Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Mar 5, 2012.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Nimepita katika group moja katika facebook nikakuta kuna post ambayo inazungumzia tuhuma za ufisadi uliofanywa na watu mbalimbali kutoka vyama vya upinzani akiwemo Dr Slaa..,si vibaya tuhuma hizi nikizileta hapa jamvini kwa kuwa Dr Slaa yupo na naamini wapo pia watu wenye uelewa katika haya yaliyozungumzwa wanaweza kuchangia ama kusaidia katika kukanusha ama kusahihisha ama kukiri tuhuma hizi..,

  extracted from TANURI LA FIKRA

  Kuchukua tuhuma za mwanachama na kuivesha tuhuma hiyo kwa chama ni makosa na hili linafanywa makusudi na wapinzani ili waendelee kichafua CCM.,haiwezekani ufisadi unasibishwe na CCM hali ya kuwa katika kila chama watu wa AINA hiyo wapo; Nikianza moja kwa moja na katibu mkuu na mgombea URAIS wa chadema Bwana WILBROD SLAA ambaye ni kiongozi mkuu wa taasisi ya CCBRT (katibu wa bodi ya wakurugenzi) ambayo inapatiwa ruzuku ya shilingi za kitanzania; 1,000,000,000/= kutoka kwa serikali kila mwaka kwa kuiendeleza taasisi hiyo kwa manufaa ya watanzania wote na taifa kwa ujumla na pia inapata misaada na harambee mbalimbali kutoka kwa watu binafsi na mashirika makubwa ndani na nje ya TANZANIA kama EUROPEAN UNION,IRISH AID, AUSTRARIAN GVT, AusAID, CBM, JOHNSON&JOHNSON nk, ili kuwaendeleza watanzania katika nyanja ya afya,.tofauti na malengo hayo taasisi hii chini ya Dr Slaa imekuwa ikitoa huduma za jamii kwa ubaguzi mkubwa na kukosekana kwa usawa; nitabainisha kama ifuatavyo;
  a) Wagonjwa wanaotibiwa kwa mwaka wanakadiriwa kufika 1,080,000 katika hawa zaidi ya nusu ni kutoka katika mikoa ya kasikazini ikiongozwa na moshi na arusha.(branch ya CCBRT iko moshi)
  b) Operesheni zilizofanywa kati ya mwaka 2003-2007 ni kama ifuatavyo.,macho 31,200 napo pia zaidi ya nusu ya wagonjwa walitoka maeneo hayo. Mimi sidhani kuwa moshi kuna watu wenye matatizo ya macho zaidi ya Dodoma, Singida na sehemu nyingine za tanzania ya kati.
  c) Operesheni za orthopaedic&plastic surgery kati ya 2003-2007 ni 6,520 bado wagonjwa wengi walitokea kaskazini
  d) Na waathirika waliokuwa wakihudumiwa na CCBRT kati ya 2003-2007 zaidi ya 60% ni kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro (ripoti ya Tom Varnneste 24 jully 2008)
  e) Taasisi hii pia inakadiriwa kuwa na waajiriwa 320 napo hapa ni uchaga, na ukaskazini umetawala, mchakato wa uajiri ukisaidiwa na Jacqueline Kweka(Advocacy Officer) uliona kuwa hakuna watu waliosoma na kustahili kufanya kazi CCBRT ila ni wachaga na watu wa kanda ya kaskazini. Katika utafiti uliosimamiwa na CCBRT, Radar development pamoja na DISABILITY AID ABROAD umeonyesha kuwa ni asilimia 0.7% ya waajiriwa ndio watu wenye ulemavu(CCBRT ikiwemo kwa kutoajiri walemavu ingawa ni taasisi ya kusimamia walemavu nchini)
  f) Lakini kama hilo halitoshi gharama za matibabu ni za juu sana katika hospitali zilizo chini ya CCBRT, takwimu zipo; Gharama ya matibabu kwa CCBRT mtu binafsi anatakiwa kulipa kati ya dola 400-714 sawa na 600,000-1,071,000/= gharama hii ni kubwa ajabu kulingana na pato la kawaida la mtanzania na pia ni gharama ya juu hata kuzidi hospitali zingine hapa nchini ambazo hazipati msaada serikali wala mashirika makubwa ya nje na pia hazifanyiwi harambee kama CCBRT.,mfano CATARACT SURGERY HINDU MANDAL 400,000/=, AGA KHAN 315,000/= REGENCY 300,000/= MISSION MIKOCHENI 180,000 WAKATI CCBRT 680,000(Tom Venneste Appendix iii-nov 2008)

  Pia CCBRT imekuwa haiko tayari kuwa wawazi juu ya kiasi cha mapato kinachochangiwa kutoka katika taasisi hizi kubwa duniani (dalili kubwa ya kuwepo ufisadi ndani yake)


  Ama ukiacha hayo ambayo yanamgusa moja kwa moja Dr Slaa, pia kuna yanayowahusu viongozi wengine wa CHADEMA kama vile DIWANI WA KATA YA SERENGETI,MKOANI MARA KUKAMATWA AKIMILIKI AK47 KINYUME CHA SHERIA kiuhalisia huu pia ni ufisadi na hata yule MBUNGE WA CUF ALIYESHUTUMIWA KUINGIZA NCHINI MAGARI YA WIZI NA KISHA KUKWEPA KODI huu pia ni ufisadi ila inapotokea mambo kama haya yakifanywa na viongozi au wanachama wa CCM yatatangazwa vyombo vyote vya habari na pia suala hilo litabebeshwa kwa chama badala ya mtu binafsi.


