ANA KADI MBILI YA CCM NA YA CHADEMA ANA MADEMU WAWILI JOSEHINE NA ROZIMARY ANA KAZI MBILI NI PADRE NA MWANASIASA NI MSOMI NA NI KILAZA NI WA MAMBO MAWILI MAWILI.. ANATAKA UBUNGE ANATAKA URAISI..
Naomba uwe mtulive zaidi wakati unasoma post ili kuepuka kuunga unga majibu na ya kuudhi. Hoja yako na wenzako kuhusu Dr Slaa ni sio tu kuwa na card ya CCM, bali kwamba analipia ada. In other words, uanachama wake uko upo hai - ni mwanaCCM. Sasa nikuulize, again, kwa nini wanaCCM wanamshambulia mwanaCCM mwenzao? tena kupitia mitandao? Na ni kama hoja ni kuwa na card mbili toka vyama tofauti, kwanini kelele zinakuwa kwa Dr Slaa? Hivi ni Dr Slaa peke yake Tanzania hii mwenye card mbili? Why only target Dr Slaa?
Pili kiongozi, naona umebobea sana kwenye uchunguzi maisha binafsi ya watu, na hata kwenye post yako umeweza kutupa results za uchunguzi wako kuhusu maisha binafsi ya Dr Slaa, na kwangu mimi nimekuwa 'insulted' kwa kupewa majibu ya dharau na yasiyo na tija kwa matatizo ninayokumbana nayo. Nina mgonjwa sasa hivi Muhimbili kalala chini! Kafanyiwa operation baada ya wanandugu kujichanga na kulipia, lakini anatoka theather, hakuna pa kulala. Yuko chini! Dawa nimununua na kumuachia nurse.
Sijakuuliza maisha binafsi yako wewe, au ya mtu yoyote yule. Nikiwa kama mtanzania, ningefaidika zaidi kama uengeelekeza ujuzi wako wa uchunguzi na kutupa majina wa watu walioweka hela Swiss, mrejesho wa hela za EPA, mwenendo mzima stimulus package, ulipaji kodi kwa makampuni ya madini. Haya kwangu ni muhimu maana yanaweza kusaidia kuboresha huduma za afya na hata mgonjwa wangu angeweza kupata kitanda, pia hela zingesaidia kujenga barabara, kulipa walimu, na hata kugharamia ujenzi wa reli mpya na za kisasa.
Ifike mahali sasa watu kama wewe muache kudharau watanzania kwa kutuleweka kwenye siasa za maji taka. Ni majibu ya kipuuzi kama hayo uliyoandika ndiyo yanafanya watanzania wakione CCM ni sawa na kikundi cha majambazi. Na kama CCM imeishiwa to the extent ya kutoa hoja za kihuni kiasi hicho badala ya kujadilia matatizo yanayowakabili wapiga kura, basi hiki chama hakifai.
Assume uliyoandika kuhusu Dr Slaa ni sahihi. Now, tell me, mgonjwa wangu amelala chini baada ya kukosa kitanda kwa sababu Dr Slaa kazi mbili - upadre na uana siasa? Liliondo as we speak wanaomboleza wenzao waliopoteza maisha kutokana na njaa kali - hawana msaada wowote toka serikalini. Hapa alaumiwe Dr Slaa kwa sababu ana 'mademu wawili?
Kwa ujumla 36% ya watanzania wote (aprox 16m poeple) ni maskini wa kutupwa. Nayo hii imeletwa na Dr Slaa?
Kesho tarehe 9/12/2012, tutasheherekea miaka 51 ya uhuru. Tanzania hata net za mbu tunaomba! Why? 51 years ago GDP ya Tanzania ilikuwa zaidi ya South Korea. Leo hii tuko wapi? Ukitizama nchi jirani na Tanzania, hakuna hata moja yenye rasilimali kutufikia, lakini angalia situation on the ground!
Then anajitokeza mtu na utashi wake anataka kujadili who is sleeping with who? Kama sio madharau kwetu sisi wavuja jasho ni nini? Ni kwanini wakubwa hawataki hata wajadili mambo ya msingi badala yake wanaleta uhuni? Kuna tatizo gani CCM? Ni lini wataacha madharau?