Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 3,129
- 4,285
Hata mi naskia ivo na anashirikiana vizuri tu na viongozi wa ccm na serikali ila kisiri sana
ulikuwa unataka ubunge wa karatu kwa maneno yako haya haufai coz siri hauwezi kutunza kuwa makinihata mimi pia nimesikia kuwa dr slaa anashirikiana kwa siri sana na viongozi wa ccm hasa wale watumishi wa umma waliompa nyaraka za epa, uingizaji wa silaha za ccm, wizi wa kura zake na ule waraka wa kufuatilia watumishi wa umma wanaounga mkono chadema ili wafukuzwa.
Ni kweli kabisa nasikia wanakutana mara nyingi sana tena usiku. Wewe nyaraka muhimu za kifisadi za serikali angezitoa wapi? Ni watumishi wa serikali ya ccm ambao ni wanaccm ndo wamempa? Tuko pamoja mkuu.
Kama hii kadi ya ccm aliyonayo faida yake ndo hizi, basi mimi naunga aendelee kuwa nayo. Ila bahati mbaya mambo yake yanaharibu ccm.
ni kweli naskia hajarudisha kadi na anawasiliana na viongozi wa ccm kwa siri kuu sana
Kama kawaida yako endelea na single nyingine hiyo haisikilizwi tena
Mkuu kimbunga mimi huwa ninakuheshimu sana kwenye augement zako. Nimekuwa nikifuatilia hoja zako sana mkuu. lakini kwa hili la udaku limenishitua sana kama na wewe unaweza kuamini hivyo.
Kwa wafuatliaji wa siasa za hapa kwetu Tanzania , mtakumbuka ya kwamba Dr Slaa alikuwa mwanachama mtiifu wa ccm kabla ya kuasi chama na kukimbilia cdm. Hata hivyo, mpaka leo hii Dr Slaa hajawahi kukabidhi kadi ya ccm.
Nimesikia leo Nape Mwanza kahoji Dr. Slaa alirudisha lini na wapi kadi ya CCM! Swali hili si dogo limenipa mawazo!
Kweli KATIBU MWENEZI wa CCM ana MUDA wa kuuliza KADI za CCM zimerudishwa WAPI? Hana MENGI yanayomkabili NDANI ya CHAMA CHAKE KITUKUFU? Wananchi wengi bado ni MASIKINI CHINI ya CCM; lakini VIONGOZI wengi Sasa NI MATAJIRI wenye UFISADI wa kupindukia; NADHANI hiyo ndio ingekuwa KAZI yake kuondosha hawa WEZI na kuwaelezea WANANCHI Kuwa PESA wanazolipa KODI zinakwenda KWENYE MIRADI MUHIMU kuliko kwenda KUKOPA kwa WACHINA kila KITU...
Hivi hata usiporudisha kadi Katiba ya CCM inasema hivi kuhusu uanachama:
7. (1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa
(3) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-(a)Kufariki.(4) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.
(b)Kujiuzulu mwenyewe.
(c)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
Nape, Katibu Mwenezi wa Chama anapaswa ajue haya.
My take:
Uongo na kuchafuana bado vinatumika kama mtaji wa kisiasa. Watu wameshaamka, tutumie mambo yenye maslahi ya nchi kufanya siasa.
Kama hajarudisha kadi, Nape anataka kuwaambia wana CCM kuwa Slaa bado mwana CCM?
Nnauye Jr, mtu akishaacha kulipa ada, au kujiunga rasmi na chama kingine si lazima arudishe kadi. Anakuwa si mwanachama kwa mujibu wa katiba ya CCM.