Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTO -CHADEMA, wenzenu wameanzisha chama kiwasaidie kimaisha! na nyie anzisheni vya kwenu!
 
hii hoja ya wachaga kila wakati ni vipi jamani? Mimi kila nikisiliza matangazo ya vifo radio one, matangazo mengi yanakuwa ya watu kutoka uchagani, au kaskazini( kilimanjaro, arusha) sasa hapa nako kuna upendeleo kwa hawa watu???

Mtoa hoja hii anajifunza nina hakika kajui Dr. Slaa ni nani pale CCBRT au kaongopewa na mafisadi wenzake ajiandikia tu. Namshauri mara nyingine awe na vyanzo vizuri kabla hajaleta mada isiyo na mashiko.
Watuhumiwa wote kesi zao hushughulikiwa na jeshi la POLISI siyo vyama vya siasa au viongozi wa vyama hivyo, au kama mtoa mada siyo RAIA wa nchi hii awezi kujua mihimili ya DOLA ilivyo.
Tandaleone jifunze kwanza kabla hujaja kwenye jukwaa la watu wenye WELEDI.
 
Umetumwa na mafisadi wenzako kuja kumchafua Dr slaa rais wetu wa moyoni na Vuvuzela Nape,umekwama,subiri mwaka 2015 uone tunavyochukua nchi yetu kutoka kwa mafisadi CCM.
 
Anzisha thread nyingine nadhani umekurupuka toka usingizni hivo kanawe kwanza uso ndo utuambie unachotaka kutueleza. mambo ya udaku wa facebk usituletee hapa jamvini kwa watu makini
 
Umetumwa na mafisadi wenzako kuja kumchafua Dr slaa rais wetu wa moyoni na Vuvuzela Nape,umekwama,subiri mwaka 2015 uone tunavyochukua nchi yetu kutoka kwa mafisadi CCM.

Kaka Pelege hoja ujibiwa na hoja Mkuu. JUST KICK OFF TO THE BOTTOM OF A CIRCLE!
 
WE NI MBUMBUMBU SANA...
Hivi docta slaa ni mchaga?!

Acha umbumbumbu wewe. Kwani ile ccbrt ni ya kwake? We vipi unaanza kuugua tukuwahishe apolo!. Eti wachaga ndo wanatibiwa wengi mbona hata wakimbizi ni wengr mno wanaotibiwa ccbrt?.

We kama huwajui wachaga nyamaza tu, hawa jamaa ni noma wamesoma sana kila idara wapo, jk mwenyewe alisema ukiona sehem mchaga hayupo hapafai kuishi, kama nchi yetu ingekuwa na watu wote kama wachaga tungekuwa mbali. Ebu waangalie 2 kwenye biashara utawajua, NDG YANGU ACHA UMBEA FANYA KAZI ACHANA NA WACHAGA WATAKUUMIZA KICHWA.
 
It all started by Tuntemeke who kicked the ball to PAA, PAA kicked the ball to TII and now it is TII who has given TOO a long pass! The game is still alive.
 
Ndugu zangu,

Kila kukicha wachaga, wachaga, hahahahahahaaaaa katika nchi yetu kuna makabila ambayo watu wake waliona jua mapema, miongoni mwao ni wachaga, wahaya, wanyakyusa!

Wakati wengine wakiwinda, kucheza unyago, au kuvua samaki pale baharini hawa wenzetu walikuwa shule walijifunza mengi ikiwemo biashara. Angalia dominants wa biashara hapa Tanzania baada ya wawekezaji ni makabila yapi. Katika ofisi nyeti angalia makabila yanayoziongoza.

Sishangai kuwaona wakichangamkia hata fursa za matibabu wakati wengine wakibanana kwa wapiga ramli. Wakati umefika badala ya kupiga majungu we have to strive for opportunities available. Opportunities are not given but taken!
 
