Baba,
Shikamoo. Majuzi nilichangia uzi wako; na leo nachangia tena. Wadogo zangu najua watashangaa najibizana na baba, lakini nia na madhumuni ni kuwekana sawa. Kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu.
Baba, naomba unipe ufafanuzi wa concerns zangu hapa chini;
1. Katiba ya CCM Ibara 13 (1) (e) inatamka bayana kwamba, uanachama wa mwanachama, utakoma iwapo
atajiunga na Chama kingine.
2. Mwaka 1995 katika mchakato wa kura za maoni kupitia CCM, wajumbe walimpitisha Dkt Wilbroad Slaa kuwa mgombea wa Ubunge wa jimbo la Karatu dhidi ya aliyekuwa mbunge wa CCM - Patrick Qorro.
3. Kutokana na sababu inazozijua yenyewe, CCM ilikata jina la Dkt Slaa na kurudisha jina la Qorro. Wananchi wa Karatu walimwomba Dkt Slaa kuondoka CCM na ajiunge na chama chochote makini, cha upinzani ili wao waweze kumchagua kuwa Mbunge wao. Kwa kuwa walimpenda. Walimwamini. Walimthamini. Narudia tena, wananchi wa Karatu.
4. Dkt Slaa akajiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kulingana na ibara tajwa hapo juu - automatically - akawa amejifuta/ameacha/amekoma kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi na kuwa mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
5. Kitendo cha kutokufuata falsafa, itikadi, ilani nk. ya CCM na kuipinga na kuikosoa kwa uwazi, by itself, ilitosha kumwondoa Dkt Slaa kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.
6. Kutoka mwaka 1995 hadi 2012 Nape (na masalia walioko kaburini kwa sasa kutokana na kurushiwa kitu kizito) alipozungumzia suala la kadi mbili; yapata miaka kumi na saba(17). Umri wa mtoto kuweza kuwa na mtoto!. Yaani umri wa Ritz, Rejao, Zomba na Chama!
7. Nape (na wewe umekumbushia tena) alisikika akisema Dkt Slaa ameendelea kulipia kadi yake kila mwezi kwa miaka yote 17 ( 17 x 12 = miezi 204).
8. Kutokana na maelezo yangu hapo juu (1 - 7) napenda baba nikuulize maswali yafuatayo:
(i) Kwa nini mmeendelea kumruhusu Dkt Slaa kulipia kadi yake, ilhali katiba yenu hairuhusu? Je, hamuoni kuwa mlikuwa mnamuibia?
(ii) Unaweza ukatuonyesha ledger (leja) na nakala ya stakabadhi (receipt) ambazo Dkt Slaa alikuwa analipia?
(iii) Alikuwa analipia tawi gani la Chama? Victoria (akiwa anaishi hapo), Bahari Beach, Karatu Mjini, Manyara Kibaoni, Rhotoa (kwa mzee Anderson), Mbulu mbulu, Mang'ola, Oldeani, Endamarariek?
(iv) Kwa nini mmekuwa na 'double standards'? Wanachama wenu wengine walioondoka kwa uwazi the same year (namzungumzia Mh. Agustino Mrema) hamkuwaruhusu kuendelea kulipia kadi zao, na mmewaacha waendelee kuwa nazo, lakini Dkt Slaa mkamuacha alipe?
(v) Hamuoni Katiba yenu kuwa 'bad law (Mayalla, 2013) kwa kuwa inazungumza hili na watendaji - tena Naibu Katibu Mkuu Bara na Katibu wa Itikadi na Uenezi - wanafanya vingine?
Baba, najua nimekuchosha na andiko langu refu. Uniwie radhi. Najua kwa umri wako huo saa hizi ulistahili kuota moto. Hivi bado unakaa kwa babu na bibi pale jirani na hospitali ya Mtukufu Agha Khan? Hivi baba, baada ya kurudi kutoka ng'ambo, unajishughulisha na kazi gani ya kukupatia kipato?
Cc
Molemo,
Pascal Mayalla,
Mwita Maranya