision air imesafirisha wazungu wengi kuliko weusi utasema Precision wanabagua weusi??

Je ungekuta 80% ya interview panelists ni wasukuma na ukakuta 70% ya walioshinda hizo interview ni wa kaskazini, hili ungeliwekaje???

Mimi nadhan ulitakiwa ujiridhishe kwanza kabla ya kuleta tuhuma jamvini, Naona kuna mambo mengi ulitakiwa kutueleza zaidi ya haya ili mada yako iwe na nguvu. Vinginevyo tutaona kuwa lengo lako kuu ni kumchafua DK. Slaa na kumuimplicate kinguvu bila kuwa na hoja ya msingi. You might have valid point, ila kwa utetezi huu hoja yako inaonekana ni kuchafauana majina. Jipange upya afu uje kivingine.
 
Back
Top Bottom