Ndugu zangu,
Kila kukicha wachaga, wachaga, hahahahahahaaaaa katika nchi yetu kuna makabila ambayo watu wake waliona jua mapema, miongoni mwao ni wachaga, wahaya, wanyakyusa! Wakati wengine wakiwinda, kucheza unyago, au kuvua samaki pale baharini hawa wenzetu walikuwa shule walijifunza mengi ikiwemo biashara. Angalia dominants wa biashara hapa Tanzania baada ya wawekezaji ni makabila yapi. Katika ofisi nyeti angalia makabila yanayoziongoza. Sishangai kuwaona wakichangamkia hata fursa za matibabu wakati wengine wakibanana kwa wapiga ramli. Wakati umefika badala ya kupiga majungu we have to strive for opportunities available. Opportunities are not given but taken!

Na fursa za kisiasa pia mkuu au?
 
Mimi naamini kabisa kama hayo si majungu, Takukuru tayari wangeshamkaba koo Dr Slaa. Nasikiavyo TAKUKURU wamepewa maagizo maalum kuhusu tuhuma zozote za ufisadi kuhusu viongozi wakuu wa CDM. Kama la kweli wasingeliacha hilo kamwe!
 
Bwana Tandaleone hii ni taasisi ya umma au? Kama ni taasisi binafsi swala la kuwa transparency ni hiari ila kwa wanaoichangia hii taasisi lazima wanapata taarifa za matumizi ya fedha wanazotoa, hivi kwa akili yako kama kweli taasisi hii inapokea ruzuku kutoka serikalini unafikiri wakitumia vibaya Slaa atapona kama ni mlengwa? Hivi hayo mashirika ya nje yanayosaidia unajua jinsi yanavyofuatilia fedha zao?

Kuhusu ajira kwanini uelekeze shutuma kwa Slaa wakati yeye sio Mchagga (Labda ungezungumza habari za Wahaya)? Kama kuna wa-iraqw wengi kwenye hiyo taasisi hebu tujuze ili angalau hoja ipate mashiko.. Hiyo bodi hakika haikosi mwenyekiti sasa mbona tusitake kujua pia upande huo unahusika vipi au ndio kusema kwakuwa yeye ni mwiba kwa mafisadi lolote linalofaa kumtuhumu ndio atuhumiwe hata pasipo ushahidi wa kutosha?
 
Chagga people are leading for nepotism and favouritism among African societies, study suggests. Famous research conducted and compiled by the late Zimbabwean professor Julius Mambubwa on 'the effects of nepotism to the economic growth of Africa' documented that 50 percent of the employed Chagga people have had their current jobs through the influence of their fellow Chagga relatives.

Additionally, it went on showing that in nearly each of the public office which is headed by a Chagga, 45 percent of the workers are coming from Chagga tribe apparently getting their employment after someone at the top had pulled strings for them.
 
Hivi kuwa mchaga ni kosa?????????????? Kuna mahali ameajiriwa mchaga kwa kuwa ni mchaga tu au kwa uwezo wa elimu yake? Ukiona watoto wako huwaoni nyumbani wakati wa chakula usigombane na majirani chukua kapu nenda kwenye bucha uone kama utawalalamikia majirani tena.......................... Mtu ahukumiwe kwa makosa yake sio kwa kabila lake!!!!!!!!!!!!!!!
 
mafisadi wapo kote hadi kwenye upinzani! utake usitake HAKUNA ALIYEMSAFI TUSIDANGANYANE
 
watu bana wako very biased,afu tena wanajiita wasomi,wanaharakati! hawako tayari kukubali kwamba wao wanapangufu au wanamakosa! GREAT THINKERS! teh teh teh
 
Mimi nadhani hoja zako kama ni za kweli zingekuwa na maana zaidi endapo ungekwenda ndani zaidi kujua ni kwa nini hao unaowaita wachagga na wakaskazini wanachangamkia zaidi huduma za CCBRT kuliko watu wa maeneo mengine. Inawezekana kabisa zilezile sababu zinazowafanya kuwa na madaktari na wataalamu wengine wengi zaidi kuliko watu wa maeneo mengine ndio zinasababisha waweze kuchangamkia zaidi huduma hizi kuliko watu wa maeneo mengine.
 
