Nilishawaambia lakini hamtaki kuelewa
Dr Slaa hana Mpango wa kurejea CHADEMA
Kafulila alienda kuongea nae kumwomba ajiunge ACT na agombee Uraisi huko
Kafulila atajiunga na ACT hivi karibuni
Dr hajakubaliana bado na ACT...Ila maongezi yako kwenye hatua nzuri
Pia Its Confirmed Kuwa Lipumba atajiunga na ACT.
Tuwe makini katika mambo tunayoandika, tunapaswa kukumbuka kuwa Dr. amefanya kazi kubwa sana ndani ya CDM. Kutokukubaliana katika maisha ni jambo la kawaida, anazo hoja ambazo kwa maoni yangu alikuwa sahihi. Isipokuwa watu kwa wakati huu wanataka mabadiliko kutokana na fursa iliyopo na mara nyingi haziji mara mbili. Hawa jamaa wakiachiwa wakati huu watajipanga na hawatafanya makosa .
Ni vizuri Dr. akaliangalia hilo na kutafuta suluhu badala ya kuwa na misimamo mikali ambayo itapunguza fursa hii muhimu kwa wakati huu. Suala la wizi wa kura hata mwaka huu huwezi kulikwepa, ikiwa wanaibiana wenyewe ndani ya chama chao sembuse za wapinzani? Lakini wizi unakuwa mgumu iwapo kunakuwa na ushindi mkubwa. Hivyo tunamhitaji Dr. sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote, yeyote anayeweza kusaidia hilo na alifanye kwa moyo wote.
Kuzungumzia chadema ni nafuu uzungumzie ACT, Mambo waloyafanya ni ya ajabu sana sana, Dr. Hawezi kukubaliana na ujinga wa namna hiyo, ww umtukane mtu na ufanye hadi kapoteza uwaziri mkuu wake na unao ushahidi wa kutosha na unathibitishia watanzania na unasema kama Lowasa anabisha na aende mahakamani kwa kuwa ni kweli Lowasa hakuwahi kwenda mahakani. Maana yake kulikuwa na ukweli, Jana ulikuwa unasema Lowasa mwizi fisadi, leo unasema mwenye ushahidi na aende mahakamani, hivi wanaona ss mabwege sana na hatuna ufahamu kabisa.
Mimi nimesikia viongozi wakubwa wa ukawa wanasema kwamba ccm hawakumtedea haki Lowasa hadi walimkata na imekuwa ni ajenda kubwa sana sana, swali langu kwao je uchaguzi wa kumpata Mgombea wa UKAWA ulikuwa wa kidemokrasia? Kwani nn nasema hivyo sijaona wagombea wa vyama washirika ambao walipata nafasi kwenye vyama vyao wakichuana na Lowasa, kilichofanyika ni kumpachika Lowasa kugombea nafasi hiyo, na kama wao wanademokrasia kiasi hicho mbona hawajafanya mazungumzo na waasisi wa ukawa? Ss Lipumba kaondoka na Dr. Slaa pia. Tena Mbowe anawaaminisha wajumbe kuwa mzee tumeamua kumpumzisha, maana yake tu ni kwamba watu wasihoji, kuhusu Dr. Slaa.
Wenye ufahamu tayari nao wameondoka kimya kimya wala wao hawatangazi, ila mwaka huu UKAWA mlikuwa na bahati sana ya kuingia ikulu ss mtabakia kuitazama tu kwa ajili ya tamaa zenu za ajabu ajabu, mimi nawapa pole sana sana, watanzania tulio waengi tunatizama picha inavyokwenda japo kusoma hatujui.
Yeye aende anakoenda na ataenda yeye na familia yake. Sisi ni wafuasi wa chama siyo wa mtu , nafikiri majibu mmeyapata kwa LIPUMBA. Wasaidieni hao watu kiuchumi lakini sisi malengo yetu yako palepale kumwondoa mkoloni mweusi CCM oktoba."DK SLAA amefunguka kwamba dakika za mwisho MBOWE aliwaburuza na kulazimisha tumpokee LOWASA , hapo nikaona nikae pembeni. muda si mrefu nitaitisha press confrence kwani watu wanapotosha sana kuhusu mimi DK SLAA."
yeye aende anakoenda na ataenda yeye na familia yake. Sisi ni wafuasi wa chama siyo wa mtu , nafikiri majibu mmeyapata kwa lipumba. Wasaidieni hao watu kiuchumi lakini sisi malengo yetu yako palepale kumwondoa mkoloni mweusi ccm oktoba.
Mimi siku zote ni mfuasi wa chama si mtu. Ukiwa mfuasi wa mtu je akifa utafanyaje? Kama yeye kachoka aende anakoenda au apumzike kama afanyavyo kwani umeona kazi zimesimama kwa yeye kutokuwapo? Kufa kufaana.leo unamkana dk
leo unamkana dk
"DK SLAA amefunguka kwamba dakika za mwisho MBOWE aliwaburuza na kulazimisha tumpokee LOWASA , hapo nikaona nikae pembeni. muda si mrefu nitaitisha press confrence kwani watu wanapotosha sana kuhusu mimi DK SLAA."