   
 2. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  TandaleOne, hizo ni shutuma au majungu na umbea?
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama haya mapesa yanayotolewa na wafadhili huwa yanafika yote!! Ngoja Dr. Slaa aje atueleweshe!!
   
 4. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  yote yaweza kuwa sahihi..,yawezekana kuwa ni shutuma, majungu ama umbea.
   
 5. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Duh........... Kweli tuhuma zingine ni ushuzi mtupu, kwanza hayo ni majungu na si tuhuma........ Mkuu TO ungepekua nyingine ulete tuone kama zitakuwa na mashiko...
   
 6. m

  moshingi JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba nijibu hapo kwenye red, Hivi katika nchi hii ni shirika gani au idara gani ya serikali ambayo inahitaji kuajiri wataalamu wa nyanja yeyote ile imeweza kuwakwepa Wachaga?

  Wachaga wasilaumiwe kwa kwenda shule kwa wingi kuliko makabila mengine maana wao hawakuwazuia wengine wasiende shule...wawalaumu wakoloni waliojipendekeza kwao wakawapelekea shule nyingi ili kupooza upinzani waliokuwa wakiupata.

  Tukianza kuangaliana kwa makabila hatufiki mbali...KUHUSU MAPATO YA CCBRT na viwango vya gharama DR. SLAA JIBU MWENYEWE
   
 7. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kupasuka kichwa ama kufa kwa presureangali u-kijana katika maisha yetu sisi waafrika hasa wa kusini mwa jangwa la sahara ni ukiamua kupima INTEGRITY ya hawa wakuu wetu...!
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ukishajibiwa halafu iweje?
   
 9. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umamluki usiokuwa na tija.. Na umeandaliwa rasmi kumchafua dr. Wa ukweli pws.
   
 10. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka TO nawe kumbe unamajungu(umbea)???
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,818
  Likes Received: 36,917
  Trophy Points: 280
  Una trakoma na unahitaji matibabu???
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tafuteni kwanza msaada wa mkaguzi endapo nyinyi wana-CCM kuna mahesabu ya kifedha hayawaridhishini vizuri CHADEMA.

   
 13. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napenda kukujulisha kuwa una hoja binafsi na huenda hujawahi kupata matibabu ccbrt ila unahisi,nina ushahidi wa kupeleka mzazi wangu pale wala sikukutana na swali la mahali ninatoka ili kupewa huduma na pia gharama iliyotumika haikufika 150,000.unachoandika huna utafiti nacho na pia hakina maana swala la ajira ni compentency ya muombaji kazi mbona huongelei wizara ya fedha wenzako wanasoma na wewe nakuomba somesha ndugu zako acha kula raha na kukalia majungu,hata waislamu wanalaumu wakristo kwa kuwa na ajira zaidi yao.cha msingi somesha,soma na ajira ziko wazi kwa kila mwenye sima.

  Kuhusu walemavu angalia ratio yao na taaluma walizonazo.
   
 14. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Bado sijapata conection ya jambo lililoelezewa na kichwa cha habari.Naona kama vile mwandishi ana hoja ya msingi ila hajajipanga vyema ,inaonyesha alikuwa ana malengo binafsi ya kumchafua mtu.Hizo Vague statement kwenye red ambazo hazina ushahidi zinaharibu picha nzima .
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Huu wa Nape sasa unatia kinyaa. Mimi ni Mngoni mamangu, dada yangu na mtoto wangu wametibiwa CCBRT zaidi ya mara kumi hakuna cha usumbufu wala kuonewa na hizo gharama sikuziona. Acheni mambo ya kisen.ge CCM
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,132
  Likes Received: 6,624
  Trophy Points: 280
  umanaleta mambo ya faicebuku huku, lol,
  jf wapo watu wenye akili zao
  mwenye under 18 humu jf ni wewe peke yako.
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  huu ni upunguani, ujuha , ukarunguyeye wa akili na mdondo wa fikra unamtafuna huyu mtu.
   
 18. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,215
  Likes Received: 10,568
  Trophy Points: 280
  kwa kuanza Dr Slaa si katibu mkuu bodi ya wakurugenzi bali ni mwenyeketi. Hivyo basi inaonyesha hata mtoa tuhuma hajui anachokiandika...
  NB:.Mtajaribu kumchafua Dr. wetu lakini hamtaweza. Magamba tafuten staili nyingine mmeishiwa na stail shwain nyie...
   
 19. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napenda kukujulisha kuwa una hoja binafsi na huenda hujawahi kupata matibabu ccbrt ila unahisi,nina ushahidi wa kupeleka mzazi wangu pale wala sikukutana na swali la mahali ninatoka ili kupewa huduma na pia gharama iliyotumika haikufika 150,000.unachoandika huna utafiti nacho na pia hakina maana swala la ajira ni compentency ya muombaji kazi mbona huongelei wizara ya fedha wenzako wanasoma na wewe nakuomba somesha ndugu zako acha kula raha na kukalia majungu,hata waislamu wanalaumu wakristo kwa kuwa na ajira zaidi yao.cha msingi somesha,soma na ajira ziko wazi kwa kila mwenye sima.

  Kuhusu walemavu angalia ratio yao na taaluma walizonazo.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  tujulishwe na hali halisi ya ufisadi wa pesa iliyotumika uzini.
   
Loading...