Kwanza kabisa huyo "Tambwe Hiza" hajui Dr.Slaa ni nani katika CCBRT.
yeye sio katibu wa bodi ya wakurugenzi,...bali ni
RAIS wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya CCBRT.

Hayo madai mengine ni upuuzi.
Sasa unasema watu wengi walotibiwa ni wa arusha na moshi,..
unataka watu wa wapi waugue?

Kama baba yako yuko Lindi mwambie augue then uone kama hata tibiwa.
Umeonesha upungufu wako wa akili kwa kuweka ukanda na ukabira,...
bora ungekuja na hoja ya ufujaji mali hapo tunge kupa support katika kutaka majibu.

Lakini kwa uongo kama huu?
Nitashangaa sana kama Dr.Slaa atajibu propaganda.
 
JF sometimes inaboa sana. Ndiyo maana watu makini wa miaka hiyo siku hizi hawachangii humu.

Mimi nilipoona tuhuma nikajua labla Dr Slaa anakabiliwa na wizi mabilioni ya CCBRT kama ilivyo EPA, Richmond etc. Hapo hakuna kitu zaidi ya witchhunting ambayo haina nafasi. Suala la nani na wa wapi katibiwa hilo si Tatizo provided ni mtanzania na ana haki ya kutibiwa.

Binafsi kuna watu kama watano wa kutoka kanda ya ziwa ninawafahamu leo hii wanaona kwa kupata matibabu CCBRT. Tuache majungu ya namna hii kwani yanaonesha ni jinsi gani uwezo wetu wa kufikiri ulivyokuwa corrupted!

Tukianza kui-politicise CCBRT watakaoumia ni watanzania wa hali ya chini. Kama CCBRT inafanya vizuri chini ya uenyekiti wa Dr Slaa ni dhahiri kabisa kuwa Dr Slaa ni kiongozi mzuri hata akipewa nafasi ingine ya kuongoza. Hii witch-hunt ni lazima inafanywa na watu wenye ufinyu wa kuona mbali zaidi ya kilichomo kwenye sahani zao za vyakula.
 
Dr.Slaa ni Muiraq, hilo la kwanza.Pili:Anayekwenda hospitali ni mgojwa,sasa wewe badala ya kushukuru ndugu zako wa kusini,mashariki,magharibi na kusini-kusini mashariki and the like ni wazima,unatamani waugue tu ili wakatibiwe CCBRT? hizo akili matope?Taasisi za Kimataifa mara nyingi hutoa misaada pasipo na Ufisadi wala matumizi mabaya ya fedha,ndio sifa kubwa ya CCBR chini ya Dr.Slaa kupata hizo hisani.

Kuhusu wachagga wengi kuajiriwa pale sidhani kama ni tatizo la Bodi ya wakurugenzi,labda unajua ni watu wangapi waliomba kazi na wakutoka makabila gani na waliokosa ni kwa sababu za kikabila?Mbona hata TRA wamejaa wachagga,CRDB ya chazi kimei pia,Bandari,Jeshi la Polisi la Said Mwema wenyewe watupu,lakini Mbona hata Vyuo vya Elimu ya Juu wanafunzi wengi wachagga,Kawambwa kawabeba nini?naye Mkaskazini?

Kaskazini hata Kagera kwa wahaya pia ni kaskazini,Je,mbona Maprofesa wengi wahaya nao wamependelewa?Naskitika kuingia kwenye kundi la wenye akili hewa kama zako kuchangia thread hii maana iko Toooooo low to be commented by People of my Calibre!!Pole mtoa uzi!!!!

KIMBUNGA #47 kamaliza kila kitu,huyu Tuntemeke makamasi sana!!!Kukosa uongozi sehemu kama inakuwa nongwa basi haina haja ya kwenda shule,maana elimu sio mkombozi tena!!!
 
Back
Top Bottom